Ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini
Mali unasema kuwa watu waliokuwa na silaha ambao walikuwa wakitumia
pikipiki wamewaua walinda amani tisa wa Umoja wa Mataifa kaskazini
mashariki mwa taifa hilo.
Uvamizi huo ndio mbaya zaidi kuwai kuwakumba wanajeshi hao wa Umoja wa MataifaWanajeshi hao kutoka nchini Niger walikuwa wakisafiri kati ya miji ya Menaka na Ansongo wakati walipovamiwa.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa amesikitishwa na kile alichokitaja kuwa vitendo vya kigaidi.
Mwandishi wa BB nchini Mali amesema kuwa kikosi hicho cha umoja wa mataifa kimelalamika kuhusu vifaa duni inavyomiliki.
Walindamani hao walitumwa miaka miwili iliyopita baada ya makundi ya wanamgambo wa kiislamu kuchukua udhibiti wa maeneo ya kaskazini mwa Mali.