Ijumaa, 5 Desemba 2014

MKUU WA USALAMA WA CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHINA AKAMATWA

 
Aliyekuwa mkuu wa usalama nchini China Zhou Yongkang amefukuzwa kutoka Chama cha Kikomunisti na atafunguliwa mashtaka huku kukifanyika uchunguzi wa ufisadi. Zhou alikuwa kiongozi wa kitengo cha usalama cha China kabla ya kustaafu miaka miwili iliyopita na atakuwa kiongozi wa ngazi ya juu kabisa chamani kutuhumiwa kwa madai ya ufisadi na kufunguliwa mashtaka. Uamuzi wa kumkamata na kumtimua afisa huyo mkuu wa Kamati kuu ya chama cha Kikomunisti yenye wanachama 9 ulifikiwa katika mkutano wa baraza kuu la chama hicho lenye wanachama 25 hapo jana, kufuatia uchunguzi rasmi uliofanyika mapema mwaka huu. Zhou anatuhumiwa kwa uhalifu ikiwa ni pamoja na "kukubali kiasi kikubwa cha hongo" na "kujihusisha na vitendo vya uasherati na wanawake kadhaa". Washirika na jamaa kadhaa wa Zhou pia wanachunguzwa kwa madai ya rushwa.

Mahakama ya ICC imetoa hukumu ya kesi iliyokuwa inamkabili Rais Kenyatta

ICC
Mahakama ya Kimataifa ya ICC imetupilia mbali kesi ya jinai iliyokua inamkabili Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta kutokana na kutokamilika kwa ushahidi.
Mwendesha mkuu wa mashitaka Fatou Bensouda ameondoa kesi dhidi ya Kenyatta ambaye alidaiwa kutenda uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa ghasia baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya.
Katika Taarifa iliyotolewa na mahakama hiyo iliyopo nchini Uholanzi imesema kesi yake haikua na ushahidi wa kutosha wa Kenyatta kuhusika moja kwa moja na mauaji ya maelfu ya Wakenya wakati wa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.
Kenyatta alishtakiwa kama mshukiwa mkuu wa ghasia baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/2008 akituhumiwa pamoja na William Ruto ambaye ni Makamu wa Rais ambapo maelfu ya wananchi walipoteza maisha.

Maadhimisho ya Mwaka mmoja tangu kufariki kwa shujaa wa Afrika, Nelson Mandela…

Mandela-superJumbo 
Ni mwaka mmoja tangu Mzee Nelson Mandela alipofariki dunia, wananchi wameedhimisha mwaka mmoja toka waondokewe na kiongozi huyo ambaye aliiongoza nchi hiyo kutoka mikononi mwa Makaburu baada ya kufungwa miaka 27 jela.
Maadhimisho hayo yametanguliwa na ibada ya maombi ambapo wamekaa kimya kwa dakika tatu, na kisha kuweka mashada za maua wakiongozwa na wazee waliopigana na makaburu wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi, kumekuwa na upulizaji wa vuvuzela nchini kote, kugonga kengele, ngoma, na kutakuwa na mechi ya mchezo wa kirafiki wa kriketi.
Mandela alikuwa Rais wa kwanza mzalendo kuiongoza Afrika Kusini kwa kipindi cha muhula mmoja wa miaka mitano kuanzia mwaka 1994 hadi 1999 alipoachia madaraka kwa hiari yake mwenyewe.
Maduka mengi ya kuchora Tatoo Nchini humo yameripoti ongezeko la watu wanaochora Tatoo za picha ya Mandela.
“… Kimwili hatuko nae lakini kiroho Mandela tuko nae siku zote mpaka mwisho haijawahi kubadilika, Madiba kiroho tuko nae kila siku, najua Madiba anatabasam, Madiba anafurahi kwa sababu yeye ni miongoni mwa familia aliyochagua kuijenga”, alisema Mjane wa Mandela, Grace Machel.
Mshindi wa tuzo ya Amani ya Nobel, Desmond Tutu katika maadhimisho hayo ametoa wito kwa wananchi Afrika Kusini kuiga mfano wa Mandela.
_79522568_79522567
_79522157_79522156
_79522564_79522158