
Waziri wa muda mrefu na mbunge wa zamani wa Bunda, Steven Wasira amewajibu wanaodai kwamba amelazimika kustaafu siasa baada ya mpinzani wake, Ester Bulaya kuwashinda wapigakura wanne waliokuwa wakipinga ushindi wake wa ubunge wa Bunda Mjini na kusema hajastaafu na uzee haumzuii mtu kudai haki yake. Juzi, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ilimpa ushindi Bulaya katika...