Supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na mama’ke mzazi, Sanura
Kassim ‘Sandra’ wamelazimika kukaa kikao kizito ili kupata muafaka wa
mzazi mwenzake na staa huyo, Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kurejea
Bongo na kuishi katika nyumba moja na mkwewe huyo ambaye walipishana
kauli hivi karibuni.
Hivi karibuni, Zari aliyekuwa akiishi na mama Diamond nyumbani kwake,
Tegeta-Madale jijini Dar, walipishana kauli na mzazi huyo sambamba na
ndugu zake hadi kufikia hatua mrembo huyo aliyezaa mtoto mmoja na
Diamond (Tiffah) kurejea nyumbani kwake Afrika Kusini kupisha kile
alichokiita ni ‘uswahili’.
Chanzo makini kimeeleza kuwa, baada ya kuona Diamond anampenda Zari na
mapenzi yao ni motomoto, familia haikuwa na jinsi zaidi ya kukaa kikao
kulijadili kwa kirefu suala hilo na kupata muafaka ambapo habari njema
ni kwamba, mama Tiffah anatarajia kutua Bongo siku chache zijazo.
“Diamond si unajua ndiyo kichwa katika familia. Amewaita ndugu
akawaeleza dhamira na mikakati yake na Zari hivyo wamekubaliana arejee
Bongo,” kilisema chanzo hicho.
Alipoulizwa Diamond kuhusiana na suala hilo, hakutaka kufunguka kwa undani akidai ni mambo ya kifamilia.
“Kila kitu kipo sawa. Zari ataibuka na maisha yataendelea kama kawaida, haya mambo ya kifamilia bwana,” alisema Diamond.
Kabla ya kufikia muafaka huo, Zari aliripotiwa kuwa anakuja nchini
Desemba 8, mwaka huu wakati mama Diamond akionekana kupinga lakini
hatimaye muafaka umepatikana.
GPL
Pages - Menu
▼
Pages - Menu
▼
SAMPLE
▼
Jumamosi, 5 Desemba 2015
Watorosha Makontena Bandarini Bila Kulipia Ushuru Hawa Hapa...Majina Yatajwa
Aidha, TRA imesema imesimamisha kazi watumishi wake 35 wanaofanya kazi katika ngazi mbalimbali, wakiwemo 27 waliokamatwa wiki hii katika Geti Namba Tano.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Dk. Philip Mpango alisema Mamlaka hiyo iliagizwa na Waziri Mkuu Majaliwa kuchukua hatua mara moja kwa kufuatilia na kubaini wamiliki wa Bandari Kavu (ICD) zilizohusika katika kashfa hiyo.
Alisema mbali na hilo walitakiwa kuwatambua wamiliki wa makontena hayo, bidhaa zilizokuwemo, kuwalipisha wahusika kodi iliyokwepwa pamoja na kuwachukulia hatua watumishi waliohusika na upotevu huo.
Dk. Mpango aliyataja makampuni hayo kuwa ni Lotai Steel Tanzania Ltd iliyokuwa na makontena 100, Tuff Tryes Centre Company 58, Binslum Tyres Company Ltd 33, Tifo Global Mart Company Limited 30, Ips Roofing Company Limited 20, Rushywheel Tyre Centre Co Ltd 12 na Kiungani Trading Co Ltd 10.
Makampuni mengine yaliyotajwa ni Homing International Limited (9), Red East Building Materials Company Ltd (7), Tybat Trading Co Limited (5), Zing Ent Ltd (4), Juma Kassem Abdul (3), Salum Link Tyres (3), Ally Masoud Dama (2), Cla Tokyo Limited (2), Farid Abdullah Salem (2), Salum Continental Co (2), Zuleha Abbas Ali (2) na Snow Leopard Building (2).
Wamiliki wengine wa makampuni ambayo yalikuwa na kontena moja moja ni Abdulaziz Mohamed Ally, Ahmed Saleh Tawred, Ali Amer, Ally Awes Alhamdany, Awadhi Salim Saleh, Fahed Abdallah Said, Hani Said, Hassan Husrin Suleyman, Humud Suleiman Humud, Kamil Hussein Ali na Libas Fashion.
Wengine ni Nassir Salehe Mazrui, Ngiloi Ulomi Enterprises Co Ltd, Omar Hussein Badawy, Said Ahmad Hamdan, Said Ahmed Said, Salumu Peculier Tyres, Sapato N. Kyando, Simbo Yonah Kimaro, Strauss International Co. Ltd na Swaleh Mohamed Swaleh.
Alisema kwa ujumla, makampuni hayo yalipitisha makontena 329 ambayo yaliondolewa kinyume cha taratibu kutoka ICD ya Azam inayomilikiwa na Said Salim Bakhresa And Company Limited.
Dk. Mpango alisema bidhaa zilizokuwemo ndani ya makontena hayo ni pamoja na matairi ya magari, samani mbalimbali, betri za magari, vifaa vya ujenzi, nguo na bidhaa zingine mchanganyiko.
27 WALIOKAMATWA
Aidha, Dk. Mpango alisema watumishi 35 wa Mamlaka hiyo wanaofanya kazi katika vitengo mbalimbali wamesimamishwa kazi, wakiwemo 27 waliokamatwa wiki hii katika geti namba tano.
Alisema watumishi hao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano huku akisisitiza kuwa mtumishi yoyote wa TRA atakayebainika kuhusika katika hujuma hiyo atachukuliwa hatua kali za kinidhamu kwa mujibu wa sheria na kanuni za kazi kulingana na makosa atakayokutwa nayo.
Alisema TRA inaendelea kupanga safu ya watumishi wake ili kuthibiti upotevu wa malipo ya kodi na kwamba wanapitia upya taratibu za utoaji leseni kwa Bandari Kavu ili kuondoa mianya na kuweka udhibiti katika uondoshaji wa mizigo katika bandari zote na bohari za forodha.
“Pamoja na hatua hizi, TRA inafuatilia kwa kina ili kubaini mawakala wote wa forodha walioshiriki katika upotevu wa makontena hayo na kuwachukulia hatua ikiwemo kuwafungia leseni pamoja na adhabu zingine kwa mujibu wa sheria,” alisema Dk. Mpango
Mwishoni mwa wiki iliyopita serikali ya awamu tano chini ya Rais John Magufuli ilibaini ukwepaji wa kodi kwa kutorosha makontena 329 ambayo yamenyima serikali kodi ya Sh. bilioni 80.
Rais Magufuli alimsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade huku Jeshi la Polisi likiwashikilia maofisa kadhaa waandamizi wa Mamlaka hiyo akiwemo Kamishina wa Forodha, Tiagi Masamaki.
Masamaki na wengine saba walifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu jana.
NIPASHE
Kigogo wa Bandari Afariki Kwa Presha...Undani wa Kifo chake Waelezwa Hapa
Kimaro alifariki dunia Novemba 30, mwaka huu kwa uthibitisho wa daktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako marehemu alikimbizwa kwa ajili ya matibabu.
Kifo cha Kimaro kimetokea wakati kukiwa na sintofahamu kubwa miongoni mwa wafanyakazi wa mamlaka hiyo kuhusiana na utolewaji wa makontena 349 kinyemela na kuisababishia serikali kukosa mapato ya kiasi cha shilingi bilioni 80.
Taarifa kutoka ndani ya familia, marehemu alisumbuliwa na maradhi hayo kwa muda mrefu. Lakini ghafla alfajiri ya Novemba 30, hali yake ilibadilika na hivyo kukimbizwa Muhimbili ambako daktari alisema alishafariki dunia.
Mwandishi aliweza kufika msibani ambapo aliwashuhudia wafanyakazi wengi wa bandarini na TRA bandarini wakiwa hapo kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.
Baadhi ya wafanyakazi hao, walisikika wakidai, marehemu alikuwa miongoni mwa vigogo waliokuwa wakichunguzwa kwa utolewaji wa makontena 349 siku chache zilizopita.
“Pia nasikia baada ya waziri mkuu (Kassim Majaliwa) kutoa mwongozo siku zile bandarini, watu wa usalama wa taifa walishamfuata hapa kwake mara kadhaa na kumhoji.
"Lakini pia, kuna madai kwamba, miamala yake ya kibenki nayo ilifuatiliwa na jamaa hao ambapo walikuta pesa nyingi,” alisikika akisema mmoja wa wafanyakazi hao ambaye alipogundua kuna waandishi wa habar alifunga kinywa.
Nao baadhi ya waendesha bodaboda wa eneo hilo, walionekana kushangazwa sana kufuatia taarifa za kifo cha kigogo huyo, wakidai siku moja kabla, walionana naye akiwa mzima wa afya.
Hata hivyo, walisema mara baada ya taarifa za kifo, walishangaa kuona magari yake ya kifahari yakiondolewa kutoka nyumbani kwake hapo:
“Labda waliyapeleka mahali ili kupata nafasi ya kuweka maturubai ya msiba. Si unajua majumba haya ya ghorofa, yana nafasi zaidi ya kwenda juu kuliko upana,” alisema mmoja wa bodaboda hao.
Mwendesha bodaboda mmoja alisema: “Mzee wa bandari alikuwa mtu poa sana. Hata madereva wa daladala zake wameumia. Unajua jamaa alikuwa na mkwanja wa maana. Hii nyumba ya hapa ‘cha mtoto’, ana nyumba nyingine Yombo (Dar), magari ndiyo usiseme. Yaani tumempoteza mtu muhimu sana.”
Marehemu Kimaro alizikwa Desemba 2, mwaka huu kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar. Ameacha mke na watoto wanne.
Credit: GPL
Taarifa Sahihi Kuhusu Hotel ya Serena Kufungwa Kwa Amri ya Serikali Kwa Kosa la Kukwepa Kulipa Kodi
![]() |
Serena Hotel |
HOTELI
ya kimataifa ya Serena jana ilikumbwa na msukosuko wa kuandamwa na
waandishi wa habari baada ya kusambaa kwa tetesi kuwa imefungwa kwa amri
ya serikali kwa kosa la kukwepa kulipa kodi.
Tetesi
hizo zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii jana asubuhi,
zikieleza kuwa maofisa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) wameifunga hoteli
kufunga kwa kukwepa kuliko kodi serikalini.
Mbali
ya kusambazwa kwa uvumi huo, zilitumwa pia picha zilizokuwa zikionyesha
sehemu ya hoteli hiyo ikiwa imezungushwa uzio uliokuwa na rangi nyeupe
na nyekundu ambao ni alama inayotumika kuonyesha kusitisha kwa huduma
katika eneo hilo.
Tetesi
hizo zilikwenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa uongozi wa hoteli hiyo
ulikuwa mbioni kubadilisha jina kwa lengo la kukwepa kulipa kodi.
Hata
hivyo, mwandishi wetu baada ya kufika hotelini hapo kwa lengo la
kufuatilia ukweli wa tetesi hizo alikuta shughuli za ukarabati wa sehemu
ya kupokea wageni zikiendelea, huku wageni wakielekezwa kutumia mlango
wa dharura ambako kumetengezwa sehemu ya muda ya kupokelea wageni.
Uongozi
wa Hoteli ya Serena kupitia Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko, Seraphine
Lusala, ulilazimika kutoa taarifa kwa vyombo vya habari ukikanusha
kufungwa kwa hoteli hiyo na kusisitiza kuwa kinachoendelea hotelini hapo
ni matengenezo.
“Si
kweli kama hoteli imefungwa, tunafanya matengenezo na yalikuwa
yafanyike tangu miaka mitatu iliyopita, kilichofanyika sasa ni
kubadilisha eneo la mapokezi yaliyohamishiwa milango mingine na tumeanza
na eneo hilo pamoja na sehemu ya mazoezi,” alisema Lusala.
Alisema matengenezo hayo yanalenga kuifanya hoteli hiyo kuwa ya kiwango cha juu zaidi na yatachukua miezi 10.
Lusala
alisema awamu ya kwanza ya matengenezo itachukua miezi minne na miezi
minne ijayo itahusu matengenezo sehemu ya vinywaji, chakula, eneo la
uwanja na baadaye maeneo mengine ya wazi.
Death Has Forgotten Me, Now I Have Lost All Hope to Die....179-Year-Old Man Cries Out (Pictured)
According to the information transmitted, Mahashta Mûrasi was born in Bangalore on January 6, 1835.
In 1903, he lived in Varanasi, where he worked until 1957, until his retirement at the already venerable age of 122.
According to WorldNewsDailyReport, all official documents to identify this man support his version.
"I have been alive for so long, that my great grand-children have been dead for years," says Mr Mûrasi. "In a way, death has forgotten me. And now I have lost all hope to die!"
Mkuu wa Mkoa Wa Dar es Salaam Awaagiza Wakurugenzi Kuwaondoa Ombaomba Waliko Barabara za Jiji
MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki amewaagiza wakurugenzi wa
halmashauri za jiji la Dar es Salaam, kuwaondoa ombaomba wote walioko
katika barabara za jiji, kwani wanachangia uchafu.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini jana, Sadiki alisema utekelezaji wa kauli
ya Rais John Magufuli ya kutumia siku ya Desemba 9 mwaka huu kufanya
usafi, utakwenda sambamba na kuwaondoa ombaomba hao, ambao wanachangia
kuongeza uchafu.
“Siwezi
kusema wao ni uchafu lakini mazingira yanayowazunguka katika maeneo
wanayofanyia shughuli zao wanayachafua, wanajisaidia kwenye mifuko na
kutupa ovyo,” alisema.
Alisema
viongozi ambao wako katika maeneo ambayo ombaomba hao wanarudi,
wahakikishe hawarudi mjini kwa sababu imekuwa ni tabia ya omba omba hao
wanaporudishwa baada ya muda kurudi tena jijini.
Rais Magufuli Amkalia Kooni Kigogo Aliyetaka Kuchukua Ufukwe wa Coco Beach na Kuwekeza...Amsema Kimafumbo
Akitumia
lugha ya mafumbo na moja kwa moja alisema hata ukiwa na fedha hata
ukiwa na uwezo wa kufoji documents jua serikali ipo tena ya Magufuli.
Siku 30 za Kuwa Madarakani Kama Rais , Magufuli Aokoa Sh1trilioni
Rais
John Magufuli leo ametimiza mwezi mmoja tangu alipoapishwa kushika
wadhifa huo huku akiweka rekodi ya kuokoa kiasi cha Sh997.4 bilioni
(karibu Sh 1trilioni) ambazo zilikuwa zitumike kwa matumuzi yasiyo ya
lazima, na ukwepaji kodi.
Sh997.4
bilioni zilizookolewa zitaweza kutumika kununua magari ya wagonjwa,
kujenga zahanati, kujenga barabara za lami, kununua madawati, kujenga
vyumba vya madarasa, kuchimba visima, kununua mashine za uchunguzi wa
magonjwa, magari ya wanafunzi, pikipiki kwa maofisa kilimo, mikopo ya
elimu ya juu au kujenga viwanja vya michezo kadri Serikali
itakavyoelekeza.
Dk
Magufuli aliapishwa Novemba 5 katika hafla iliyofana na alianza kazi ya
kutafuta na kuziba mianya ya upotevu wa fedha Novemba 6 alipotembelea
Hazina. Katika mazungumzo ya watendaji wa wizara hiyo Rais Magufuli
alipiga marufuku safari zote za nje na kwamba zitakuwa zinaruhusiwa kwa
kibali maalumu.
Novemba
7 alitembelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako aliagiza mashine
za MRI na CT-Scan zitengenezwe na aliagiza Sh3 bilioni zitolewe
kugharimia matengenezo kati ya Sh7 bilioni zilizokuwa zinahitajika.
Novemba
19, Dk Magufuli aliwasilisha bungeni jina la Kassim Majaliwa, mbunge wa
Ruangwa kwamba ndiye alimpendekeza kuwa Waziri Mkuu. Baada ya jina
kupitishwa na Bunge, Novemba 20 Kassim Majaliwa aliapishwa.
Jioni
alilihutubia Bunge akionyesha mwelekeo wa Serikali yake ya awamu ya
tano. Katika hotuba hiyo iliyowasisimua wabunge na hata wananchi
waliosikiliza kupitia televisheni na redio, Dk Magufuli aliahidi
kupambana na mafisadi, kubana matumizi, kuhimiza utendaji kazi, kuinua
uchumi na kulinda amani na utulivu.
Baada
ya hapo Magufuli na Waziri Mkuu, Majaliwa wamekuwa wakitembelea maeneo
muhimu kwa uchumi wa nchi kama Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bandari
na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL)
Utendaji
huo wa Serikali wa Magufuli ndani ya mwezi moja na kipindi kabla
hajaunda baraza la mawaziri, umetazamwa na jamii kuwa ni mbinu ya
kusafisha nchi na kutengeneza mazira safi ili mawaziri watakaoteuliwa
wafuate kasi hiyo.
Fedha zilizookolewa
Kwa
kuzingatia ripoti ya matumizi ya fedha za safari zilizolipwa kama nauli
na posho kwa kipindi cha kati ya mwaka 2013 na 2015 kiasi hicho ni
pamoja na Sh356.3 ambazo zingeweza kutumika kwa safari hizo. Dk Magufuli
aliagiza kwamba baadhi ya shughuli zitafanywa na mabalozi wa Tanzania
walioko nje.
Novemba
19 alipozindua Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano mjini Dodoma, Dk
Magufuli aliagiza Sh225 milioni zilizokuwa zimekusanywa kwa ajili ya
hafla ya wabunge, zipelekwe kununua vitanda katika Hospitali ya Taifa
Muhimbili. Fedha hizo zilinunua vitanda 300, magodoro 300, mablanketi
1675, na viti vya magurudumu 30.
Pia,
katika hotuba yake bungeni, Dk Magufuli alirejea uamuzi wake wa kufuta
safari za nje kwa watendaji wa Serikali na kueleza safari hizo
zimeigharimu Serikali Sh356.3bilioni ambazo zingeweza kujenga barabara
ya lami yenye urefu wa kilomita 400.
Novemba
23, Dk Magufuli alitangaza kufutwa kwa maadhimisho ya Siku ya Uhuru
Desemba 9 na akaagiza Sh4 bilioni ambazo zingetumika zitumike kufanya
upanuzi wa barabara ya Morocco kwenda Mwenge. Kazi hiyo imeanza.
Novemba
25, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alitangaza kufutwa
maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani na akaelekeza kwamba fedha
zilizopangwa kwa ajili ya sherehe hizo zitumike kununua dawa za kufubaza
makali ya ukimwi (ARVs).
Novemba
27, Waziri Mkuu Majaliwa alitembelea bandarini na kubaini makontena 349
ambayo yalitolewa bandarini bila kulipiwa ushuru na kuifanya Serikali
kukosa mapato ya Sh80 bilioni.
Tayari
wenye makontena hayo wameanza kulipia na jana TRA ilitangaza kukusanya
Sh6.3 bilioni kati ya hizo Sh80 bilioni. Katika ziara yake nyingine ya
kushtukiza Desemba 3 Majaliwa alibaini makontena 2,431 yalitolewa bila
kulipiwa kodi. Ikiwa makontena hayo yangelipiwa kodi viwango sawa na
yale 349 Serikali ingepata Sh557.2 bilioni.
Desemba
3, Dk Magufuli alifanya mazungumzo na jumuiya ya wafanyabiashara nchini
na akawataka wote ambao waliondoa mizigo yao bandarini bila kulipa
kodi, wajitahidi kulipa katika kipindi cha siku saba kuanzia juzi
vinginevyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Makontena ni shida
Desemba
1, makontena mengine tisa yalikamatwa na TRA eneo la Mbezi, Tangibovu
yakiwa yametoroshwa bila kulipuiwa ushuru wa Sh58 milioni. Jumla ya
Sh637.2 zimeokolewa kutokana na mkakati wa kukusanya fedha kutoka kwenye
makontena 2,431 pamoja na 349 na hayo tisa.
Matumizi ya Sh 997.4 bilioni
Kwa
muda mrefu, Serikali imekuwa ikikwama kutekeleza miradi mbalimbali ya
maendeleo kutokana na kukosa fedha. Dk Magufuli alikiri juzi kuwa hakuna
fedha za maendeleo zilizokuwa zimetolewa kwa wizara zote katika mwaka
huu wa fedha wa 2015/16, lakini baada ya miezi sita juzi ndiyo
zimetolewa Sh120 bilioni.
Dk
Magufuli hakusema Serikali imepata wapi fedha hizo, lakini huenda ni
sehemu ya fedha ambazo ameokoa katika kipindi cha mwezi mmoja.
Kama
fedha hizo zingeelekewa katika ujenzi wa barabara, na kwa kuzingatia
kilomita moja inajengwa kwa Sh1 bilioni, fedha hizo zitaweza kujenga
karibu au zaidi ya kilomita 1,000, ambao ni umbali kutoka Dar es Salaam
hadi Kigoma au Dar es Salaam mpaka Tunduma.
Aidha,
Sh997.4 bilioni zingeweza kununua magari 3,325 ya kubebea wagonjwa kwa
gharama ya Sh300 milioni kwa kila moja na kuwezesha kila mkoa kupata
magari 133 ya aina hiyo.
Pia,
zahanati moja yenye vifaa vyote muhimu ujenzi wake unagharimu kati ya
Sh600 milioni na Sh700 milioni. Hivyo, fedha hizo zingeweza kujenga
zahanati 1,425 yaani kila mkoa ungepata zahanati 57.
Vilevile,
wakati maelfu ya wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari wanasoma kwa
kukaa chini kutokana na kukosa madawati, Sh997.4 bilioni zitaweza
kutengeneza madawati yenye miguu ya chuma 33,249,142 kwa gharama ya
Sh30,000 kwa kila moja na kuwezesha kila mkoa kupata madawati 1,329,966.
Pengine,
fedha hizo zinaweza kujenga vyumba vya madarasa 132,996 kwa bei ya
Sh7.5 milioni kwa darasa moja, hatua ambayo itawezesha kujengwa kwa
vyumba vya madarasa 5,319 kila mkoa nchini.
Kipimo
maarufu cha CT-Scan ambacho ufanyaji wake wa kazi unasuasa Muhimbili
kwa muda mrefu, kinauzwa kwa wastani wa Sh900 milioni, hivyo, Sh997.4
bilioni zitaweza kununua mashine 1,108 ambazo zingesambazwa na kila mkoa
ukapata mashine 44.
Gharama
za kuchimba kisima kifupi ni kati Sh1 milioni na Sh3 milioni kulingana
na jiografia ya eneo husika, hivyo Sh997.4 bilioni zitaweza kuchimba
visima 332,491; kila mkoa ukapata visima 13,299.
Pia,
kwa kuwa Serikali inahimiza uboreshaji wa sekta ya kilimo, Sh997.4
bilioni zitaweza kununua pikipiki 332,491 na kugawiwa kwa maofisa kilimo
kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa kilimo vijijini na kila mkoa
ungepata pikipiki 13,299.
Kama
fedha hizo zitaelekezwa kwenye mikopo ya elimu ya juu, zitaweza
kugharamia wanafunzi 249,368 wa mwaka wa kwanza kwa asilimia 100 kwa
wastani wa Sh4 milioni kwa kila moja kwa ajili ya chakula, malazi na
ada.
Wabunge: Magufuli Futa Wakuu wa Wilaya na Mikoa
BAADHI
ya wabunge kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka mkoa wa Dodoma
wamemshauri Rais John Magufuli kuondoa nafasi za Ukuu wa Mikoa na Wilaya
na badala yake kazi hizo zifanywe na Makatibu tawala wa mikoa na
Wakurugenzi wa halmashauri husika.
Wakizungumza
kwa masharti ya kutokutaka kutajwa majina wabunge hao walisema hakuna
sababu yoyote ya kuwepo kwa Mkuu wa Mkoa wala Mkuu wa wilaya kwani
hawana kazi na badala yake ni kuiogezea mzigo serikali.
Mmoja
wa wabunge kutoka kati ya majimbo ya Nyanda za juu kusini,alisema ili
kudhiilisha kuwa wakuu wa mikoa na wilaya hawana kazi ni hivi tu ambavyo
wanaonekana kukurupika kwa kuwawajibisha watumishi waliopo chini yao.
“Inasikitisha
kuona wakuu wa Wilaya na Mikoa wanavyokurupuka kwa sasa kuwawajibisha
watendaji ambao wapo chini yao kwa kuwanasa vibao ama kuwasweka rumande.
“Hapo utajiuliza muda wao walikuwa wapi hata hivyo ukiangalia vizuri utagundua wazi kuwa wakuu wa
Mikoa
na Wilaya hawana kazi yoyote ya kufanya na badala yake watendaji wakuu
ni Makatibu tawala wa Mikoa au wakurugenzi wa Halmashauri husika”
amesema Mbunge huyo.
Wabunge
wakipendekeza hayo baadhi ya watumishi katika halmasauri ya Dodoma,nao
kwa masharti ya kutokutaka kutajwa majina wamesema kwamba kutokana na
kasi ya utendaji wa Rais Magufuli sasa wanasiasa wanalazimisha kuingilia
masuala ambayo ni ya kitaalam.
“Tunashangaa zaidi kuona wanasiasa kama vile wakuu wa wilaya na wakuu wa Mikoa wakiwakaripia watumishi ambao ni wanataaluma.
“Na
pale wanasiasa wanaposhauriwa juu ya utendaji wao wanakuwa wakali
wakali zaidi kwa sasa kilichobaki ni watumishi kukaa kimya ili
wawasikilize wanasiasa lakini matokeo yake kazi zitalala” alisema
Mtumishi huyo.
Yapo
mambo mengine kwa sasa ambayo uwezi kuyafanya kutokana na kuhitajika
kwa vitendea kazi,wakati mwingine unatakiwa kutoa tiba wakati huo hakina
vifaa.
Watumishi
hao wanalazimika kutoa yao ya moyoni kutokana na taarifa mbalimbali
zinaziripotiwa kuwa wapo baadhi ya wakuu wa Wilaya na wakuu wa Mikoa
ambao wanawazaba watumishi vibao na kuwashweka ndani watumishi.
Wakati
huohuo baadhi ya wanasheria mkoani Dodoma wamewataka baadhi viongozi wa
serikali kuacha kutumia madaraka yao vibaya kwa kuwadhibu baadhi ya
watumishi wanaochelewa kazini kwani kufanya hivyo ni kosa.
Siku
za hivi karibuni vyombo vya habari kumezagaa taarifa za baadhi ya
viongozi ndani ya serikali wamedaiwa kutumia nyadhifa zao vibaya kwa
kuwapiga au kuwasweka lumande watumishi wa ngazi ya chini pindi
wanapobainika kuchelewa kufika kazini.
Wanasheria
hao kwa kuweka weka sawa suala la wakuu wa mikoa na wilaya au kiongozi
yotote kumpiga mtumishi walisema kwa kufanya hivyo ni kosa la jinai.
Wakizungumza
na MwanaHalisi online mjini hapa juzi, bila kumlenga kiongozi yeyote,
Wanasheria hao walisema ni kosa kwa mtumishi wakiwemo viongozi kupigana
katika sehemu za kazi.
Mmoja
wa mawakili wa Kituo cha Sheria cha Goldmac Attorneys Advocates,
Modester Mganga, alisema watumishi wote wa Idara za serikali wanapaswa
kuzingatia sheria sehemu za kazi pamoja na utawala bora na si
vinginevyo.
Alisema
kuwa endapo kama ni kweli kuna mfanyakazi ambaye amefanyiwa vitendo
hivyo vya kupigwa au kuwekwa rumande anayo haki ya kwenda kushitaki
kwenye vyombo vya sheria kwa vile sheria za kazi ziko wazi kwamba zina
kataza watumishi kupigana sehemu za kazi.