Jumapili, 1 Novemba 2015

BUTIKU: WAZANZIBAR MSIKUBALI KURUDIA UCHAGUZI

Taasisi ya mwalimu Nyerere imeitaka tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC kufanya kazi kwa kuzingatia katiba ya nchi na sheria na sio kutanguliza mbele maslahi binafsi ya kisiasa hatua ambayo inaweza kusababisha machafuko na umwagaji wa damu.

Akizungumza na vyombo vya habari mjini Musoma, mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo mzee Joseph Butiku, amesema amekerwa na tabia ya ZEC kusitisha uchaguzi na kushindwa kuwatangazia wananchi kiongozi wao waliomchagua, huku ikishindwa kuheshimu matakwa ya wananchi waliopiga kura katika visiwa vya Zanzibar.

Aidha mzee Butiku amewataka wananchi wa Zanzibar kutokubali tena kurudia upigaji wa kura hadi hapo yatakapotolewa maelezo ya kuridhisha na wahusika waliosababisha uchaguzi huo kufutwa pia waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria

Kwa sababu hiyo amewataka viongozi kuheshimu sheria na katiba ya nchi na kwamba chama ambacho kinadhani kimeshindwa katika uchaguzi huo kikubali matokeo badala ya kuifanya zanzibar ni mali ya chama fulani pekeee.

CCM Washikana 'Uchawi' Baada ya Kulipoteza Jimbo La Bunda

BAADHI ya vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Bunda wamemtuhumu mwenyekiti wa chama hicho wilayani hapa, Chacha Gimanwa, kwamba alichangia jimbo la Bunda Mjini kuchukuliwa na mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Vijana hao walitoa tuhuma hizo, juzi wakati wakitembea matembezi ya amani ya kushangilia ushindi wa mgombea urais wa CCM, Dk Jonh Magufuli katika mitaa mbalimbali ya mji wa Bunda.

Katika uchaguzi mkuu uliopita CCM ilipoteza jimbo hilo, baada ya Stephen Wasira aliyekuwa akitetea kiti hicho kushindwa na mgombea wa Chadema, Ester Bulaya.

Hata hivyo Wasira ambaye pia ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika hivi karibuni akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza alidai kuwa katika uchaguzi huo kulikuwa na hujuma.

Wanachama hao wa CCM wakiwa wamebeba mabango baadhi yao walisikika wakimtaja moja kwa moja Gimanwa kwamba ndiye alisababisha CCM kushindwa katika jimbo hilo na kuomba uongozi wa juu wa chama hicho umchukulie hatua.

Hata hivyo, Gimanwa akizungumza na mtandao huu kwa njia ya simu jana alisema kuwa tuhuma hizo hazina msingi wowote na kwamba kamwe hawezi kukihujumu chama chake.

“Hicho ni kikundi cha watu wachache tu wanaotaka kuniharibia jina.Mimi kura yangu ni moja na wapiga kura ni wengi, sasa iweje mimi nisababishe mgombea wa jimbo la Bunda mjini ashindwe?” Alihoji.

 Alisema yeye kama mwenyekiti wa CCM alikuwa akifanya kampeni pia katika jimbo la Bunda vijijini, na siku tatu kabla ya uchaguzi mkuu alirudi tena Bunda mjini na kuendelea na kampeni.

Watu Sita Wapoteza Maisha Katika Ajali ya Gari Morogoro

Watu sita wamefariki dunia baada ya gari ndogo waliokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na basi la abiria mali ya kampuni ya Princess Muro, lililokuwa likitokea Dar es salaam kuelekea Tunduma, katika eneo la hifadhi ya taifa ya Mikumi, barabara kuu ya Morogoro-Iringa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Leonard Paulo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika eneo la hifadhi ya taifa ya Mikumi, ikihusisha gari ndogo la abiria aina ya Toyota Noah lenye namba za usajili T 359 BBA iliyokuwa imebeba abiria sita wakiwemo wanawake wawili na wanaume wanne ambayo ilipasuka tairi ya Mbele ya kuyumba ovyo barabarani na kugongana na basi hilo la Princess Muro lenye namba T 160 BBC na kusababisha vifo kwa abiria wote wa Noah.

Amesema basi hilo la abiria aina ya Zangton lililoharibika zaidi mbele huku Noah ikiharibika kabisa, likuwa likiendeshwa na Silos Wilfred (55) mkazi wa Mbeya ambaye anahojiwa na polisi kuhusiana na tukio hilo, na kwamba basi alilokuwa akiendesha lilikuwa na abiria 59 ambao hawakupata madhara makubwa, isipokuwa michubuko kidogo kwa baadhi yao na walitafutiwa usafiri kuendelea na safari.

Katika upekuzi wa miili ya abiria waliokuwa kwenye Noah inayodaiwa kuhusika na ubebaji wa magazeti, viligundulika vitambulisho vimne vya Ali Nduti Mohamed (27), mkazi wa Mbeya,Sani Elion Mkwabe (24) mkazi wa Kunduchi, Patrick Mkelegene (43) mkazi wa Buguruni Malapa na Selemani Omary (30) ambaye makazi yake hàyajaweza kujulikana Mara moja.

Miili ya watu hao waliopoteza maisha imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

Nimeikumbuka Kauli ya DK SLAA "Chama Changu Chadema Hakiwezi Kushinda Urais Mwaka huu 2015 Kutokana na Kula Matapishi Yetu..."

DK Slaa
"Chadema hakikuwa chama cha kukumbatia ufisadi na mafisadi..hakikuwa chama cha kusomba watu na magari mikutanoni...hakikuwa chama cha kuiba na kununua kura...sasa Chadema hii si ile tulioijenga....
nimeamua kustaafu siasa maana najua chama changu hakiwezi kushinda urais mwaka huu 2015 kutokana na kula matapishi yetu..." Dk Slaa:

Je Slaa ni mkweli??

Mengi Azomewa Diamond Jubilee, Aokolewa na Membe

Mzee yamemkuta leo pale kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee leo.Ameokolewa na Mh Membe ambaye amemtoa kwa gari lake(pichani).Lakini pia Mwandishi Sam Maela wa ITV leo mchana kapata mshike mshike wa kushiba pale Lumumba,ilibidi aokolewa na polisi.Jamani haste haste.Kuna maisha baada ya Uchaguzi.Lile lilikuwa gemu tu.Mwacheni huyo Mzee,
 SOURCE - JAMII FORUMS

Bella Amfumania Kalama na Mchepuko Ambae ni Mdogo wake...Avua Pete ya Uchumba

Isabelah na Wagoni wake
Tukio hilo lilijiri nyumbani kwa Bella, Makumbusho jijini Dar es Salaam baada ya kurejea ghafla kutoka safari ya kimuziki kwenye kampeni za udiwani katika Mikoa ya Iringa na Morogoro.

Siku ya tukio, paparazi wetu alikuwa akipita na hamsini zake katika eneo hilo ndipo alipokutana na songombingo hilo ambapo kelele za Bella zilifika nje huku milio ya vyombo kuvunjwa ikitawala.Paparazi wetu alitia nanga kwenye nyumba hiyo ambapo majirani nao walianza kufika na kumkuta Bella akimshushia kipondo mdogo wake huyo huku akianika uhusiano wao.



Isabelah Akivua pete ya Uchumba



“Huyu ni mdogo wangu kabisa. Tunachangia mama. Nilimleta hapa kwa ajili ya muziki. Sasa mimi nikiwa safarini, kuna mtu alinipigia simu na kuniambia Winnie anaingia na kulala na Kalama chumbani kwangu.

“Sikutaka kumwambia Kalama kuhusu nilichoambiwa, nikaamua kuja ghafla ili nithibitishe. Kumbe kweli. Yaani mdogo wangu kabisa ananifanyia hivi jamani?” alihoji Bella huku akivua pete ya uchumba aliyovalishwa na Kalama na kumtupia.
Mazingira ya eneo la tukio, sakafuni kulikuwa na vipande vya chupa ambavyo vilitokana na Bella kuvunja glasi kwa lengo la kutaka kumpasua kichwani mdogo wake.

Juzi, paparazi wetu alifika tena nyumbani hapo na kuambiwa na msichana mmoja kwamba, Kalama aliondoka baada ya tukio huku Winnie akipokea msamaha wa ‘damu nzito kuliko maji’.Bella alipopigiwa simu na kuulizwa hatima yake na Kalama, alisema: “Mimi na Kalama basi japo ananipigiapigia simu kuniomba msamaha.”
Kalama hakupatikana kuzungumzia hilo.
GPL