Kupitia You heard ya August 04,Weusi wamesemekana kucopy wimbo na
kuurudia kuanzia namna wanavyorap mpaka beat iliyotumika kwenye wimbo
huo,Joh Makini kaongea na kapatikana pia producer wa wimbo huo NahReel
nae kazungumza.
88.0 Clouds Fm inasikika ukiwa Tabora.
Bonyeza play kusikiliza.
Icon
Weekly magazine walitoa habari kwamba 2 Face Idibia ametoka nje ya ndoa
yake na kuanzisha uhusiano na mfanyakazi wa benki. Magazine hiyo
haikuishia hapo iliendelea kusema kwamba 2 face amempa ujauzito mwanamke
huyo.
Habari hiyo ilimchafua 2 face kwasababu yupo ndani ya ndoa na ndio
ilikuwa habari kubwa ya magazine kwa kuwekwa mbele ya cover. Baada ya
magazine kutoka 2 face alifungua mashtaka dhidi ya magazine hiyo kwa
kudai fidia ya Naila millioni 100.
Baada ya magazine kushindwa kuthibitisha habari hiyo wametumia page
moja nzima ya tolea jipya kumuomba msamaha 2 face. Japokuwa Idibia
hajajibu hadharani kuhusu msamaha huo, taarifa zinasema kwamba amekubali
maombi yao.
Baada ya jana usiku katibu mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA)
Nicholas Musonye kutoa onyo kwa Yanga kuwasilisha majina mapya ya
wachezaji wa kikosi cha kwanza kwa ajili ya Kagame Cup, leo hii CECAFA
wametoa uamuzi mpya dhidi ya Yanga.
Yanga SC sasa rasmi imeondolewa kwenye michuano ya Kagame
kutokana na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati kupinga
kupeleka timu ya vijana.
Yanga ilitaka kupeleka timu yenye vijana wengi iliyochanganyika na wakongwe wachache.
Lakini Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye akasema hizo ni
dharau. Wanasema ni timu ina wachezaji wa timu ya kwanza, vipi Maximo
abaki Dar es Salaam.
“Halafu timu isafiri kwenda kwenye mashindano makubwa kama ya Kagame. Huu ni utani, ndiyo maana sasa tumeipa nafasi Azam,”alisema jana.
Mabingwa wa Tanzania Bara, Azam FC, watapambana Kundi A lenye
timu za Rayon Sport ya Rwanda, Coffee ya Ethiopia, Atlabara ya Sudan
Kusini na KMKM ya Zanzibar.
Kundi B lina timu za APR ya Rwanda, KCC ya Uganda, Flambeau de
L’Est ya Burundi, Gor Mahia ya Kenya na Telecom ya Djibouti wakati Kundi
C linaongozwa na mabingwa watetezi, Vital’O ya Burundi, El Merreikh ya
Sudan, Polisi ya Rwanda na Benadir ya Somalia.
Rais Paul Kagame wa Rwanda ndiye mlezi wa mashindano haya ambaye hutoa dola za Kimarekani 60,000 kila mwaka kwa ajili ya zawadi.
Kwa kuwa Azam imechukua nafasi ya Yanga, sasa itacheza mechi ya
ufunguzi dhidi ya wenyeji Rayon Sport Uwanja wa Amahoro Agosti 8, mwaka
huu.
Mechi ya saa 8 mchana itakuwa ni kati ya KMKM ya Zanzibar dhidi ya Atlabara ya Sudan Kusini.
Mechi ya pili ya Azam FC itakuwa Agosti 10 dhidi ya KMKM, kabla
ya kuivaa Atlabara Agosti 12, halafu itamaliza makundi dhidi ya Coffee
ya Ethiopia Agosti 16.