Jumamosi, 29 Novemba 2014

DIAMOND PLATNUMZ ANYAKUA TUZO 3 ZA CH0AMA14

 
Tar 29 Noember ni siku ambayo imewekwa historia kwenye tasnia ya muziki wa bongo fleva baada ya Diamond Platnumz kuchukua tuzo tatu za chanel O, pia ni historia kwa Afrika nzima.
Diamond alikua ametajwa kwenye vipengele vinne. Vipengele hiyo ni pamoja na Most Gifted East Video, Most Gifted Afro Pop video na Most Gifted Newcomer.
Kwenye tuzo hizo Diamond amefanikiwa kuwapiku wasanii nguli wa Afrika  wakiwemo Iyanya, Daido, Flavor, Mafikizolo na Sauti Sol.

 "TANZANIA STAND UP! HE DID IT! @ diamondplatnumz", amepost Davido



Ifahamu idadi ya majeraha kwa Manchester United.

2397624900000578-2854114-image-12_1417275965806
Unapozungumzia suala la majeraha ya wachezaji bila shaka mashabiki wa Manchester United wanapata homa ya ghafla .
Hii ni kwa sababu timu hii imekuwa na orodha isiyoisha ya wachezaji wenye majeraha .
Mbaya zaidi ni kwamba kila orodha hii inapoonyesha dalila za kungua mchezaji mwingine anaemia na inazidi kuwa ndefu .
239764A900000578-0-image-5_1417275401405
Orodha hii iliongezeka kwenye mchezo dhidi ya Hull City wakati ambapo kiungo mshambuliaji Angel Di Maria alipoumia misuli ya nyonga kwenye dakika ya 14 ya mchezo na kulazimika kutoka.
Bado haijafahamika Di Maria atakaa nje ya uwanja kwa muda gani lakini kwa kawaida jeraha kama hili huhitaji kati ya siku 7 mpaka 10 ili kupona na wakati mwingine kuendana na ukubwa wake linaweza kuhitaji muda mrefu zaidi .
2397647A00000578-2854114-image-11_1417275874223
Kwa jumla Jeraha la Di Maria ni jeraha la 41 kwa mchezaji wa Manchester United kwa msimu huu tangu kuanza kazi kwa kocha Mholanzi Louis Van Gaal .
Idadi hii ndio idadi kubwa ya majeraha kwa wachezaji kwa timu yoyote ya ligi kuu ya England msimu huu hali inayowafanya United waamini kuwa huenda timu yao ina mkosi wa aina Fulani.
239745C000000578-2854114-image-21_1417276088569     

Haya hapa majina yaliyoteuliwa na PAC kuandika maazimio ya kuwawajibisha watuhumiwa wa Escrow

PAC 
Baada ya Spika wa Bunge kuahirisha Bunge mara mbili siku ya leo Novemba 29 ili kuipa nafasi kamati ya PAC iweze kufanya marekebisho ya maneno yaliyoandikwa kwenye maazimio yaliyowasilishwa na Kamati ya PAC, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Zitto Kabwe ametaja majina ya walioteuliwa na Kamati hiyo kuandika maazimio ya kuwajibisha watuhumiwa wa Tegeta Escrow.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook (@Zitto Kabwe) ameandika majina ya wajumbe hao.
Zitto Leo

Kilichosemwa na Kamanda Kova na Waziri Lazaro Nyalandu kuhusu ajali ya Helikopta

Name:  jf2.jpg
Views: 0
Size:  163.2 KB

Taarifa ambayo imeripotiwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ni kuhusu watu wanne kufariki kutokana na ajali ya Helikopta inayomilikiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, yenye namba 5HTWA kuanguka katika eneo la Kipunguni B, Ukonga Dar es salaam.
Akizungumza na kituo cha ITV Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kutoa taarifa kamili juu ya tukio hilo muda mfupi ujao.
 Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Waziri wa Maliasili na Utalii  ameandika hivi; “Naelekea Dar kutokea Dodoma kwenda kwenye eneo la tukio la ajali ili kuwapa pole wafiwa. Nitazidi kuwafahamisha.”
Name:  jf.jpg
Views: 0
Size:  178.8 KB                      Muonekano wa Helikopta eneo la tukio

Hiki ndicho alichokiongea yule Msichana aliyempiga Mtoto Uganda.

baby021
Baada ya story ya yule msichana kwa anayefanya kazi za ndani Uganda kuchukua headlines katika vyombo mbalimbali vya Kimataifa Duniani, leo kipo ambacho amekizungumza kwa mara ya kwanza tangu afanye kosa hilo.
Msichana huyo Jolly Tumuhiirwe ambaye kwa sasa amekamatwa na Polisi amesema sababu iliyomfanya amtese mtoto Arnella Kamanzi, ni kutokana na kuchanganyikiwa baada ya waajiri wake kutompatia pesa ili amtumie baba yake ambaye alikuwa anaumwa.
Amesema anajiona mwenye hatia kwa alichokifanya japo anadhani alifanya hivyo kama njia ya kumkanya mtoto huyo kwa kuwa alikuwa akimuona mama wa mtoto huyo akimpiga kama njia ya kumkanya.
Jolly amelalamika kuwa anajisikia vibaya pale ambapo wafungwa wenzake wamekuwa wakimtenga sana na kutaka kumpiga.