Magazine yamuomba msamaha 2 Face Idibia baada ya kesi ya Naila milioni 100.
Icon
Weekly magazine walitoa habari kwamba 2 Face Idibia ametoka nje ya ndoa
yake na kuanzisha uhusiano na mfanyakazi wa benki. Magazine hiyo
haikuishia hapo iliendelea kusema kwamba 2 face amempa ujauzito mwanamke
huyo. Habari hiyo ilimchafua 2 face kwasababu yupo ndani ya ndoa na ndio
ilikuwa habari kubwa ya magazine kwa kuwekwa mbele ya cover. Baada ya
magazine kutoka 2 face alifungua mashtaka dhidi ya magazine hiyo kwa
kudai fidia ya Naila millioni 100. Baada ya magazine kushindwa kuthibitisha habari hiyo wametumia page
moja nzima ya tolea jipya kumuomba msamaha 2 face. Japokuwa Idibia
hajajibu hadharani kuhusu msamaha huo, taarifa zinasema kwamba amekubali
maombi yao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni