Ijumaa, 26 Septemba 2014

Waaga mchuano baada ya kuagizwa kuvua hijab

Timu ya wanawake ya Qatar ya mchezo wa mpira wa kikapu imejiondoa kutoka mashindo ya bara Asia.
Timu ya wanawake ya Qatar ya mchezo wa mpira wa vikapu imejiondoa kutoka mashindo ya bara Asia yanayofanyika huko Korea Kusini baada ya kuagizwa kuvua hijab kabla ya mechi yao dhidi ya timu ya Mongolia .
Wanawake hao walikataa kata kata kuvua vazi hilo na wakajiondoa mashindanoni wakidai inakiuka maagizo ya dina ya Kiislamu inayomtaka mwanamke kujistiri nywele zake haswa akiwa faraghani.
Sheria za shirika la mchezo huo duniani haziruhusu kuvaliwaj kwa vitambaa vya kichwani wakati wa mechi lakini sasa wamekuwa wakijadili iwapo sheria hiyo itaondolewe.
Hata hivyo ilipowadia wakati wa mechi yao dhidi ya Nepal sheria hiyo haikuwa imebadilishwa na hivyo iliwabidi kuyaaga mashindano.
Fani nyengine za michezo katika mashindano hayo ya Bara Asia zinaruhusu uvaliwaji wa hijab.
Timu ya taifa ya unyanyuaji uzani ya Iran imekuwa ikishiriki mashindano hayo huku wakiwa wamevalia hijab.
Baraza la mashindano ya Olimpiki ya Bara asia OCA imesema kuwa haki za wachezaji ni zinapaswa kupewa kipaombele .
Sheria za shirikisho la mpira wa vikapu haziruhusu mavazi kichwani 
Baada ya kuyaaga mashindano hayo mchezaji wa Qatar Amal Mohamed A Mohamed alisema kuwa walikuwa wamehakikishiwa kuwa wataruhusiwa kushiriki mashindano hayo wakiwa wamevalia hijab na hivyo hawaelewi kwanini sheria hiyo haijabadailishwa.
''nina hakika kuwa hatutashiriki mashindano yeyote ya Bara Asia hadi sheria hiyo ibadilishwe''
Mashindano hayo hufanyika kila baada ya miaka 4 na huwaleta pamoja washiriki 9000 kutoka mataifa 45 yakishindana katika fani 36 ya michezo.
Mashindano hayo yatamalizika tarehe 4 Oktoba.

Van Gaal:tuna mlinzi wa kati mmoja tu

 
Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal.
Kocha wa machester United, Louis van Gaal amesema Manchester united ina mlinzi wa kati mmoja tu mwenye uzoefu wakati huu kikosi hicho kinapotarajia kukipiga na west ham katika michuano ya ligi kuu ya England.
Marcos Rojo yuko fiti, lakini timu hiyo ina majeruhi kama Chris Smalling ana jeraha la mguu, Phil Jones ana jeraha kwenye, Jonny Evans ana jeraha la kifundo cha mguu na Tyler Blackett hatacheza mchezo huo.
Van Gaal analazimika sasa kuchukua wachezaji kwenye kikosi cha vijana ili kuziba mapengo yaliyopo kwenye timu yake.miongoni mwao ni vijana Tom Thorpe na Paddy MacNair ambao wataungana na kikosi cha kwanza cha Manchester United kwa mara ya kwanza.

'VIPIMO VYA SKETI KIGEZO CHA SARATANI'

 
Baadhi ya watafiti wana sahuku ikiwa vipimo vya sketi vitamtahadharisha mwanamke kuhusu tisho la Saratani.
Utafiti unaonyesha kuwa wanawake wanaonenepa maishani bila ya kuwa waangalifu wanajiweka katika hatari ya kupata Saratani.
Watafiti kutoka chuo Kikuu cha London wanasema kwamba wanawake walio kati ya umri wa miaka 24-28 ambao huendelea kunenepa kila baada ya miaka 10, wako katika hatari zaidi ya kupata Saratani ya Matiti baada ya kupitisha umri wa kuzaa.
Sasa je ni nini ishara ya mwanamke kunenepa? Watafiti wanasema vipimo vya sketi yake vinaweza kukusaidia kujua ikiwa uko katika hatari ya kpatwa Saratni ya Matiti au la.
Kila unapogundua kuwa sketi yako inaendelea kuwa ndogo kiunoni, basi inakubidi ujue kuwa mwili wako unaongekeza kwa unene. Na pia ni rahisi kwa wanawake kukumbuka kipimo cha sketi kuliko kitu kingine chochote.
Kwa hilo watafaiti wanasema mwanampe anapaswa kutahadhari kila sketi yake inapoendelea kuwa ndogo kwake maana kwamba amenenepa zaidi. Ikiwa ukubwa wake unazidi kwa kipimo cha sketi mbili katika kipindi kimoja basi mwanamke anakuwa katika hatari ya kupatwa na Saratani hata zaidi.
'Mfumo wa maisha'
 
Tisho hili linawakabili zaidi wanawake waliopitisha umri wa kupata watoto 

Akizungumzia utafiti huo, Simon Vincet kutoka shirika la kupambana na saratani ya Matiti la Breakthrough Breast Cancer, alisema kuwa saratani ya Matiti miongoni mwa wanwake inaweza kupunguka ikiwa watu watabadilisha mfumo wa maisha kwa kujiuzia kunenepa kupita kiasi na kufanya mazoezi sana.
Utafiti huu unaangazia njia rahisi sana kwa wanawake kuwa waangalifu kuhusu unene wa miili yao.
Kuangalia kipimo cha sketi kati ya wanawake walio kati ya miaka 24 na 28 wenye miaki katikati ya 20 na zaidi wanaweza kuwa na njia rahisi ya kufuatilia uzito wa miili ya Unene wa kupita kiasi unajulikana kwa sababu ni hatari kubwa inayochangia katika ugonjwa wa saratani , hususan mafuta ya yaliyoko tumboni.
Prof Usha Menon wa shirika lakupambana na satratani ya matiti, ndiye aliyeongoza utafiti huo na kuambia BBC kuwa "Kama kipimo cha sketi kinaweza kuthibitishwa na wengine kama kigezo cha wanawake watu wazima kuapa Saratani, basi hii itakuw anjia nzuri na rahisi ya mtu kuwa mwangalifu ili asinenepe kupita kiasi.
'Changamoto'
 Unene kupita kiasi ni moja ya mambo yanayohatarisha afya ya wanawake waliopitisha umri wa kuzaa.

Watafiti hao walisema utafiti wao ulikuwa na changamoto kadhaa kwamba uliangazia zaidi wanawake kukumbuka vipimo vya sketi zao tangu tangu wawe na umri wa miaka 20
Lakini ikiwa matokeo ya utafiti huo yatathibitishwa, itakuwa njia rahisi kwa wanawake kuelewa hatari zinazowakabili hasa wanapoendelea kunenepa.
Tom Stansfeld kutoka shirika la utafiti wa Saratani nchini Uingereza,anasema utafiti huo unaweza kuaminika lakini unazingatia zaidi wanawake kukumbuka vipimo vya sketi walizovalia miaka ya zamani.
Utafiti unasema kuwa baadhi ya mambo muhimu ambayo mwanamke anaweza kufanya kupunguza tisho la kuugua Saratani ya Matiti , hasa baada ya kupitisha miaka yake ya kuzaa ni pamoja na kufanya mazoezi , kula vizuri na kupunguza ulevi.
Kupunguza unene ni njia moja wapo ya kupunguza tisho la kupata Saratani baada ya kupitisha miaka ya kuzaa na kuangalia vipimo vya sketi za wanawake kuwahamasisha wanawake.

KILICHOWAKUTA CHADEMA WALIOANDAMANA MWANZA Sept.25

news 1 
Kutoka 88.1 Mwanza ambapo Polisi wamekamata viongozi sita na wafuasi kadhaa wa (CHADEMA) waliokuwa wakijiandaa kuandamana baada ya kukaidi amri ya polisi kusitisha maandamano.
Ni September 25 saa 5.40 asubuhi muda mfupi baada ya wafuasi hao kujipanga kwa maandamano yaliyokuwa yaanzie viwanja vya Sahara mpaka ofisi za mkuu wa wilaya ya Nyamagana na kufanya mkutano mfupi wa hadhara kufikisha ujumbe.
Purukushani ilidumu kwa zaidi ya dakika 120 ikiambatana na wafuasi hao kupigwa virungu huku taarifa zisizo rasmi zikisema Polisi wamewatia mbaroni watu 14 wanaodaiwa kuandamana bila kibali.
Kwa mujibu wa ripota wa nguvu Paul Luvega, licha ya kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza bado halijatoa taarifa kamili ambapo John Nzwalile katibu wa CHADEMA Mwanza amesema >>> ‘naweza kusema kwa ujumla tumefanikiwa, Polisi ndio wameandamana kwa wingi kuliko hata sisi, tokea asubuhi ukienda chooni au kunywa chai Askari kanzu wanakufatili, ukinywa chai na wao wanajifanya wanakunywa chai
 ‘Niseme maandamano yetu yamefanikiwa kwa sababu yalikua yamepangwa kwa akili kubwa sana, tuliandamana kuanzia kichwani… hatukuandamana ovyoovyo, hawakujua tunaanzia wapi tunaishia wapi…. tumeshangaa Polisi wamekuja na vifaa utadhani unaangalia movie ya vita’
‘Mpaka sasa taarifa nilizonazo mwenyekiti wangu wa Nyamagana amekamatwa, Katibu mwenezi Nyamagana, Mwenyekiti kata ya Bugogwa, Katibu wilaya ya Ilemela wamekamatwa…. watu ambao kosa lao ni kuwaambia Watanzania kuna pesa inaliwa na Wabunge kwenye batili la katiba’
‘Kwa kauli moja ya chama niseme tu kwamba maandamano na migomo isiyokua na kikomo itaendelea…. tunazidi kujipanga vizuri kuangalia namna bora zaidi ya kuandamana, tunataka watu wetu watoke Wanasheria wetu wanajipanga…. kuhakikisha wanatoka bila masharti’

Hukumu ya muuguzi aliesababisha kifo cha mjamzito mwaka 2009.

hosp 1 
Kwenye moja kati ya taarifa kubwa za Kenya September 25 2014 ni pamoja na hii ya Muuguzi mmoja ambae kesi yake ilianza kusikilizwa toka mwaka 2009 nchini humo kwenye kaunti ya Kyambuu.
Kituo cha Radio Jambo kimeripoti kwamba muuguzi huyu Jackson Tali mwenye umri wa miaka 41 amehukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia ya kusababisha kifo cha msichana aliyetafuta huduma za ujauzito wake kwa muuguzi huyu.
Jackson anadaiwa kutenda kosa hilo July 27 2009 huko Kyambuu.