Alhamisi, 24 Julai 2014

Ban Ki Moon asema Iraq inapaswa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa

Watu waliokuwa na silaha wameushambulia msafara uliokuwa umewabeba wafungwa kaskazini mwa mji mkuu wa Iraq, Baghdad, na kusababisha makabiliano makali na majeshi. Wafungwa zaidi ya 50 na wanajeshi kumi wameuawa katika shambulizi hilo lililodhihirisha hali ya kutokuwa na amani nchini Iraq. Hii ni hata baada ya wabunge kumchagua leo mwanasiasa kigogo wa Kikurdi Fouad Massoum...

Ndege ya abiria ya Algeria yaripotiwa kuanguka kaskazini mwa Mali

Maafisa wa Jeshi wa Burkina faso wamesema ndege hiyo iliyokuwa chini ya shirika la ndege la Algeria imeanguka karibia kilomita 50 kutoka mpaka wa Burkanafaso. Waongoza ndege walipoteza mawasilino na ndege hiyo muda mfupi baada ya kupata taarifa kutoka kwa Rubani kuwa alikuwa kwenye eneo lenye hali mbaya ya hewa. ...

Mnigeria aliebeba dawa za kulevya alivyokamatwa Nairobi baada ya rubani kuugua.

Mwanamume mmoja Raia wa Nigeria imebidi alazwe kwenye hospitali ya taifa ya Kenyatta Nairobi Kenya baada ya kugundulika alikua na mzigo wa dawa za kulevya wa vidonge 57 tumboni mwake. Huyu jamaa alikua anazisafirisha hizi dawa kutoka Lagos kwenda Bangkok lakini ghafla akaanza kupata maumivu baada ya kuchelewa kufikisha mzigo aloubeba tumboni mwake baada ya ndege waliyokua...

Mwanamke wa Sudan aliehukumiwa kifo kwa kuolewa na Mkristo amewasili Italia.

Huyu wa kwanza kushoto aliembeba mtoto ni Makamu wa waziri wa mambo ya nje ya Italy Lapo Pistelli Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Pope Francis Alhamisi ya July 24 2014 nchini Italia amekutana na Meriam mwanamke wa Sudan ambae alihukumiwa kunyongwa nchini Sudan kwa kosa la kuolewa na mume Mkristo mwaka 2011. Meriam na watoto wake wawili akiwemo huyu wa mwisho aliezaliwa...

Ratiba ya Serengeti Fiesta 2014 imetoka mdau wangu..

Fiesta ni tamasha linalowakutanisha wasanii mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania kwenye msimu wa mafanikio pamoja na mashabiki wao kila mwaka ambapo kwa mwaka huu kuna mikoa kadhaa imeongezeka. Kupitia show ya XXL, Sebastian Maganga ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fiesta 2014 amesema mwaka huu kuna mikoa minne imeongezeka lakini kwa utangulizi kwa kanda ya ziwa...

NDEGE NYINGINE YAPOTEA HUKO ALGERIA

Maafisa wa masuala ya anga nchini Algeria wanasema wamepoteza mawasiliano na ndege ya shirika la ndege la Air Algerie, iliyokuwa katika anga ya Sahara. Shirika la habari za Algeria limesema ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kwenda Algiers na kupotea kwenye rada takriban dakika 40 baada ya kupaa kutoka jijini Ouagadougou, mji mkuu wa Burkina Faso. Air Algerie imesema imeanza...

TETESI ZA SOKA ULAYA

Liverpool wapo tayari kumfuatilia tena Ryan Bertrand, 24, kutoka Chelsea, wakati Brendan Rodgers akisaka beki wa kushoto (Daily Mail) kiungo wa Borussia Dortmund Marco Reus, 25, na beki wa Southampton Dejan Lovren, 25, ni miongoni mwa wachezaji Brendan Rodgers anawafuatilia (Daily Mirror) Everton wanakaribia kumsajili Muhamed Besic, 21, kutoka Bosnia (Daily Mirror),...

Sakata la Viungo vya Binadamu kutupwa Dar, Chama cha Madaktari chataka Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Matibabu na Teknolojia (IMTU) Kifungwe

Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kimesema Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Matibabu na Teknolojia (IMTU)  sanjari na hospitali iliyo chini yake, vinastahili kufungiwa.   Tamko hilo la chama limekuja huku mamlaka mbalimbali zinazohusika na usimamizi wa karibu wa vyuo vikuu vya matibabu zikikiweka chuo hicho kiporo,  kusubiri uchunguzi wa tuhuma zinazokikabili...

Binti wa SUDAN aliyehukumiwa kifo kwa kuasi dini ya UISLAMU ahamishiwa ITALIA

Meriam Ibrahim akiwa na mumewe Daniel Wani pamoja na mtoto wao wa kwanza. MWANAMKE wa Sudan aliyehukumiwa kifo kwa kuasi dini ya Kiislamu na kuolewa na Mkristo, Meriam Ibrahim, amesafirishwa kuelekea Italia baada ya kukaa ubalozi wa Marekani mjini Khartoum, Sudan kwa zaidi ya mwezi mmoja. Meriam na familia yake wameondoka na ndege ya Serikali ya Italia wakisindikizwa...

Kiiza, Okwi, Twite, Niyonzima, nani kumpisha mbrazil Genilson Santos ‘Jaja’ Yanga?

Kuwasili kwa wabrazil wawili katika klabu ya Yanga kumeweka rehani ajira za wachezaji Emmanuel Okwi, Hamis Kiiza, Mbuyu Twite na Haruna Niyonzima kwasababu mmoja wao inabidi atemwe ili timu hiyo iweze kutimiza masharti ya kuwa na wacheza kigeni watano tu. Lakini kwa mujibu wa taarifa zilizopo ni kwamba Kiiza ndio atatemwa na kumpisha mshambuliaji  Genilson Santos...

Magazeti ya leo July 24 2014

. Kama kawaida youngluvega.blogspot.com inakupa vichwa vya habari vya magazeti yote ya kila siku. Leo pia kuna headline mpya kwenye magazeti mbalimbali. Chukua muda wako kupitia kila kilichoandikwa kwenye kurasa za mbele za magazeti ya leo. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . ...