Upelelezi wa kesi inayomkabili Salum Njwete maarufu kama Scorpion
anayetuhumiwa kumsababishia upofu wa kudumu Saidi Mrisho umekamilika na
hatimaye shauri hilo litasomwa Novemba 30 mwaka huu katika mahakama ya
manispaa ya Ilala.
Njwete anatarajiwa kusomewa mashtaka yake baada ya yale ya kwanza
kufutwa ambapo itakuwa ni mara ya kwanza kusikilizwa baada ya
kufunguliwa mashtaka mapya.
Huyu ndiye Scropion, kijana aliyejizolea umaarufu ambapo watu wengi
hupenda kumshuhudia kila aingiapo na kutoka mahakamani huku kila mmoja
akizungumza lake kwa kesi inayomkabili.
Alipoingia mahakamani leo, aliomba ufafanuzi wa wazi juu ya mashtaka
yanayomkabili ambapo upande wa jamhuri kupitia kwa wakili wake Chesensi
Gavyole walisema ushahidi umekamilika.
Kutokana na kuombwa ufafanuzi, Hakimu anayesimamia kesi hiyo Flora Haule
amesema baada ya upelelezi huo kukamilika kesi hiyo itasomwa Novemba 30
mwaka huu, hivyo mshtakiwa atapata ufafanuzi wa mashtaka yake .
Ikumbukwe kwamba Oktoba 19 mwaka huu, Salum Njwete maarufu kama Scropion
alifutiwa kesi na kisha kusomewa upya mashtaka yake kutokana na uamuzi
wa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) aliyeomba kufanya hivyo baada ya hati ya
awali kuwa na mapungufu ya kisheria
Ijumaa, 18 Novemba 2016
Home »
» Taarifa Kuhusu Kinachoendelea Kwenye Kesi ya Scorpion Mtoa Macho Mahakamani
0 comments:
Chapisha Maoni