Rais John Magufuli anaongoza kura za kuwania tuzo ya ‘Forbes Africa
Person of The Year’, ambayo hutolewa kwa watu walioonyesha mchango kwa
jamii.
Huku zikiwa zimebaki siku 21 kwa mshindi wa tuzo hiyo kutangazwa, Rais
Magufuli anachuana na Rais wa Mauritius, Ameenah Gulib; Mwendesha
Mashtaka wa Afrika Kusini, Thuli Madonsela; Mwanzilishi wa Capitec Bank,
Michiel Le Roux na Taifa la Rwanda.
Mpaka jana jioni, Dk Magufuli alikuwa anaongoza kwa asilimia 75
likifuata Taifa la Rwanda na nafasi ya tatu alikuwa Madonsela wa Afrika
Kusini.
Rais Magufuli anayetimiza mwaka mmoja madarakani wiki ijayo, utendaji
wake umeonekana kuwagusa wananchi wa kipato cha chini, hasa kwa falsafa
yake ya Hapa Kazi, uwajibishaji na mikakati yake ya kubana matumizi ili
kuokoa fedha kwa kuzuia sherehe zisizo na tija.
Jumatano, 26 Oktoba 2016
Home »
» Rais Magufuli Aongoza Kura Kuwania Tuzo ya ‘Forbes Africa Person of The Year’
0 comments:
Chapisha Maoni