Jumatano, 2 Julai 2014
New AUDIO | SNAIDA - MUHTASARI WA HABARI | Download
ARTIST-SNAIDA.
SONG-MUHTASARI WA HABARI.
STUDIO-BANTU MUSIC.
PRODUCED BY LUSUNGU
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiYh_iqvVbGTqdX8O2R6FpqP8Jot3LTk6a5V2ValJu2sODDSoid6ivcGTcb5_JN64qKkLvdij2JD721xHBFg4guND-LS15iq3PUI2KFKYQU5X_3R7YJxXJigsZ-HHf-beDcp8x2UrYPi-Rg/s1600/DJMwanga+download+Logo.png

Sikiliza hapa ugomzi uliotokea dakika 5 kabla ya Show ya XXL Clouds Fm kumalizika Julai 02
Kilichosababisha haya yote ni mabishano ya mauzo ya album ya Fiesta ambayo kila mmoja alikua anataka aiandae alafu aiuze yeye….. ilitokea B12 alisema ni wazo lake lakini kumbe Fetty na Adam nao wanasema waliwahi kuwa na wazo kama hili.
Watangazaji hawa walianza kugombana studio kama wanavyosikika hapa chini

Full time ya USA vs Belgium – walichofanya Lukaku na De Bruyne
Mechi za hatua ya 16 zimemalizika rasmi usiku wa kuamkia leo kwa mchezo kati ya Marekani dhidi ya Belgium.
Katika mchezo huo uliokuwa mgumu kwa pande zote, mpaka dakika zote 90 zinamalizika hakukuwa na mtu aliyefanikiwa kuliona lango la mwenzie, japo kulikuwa na kosa kosa nyingi katika lango la Marekani na bila ushujaa wa kipa Tim Howard basi hadithi ingekuwa nyingine.
Baada kwa kumalizika kwa dakika 90, zikaongezwa dakika 30 za nyongeza na mnamo dakika ya 105, Kelvin De Bruyne akaifungia Belgium bao la kwanza, dakika 2 baadae Romelu Lukaku akapiga goli la pili, kabla ya Green kuifungia Marekani goli la kufutia machozi.

Taarifa kuhusu ndege iliyodondoka alfajiri ya July 02 Kenya.
Imeripotiwa kuwa wanne waliokua kwenye Ndege iliyokua ikitokea uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta Nairobi, Kenya kuelekea Mogadishu, Somalia wamepoteza maisha baada ya Ndege hiyo kuanguka katika eneo la Utawala dakika chache baada ya kupaa,
Ajali hiyo imetokea alfajiri ya Julai 02 na inaaminika kwamba ndege hiyo ilikua iondoke mapema kusafirisha zao la Mirungi na bidhaa nyingine kuelekea Somalia.
Walinzi wawili wamejeruhiwa katika ajali hiyo ambapo mmoja amekwishapatiwa matibatibu na kuruhusiwa huku mmoja akiwa bado anaendelea na matibabu katika hospitali ya Mama Lucy.
Kwa mujibu wa Mkuu wa polisi Jijini Nairobi Benson kibue, ajali hiyo imetokea baada ya Ndege hiyo yenye nambari 5Y-CET kuanguka juu ya Paa la jengo la kibiasharawakati ikijaribu kutua ghafla na kushika moto papo hapo.
Polisi wanaendelea na uchunguzi kufuatia ajali hiyo ndani ya mabaki ya ndege.

Zawadi kutoka kwa Barakah Da Prince – Sio Fine
Kutoka Mwanza anaitwa Barakah Da Prince Mwanzoni ulimsikia na wimbo wa Jichunge ambao video yake ilifanywa na Director Nisher kutoka Arusha,leo July 02 ameamua kuachia wimbo wake ambao kasema ni zawadi maalum kwa mashabiki wake waliompokea vizuri na wimbo wa Jichunge.
Huu unaitwa Sio Fine amautoa wakati akijiandaa na single yake maalum itakayotoka October, wimbo huu uliwahi kusikia kwenye vituo vya Mwanza na kanda ya ziwa ila katika aina tofauti na hii,ingawa haukutoka rasmi kwa sasa ameamua kuurekodi upya na kwa kiwango bora zaidi ili uweze kuwafikia mashabiki wote wapya na wa zamani.
Bonyeza play kuusikiliza na kudownload.

Kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa wa mauaji ya Sista aliyepigwa risasi Ubungo.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam inawashikilia watuhumiwa wawili wa ujambazi ambao wanahusishwa na mauaji ya Mtawa wa Kanisa Katoliki Sista Clezensia Kapuli.
Mbali na watuhumiwa hao pia watu wengine sita wanashikiliwa wakihusishwa na matukio mbali mbali ya ujambazi hapa nchini.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Suleiman Kova, amewataja majambazi wanaohusishwa na mauaji ya Sista huyo kuwa ni Manase Ogenyeke “mjeshi” (35) mkazi wa Tabata Chang’ombe na Hamis Shaban “Carlos” mkazi wa Magomeni mwembechai.
Wengine waliokamatwa kutokana na matukio mengine ya ujambazi ni Beda Mallya miaka (37) mkazi wa Mbezi msakuzi, Michael Mushi (50), Sadick Kisia (32), Elibariki Makumba (30), Nurdini Suleiman (40) pamoja na Mrumi Salehe (38).
Majambazi hao wamekamatwa kutokana na Operesheni inayoendelea jijini Dar es Salaam baada ya kifo cha Mtawa huyo kilichotekea Juni 23 mwaka huu, kamanda Kova amesema majambazi hao wawili pia wanahusika na tukio la uporaji fedha katika Benki ya Barclays tawi la Kinondoni lililotokea miezi michache iliyopita.

Jinsi Facebook ilivyowafanyia utafiti wa kisaikolojia watumiaji bila kuwajulisha.
Mtandao wa kijamii wa Facebook umelaumiwa kwa kuwafanyia wateja wake utafiti wa kisaikolojia bila ya kuwajulisha.
Shirika la habari la BBC limeripoti kuwa, nia ya utafiti huo ilikuwa kujua kama wateja wake wamebadili tabia ya kuweka picha na mawazo yao katika mtandao huo kutokana na kukasirishwa na tabia za baadhi ya watumiaji wenzao.
Utafiti huo uliohusisha takribani watumiaji 700,000 unaonyesha kuwa Facebook inacheza na taarifa za watumiaji wake ili kupata hisia zao katika kile wanachokiweka kwenye mtandao huo.
Hata hivyo mtandao wa Facebook umekanusha madai hayo na kwamba hakuna mtumiaji binafsi aliyelengwa na utafiti huo uliofanywa na mtandao huo kwa ushirikiano na chuo kikuu cha Cornell na California.
Hata hivyo Profesa wa Saikolojia katika chuo cha Elmhurst , Illinois, Katherine Sledge Moore, amesema kwa jinsi ambavyo Facebook wamekuwa wakishughulika na taarifa za wateja wake makubaliano yaliyopo katika utafiti huo hadhani kama yapo nje ya hali ya kawaida.
Adam Kramer kutoka Facebook mmoja kati ya walioandaa taarifa ya utafiti huo anasema wanadhani kuwa ilikuwa muhimu kwao kutafiti mashaka yanayowakumba watumiaji hasa katika mawazo yanayowekwa na marafiki zao na jinsi yanavyowafanya wafikirie tofauti .

Kinachoendekea kuhusu kesi ya Pistorius, Inadaiwa yupo katika hatari ya “kujiua”.
Ripoti ya daktari wa magonjwa ya akili iliyowasilishwa katika kesi dhidi ya Mwanariadha wa Afrika kusini, Oscar Pistorius, inaashiria kuwa anaugua msongo wa kimawazo na yumo katika hatari ya kujitoa uhai.
Ripoti hiyo iliyowasilishwa na wakili wake, inasema kuwa Pistorius yupo katika maombolezo ya mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Siku ya Jumatatu, mahakama ilielezwa kwamba Pistorius hana matatizo ya akili wakati alipompiga risasi mpenzi wake Steenkamp.
Pistorius anakanusha kutekeleza mauaji hayo, akieleza kuwa ilikuwa bahati mbaya kwakuwa alihofia kuwa nyumba yake imevamiwa.

Single mpya ya Madee umeipata?inaitwa Ni sheedah isikilize hapa.
Kwa mfumo wa muziki wa Madee huu anauita muziki wa Kwata ambao ni muunganiko wa Kwaito na Takeu ndio unautengeneza Kwata,single ya 3 kutoka kwake baada ya Pombe Yangu,Tema mate tuwachape na hii Nisheeeda.
Bonyeza play kusikiliza.
Bonyeza play kusikiliza.
Malalamiko ya Shilole kuhusu Dj wa Club anayetaka kumdhulumu Laptop yake.
Kutoka kwa Soudy Brown kupitia You heard ya leo Shilole amelalamika juu ya mtu anayedai kumuazima laptop yake lakini anaonekana ana dalili za kumdhulumu baada ya simu zake kuwa hapokei, amemtaja kwa jina la Dj Ommy Crazy ambae ni Dj wa Club.
Bonyeza play kusikiliza.
Bonyeza play kusikiliza.
Jinsi Beyonce alivyobadilisha mistari ya wimbo wake jukwaani kufuatia matatizo ya ndoa yake.
Wanandoa Beyonce na Jay Z wamekuwa wakipambana na uvumi kuwa sasa ndoa yao iko juu ya mawe kutokana na matatizo makubwa yanayoendelea tangu kusambaa kwa video ikimuonyesha dada wa Beyonce Solange akimshambulia Jay Z.
Na sasa Beyonce amezidi kupalilia moto zaidi kuhusiana na uvumi huo baada ya kubadilisha mistari kwenye wimbo wake kuhusu usaliti wakati akiwa jukwaani aki “perfom” kwenye ziara ya muziki na mume wake ya On The Run mjini Ohio.
Nyota huyo wa muziki wa R&B amesema kuwa Jay Z anaweza kuwa sio mwaminifu wakati akiimba wimbo wake uliotoka mwaka 2008, Resentment, ili kuendana na matukio yanayoendelea katika mahusiano yake na mumewe
Imekuwa ikivumishwa kuwa Jay Z yupo katika mahusiano ya nje ya ndoa na mwanamuziki Mya wakati wote si Jay wala Mya aliyejibu tuhuma hizo ambapo mashabiki wameendelea kuwafutilia kwa karibu hasa muziki wa Beyonce.

Angalia magoli 10 bora ya kombe la dunia – Messi vs Van Persie nani katisha?
Michuano ya kombe la dunia ipo kwenye hatua ya robo fainali ambayo itaanza rasmi Ijumaa hii. Michuano hii ya mwaka huu imekuwa na magoli mengi na bora katika historia ya michuano hii mikubwa kabisa katika soka.
youngluvega.com inakuletea video ya magoli 10 bora ya kombe la dunia kwenye hatua ya makundi.

Dar es salaam Julai 02, 2014, Gari hili la Magereza lapigwa risasi likiwa na wafungwa ndani.
Taarifa za awali zinadai kuwa Basi lililokuwa limebeba wafungwa limeshambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana eneo la Mayfair Mikocheni jijini Dar es salaam.
Basi hili lilikuwa likitokea mahakama ya Mwanzo Kawe ambapo kwasasa Basi hilo liko polisi Osterbay na wafungwa hao ndani yake.

Picha zote ni kutoka Ukurasa wa Twitter wa @Switi soleji
Taarifa ya Kaimu Balozi wa Libya, Tanzania aliyejiua kwa kujipiga risasi.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania leo imepokea taarifa kutoka ubalozi wa Libya nchini ikieleza kuwa aliyekuwa Kaimu Balozi wa Libya Bw. Ismail Nwairat, amefariki dunia jana kwa kujipiga risasi.
Taarifa hiyo ya ubalozi imeeleza kuwa kifo hicho kimetokea majira ya saa saba mchana ofisini kwa Kaimu Balozi huyo katika jengo la Ubalozi wa Libya ambapo imeelezwa kuwa marehemu alijifungia ofisini na kujifyatulia risasi kifuani upande wa kushoto.
Maafisa ubalozi walivunja mlango waliposikia mlio wa bunduki na kumkuta Kaimu Balozi Nwairat ameanguka chini na kuamua kumkimkimbiza hospitali ya AMI iliyopo Oysterbay ambako alitangazwa kuwa amekwishafariki dunia, kifo ambacho kimethbitishwa pia na jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam.
Mwili wa marehemu Nwairat umehamishiwa hospitali ya taifa Muhimbili na kwa sasa ubalozi unafanya maandalizi ya kusafirisha mwili wake kwenda nchini Libya kwa mazishi.

Mwanaume aliyebakwa baada ya kupanda lifti ya mtu asiyemjua.
Mwanaume mmoja amebakwa katika barabara ya daraja lenye shughuli nyingi mjini Newcastle baada ya kukubali kupanda lifti ya mtu asiyemjua.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 24 aliingia kwenye gari hilo dogo mapema alfajiri ambapo alifanyiwa kitendo hicho cha ubakaji katika eneo lenye nyasi nyingi karibu na daraja la Redheugh, Newcastle.
Timu ya uchunguzi wa makosa ya ubakaji hivi sasa inaendesha msako wa mtu aliyetekeleza kitendo hicho na kuwataka mashuhuda kujitokeza hadharani.
Afisa upelelezi kutoka mji wa Newcastle, Caroline Ord, amesema hili ni tukio baya zaidi kutendewa kwa kijana huyo ambapo sasa polisi wanafanya kazi bega kwa bega na mtu huyo kuhakikisha wanampata aliyetenda kosa hilo.

Mwanamke aliyelazimika kunyoa kipara baada ya nywele zake bandia kunasa kwenye Super glue.
Mwanamke mmoja Alexis Stanton amelazimika kunyoa nywele zote kichwani baada ya nywele zake bandia kunasa kwenye gundi aina ya super glue.
Mwanamke huyo alilazimika kubaki na kipara na majeraha kidogo ambapo amesema alifanya hivyo baada ya kujikuta nywele zake alizokuwa amebandika kichwani kunasa kwenye gundi ambayo ilishindikana kutoka.
Mwanamke huyo kutoka Newcastle anasema kuwa bado anahisi maumivu kwenye kichwa chake na kwamba amelia sana tangu tukio hilo lilipotokea na bado yupo kwenye majonzi makubwa
Amesema polisi wanamsaka mtaalamu wa saluni aliyemtengeneza nywele zake mara ya mwisho ambaye aliamini anajua kazi yake lakini badala yake alimwekea super glue badala ya gundi inayotakiwa kugandishia nywele zake.