Ijumaa, 6 Novemba 2015

Mchumba Wangu Ameanza Kuvaa ''SHANGA" Miguuni...Nahisi Ameanza Kamchezo....

Nimekuwa kwenye mahusiano ya takribani miaka mitatu(3) sasa na msichana ambaye awali alikuwa yupo chuoni ila kwa sasa ni mfanyakazi taasisi fulani hivi (jina kapuni). Amepangiwa nje ya MKOA wa DAR nilipo.

Tulipoanza mahusiano haya hakuwahi kunionyesha anayonionesha hivi sasa.

Amekuwa akipost pictures mbalimbali akiwa amevaa ''vimini'' na ''vishanga (vikuku)'' miguu yote Miwili....

Nimejaribu kumuuliza nini MANTIKI ya hizo picha, kanijibu eti "...mbona kawaida tu,..

NIPO SO FRUSTRATED; ISIJE IKAWA KAANZA KALE KATABIA... MAANA NILISHA MTAMBULISHA KWA BAADHI YA NDUGU.

Mke wa Deo Filikunjombe Ampigia Kampeni Mdogo wa Filikunjombe Achukue Ubunge Jimbo Aliloliacha Mmewe..Adai Wengine Msiwasikilize Hawana Hata Mahali pa Kufikia Ludewa

Tanzania bado iko kwenye majonzi baada ya msiba wa aliyekuwa mbunge wa Ludewa,Deo
Najua kuna watu walikuwa na maswali juu ya atakayewaongoza wakazi wa Ludewa, sasa leo Novemba 5, 2015 mke wa marehemu Deo Filikunjombe ‘ Saraha’ ameyaandika maneno haya kupitia akaunti yake ya instagram kuhusiana aliyeteuliwa kugombea jimbo la Ludewa.

Nawaombeni wana ludewa wote kwa heshima nawaomba niwaambie ukweli kuwa huyu ndie anayeweza kuvaa viatu vya mume wangu mpendwa kwani mara nyingi amewahi kumchangia kaka yake ada za watoto tuliokuwa tunawasomesha huko ludewa naombeni msidanyike na maneno ya hao wagombea wengine mbona leo ndo wamekuja ludewa walikuwa wapi kujakuleta maendeleo mpaka iwe baada ya deo kufariki kati ya wagombea wote hakuna rafiki wa mume wangu’ – Saraha
‘hata mmoja tena kwa macho yangu nimewaona wakipewa misaada walete Ludewa na hawakufikisha na mara nyingi amelalamika na kuwaomba jamani tupeleke maendeleo nyumbani hakuna aliesikia hata mmoja ndo maana hawana nyumba ya kufikia matokeo yake wanawaomba kura ilingali hata hawana pakufikia wamefikia nyumba ya kulala wageni mkitaka kumwona mbunge mta mkuta wapi tuwemakini Deo amefanya mengi mpeni mdogo wake amalizie aliyoahidi asanteni sana wanaludewa niwaganili sana mdalikhe sana ccm hoyeeeeeeechagua ccm chagua Philipo filikunjombe hapa kazi tu’ – Saraha

Rais Kikwete Aachia Madara Kistaili...Awasamehe Wafungwa 4,160 Watoke Gerezani

RAIS mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete ametoa msamaha kwa wafungwa 4,160 katika kuaga na kukabidhi madaraka ya Serikali kwa Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli.

Dk Magufuli aliapishwa jana kuwa Rais wa Tano wa Tanzania katika sherehe zilizofana kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam huku Kikwete akimaliza miaka yake 10 ya kuongoza nchi kama ilivyoelekezwa na Katiba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe kwa vyombo vya habari jana Dar es Salaam, kati ya wafungwa hao, wafungwa 867 wataachiwa huru na wafungwa 3,293 watapunguziwa vifungo vyao na kubaki gerezani wakitumikia sehemu ya vifungo vyao vilivyobaki.

“Ni mategemeo ya Serikali kwamba wafungwa watakaoachiwa huru watarejea katika jamii kushirikiana na wananchi wenzao katika ujenzi wa Taifa na watajiepusha na utendaji makosa ili wasirejee tena gerezani,” alisema Chikawe katika taarifa hiyo.

Chikawe aliwataja walionufaika na msamaha huo kuwa ni wafungwa wote wapunguziwe moja ya sita ya vifungo vyao zaidi ya punguzo la kawaida linalotolewa chini ya Kifungu cha 49(1) cha Sheria ya Magereza Sura ya 58 isipokuwa wafungwa walioorodheshwa katika ibara ya 1 (i-xix).

Aliwataja wengine kuwa ni wafungwa wagonjwa wenye magonjwa kama Ukimwi, kifua kikuu, saratani ambao wako kwenye hatua ya mwisho ambao watathibitishwa na waganga chini ya Mganga mkuu wa mkoa au wilaya.

Pia wazee wenye umri zaidi ya miaka 70, wafungwa wa kike walioingia na mimba gerezani na walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya na walemavu wa mwili na akili na ulemavu huo uthibitishwe na jopo la waganga.

Kwa mujibu wa Chikawe, msamaha hautawahusu wafungwa wenye adhabu za kunyongwa, waliohukumiwa kunyongwa na adhabu hiyo baadaye kubadilishwa kuwa kifungo cha maishaau kifungo gerezani.

Wengine ni wafungwa waliotumikia kifungo kwa makosa ya usafirishaji na utumiaji wa dawa za kulevya, makosa yanayohusu uombaji, upokeaji na utoaji rushwa, unyang’anyi na kujaribu kutenda makosa hayo, kubaka, kulawiti au kujaribu kutenda makosa hayo.

Aidha, makosa mengine ambayo vifungo vyake haviko kwenye msamaha huo ni makosa ya kuwapa mimba wanafunzi, wizi wa magari, pikipiki au kujaribu kutenda makosa hayo, matumizi mabaya ya madaraka, waliowahi kupunguziwa vifungo na Rais.

“Wengine ni waliopatikana na hatia kwa kuwazuia watoto kupata masomo, utekaji watoto, usafirishaji binadamu, ukatili dhidi ya albino, usafirishaji nyara za Serikali na ujangili,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Mengine ni wanaotumikia vifungo kwa makosa ya wizi na ubadhirifu wa fedha za Serikali, kutoroka au kujaribu kutoroka wakiwa chini ya ulinzi halali na wafungwa wanaotumikia vifungo chini ya Sheria ya Bodi ya Parole Sheria Namba 25 ya Mwaka 1994 ya Sheria ya Huduma kwa Jamii Namba 6 ya Mwaka 2002.

Nchi Ina Wanafiki Sana wa Kisiasa...Ukawa Wamsusia Magufuli Uwanja wa Taifa ila Bungeni Wamejiandikisha Kwenda Kumsikiliza Kwasababu Kuna Posho-Habibu Mchange


Mwanasiasa Habibu Mchange Ameandika yafutayo katika ukurasa wake wa Facebook kuhusu Ukawa:

'Nchi ina WANAFIKI SANA WA KISIASA HII..
Ukawa wamesusia kuapishwa Rais lakini UKAWA HAO HAO wameenda Bungeni kujiandikisha kama watahudhuria hotuba ya Rais BUNGENI na wamelipwa posho inayoendana na shughuli hiyo. sasa hii ndio kusema Baniani Mbaya kiatu chake Dawa ama? Au kwa kuwa Uwanja wa Taifa hakukuwa na POSHO?.. kungekuwa na POSHO kama kawa asingesusa mtu?...ukiamua kususa unasusa jumla sio nusu nusu. Utapeli wa kisiasa wa namna hii haufai..wangesusia vyote! 
By Habibu Mchange

Maalim Seif Aweka Ngumu Adai Hawawezi Kurudia Uchaguzi Zanzibar

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema CUF inaendelea kutafuta haki ya Wazanzibar ya kutaka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec) kuendelea kutangaza matokeo ya uchaguzi ili mshindi ajulikane na hatimaye kuapishwa.

Aliyasema hayo wakati akizungumza na wafuasi wa chama hicho katika makao makuu ya CUF Mtendeni juzi, baada ya kurudi safari yake ya kuonana na rais wa awamu ya nne, Dk. Jakaya Kikwete, Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Aliwaambia wanachama hao kuwa hakuna kurudi nyuma katika kudai haki yao kwa njia ya amani na utulivu ili matokeo yatangazwe na mshindi wa urais ajulikane.

“Niwahakikishieni vijana na wanachama wa CUF kuwa hakuna kurudi nyuma, tunaendelea kudai haki yetu na tunashukuru dunia nzima inatuunga mkono kwa hili,”alisema Maalim Seif, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK).

Alisema kuwa wapinzani wao, Chama Cha Mapinduzi (CCM) mpango wao ni kutaka kuendelea kuwa katika madaraka wakijua kuwa muda wa Dk. Ali Mohammed Shein wa kukaa madarakani umekwisha, lakini wanang’ang’ania aendelee kinyume cha Katiba.

Aidha, alisema kuwa hakuna dawa yoyote ya kumaliza mgogoro ulipo Zanzibar isipokuwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec) kuendelea kutoa matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka huu ili mshindi ajulikane na kuapishwa.

“Wanaosema kuwa uchaguzi urejewe waachieni wenyewe, sisi katika CUF hakuna msamiati huo kwa sasa kurejea uchaguzi, huo ndio msimamo wetu,” alisisitiza Maalim Seif.

Alisema kuwa kwa uwezo wa Mungu haki yao wataipata na kuwataka vijana kuendelea kuwa watulivu na kuendelea kutunza amani ya nchi kwa kutokubali kuchokozeka. Alisema CUF na viongozi wake hawatakubali kuwa chanzo cha kuvuruga amani ya nchi na wataendelea kuhubiri amani wakati wote.

Mvutano wa kisiasa unaoendelea Zanzibar ulisababishwa na Mwenyekiti wa Zec, Jecha Salim Jecha, kutangaza kufuta uchaguzi wa Zanzibar wa rais na wawakilishi Oktoba 28, kwa madai kuwa ilibaini kuwapo kwa kasoro kadhaa kisiwani Pemba.

Hata hivyo, waangalizi wa nje na ndani wameeleza kushangazwa ha hatua ya Jecha, kwa kuwa hawakushuhudia kasoro zozote hadi walipotoa ripoti ya awali.

Aidha, asasi za nchini na mataifa kadhaa yakiwamo Uingereza, Ireland na Marekani yameshatoa taarifa ya kushangazwa na uamuzi wa Jecha na kushauri mchakato wa kutangaza matokeo uendelee.

MTOTO WA KARUME AIBUA MAPYA
Mjadala kuhusiana na hatma ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliofutwa na Jecha, umechukua sura mpya, baada ya mmoja wa watoto wa Rais wa zamani, Dk. Amani Abeid Karume, kuibuka na kufichua kile anachoamini kuwa ni sababu ya utata uliojitokeza sasa.

Mtoto huyo ni Mwanasheria, Fatma Karume, ambaye akiwa pamoja na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Zanzibar (ZLS), Awadh Ali Said, waliuambia umma kupitia mahojiano ya moja kwa moja kwenye kituo kimoja cha televisheni jijini Dar es Salaam juzi kuwa sababu mojawapo ya kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar ni muundo wa uongozi unaomruhusu rais wa visiwa hivyo kuwa mmoja wa wajumbe katika Baraza la Mawaziri la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akifafanua, Fatma alisema kuwapo kwa nafasi ya moja kwa moja ya Rais wa Zanzibar kwenye Baraza la Mawaziri kunaibua mgongano inapotokea mshindi wa upande mmoja akiwa ni wa kutoka chama kingine na hiyo ni sababu mojawapo wanayoamini kuwa imechangia kufutwa kwa uchaguzi na pia kukwaza ukuaji wa demokrasia visiwani humo.

Alisema ni dhahiri hali huwa ngumu kwa baraza la mawaziri linaloundwa na watu wa itikadi ya chama kimoja kuchanganyika na mwingine mwenye itikadi tofauti, hasa katika mazingira ya kuwa na usiri katika baadhi ya mambo na kwamba, hilo huchangia kusuasua kwa maendeleo ya kidemokrasia visiwani Zanzibar.

Hata hivyo, ili kuondokana na mgogoro kama uliopo sasa, Fatma alisema ni muhimu kwa viongozi wa kisiasa nchini na kwingineko barani Afrika kuzingatia sheria na katiba zilizopo.

Awali, ilisisitizwa na wanasheria hao kuwa uamuzi wa kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar uliochukuliwa na Mwenyekiti wa Zec peke yake, haukuzingatia sheria na katiba na ndiyo maana sasa kumeibuka mgogoro wa kikatiba kwani kifungu kinachotumika kuhalalisha hoja ya kuendelea kubaki madarakani kwa Dk. Shein kimekuwa kikitafsiriwa vibaya kwa maslahi ya kisiasa.

Akielezea zaidi, Awadh alisema hakuna kifungu chochote kinachomruhusu Jecha kufuta uchaguzi na ndiyo maana hadi sasa hakuna mtu aliyethubutu kutaja kwa uwazi ni sheria ipi imempa nguvu mwenyekiti huyo wa Zec kufuta uchaguzi wa Zanzibar.

Source: Nipashe

Luis Munana Afichua Siri ya Jinsi Alivyojikuta Akipendana na Wema Sepetu

Wiki iliyopita picha za mtandaoni zilionesha kuwa Wema Sepetu na mshiriki wa Big Brother Hotshots kutoka Namibia, Luis Munana wamefunga ndoa.

Hakuna taarifa rasmi kutoka kwa wawili hao baada ya ‘ndoa’ hiyo kufungwa lakini Luis ameimbia Clouds E ya Clouds FM kuwa picha zilizosambaa n halisi na zilipigwa kwenye tukio hilo lililoshuhudiwa na familia zao zote mbili.

“Kwa sasa siwezi kuzungumzia chochote kuhusu picha hizo na ndio maana niliamua kuzifuta kwenye akaunti yangu kwakuwa lilikuwa tukio la faragha,” alisema Luis.

Luis alisema alikutana na Wema kwenye Instagram Party na kubaini kuwa wote walikuwa wakipendana bila kujua. “Alikuwa crush wangu, nami nilikuwa crush wake,” alisema.

Edward Lowassa/Zitto Kabwe Wapeleka Kilio CCM

Hawa jamaa wawili kwa kweli kwa pamoja tunaweza kusema wamepeleka kilio mtaa wa Lumumba, waswahili husema kwa mjinga huenda kicheko lakini kwa mwelevu huenda kilio.

Ujio wa Lowassa UKAWA umepeleka kilio kikubwa sana CCM japo kuwa wanajikazakinyasa wanakufa na Tai shingoni. Majuzi Mh. January Makamba aliita waandishi wa habari na kujinasibu eti CCMimepata wabunge 176 mpaka sasa na kufanikiwa kugomboa majimbo 11 yaliyokuwa yawapinzani.

Sasa habu ona hapo chini kilio Lowassa alichokipeleka CCM ambacho Makamba hakupenda kutaja.

1. Viti maalumu vya CCM vimepungua kwa 40% toka 79bunge lilopita la10 mpaka 62 bunge la11. Wakati CHADEMA na CUF viti hivyo vimeongezeka haya ni maumivu makubwa

2. CCM imenyang`anywauongozi wa majiji 4 kati ya majiji 5imebakiwa na uongozi katika jiji moja tu la Mwanza,. Majiji yafuatayo CCM nichama cha upinzani , Jiji la Mbeya, Jiji kuu la Dar-es-Salaam, Jiji la kitaliila Arusha na jiji la Tanga ambalo ilikuwa ni ngome yao, ngome imevunjwa.

3. Ruzuku ya CCM imepungua kwa 40% kutokana na kuraza rais alizopata , mgao wa ruzuku utakuwa 60 kwa 40 kwa maana 58% alizopataRais Magufuri kwa desilimali ya karibu itakuwa 60, na 39.8% ya kura za Lowassaalizopata kwa desilimali ya karibu itakuwa 40. Kwa hiyo CHADEMA imeinya`anyaCCM 20% ya ruzuku, je! Siyo maumivu hayo?

4. Uongozi wa halmashauri ndiyo usiseme. Kabla yaLowassa halmashauri zilizokuwa zinaongozwa na wapinzani zilikuwa 5 sasahalmashauli hizo zimeongezeika na kufika 30, katika halmashauri hizo CCMwatakuwa bachbancher.

5. Kilio kikubwa zaidi ni cha Zitto Kabwe alichowapaCCM katika halmashauri ya Kigoma/ujiji. Katika halmashauri hii hakuna mkuu wawilaya au mkuu wa mkoa kutia pua, halmashauri hii ni mali ya Zitto Kbakwe kwamaana ya Meya hadi madiwani. Halmashauri hii mwenyekiti wa CCM au mkuu wawilaya au mkuu wa mkoa wataenda kufanya nini? Wakati wakuu hao wameng`ang`anakumnyang`anya Kafulila ubunge wake huku nyuma Zitto anachukua halmashauri ya mjini,shame on them

6. Kuna kilio manispaa ya Mtwara/Mkindani na Mtwaravijijini kwa Hawa Ghasia, huenda Umeya wa Shilingi na wa Ndazigula umeotambawa.

Haya ndo ilitakiwa Mh. January Makamba ayaseme katika kile kikao chawaandishi wa habari alichokiitisha.

Source: ebaeban/Jamii Forums

TB Joshua ni Mgeni wa Nani Nchini Tanzania? Maswali Yazidi Baada ya Kutoonekana Uwanja wa Taifa Katika Sherehe za Kuapishwa

Kinyume na ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari Hajaonekana kwenye sherehe za kupishwa kwa Mh. Rais na wala jina Lake halikuwemo kwenye orodha ya wageni.

Hivi majuzi muhubiri maarufu kutoka nchini Nigeria TB Joshua aliwasili nchini kwa kile kilichoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari ikiwemo gazeti la Mwananchi kwamba muhubiri huyo amekuja nchini kushuhudia kupishwa kwa Rais Dr. John Pombe Magufuli.

Alipowasili uwanja wa ndege hapa Tanzania alipokelewa na baadhi ya viongozi walioongozwa na Dr. John Pombe Magufuli na akaenda moja kwa moja kumsalimia Rais Kikwete Ikulu magogoni Dar es Salaam.

Baada ya kutoka Ikulu muhubiri huyo alielekea nyumbani kwa aliyekuwa mgombea urais wa UKAWA na waziri mkuu mstaafu Mh. Edward Lowassa eneo ambalo ameonekana kuwepo kwa Muda mrefu akizungumza na Lowassa na viongozi wengine wa UKAWA.

MASWALI

1. Je, ujio wa Muhubiri huyo ilikuwa ni msafara binafsi Kinyume na ilivyoripotiwa na vyombo vya habari?

2. Vyombo vyetu vya habari havikupewa taarifa sahihi kuhusu sababu za ujio wa kiongozi huyo?

3. Kama ni msafara binafsi kwanini apokelewe na rais mteule na kutembelea Ikulu?

4. Je ni viongozi wa UKAWA wamemzuwia kuhudhuria sherehe hizo za kupishwa Rais kutokana na wao kugomea kusaini matokeo?

5. Je, bado yupo nchini? Maana kama tulijulishwa kuhusu ujio wake si vibaya tukajuzwa kuhusu kuondoka kwake.

Nawasilisha:

Forget About Zari ! .....Lulu And Diamond In Love !.....His Family Wants Him To Marry Lulu ?

Hot gossip is that, Lulu Elizabeth Michael and Diamond Platnumz are in love secretly and Diamond's family has no problem about it. This comes after reports broke Diamond and his baby mama Zari The Boss Lady are in bad terms. Reports further say that Zari frequently saw Lulu's messages to Diamond ones of them being so romantic, and when Zari questioned Diamonds sisters kept telling Lulu and Diamond's are close friends for a long time.

Recently gossip and entertainment newspapers and blogs have been reporting Lulu and Diamond's so sudden closeness, even during Romy Jonesi birhday(Diamond's cousin) Lulu spent most of her time with Diamond and weeks later which was Diamond's birthday the two were together most of the time too.

When Diamond's sister Esma Platnumz approached by GPL paparazzi to give a comment on Lulu and Diamond's friendship she had this to say "yeah, you guys we have told you our brother(Diamond) has no problem with anyone, to Lulu he has no problem their relationship is open, first of all Lulu is beautiful, she is cool and she has what it takes to be someone's wife, we have no problem with her, if she and Diamond agree to one another we will welcome her warmly" said Esma

When Diamond asked he replied "please these are family issues, sometimes it is better to let somethings pass as they are, I have been close to Lulu for a long time, let it be that and end there"

After Diamond, paparazzi started looking for Lulu and finally the talented actress was spotted at Wema Sepetu's birthday over the weekend. When Lulu asked about being in love with Diamond she denied it claiming she can't do it because Diamond used to date Wema Sepetu "to date Diamond ! where can I start ?, and how could I have come here at Wema's birthday while Diamond is Wema's ex ?, nothing like that, he is my close friend"

 Leave that alone, Recently it was reported Lulu and Wema were in cold war because Wema was unhappy the way Lulu supports Diamond in every move let alone their closeness which frightened Wema who used to date Diamond and rumors suggest Wema still loves Diamond despite their separation. However Lulu attended Wema's Royal birthday over the weekend and they were snapped together.

Do you believe Lulu and Diamond are new couple in town ?