Alhamisi, 4 Desemba 2014

SERENKUMA AJIUNGA NA KLABU YA SIMBA

 
Mshambuliaji matata wa kilabu ya Gor Mahia nchini Kenya Dan Sserenkuma aihama kilabu hiyo na kujiunga na Simba SC ya Tanzania 

Aliyekuwa Mshambuliiaji wa mabingwa wa soka nchini Kenya Gor Mahia Dan Serenkuma amejiunga na kilabu ya Tanzania Simba SC.
Raia huyo wa Uganda alijiunga na kilabu hiyo ya Ligi ya Vodacom na kutamatisha kazi yake ya miaka mitatu katika ligi ya Kenya ambapo alianza kwa kuichezea Nairobi City Stars kabla ya kujiunga na Gor ambapo alikuwa kiungo muhimu katika ushindi wa ligi mara mbili.
''Nimefurahia miaka miwili na nusu katika kilabu ya Gor Mahia,lakini huu ndio wakati muhimu wa kuaga.Tumefurahia nyakati maalum na mafanikio pamoja,na habiki wamenisaidia sana hususan wakati mgumu'',Mfungaji huyo wa mabao mengi katika ligi ya Kenya aliandika katika mtandao wake wa Twitter.
''Ningependa kumshukuru kila mtu katika usimamizi wa kilabu kwa kunipa fursa muhimu ili kuonyesha kipaji changu.

                                                   Dan Sserenkuma

Mchezaji huyo wa kimataifa katika timu ya Uganda Cranes alipigwa picha katika mtandao wa kilabu hiyo akifanyiwa majaribio pamoja na kupimwa afya na sasa anatarajiwa kujiunga na wachezaji wenzake katika barabara ya Msimbazi mjini Daresalaam tayari kwa maandalizi ya mechi za ligi ya Tanzania.
Wakati huohuo imebainika kwamba Kilabu ya Gor Mahia ilishindwa kumzuia mchezaji huyo.
Duru zimearifu kuwa mchezaji huyo aliandamwa na kilabu ya Gor mahia kufuatia ripoti za vyombo vya habari kwamba alitarajiwa kujiunga na Simba.
Lakini Gor Mahia haikuwasilisha ombi lolote la fedha kwa kuwa mchezaji huyo tayari alikuwa ameweka kandarasi yenye thamani ya shilingi millioni 3 pamoja na mshahara wa ksh.250,000 kwa mwezi na kilabu hiyo ya Tanzania ambapo atajiunga na mchezaji mwengine wa Gor Mahia Mungai Kiongera.

MCHEZAJI AFARIKI BAADA YA KUPIGWA KICHWA

Mchezaji Franco Nieto aliyefariki baada ya kupiwa na jiwe kwenye kichwa wakati wa mechi nchini Argentina

Mchezaji wa Argentina Franco Nieto ,mwenye umri wa miaka 33 amefariki baada ya kupigwa kwenye kichwa wakati wa mechi siku ya jumamosi.
Nieto ,nahodha wa kilabu ya kijimbo ya Tiro federal alishambuliwa na genge baada ya mechi kati ya wapinzani wao wa jadi Chacarita Juniors katika mji wa Aimogasta kazkazini magharibi mwa Argentina.
Mechi hiyo ilisimamishwa kwa dakika 15 kabla ya kukamilika baada ya refa kuwapa kadi nyekundu wachezaji wanane kwa kupigana.
Mwaka huu watu 15 wamefariki katika ghasia zilizosababishwa na soka nchini Argentina,Binamu wa Nieto,Pablo Nieto amesema kuwa watu watatu walimzunguka mchezaji huyo alipokuwa akielekea katika gari lake na mkewe na mtoto wao wa mwezi mmoja.
Walimpiga kwa ngumi na mateke kabla ya mmoja ya watu hao kumpiga na jiwe katika kichwa na kumwacha bila fahamu.
Alifanyiwa upasuaji siku ya jumanne lakini akafariki siku ya jumatano.
Afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo Fabian Bordon ameviambia vyombo vya habari kwamba watu watatu wamekamatwa kutokana na shambulizi hilo.
Ghasia zinazosababishwa na soka ni tatizo kubwa nchini Argentina.
Kulingana na shirika moja lilisokuwa la kiserikali Salvemos el Futbol,vifo vinavyosababishwa na ghasia za soka vimeongezeka mwaka huu.
Washukiwa wakuu ni genge la Barras Bravas ambao hudhibiti maneo ya kukalia katika viwanja vya mpira na barabara karibu na viwanja hivyo.
 

AISHI NA MAITI AKITARAJIA ITAFUFUKA

                                                                                 Maiti


Familia moja nchini Canada iliishi na maiti katika chumba cha juu cha nyumba yao kwa miezi sita kwa kuwa waliamini marehemu atafufuka iwapo wataendelea kumuomba mungu,lakini mwili huo ukapatikana baada ya familia hiyo kushindwa kulipa mkopo waliochukua kununua nyumba hiyo.
Kaling Wald mwenye umri wa miaka 50 alipatikana na makosa ya kushindwa kuwaarifu maafisa wa polisi kwamba mumewe alifariki ,kosa ambalo na akahukumiwa kuwekwa katika muda wa majaribio na ushauri,wakili wake alikiambia chombo cha habari cha Reuter siku ya Jumanne.
Peter Wald mwenye umri wa miaka 52 alifariki mnamo mwezi machi mwaka 2013 kwa kile mamlaka inasema ni sababu za kawaida kufuatia maambukizi ya mguu wake yanayodaiwa kusababishwa na ugonjwa wa sukari.
Mkewe Kaling Wald alimwacha kitandani na kufunga chumba hicho katika nyumba yao ya Hamilton ,Ontario ili kuzuia harufu kali iliokuwa ikitoka chumbani humo kuwafikia watu waliokuwa wakiishi nyumbani humo.
Kama vile Yesu alivyomfufua Lazaro baada ya siku ya nne ,pia yeye aliamini kwamba Mungu atamfufua mumewe wakili wa mwanamke huyo alisema.

Binti aliyeongoza Matokeo ya darasa la saba kuozeshwa kwa mahari ya kilo 2 za sukari

girl
Pamoja na Serikali kuendelea kupiga vita wazazi kuwaoza mabinti zao wakiwa bado wadogo lakini bado kuna baadhi ya makabila hapa nchini wameendeleza utamaduni huo kwa kuwaoza mabinti zao sababu kubwa ikitajwa kuwa ni tamaa za kutaka kujilimbikizia mali.
Lakini kwa msichana huyu wazazi wake wameonekana kutoijali hata ile mali waliyopewa kwani wameweza kumwozesha binti yao wa kike kwa mahari ya kilo mbili za sukari toka kwa mfugaji wa kabila la kimasai.
Gazeti la NIPASHE limeripoti kuwa mmoja wa wanafunzi walioongoza darasa wa Taifa wa Darasa la saba mwaka huu mwenye umri wa miaka 16 anadaiwa kuozwa kwa mwanaume mwenye miaka 50 baada ya wazazi wake kupewa sukari kilo mbili kama mahari.
Kutokana na hali hiyo mtandao wa kuelimisha jamii kuhusu ukeketeji Mkoani Kilimanjaro NAFGEM umefanya jitihada za kumuokoa pamoja na wanafunzi wengine15 waliotaka kufanyiwa vitendo vya ukeketaji kwa ngariba.
Msichana huyo wa miaka 16 wa kabila la kimasai ambaye jina lake limehifadhiwa baada ya kufaulu mtihani huo kwa asilimia kubwa huku akitajwa kuwa miongoni mwa wasichana waliofanya vizuri aliozeshwa kwa mwanaume mmoja ambaye ni mfugaji wa kabila hilo.
Meneja Mpango wa mtandao wa kuelimisha jamii kuhusu ukeketaji Mkoani Kilimanjaro Honoratha Nasua alitoa taarifa za kuolewa kwa binti huyo walizipata huku wanafunzi wengine 15 wakisubiri tarehe ya kufanyiwa ukeketaji ili waozeshwe baada ya tendo hilo.
Alisema suala la mwanafunzi huyo aliyeozeshwa limefikishwa katika dawati la jinsia la Polisi Wilayani Siha kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi za kisheria.
Alisema wazazi wa mwanafunzi huyo wamechangia kudidimiza maendeleo ya mtoto wao kwa kukubali aolewe na kubuni mbinu mpya ya kukeketa watoto wachanga ili kukwepa mkono wa dola na vyombo vya wanaharakati.
Mtandao huo wa kupinga ukeketaji unaendelea na shughuli zake katika Wilaya hiyo ikishirikiana na Shirika la kimataifa la Elimu kwa ufadhili wa Shirika la misaada la kimataifa la Marekani USAID kupitia mpango wa pamoja wa TUWALEE.

Yule mama aliyejiuzulu kwa kukosoa mavazi ya watoto wa Obama kumbe bado anafuatiliwa?

sasha-malia-2-477 
Moja ya story ambazo zilichukua uzito wa juu katika vyombo vya habari wiki iliyopita ilikuwa ni kitendo cha yule mama mfanyakazi wa Chama cha Republican Marekani, Elizabeth Lauten ambaye alikuwa kitengo cha Mawasiliano kukosoa mavazi ya watoto wa Obama bado ni story inayoendelea kuzungumziwa.
Mama huyo aliwaponda Sasha na Malia kuwa wamekosa ustaarabu kutokana na kuvalia sketi fupi katika hafla ya chakula katika Ikulu ya White House, pia alisema kuwa watoto hao ni kama hawakuwa na nyuso za furaha kuwa katika hafla hiyo, ambapo baada ya kushambuliwa na watu kwenye ukurasa wake wa Facebook aliomba radhi, na baadaye akajiuzulu.
141130152136_turkey_640x360_getty
Leo ni siku ya nne tangu amejiuzulu lakini story ni kwamba bado ameendelea kufuatiliwa na vyombo habari, huku wengine wakipiga kambi nyumbani kwa wazazi wake kuchunguza vitu mbalimbali ikiwemo rekodi ya maisha yake ya utotoni ambapo watu kwenye mitandao ya kijamii wamekosoa kwa kusema hiyo haikuwa ‘big deal’ ya kufanya vyombo vya habari kumfuatilia kiasi hicho.