Jumatatu, 6 Aprili 2015

JESHI LA KENYA LAFANYA SHAMBULIO SOMALIA


 
     Ndege za kijeshi za Kenya zashambulia Somalia 

Jeshi la Kenya limeshambulia maeneo mawili ya jimbo la Gedo nchini Somalia,ambalo ni makao ya wapiganaji wa kundi la Alshabaab,ikiwa ni shambulizi la kwanza la kulipiza kisasi tangu shambulio la chuo kikuu cha Garissa,mashariki mwa Kenya ambapo watu 148 waliuawa.

Chelsea yashinda huku Costa akijeruhiwa

Diego Costa akianguka katikakati ya wachezaji wa stoke city


Mkufunzi wa kilabu ya Chelsea Jose Mourinho amesema kuwa ilikuwa hatari kumchezesha mshambuliaji Diego Costa baada ya kujeruhiwa wakati wa ushindi wa Chelsea wa 2-1 dhidi ya kilabu ya Stoke City siku ya jumamosi.
Costa alichukua mahala pake Oscar wakati wa mapumziko huku mabao yakiwa 1-1, lakini alicheza kwa dakika 10 pekee kabla ya kulazimika kutoka nje baada ya kupata jeraha jengine.
''Kama matokeo yangalikuwa 2-0 asingecheza.Lakini ilibidi tumchezesha .Kitengo changu cha matibabu kiliamua kumchezesha'', alisema Mourinho.
Amsema kuwa mshambuliaji huyo atakuwa nje kwa wiki mbili .
Hii inamaanisha kwamba Costa ataikosa mechi dhidi ya QPR tarehe 12 mwezi Aprili na ile dhidi ya Manchester United katika uwanja wa Stamford Bridge tarehe 18 mwezi Aprili.

SHAMBULIZI GARISSA:SERIKALI YAJITETEA

William Ruto 

Serikali ya Kenya imeitetea idara yake ya usalama kufuatia shutma kwamba ilichelewa kukabiliana na shambulio la chuo kikuu cha Garissa ambapo takriban watu 150 waliuawa.
Shambulio hilo lilisitishwa baada wapiganaji wanne waliohusika kuuawa na maafisa wa polisi saa 15 baada ya kuvamia chuo hicho.

 
Wanajeshi wa kenya 

Lakini naibu wa rais William Ruto anasema kuwa kundi la kwanza la polisi liliwasili katika chuo hicho saa moja baada ya shambulizi.
Amelipongeza jeshi la Kenya KDF kwa kile alichokitaja kua hatua za haraka.Lakini vyombo vya habari vimekuwa vikisema kuwa vikosi maalum vilivyowaua wapiganaji hao vilichelewa kufika katika eneo hilo kutokana na mfumo wa usafiri waliotumia.

 
Wanajeshi wa kenya

 Pia kuna madai kwamba maafisa wa polisi walifeli kuchukua hatua za dharura baada ya kupewa habari kwamba mmoja ya wauaji ambaye sasa ametambuliwa kama Abdirahim Abdullahi ni wakili na mwana wa chifu mmoja katika eneo la kazkazini mashariki.