
SERIKALI ya Awamu ya Tano imeanza kutekeleza kwa vitendo azma yake ya kujenga uchumi unaotegemea viwanda baada ya kuzindua ujenzi wa mradi maalumu wa uwekezaji wa viwanda mkoani Morogoro ili kukuza uchumi na kuongeza ajira nyingi kwa vijana nchini.
Utekelezaji huo ni kutokana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage juzi kuzindua eneo maalumu la ujenzi...