Jumanne, 25 Oktoba 2016

Mastaa wa Kike Kutoka Familia za Mboga Saba Bongo

NAIJUA familia ya mboga saba? Wengine wanapenda kuwaita watoto wa kishua ama familia bora. Hii ikiwawakilisha watoto wanaozaliwa kwenye familia yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi, kiasi cha kutumia mlo mmoja ukiwa na mboga tofauti na zinazobadilishwa kila uchao. Ndio, kuna familia nyingine bhana mlo unakuwa na mboga moja na huwa ni hiyo hiyo deile mpaka inachosha.

wee
Ingawa kuna dhana kuwa watoto wa kishua huwa wavivu kujitafutia kwa sababu kila anachokotaka hukipata tu nyumbani, lakini ukweli sio wote. Kuna wengine wanaamua kuchakarika kutafuta maisha yao wenyewe, hata hawalingani na wale waliotokea familia za watu duni ambao walikatisha masomo ili kusaka noti wakiwa kwenye umri mdogo kabisa.

Mwanaspoti inakuletea baadhi ya mastaa wa kike waliozaliwa kwenye familia ya mboga saba, lakini wanakomaa kivyao vyao ile mbaya wakijichanganya na wenzao kusaka noto kwa jasho na damu.

VANESSA MDEE

Vanessa Mdee maarufu kama Vee Money alizaliwa mjini Arusha mwaka 1988. Vanessa anatokea familia bora ya Sammy Mdee ambaye kwa sasa ni marehemu. Enzi za uhai wake, baba ya Mzee alikuwa mtu mzito kwenye nchi hii akiwa mume wa Sophia.

Akiwa na umri mdogo Vanessa aliweza kusafiri nchi mbalimbali duniani. Vanessa Mdee alikulia miji ya New York , Paris, Nairobi na Arusha, lakini kwa sasa jamaa anatisha mbaya kwenye fani ya muziki akitamba ndani na nje ya Afrika.

JOKATE MWENGELO

Huyu unaweza kumuita mtoto wa Oysterbay kwani ndio alipokulia huku baba yake akifanya kazi serikalini.

Kumbuka Jokate alizaliwa Washington DC, Marekani ambapo wazazi wake walikua wakifanya kazi huko. Alipomaliza masomo ya juu ya Sekondari pale Loyola ndipo alipoanza kujichanganya kwa kuwania taji la Miss Tanzania mwaka 2006 na kushika nafasi ya 2 nyuma ya Wema Sepetu, kisha kuhamia kwenye fani ya muziki, utangazaji, mitindo na ubunifu na sasa akipiga fedha.

WEMA SEPETU

Wema Sepetu ni msichana anayetoka kwenye familia ya kibalozi akiwa ni mtoto wa mwisho katika familia ya wasichana wanne wa marehemu Balozi Isaac Sepetu.

Wema alizaliwa mwaka 1988 katika hospitali ya St. Andrew ya Dar es Salaam na amesoma elimu yake ya awali mpaka sekondari kwenye Shule ya Academic International iliyopo Dar es Salaam kabla ya kwenda Malaysia kusomea mambo ya biashara za kimataifa katka Chuo Kikuu cha Limkokwing.

Alianzia shindano la urembo akitwaa mataji kadhaa ikiwamo la Miss Tanzania 2006 kisha kuhamia kwenye filamu na sasa anaendelea kukimbiza akimiliki kampuni yake na akizalisha bidhaa zenye jina lake. Achana kabisa, ila ukiamua kubisha we bisha tu.

Kutana na Mwanamke Mnene Kuliko Wote Duniani… Ana Uzito wa Kilo 500

Kwa mujibu wa jarida la Daily Mail, inaelezwa kuwa mwanamke huyo aitwaye Iman Ahmad Abdulati mwenye miaka 36 hajawahi kutoka ndani kwa miaka 25 na amekua akiongezeka uzito wake kwa haraka mpaka kufikia kilo 500 zinazompa shida ya kujifanyia usafi na hata kula. Ripoti ya madaktari inaonesha kuwa mwanamke huyu anasumbuliwa na maambukizi ya bakteria wanaoshambulia ukuaji wa mwili.

Akiwa na miaka 11 alianza kusumbuliwa na tatizo hilo ingawa wazazi wake wanakiri kuwa hawakudhani kuwa ni tatizo lakini siku zilivyozidi kwenda ndipo wakabaini kuwa halikua jambo la kawaida hivyo wakaamua kutafuta wataalamu ambao walitoa ripoti kuwa ana matatizo ya mwili wake kukaa na maji mengi bila kuyatoa nje kitu ambacho sio cha kawaida kwa binadamu.

Baada ya Ali Kiba Kusemwa Kuwa Anaishi Kwa Mama yake Kariakoo...Aamua Kuonyesha Nyumba yake

Baada ya kusemwa sana kuwa hana nyumba na anaishi kwa mama yake kko, hatimaye Ali Kiba. king kiba, King wa bongo flavour kaamua leo kuachia picha za mjengo wke uliopo Tabata thamani ya jiko la ndani ni milioni 19 soon nitawapa updates gharama za nyumba hii ambayo ni ghorofa na naamini ni kwake maana namuonaga hapo 
Pongezi kwa king kiba yooooh 

Nimekuta Chupi ya Mke Wangu Chumbani Kwa Mdogo Wangu wa Kiume

Jamani Leo ni Siku ya saba tangia nikute chupi ya mke wangu chumbani kwa mdogo wangu wa kiume,nimekaa nalo moyoni naona niwashikirikishe wenzangu nione mnishauri nini

Ni hivi Ninaishi na mke wangu,mwaka wa NNE sasa,tuna mtoto mmoja,nina Mdogo wangu,anaishi hapa tangia January niliponunua bajaj ili awe anaendesha ili kusaidia wazazi wetu nyumbani kijijini,sasa jumapili iliyopita Wife aliwahi sana asubuhi kwenda kanisani pamoja na mtoto, Mimi nilibaki nimejilaza mpaka kama SAA moja na nusu Hivi, nilivyokumbuka kuwa nilikuwa na Ahadi Fulani, katika kufanya maandalizi sikiweza kuiona pass, so nikaenda straight chumbani kwa dogo katika kuitafuta ndo nilipo kutana na chupi ya mke wangu, ambayo Mimi mwenyewe nilimununulia so imechoka choka kiasi chake,nilishikwa na butwaa kwani namwani sana wife, dogo mwenyewe heshima kwa sana, nilichukua simu na kupiga picha kadha na kuzificha kwenye private vault, ile chupi nikaaicha palepale, wife hajasema chochote mpaka sasa, nawaza namna ya kuanza kumuulizia japo ameshahisi kuwa siko normal,coz nikimuona usoni nakuata hasira imepnada sana,kwa kifupi naogopa ukweli kuwa mke wangu amenisaliti kwa mdogo wangu,mpaka sasa simuoni kama mke wangu tena, namuona kama bundi kajificha chumbani kwangu, naomba mnishauri kwani Mimi kwa haraka haraka naona nimwite kaka yake aje amchukue kabla sijamfanya kitu mbaya, tatizo hasira zangu hupanda pole pole sana, kuzishusha ni kazi sana

Thomas Ulimwengu Aondoka TP Mazembe, Afuata Ndoto zake Kucheza Ulaya

Baada ya kucheza misimu mitano kwenye klabu ya TP Mazembe, mchezaji wa Taifa Stars, Thomas Ulimwengu ameondoka kufuata ndoto zake kucheza Ulaya.

Mchezaji huyo aliyekuwa akivaa jezi namba 28 na aliyepewa jina la utani ‘Rambo’ alichukuliwa na klabu hiyo akiwa na umri 18 kutoka AFC Academy ya Stockholm, Sweden. Akiwa na TP Mazembe, Ulimwengu amecheza mechi 130 na kufunga mabao 35.

Wakati anachezea klabu hiyo klabu nyingi zilitaka kumchukua lakini aliamua kumaliza kwanza mkataba wake na Mazembe. Aliamua kutoongeza tena mkataba na TPM. Na sasa Ulimwengu anataka kufuata nyayo za Mtanzania mwenzake Mbwana Samatta wa Genk ya Ubelgiji.

Kabla ya kuondoka Lubumbashi, Ulimwengu alisema kupitia taarifa kwenye tovuti ya klabu hiyo, “Kwa miaka mitano Mazembe imeniruhusu kuendelea kukua kisoka na nataka kuwashukuru wote walioniunga mkono na kusaidia kushinda vikombe wakiongozwa na Rais Katumbi na Mrs Carine, viongozi na makocha.”

Vyakula Vinavyoongeza Hamu na Nguvu ya Kufanya Tendo la Ndoa

Tatizo la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4 kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu za kiume.

Pamoja na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili.

Kwa kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini aina mbalimbali ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya kufanya tendo la ndoa.  Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo:

1. PILIPILI
Kama tunavyojua wote mara nyingi chakula ambacho kimeungwa pilipili hufanya hata mapigo ya moyo kuwa tofauti na wakati mwingine hata jasho au kamasi hutoka. Ndani ya pilipili kuna kitu kinaitwa capsaicin ambacho hufanya pilipili iwe na hali ya ukali. Capsaicin huwezesha ubongo kutoa homoni ya endorphins ambayo huleta mgusu wa hisia za raha wakati wa kufanya tendo la ndoa.
Pia pilipili husisimua mfumo wa fahamu (nerves) wa ubongo na katika kufanya hivyo huwezesha kuamshwa haraka kimapenzi (kunyegeka) wakati wa tendo la ndoa na pia ukiguswa au kubusiwa au kunyonywa au kupapaswa unapata hisia kila sehemu ya mwili.

2. MATUNDA NA MBOGA ZA MAJANI
Ulaji wa matunda na mboga za majani una matokeo makubwa sana katika hamu ya tendo la ndoa kwa njia nyingi. Kwanza matunda na mboga za majani hupunguza kiwango cha mafuta na unene (cholesterol).  Kuongezeka kwa mafuta mwilini huzuia mzunguko wa damu kwa kubana mishipa ya damu.

Pia kula matunda na mboga za majani huhakikisha balance ya uzito kwani unene (obesity) kwa wanaume kuna matokeo mabaya katika kuzalisha homeni za testoeterone na hatimaye jogoo kushindwa kuwika na kuwa na pia mwanaume anakuwa na hisia za mapenzi (libido) kidogo.
Na pia wanandoa wanapozidi kunenepeana ndipo na hali ya kufurahia au kuwa na hamu ya tendo la ndoa huzidi kupungua. Kitalaam inashauriwa kula milo (potions) 3-5 za matunda kwa siku.

3. NAFAKA ZISIZOKOBOLEWA
Nafaka hasa zisizokobolewa kama mahindi, ngano, uwele, nk zina nyuzinyuzi (fibre) na sukari ngumu (complex sugar) ambazo kusaidia kutunza uzito wa mwili. Nafaka husaidia katika kuzalisha homoni za testosterone kwenye damu. Na pia nafaka huwezesha mtu kuwa na nguvu hatimaye kwenda masafa marefu wakati wa tendo.

Kula nafaka nzima kama vile brown bread badala ya white bread, pia kula nafaka halisi badala ya cornflakes ni jambo zuri linalokuhakikisha afya nejama na mahusiano mazuri ya ndoa yako.

4. TANGAWIZI
Tangawizi ni kiungo cha mboga ambacho husisimua sana na kusaidia mfumo wa mzunguko wa damu mwilini. Tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume hivyo kuwa na umuhimu sana katika kuboresha ufanyaji wa tendo la ndoa. Inaweza kuliwa mbichi, au kuliwa ikiwa imeungwa kwenye chakula au kusagwa na kuwa kama unga na kutumiwa kama chai.

5. ASALI
Asali ina madini yanayoitwa boron, ambayo husaidia mwili kutumia homoni ya estrogen ambayo ni homoni inayohusika na viungo ya uzazi na mapenzi kwa mwanamke.
Pia kuna utafiti unaoonesha kwamba asali huongeza nguvu, kitendo ambacho kitapelekea mwanamke kuwa uwezo na hamu ya tendo la ndoa au libido.

6. KARANGA
Karanga huhusika katika kuchochea mfumo wa mzunguko wa damu (vascular system). Mzunguko wa damu ulio sawasawa katika uke na uume huwezesha mwanaume na mwanamke kupata msisimko wa mapenzi haraka hatimaye tendo la ndoa kuwa murua. Pia karanga zina madini muhimu kama vile magnesium, asidi ya folic na zinc ambayo ni muhimu sana katika usalishaji wa mbegu za mwanaume.

7. CHAZA (OYSTERS) NA PWEZA
Hawa ni aina ya samaki ambao hupatikana katika maji chumvi. Huwa na kiasi kikubwa sana cha madini ya zinc na haya madini ndiyo huhusika zaidi na uzalishaji wa homoni ya testosterone kwa wanaume.
Pia imethibitika kwamba wanaume wenye ukosefu wa madini ya zinc huwa na matatizo ya nguvu za kiume.  Pia madini mengi ya zinc mwilini huongeza kiwango cha shahawa kwa wanaume.

8. SOYA
Pamoja na kuwa na kiwango kidogo sana cha mafuta (fat) na pia kuwa na kiwango kizuri cha protein, soya zina phytoestrogens ambayo husaidia sana wanawake ambao wamefikia menopause kutengeneza homoni estrogen ya ziada.
Husaidia uke kuwa laini (wet, lubricated) mwanamke akisisimuliwa wakati wa tendo la ndoa.

9. CHOKOLETI
Chocolate ina phenylethylamine, kemikali ambayo husababisha hisia (feelings) za furaha wakati wa mwanamke au mwanaume kufika kileleni (orgasm). Inasaidia sana kula chocolate masaa machache kabla ya kuanza kufanya tendo la ndoa.

10. PARACHICHI
Aina nyingine ya chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya tendo la ndoa ni Parachichi. Tunda hili linauwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni. Inatajwa kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwana msisimko mkali wa kimapenzi na kwa upande wa wanawake husaidia kuongeza majimaji yenye utelezi sehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa kujamiiana.

Huyu Hapa Mpenzi Mpya wa Idriss Sultan....Wagandana Kama Ruba Huko MTV Awards

 Inasemekana eti Idriss na Mrembo ajulikanaye kama Sanchoka kwa sasa ni wapenzi baada ya kuonekana pamoja huko Afrika Kusini walipoenda kwa ajili ya MTV awards...
Picha na Video mbali mbali wakiwa pamoja zainazagaa huku instagram