Man City ilipata kichapo cha goli moja bila jibu
Mechi zilizochezwa usiku wa kuamkia leo za Klabu
Bingwa barani ulaya ambapo Manchester City walianza vibaya michuano
hiyo baada ya kupata kichapo cha goli moja bila majibu kutoka kwa
wenyeji wao Bayern Munich ya Ujerumani.
Goli la Bayern Munich lilifungwa na Jerome Boateng katika dakika 90
Wakati
Man City wakiadhibiwa ugenini na Bayern Munich, wenzao Chelsea wakiwa
nyumbani Stamfode Bridge walitoka sare ya goli moja kwa moja na Schalke.
AC
Roma ya Italia wao waliadhibu CSKA Moscow ya Urusi kwa jumla ya magoli 5
-1 huku Ajax na Paris St. Gamaine ya Ufaransa zikitoka sare ya moja kwa
moja.
Bacelona wao waliamua kuushikisha adabu Apoel ya Syprus kwa
kuifunga goli moja bila majibu wakati FC Porto ya Ureno wakifungulia
mvua ya magoli iliyoambatana radi pale ilipowanyeshea wapinzani wao Bate
Borisov ya Belarus kwa jumla ya magoli 6 bila majibu.
Matokeo
mengine NK Maribor ya Slovenia ilitoka sare ya 1 - 1 na Sporting Lisbon
ya Ureno huku Athletic Bilbao ya Hispania zikitoka uwanjani bila
kufungana na Shaktar Donetsk ya Ukraine.