Rais wa FIFA Sepp Blatter akimkabidhi rais wa Urusi Vladmir Putin Haki za kuandaa dimba la dunia la mwaka 2018
Madai zaidi yameibuka kuhusu
ufisadi uliofanyika wakati wa shughuli ya kuwatafuta waandalizi wa kombe
la dunia la mwaka 2018 na 2022.
Nafasi hizo zilichukuliwa na
Urusi pamoja na Qatar. Gazeti la Sunday Times nchini Uingereza limesema
kuwa rais wa Urusi Vladimir Putin alihusika pakubwa wakati nchi yake
ilipokuwa ikitafuta nafasi hiyo na hata alimuomba rais wa FIFA Sepp
Blattter kuisaidia kupata kura.Rais wa FIFA Sepp Blatter akiikabidhi Qatar mkataba wa kuandaa kombe la dunia la mwaka 2022.
Pia kuna madai kuwa nchi ya Qatar ilitumia ushawishi wake katika sekta ya gesi kupata kura kupitia kandarasi za kibiashara.
Urusi na Qatar zimekana kuhusika kwenye vitendo hivyo na ziliondolewa lawama na shirikisho la soka duniani FIFA hivi majuzi.