Alhamisi, 27 Novemba 2014

Mnigeria mwingine kwenye hatia ya kusafirisha dawa za kulevya

Man-looks-out-of-prison-w-010 
Idadi ya raia wa Nigeria wanaokamatwa na dawa za kulevya inazidi kupanda siku hadi siku, ambapo taarifa iliyopo ni kwamba mtu mmoja mwenye umri wa miaka 35 amehukumiwa kunyongwa baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya.
Jamaa huyo Abuchi Ngwoke alikamatwa mwaka 2012 uwanja wa ndege wa Malaysia baada ya kukamatwa na dawa hizo zenye uzito wa gramu 251.66 aina ya Methamphetamine  ambazo alikuwa akisafirisha kutoka Nigeria kwenda Malaysia.
Ni mara nyingi tumekuwa tukisikia kuhusu watu wanaokamatwa kwa kusafirisha dawa hizo huku wengi wao wakitajwa kuwa ni Wanigeria.
Abuchi-Ngwoke

Baada ya ishu ya Escrow, haya ni majibu mawili ya Waziri Mkuu Pinda ikiwemo kujiuzulu

question_mark_20166
Kikao cha Bunge leo Novemba 27 kimeanza kwa maswali mawili kuulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

…Chini ya uongozi wako kama Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ukiwa kiongozi wa shughuli za Kiserikali Bungen, tumeiona Serikali ikikumbana na matatizo na vikwazo vingi ikiwemo ‘Operesheni Tokomeza’ ambayo ilipelekea wananchi wengi kupoteza maisha na wengine kupata vilema…“– Mbowe.
Tumeona mauaji ya raia yakiendelea Kiteto, kashfa kubwa ambayo iko current sasa hivi ikiwa ni pamoja na kauli zako ulizowahi kuzisema kwamba fedha zilizopotea za akaunti ya Escrow hazikuwa fedha za umma bali zilikuwa fedha za watu binafsi…“– Mbowe.
Baada ya Ripoti ya CAG kutolewa hadharani kuhusiana na fedha za Escrow na baada ya Ripoti ya PCCB kutolewa na hatimaye jana hapa Bungeni kusomwa taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, nini msimamo wako kuhusu kauli yako ya awali kwamba fedha zile zilikuwa ni za watu binafsi na sio fedha za umma?Mbowe.
Kwa uzito huo ukichanganya na matukio mengine mbalimbali ambayo yamepelekea fedheha kubwa kwa taifa letu, huoni kama ingekuwa muafaka kwako binafsi na taifa kupumzika kidogo ili kupisha nafasi kwa watu wengine kuweza kumalizia ngwe hii ya utawala wenu?”– Mbowe.
Akijibu maswali hayo, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema; “…Inawezekana Mheshimiwa Mbowe una shauku ya kutaka litokee hilo lakini mambo haya yanategemea kama ndivyo Mungu kapanga au hapana…
Ningeweza nikajaribu kukujibu lakini sina sababu ya kufanya hivyo, sina sababu ya kufanya hivyo kwa sababu suala lenyewe ndiyo subject ya mjadala hapa Bungeni ambao unaanza leo.. Tusubiri mjadala utakavyokwenda naamini na mimi nitapata nafasi ya kusema mawili matatu, kwa hiyo nadhani mwisho wa yote Bunge litakuwa limefikia mahali ambapo tunaweza tukasema kwa uhakika ni hatua stahiki namna gani inaweza kuchukuliwa…” Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Baada ya majibu hayo, Mbowe alipata nafasi ya kuuliza swali la nyongeza kwa Waziri Mkuu; “…Pamoja na kwamba jambo hili litajitokeza baadaye katika mijadala ya leo, bado haiondoi ukweli kwamba una wajibu wa kulijibu swali langu. Naomba kwa heshima sana nikuulize tena kwa mara nyingine, taifa limepata fedheha kubwa sana kutokana na sakata hili, nchi nzima inasikiliza tatizo hili…“– Mbowe.
…Una heshima kama kiongozi wa Serikali lakini heshima ambayo itakuwa imethibitishwa zaidi kama utaamua kujiwajibisha mwenyewe ili kuweka heshima yako na heshima ya Serikali, je kwa mara nyingine huoni ingekuwa vema kama basi utujibu kama unafikiri bado zile fedha ni za umma kama hutaki ku-declare kujiuzulu katika hatua ya sasa?”– Mbowe.
Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu amesema; “…Naomba nirudie nilichosema, suala la kujiuzulu si jipya lakini maadam jambo hili liko hapa Bungeni, unatanguliza hili jambo kwanini? Tungoje tujadili tufikie mwisho halafu tutaamua…”– Mizengo Pinda.
Nimekurekodia sauti ya wakati maswali hayo yakiulizwa na kujibiwa Bungeni leo Dodoma, unaweza kusikiliza kwa kubonyeza play.

Picha ya kwanza ya mbrazil mpya wa Yanga mazoezini, je atafuzu majaribio

kelvingoalWiki iliyopita nilikuletea taarifa juu ya ujio wa mchezaji mpya wa kimataifa wa klabu ya Yanga Emerson de Oliveira Neves Roque  – mbrazil ambaye ameletwa nchini kuja kufanya majaribio na endapo ikifuzu basi ndio itachukua nafasi ya mbrazil aliyeondoka Jaja.
Jana jioni mchezaji huyo huyo aliwasili na leo hii mchezaji huyo ameanza mazoezi mepesi asubuhi katika Uwanja wa shule ya Sekondari Loyola kufuatia kusaifri kwa zaidi ya masaa 11 kutoka jijini Rio de Janeiro.
emrsn
Kiungo mbarazil Emerson de Oliveira a(wa pili kutoka kulia) akiwa mazoezini leo asubuhi katika uwnaja wa shule ya sekondari Loyola, wengine ni Kizza, Javu na Coutinho
Emerson ameungana na wachezaji wengine wa Young Africans katika mazoezi ya leo asubuhi ikiwa ni siku yake ya kwanza katika ardhi ya Tanzania na kufanya mazoezi mepesi mepesi chini ya kocha msaidizi Leonardo Neiva kuijiweka fit na kutoa uchovu safari.
Kiungo huyo mwenye umbo lililonyumbulika ambae alikuwa akichezea timu ya Bonsucesso FC iliyopo lii daraja la pili nchini Brazi katika jiji la Rio de Janeiro pia msimu uliopita alikua akicheza soka la kulipwa katika nchi ya Poland latika klabu ya Piotrkow Trybunalski FC.
Kocha mkuu wa Young Africans Marcio Maximo amesema mchezaji huyo leo alikua na programu ya mazoezi mepesi tu kutokana na uchovu wa safari na kesho anatarajiwa kuendelea na mazoezi na wenzake kulingana na ratiba iliyopo.
Endapo Emerson atafanikiwa kulishawishi benchi la Ufundi kumsajili  basi moja kwa moja ataingia makubaliano na klabu ya Young Africans kwa ajili ya kuitumikia kwenye michuano ya kimataifa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanznaia bara.

Picha: Diamond Platnumz na Fally Ipupa kwa mara nyingine tena kwenye Mjengo wa BBA

.
Hii ni mara ya pili kwa msanii Diamond Platnumz kualikwa ndani ya jumba la BBA akiwa na mwanamuziki kutoka Congo, Fally Ipupa ambapo wameshiriki chakula cha mchana pamoja na washiriki waliobaki kwenye Jumba hilo, safari hii wasanii hao wameingia kwa ajili ya kuhamasisha ONE Campain ambayo inahusu kilimo, moja ya Project zilizowahi kufanywa na Kampeni hiyo ni ile nyimbo ya Cocoa na Chocolate ambayo wameshiriki pia mastaa wengine kibao kutoka Afrika.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

NI MWINGINE TOKA KIGOMA,DIAMOND NA KIBA MJIPANGE KIJANA AMEKUJA NA SPIDI KALI

Ni msanii mwingine hatari ambae anachipukia kwenye game Mkasulu Junior huku akisindikizwa ngoma yake kali inayokwenda kwa jina la tulichart ambayo amefanya kwa producer makini MARO.Hofu yangu mi kuwapoteza hawa wakongwe ambao ametoka nao mkoa mmoja,mkoa ambao unatamba katika game ya muziki Tanzania si mwingine nazungumzia Kigoma.Tumpokee kwa mikono miwili wapenzi wa bongo fleva ili alete ushindani ndani ya sanaa ya muziki Tanzania.
Download ngoma yake hapo chini au kwenye link Mkasulu - tulichart ili upate kuisikiliza.
http://www.hulkshare.com/youngluvega/unknown-artist-unknown-album-01-01-track-01-01