Jumanne, 21 Julai 2015

Mtoto huyu ameweza kuishi kwa miaka 12 na virusi vya Ukimwi bila kutumia dawa yoyote!


HIV
Nimekutana na stori mmoja kutoka Ufaransa inayomhusu mtoto wa miaka 18 aliyeweza kuishi na Ukimwi kwa miaka 12 bila kutumia dawa zozote wala vidonge vyovyote vya ARV.
Kitendo hiki kimeweka headlines nyingi sana nchini Ufaransa na kimeleta matumaini mapya ya kupata tiba ya ugonjwa wa Ukimwi, kwa njia ya kushusha virusi kwa viwango vya chini mwilini bila kutumia tiba ya kupunguza makali.
HIV2
Msichana huyo alikuwa akitumia tiba ya kupunguza makali mpaka alipotimiza miaka 6 na baada ya mwaka mmoja timu ya madaktari iligundua kuwa virusi vya mtoto huyo haviongezeki, havipungui wala kuathiri mwili wake kwa namna yoyote ile.
Na tangu kipindi hicho ameweza kuishi na virusi hivyo bila venyewe kuonekana kwenye damu yake na bila kutumia dawa yoyote hali inayojulikana kama “remission” – virusi kutokuongezeka wala kupungua mwilini, kwa miaka 12.
HIV3
Madaktari wanaamini kutakuwa na kitu cha tofauti kwenye mfumo wake wa damu iliyoiwezesha dawa alizokuwa anazitumia akiwa mtoto kudhibiti ongezeko la virusi, lakini kwa sasa hali nzima juu ya uvumbuzi huu bado ni utata kwa madaktari.
HIV4
Daktari kutoka The Institut Pasteur nchini Ufaransa amesema kwamba hii ni mara ya kwanza ndani ya miaka mingi kwa hali hii kujitokeza kwa watoto ama kijana kwenye ripoti aliyowasilisha kwenye Press Conference ya The 8th IAS Conference on HIV Pathogenisis Treatment and Prevention mjini Vancouver wiki hii.