Alhamisi, 15 Oktoba 2015

ZARI NA DAIMOND ETI BASI TENA..BIASHARA KWISHNEY

BIASHARA imekwisha! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia ‘kapo’ ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kudaiwa kuwa waliweka misingi ya penzi zito ili Diamond apate mtoto hivyo baada ya mrembo huyo kujifungua Latifah ‘Tiffah’ miezi miwili iliyopita, penzi halitakuwa motomoto kama zamani, Risasi Jumamosi lina ‘full’ stori.

Chanzo cha uhakika kilicho karibu na wawili hao, kimesema makubaliano ya awali baina ya wazazi hao, yalikuwa ni kwa mwanamke huyo raia wa Uganda, kumzalia mtoto Diamond ambaye alikuwa akisaka ubaba kwa udi na uvumba.

TUJIUNGE NA CHANZO
“Wote mnajua jinsi Diamond alivyokuwa akihangaika kupata mtoto, maana wapenzi wake wote wa awali hawakuweza kumzalia. Sasa alipokutana na Zari ambaye tayari alikuwa na watoto, wakakubaliana kwa masharti kuwa ndani ya muda f’lani, amzalie.

“Sasa ndiyo ikawa hivyo, baada ya Tiffah kuzaliwa, kila mtu sasa yupo huru kufanya yake, ndiyo maana Zari amerudi kwake Afrika Kusini ‘Sauz’ na hawezi kuja kuendelea kuishi na Diamond kama wakati ule wa ujauzito.
“Kule Sauz, Zari anaendelea na biashara zake na nimesikia kwa sasa anaandaa Zari All White Party kama ile aliyoifanya Mlimani City hapa Bongo,” kilisema chanzo chetu.

Msanii chipukizi wa lebo ya Wasafi Classic Baby ‘WBC’ aitwaye Harmonizer akilishwa keki na Rose.

KWA NINI HAWEZI KURUDI?
Chanzo hicho kiliendelea kutoboa siri kwamba, pamoja na makubaliano ya kuzaa, lakini pia mazingira ya sasa ya makazi ya Diamond hayatoi nafasi kwa mwanamke huyo mwenye fedha ambaye pia ni msanii, kuweza kuishi.
“Sasa hivi pale nyumbani kwa Diamond kumejaa, imekuwa familia kubwa. Maana kuna mjomba wake Diamond anaishi pale, dada zake wawili, Esma na Queen Darleen wanaishi pale. Mama yake Diamond (Sanura Kasim) yupo pale.
“Haya, achana na ndugu wengine. Lakini pia kuna wasichana wa kazi wawili na mlinzi mmoja. Sasa kwa mtu kama Zari ambaye maisha yake ni ya kisupastaa hawezi kuishi kwenye nyumba yenye watu wengi hivyo.”

ZARI ANAOGOPA UMBEYA
“Pia inasemekana Zari hataki kuishi na wifi zake kwa sababu anaogopa umbeya. Hata wakati ule alipokuwa mjamzito mpaka kujifungua, hakuwa mtu wa kujichanganya nao sana. Alikuwa mtu wa peke yake peke yake tu.”

HAKUNA TENA MAPENZI?
“Taarifa nilizonazo ni kuwa, Diamond na Zari watakuwa wanaendelea na uhusiano wao wa kimapenzi lakini si ule wa kama awali. Ila wataendelea kuwa watu waliozaa mtoto na maisha ya Tiffah yataendelea kuwa kwa mama yake hadi hapo watakapoamua vinginevyo. Zari anaweza kuja Bongo na Diamond anaweza kwenda Sauz kwa Zari.”
“Zari hataki kuishi Tanzania, anataka Tiffah aishi na ndugu zake kule Sauz hadi akue na kuanza masomo. Kwa hiyo usitegemee ule ukaribu kama wa mwanzo.”

KUHUSU DIAMOND!
Jitihada za kumpata Diamond ili aweze kuzungumzia suala hilo ziligonga mwamba ikielezwa kuwa yupo nchini Marekani katika shughuli za kimuziki. Hata alipotumiwa meseji kwa njia ya Mtandao wa WhatsApp hakujibu.
Hata hivyo, mtu wake wa karibu ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini, alitatizwa na suala hili akisema:

“Dah! Wabongo bwana! Ninachojua mimi ni kuwa, bado watakuwa wapenzi japokuwa siwasemei maana Diamond naye haaminiki sana. Si unajua ameshapata mtoto, lolote linaweza kutokea.
“Ila Diamond akimhitaji Zari aje Tanzania anaweza kuja, akitaka aende Sauz atakwenda kwa sababu Tiffah lazima alelewe na wazazi wote.
“Halafu lazima ujue kwamba, Zari ni mfanyabiashara, ana biashara zake Afrika Kusini na Uganda. Kwa hiyo siyo mtu ambaye unaweza kumtegemea akae sehemu moja tu.”

RAISI KIKWETE AWAONYA WANAOPANGA KULINDA KURA VITUONI

Rais Jakaya Kikwete amesema watu wanaopanga kubaki katika vituo vya kupigia kura baada ya kumaliza zoezi hilo kwa lengo la kulinda kura kunaashiria uvunjaji amani, hivyo serikali imejipanga kupambana na hali hiyo siku ya uchaguzi.

Rais amesisitiza kwamba wanaopaswa kulinda kura ni mawakala pekee na si wafuasi wa mgombea ama vyama.

Akizungumza jana katika sherehe za Kilele cha Mwenge wa Uhuru zilizofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, kiongozi huyo anayemalizia muda wake madarakani alisema viongozi wanaowaagiza wafuasi wao kulinda kura wana nia mbaya dhidi ya amani ya nchi.

“Mnatakiwa muondoke kwenye vituo baada ya kupiga kura….kura utazilindaje? Mawakala ndio pekee wanaoweza kulinda. Mkikaidi hilo, hatutawavulimia. Serikali imejipanga kupambana na wale wote watakaokaidi agizo la Tume ya Uchaguzi (NEC),” alisisitiza Rais Jakaya Kikwete.

Katika shehere hizo za mwenge zilizoendana sambamba na maadhimisho ya siku ya kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Rais Kikwete aliwataka Watanzania kuchagua watu waadilifu ambao wana dhamira ya kupambana na rushwa kwa vitendo.

“Tumchague mtu ambaye hana ukabila, udini na ubaguzi wa rangi…tumchague kiongozi atakayetetea maslahi ya makabila yote 126,” alisema rais huku akimnukuu Mwalimu Nyerere aliyefariki miaka 16 iliyopita.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa pia na Spika wa Bunge anayemaliza muda wake, Anne Makinda, wakuu wa mikoa na viongozi wengine wa ngazi tofauti serikalini na kupambwa na nyimbo za makabila na wanafunzi wa shule mbalimbali mjini Dodoma.

MGOMBEA WA URAISI CCM DR. JOHN POMBE MAGUFULI AMFAGILIA DAIMOND PLATNUMZ

MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli amemmwagia sifa lukuki, mkali wao ndani ya muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kutokana na ushindi wa tuzo tatu za Afrimma zilizofanyika wikiendi iliyopita nchini Marekani
Tukio hili lilitokea katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mpilipili mkoani Lindi baada ya staa wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba kushuka jukwaani kukamua kwenye kampeni za mgombea huyo wa urais, ndipo Magufuli alishika kipaza sauti na kumsifia Diamond aliyeshinda tuzo za Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki, Msanii Bora wa Mwaka na Utumbuizaji Bora wa Video.

“Ukweli nampongeza sana msanii Diamond kwa jinsi anavyojituma na kuipeperusha vyema bendera ya taifa letu…,” alisema Magufuli huku pia akiwapongeza Ommy Dimpoz na Vanesa Mdee walioshinda tuzo tofauti katika kinyang’anyiro hicho.

Aidha, katika kampeni hizo Magufuli aliwaahidi wakazi wa mji huo kuwajengea Lindi mpya ambayo itakuwa ya neema kupitia gesi inayopatikana kwenye ukanda huo, unafuu wa vifaa vya ujenzi ikiwemo saruji ‘cement’ iliyoanza kupatikana kwa bei ya shilingi 8,000 kwenye kiwanda cha Dangote kilichopo Mtwara, zao la korosho ambalo Magufuli alijinandi kuwa na digrii ya zao hilo.

Rihanna:NINA HAMU YA KUFANYA MAPENZI LAKINI.......(PICHA)

Rihanna anasema yeye ni kama wanawake wengine kiasi cha kuwa na hamu ya kufanya mapenzi na kwamba hajavunja amri ya sita kwa muda mrefu sasa.

rihanna-cover

Akiongea kwenye jarida la Vanity Fair, Rihanna alisema hawezi tu kufanya mapenzi na mtu ambaye hajamuingia moyo.

Haya ndio aliyoyasema:

If I wanted to I would completely do that. I am going to do what makes me feel happy, what I feel like doing. But that would be empty for me; that to me is a hollow move. I would wake up the next day feeling like s–t,” she shared. “That’s why I haven’t been having sex or even really seeing anybody. Because I don’t want to wake up the next day feeling guilty. I mean I get horny, I’m human, I’m a woman, I want to have sex. But what am I going to do—just find the first random cute dude that I think is going to be a great ride for the night and then tomorrow I wake up feeling empty and hollow? He has a great story and I’m like … what am I doing? I can’t do it to myself. I cannot. It has a little bit to do with fame and a lot to do with the woman that I am. And that saves me.

Kwenye mahojiano hayo pia, Rihanna alizungumza uhusiano wake na Chris Brown. “Nilikuwa msichana yule,” alisema Rihanna kueleza kwanini alimrudia Chris Brown licha ya kumjeruhi vibaya mwaka 2009.

Msichana yule aliyehisi maumivu makali kama uhusiano huu ulivyokuwa, pengine watu wengine wameumbwa kuwa na nguvu kuliko wengine. Pengine mimi ni miongoni mwa wale watu ambao wameumbwa kumudu mambo kama haya. Pengine mimi ni mtu ambaye ni kama malaika wa ulinzi kwa mtu huyu, kuwepo pale wanapokuwa hawajiwezi, pale wanaposhindwa kuielewa dunia, pindi wanapohitaji tu mtu wa kuwapa moyo katika njia chanya na kusema mambo sahihi.”

Rihanna anadai alidhani angembadilisha Breezy.

“Kwa asilimia mia. Nilikuwa nikimtetea sana,” alieleza Rihanna.

Nilihisi kwamba watu walikuwa hamwelewi. Lakini unajua, unagundua baada ya muda kuwa katika mazingira hayo wewe ndiye adui. Unataka mambo mema kwao, lakini unapowakumbusha kuhusu waliyokosea, ama kama ukiwakumbusha vipindi vibaya katika maisha yao, ama tu ukisema nipo tayari kuvumilia jambo fulani, hawakufirii – kwasababu wanajua haustahili kile wanachoenda kukupa.

Pamoja na hayo, Rihanna amesema hamchukii CB.

“Nitamjali mpaka siku nakufa. Sisi sio marafiki lakini si kwamba ni maadui. Hatuna uhusiano mkubwa sasa.”

MADUKA YA UCHUMI SUPERMARKET YAFUNGWA TANZANIA NA UGANDA

Uongozi wa Uchumi Supermarket umetangaza kufunga shughuli zake katika maduka yake yaliyopo Tanzania na Uganda ili kutoa nafasi ya kuzuia mtikisiko wa kifedha unaoikumba kampuni hiyo.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Uchumi, Dk Julius Kipng'etich, amesema Bodi imeamua kufunga vitengo vya kikanda ili kuimarisha shughuli zake nchini Kenya baada ya kupata hasara katika maduka yake ya Uganda na Tanzania.

"Maduka yetu ya Uganda na Tanzania huchangia asilimia 25 tu ya gharama za uendeshaji. Matawi hayo mawili hayajapata faida yoyote kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita jambo linaloyumbisha shughuli zetu," amesema Dk Julius

"Tuna uhakika kwamba tunaweza kuigeuza Uchumi kwa kulenga asilimia 95 ya biashara ambazo zinaleta fedha kwa wanahisa ambao wana matumaini kwamba tutafanikisha hili ndani ya muda mfupi," ameongeza Dk Kipng'etich.

Kwa upande wa Tanzania, juzi wafanyakazi zaidi ya 400 waligoma kwa kujifungia ndani ya ofisi zao kwa zaidi ya saa 20 wakitaka kujua hatma yao kwenye makao makuu ya duka hilo yaliyopo katika jengo la Quality Center jijini Dar es salaam.

KILA KITU AANIKA:HATIMAYE AGNESS MASOGANGE AFUNGUKIA PENZI LA DAVIDO

VIDEO Queen mwenye umbo tata Bongo, Agness Jerald ‘Masogange’ alifungukia penzi lake na staa wa muziki kutoka Nigeria, Davido.

Akizungumza na Amani Masogange alisema kuwa kuna uvumi unaovumishwa na baadhi ya watu kwamba amekuwa akitoka kimalovee na Davido jambo ambalo halina ukweli wowote.


“Kwanza kabisa Davido ni shemeji yangu lakini pia kuna ‘project’ kubwa ambayo tunaiandaa. Mtakuja kuelewa tu hapo mbeleni na si jambo la kusema ni wapenzi bila kuthibitisha,” alisema Masogange.