Leo ni siku ambayo mwili wa Marehemu Kapteni John Damian Komba umepumzishwa katika makaburi ya Kijijini kwao Lituhi, Mbinga mkoa wa Ruvuma.
Leo kwenye kipindi cha Power Breakfast Clouds FM, alisikika Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe akizungumzia mchango wa Marehemu Komba kwenye suala la mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya Tanzania na Malawi.
“Kwenye mgogoro wetu wa Malawi tulimchukua Kapteni Komba kwenda kutoa ushuhuda unaoonyesha kwamba Ziwa Nyasa kwa kweli mpaka ni katikati, ndio alikwenda kutoa ushuhuda.. Kapteni Komba alieleza
 kwamba toka enzi za mababu zake na mabibi zake makaburi ya wazee wake 
yako ndani ya maji, ukifika pale Lituhi na huwa wanachukua mitumbwi 
wanakwenda kunyunyizia na kutoa baraka zao makaburi yale yako ndani ya 
maji na bado yapo misalaba iko kule kwa hiyo akawa anauliza na yale 
makaburi sasa yawe mali ya Malawi?“
Maji 
ya Ziwa Nyasa yanakuja kwenye ardhi miaka yote na huchukua Shule, 
huchukua Mahakama na makaburi ya wazee mbalimbali, huu ni ushuhuda 
alioutoa Kapteni Komba tulipokwenda Malawi na ushuhuda uliochukuliwa na wasuluhishi kuonyesha kwamba Ziwa lile linakula ardhi ya Tanzania.
Komba
 lilimleta hilo na alizungumza vizuri sana kwa hiyo katika diplomasia ya
 mgogoro wa Ziwa Nyasa kati yetu na Malawi huyu alikuwa miongoni mwa 
watu waliozungumza kwa niaba ya watu wanaokaa kwenye mwambao wa Ziwa 
Nyasa kwamba mpaka kwa kweli upo pale katikati“
Aliwahi
 kualikwa kwenda kusaidia kampeni kwa nyimbo zake, kwa hamasa zake na 
wengine waliogopa wakimuona ameingia kwenye nchi, wanatuletea barua 
kutuambia bwana muondoeni haraka sana.. akikupigia kampeni kushindwa 
haiwezekani.. tumepoteza mtu, tumepoteza shujaa, tumepoteza mkereketwa, 
tumepoteza kiongozi aliyekuwa mstari wa mbele kukiletea chama cha 
mapinduzi ushindi miaka nenda rudi“– Waziri Bernard Membe.






 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
