Wanaowania tuzo ya Ballon d’Or 2014 walishatangazwa ambapo list hiyo pia inawahusisha mastaa wa soka kama Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, huku list hiyo ikiwa pia na wachezaji wa Ujerumani iliyoshinda kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil. Baada ya ushindi wa Ronaldo na Messi kuchukua headlines sana kocha wa Manchester United Louis van Gaal
(63) ameamua kuyatoa ya moyoni na kusema mwaka huu Ronaldo na Messi
hawatakiwi kuchukua hiyo tuzo bali ni halali ikachukuliwa na mchezaji wa
Ujerumani. Wajerumani wanaowania tuzo hiyo ni Mario Gotze, Toni Kroos, Philipp Lahm, Thomas Muller, Manuel Neuer na Bastian Schweinsteiger. Anasema ‘Naamini
Ujerumani inafaa kuchukua hii tuzo, mara nyingi imekua tu ni wachezaji
maarufu/wanaofahamika ndio wanashinda hii tuzo, kitu kikubwa kushinda ni
kombe la dunia ndio maana naamini itachukuliwa na mchezaji wa Ujerumani
sababu kiukweli wanastahili‘ Umeonaje
mawazo ya Van Gaal? ungependa nani ashinde Ballon d’Or ya 2014 mtu
wangu? naomba niachie maoni yako kwenye comment hapa chini.
Ni
stori nyingi tunakutana nazo kwenye vyombo vya habari kila tunapoamka
na mara nyingi tunaamka nazo kwenye mitandao ya kijamii moja wapo ikiwa
hii ya mwimbaji wa Uganda Jose Chameleone kudaiwa kumuomba Diamond wafanye collabo. Kwenye interview na Mambo Mseto ya Radio Citizen November 19 2014 Chameleone amekanusha hizo taarifa kwa kusema ‘kitu
ambacho nitakwambia kabla ya kusema chochote, mimi naheshimu wasanii
wote mashariki na duniani na nataka niwakumbushe kitu kingine, nimekaa
kwenye muziki kwa miaka kumi na nne… mimi sio msanii mchanga’ ‘Ilikua
ni uongo sijui umetokea wapi eti mimi nimemuomba collabo, Yes….
tunaweza kufanya collabo lakini mimi sijamuomba collabo, wamesema mimi
nimezungumza na Diamond kwenye whatsapp… yes tumezungumza lakini ilikua
ni kirafiki wala hatujaongea maneno ya kimuziki’ – Jose ‘Mimi ni msanii mkubwa, sio msanii mchanga… naheshimu kila msanii
kuanzia mchanga mpaka mkubwa na vilevile mimi pia ni msanii mkubwa na
siwezi kuomba collabo kama hivyo, nimeshangazwa sana’
Siku chache baada ya dirisha la usajili kufunguliwa kumekuwepo na
tetesi za usajili kumhusu mshambuliaji wa kinigeria Emeh Izuchukwu
kurudi Msimbazi. Lakini Rais wa Simba SC, Evans Elieza Aveva amesema kwamba hawana
nafasi ya kusajili ya mshambuliaji wa kigeni na kwamba Emmanuel Okwi,
Amisi Tambwe na Paul Kiongera wanawatosha.
Kauli hiyo ya Aveva inakuja wakati tayari vyombo vya habari vimekuwa
vikiwahusisha washambuliaji Mnigeria, Emeh Izuchukwu na Mganda Danny
Sserunkuma kusajiliwa na Simba.
Aveva amesema kwamba Izuchukwu ambaye ni mchezaji wao wa zamani, ameomba
mwenyewe kurejea kuchezea klabu hiyo, lakini anasikitika hawana nafasi
ya mchezaji
wa kigeni.
“Hao wachezaji wengine hao, ni magazeti tu yamekuwa yakiandika, lakini ukweli ni kwamba hatujazungumza nao,”amesema Aveva
Huenda
wewe ni mmoja kati ya walaji wa mbogamboga za majani lakini hujui mboga
hizi zinalimwa katika mazingira gani… sasa baraza la mazingira Tanzania
NEMC limebaini kuwa wakulima wa mboga za majani Dar wamekuwa wakitumia
majitaka kumwagilia hizi mboga. Afisa wa NEMC amezungumza na ITV na kusema; “…
Kama Serikali hatuwezi kuruhusu kitu kama hicho.. hatutaruhusu tena
kumwagilia kinyesi kwenye mchicha, haturuhusu hicho kitu, hakuna
serikali hiyo ambayo itaruhusu vitu hivi…” Kama unataka kuisikiliza taarifa hiyo bonyeza play hapa.