Jumanne, 30 Septemba 2014

Raila Odinga atandikwa kiboko

 
Raila Odinga alichapwa mara mbili kwa kiboko katika tukio ambalo limewashangaza wengi 
Hali ya taharuki iliibuka katika mkutano wa hadhara katika jimbo la Kwale nchini Kenya, baada ya mwanamume mmoja kwenda ukumbini na kuanza kutandika bakora kiongozi wa upinzani Raila Odinga pamoja na wanasiasa wengine.
Raila alikuwa amejiunga na kikundi cha wanawake waliokuwa wanacheza densi ya kitamaduni kuwatumbuiza wageni, pamoja na gavana wa jimbo la Kwale Pwani ya Kenya Salim Mvuruya katika mkutanmo wa kisiasa.
Walikuwa wameambatana na viongozi wengine, wakiwemo, Seneta Juma Boy, Hassan Omar, Agnes Zani, James Orengo, Johnstone Muthama na wengineo.

 
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga 

Mwanamume huyo alimshambulia Odinga ambaye ni waziri mkuu wa zamani na kumchapa mara mbili kabla ya kumgeukia gavana wa jimbo hilo na pia kumchapa mara mbili. Hata hivyo mwanamume huyo alishindwa nguvu na walinzi wa Raila Odinga.
Polisi walithibitisha kuwa walimkamata mwanamume huyo na kumwachilia baada ya kugundua kuwa alikuwa na matatizo ya kiakili.
Haijulikani kwa nini mwanammume huyo alimshambulia Raila ila baadhi wabnasema ni kwa sababu alighadhabishwa pale waziri mkuu alipocheza densi na mwanamke aliyesemekana kuwa mke wake ambaye alikuwa katika kikundi cha wanawake waliokuwa wanawatumbuiza wageni waheshimiwa.
Viongozi waliofika walilazimika kusitisha densi hiyo kabla ya mwanamume huyo kushindwa nguvu.

Eti umoja wa Ma-Girlfriend wamekuja na hii baada ya Diamond kutoa zawadi ya Gari kwa Wema…

zawadi 
September 26 ilikua ni siku ambayo mrembo kutoka Tanzania Wema Sepetu alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo ndani ya siku yake hii ukitoa party aliyoifanya kulikuwa na vitu mbalimbali vya kuvutia.
Siku hiyo Diamond platnumz aliamua kumzawadia zawadi ya gari mpenzi wake Wema Sepetu gari aina ya Nissan Murano ambapo alipost instagram na kuandika maneno yafuatayo yaliyoambatana na picha ya zawadi hiyo.
zawadi
msg 
Mbali na zawadi aliyoitoa Diamond Platnumz ya gari hilo pia Meneja wake Martin Kadinda nae alimpatia Wema Sepetu zawadi ya Gari aina ya BMW mpya kabisa ikiwa na namba mpya za sasa.
bmw
Sasa baada ya zawadi hizo kuonekana eti umoja wa Ma-Girlfriend Tanzania nao wameamua kutoa Ya moyoni kwa Ma-Boyfriend wao kuhusu birthday zao inapofika muda wa kusherehekea,hiki ndicho walichokiandika.
www

Maneno ya Rais wa Simba baada ya hizi droo zao ligi kuu

soccer 
Rais Simba Evans Aveva kwa mara ya kwanza amefungua mdomo wake na kulizungumzia suala la sare mbili katika mechi zao za Ligi kuu bara ambapo Rais huyu amewataka mashabiki na wanachama wa Simba kuungana na kuwa pamoja katika kipindi ambacho alikiita hawajapoteza wala kufanya vizuri.
Baada ya hayo akasema anamuamini Kocha Patrick Phiri hivyo wampe muda kidogo kwa kuwa wanapita kwenye kipindi cha mpito >>>  “Hatujafanya vibaya wala kufanya vizuri, sare mbili na hakuna mchezo tuliopoteza, ni suala la kujipanga ili kuangalia tutafanya nini katika mechi zinazofuatia, uongozi una changamoto nyingi utaona tulifanya kila linalowezekana kwenye uchaguzi baadaye kwenye usajili lakini sasa bado mambo hayajakaa vizuri, ni suala la kupambana tu

Ulisikia ile show ya Jose Chameleone ambayo kiingilio ni milioni moja? amezitaja sababu 3 hapa

stage 1 
Kwa hapa Tanzania tumezoea show kubwa kama Fiesta tunaona mastaa wakubwa kama Rick Ross, Ludacris na wengine kwa kiingilio kisichozidi elfu 20 ambapo mwaka huu anashuka T.I October 18 lakini tukirudi kwenye show binafsi za Wasanii, kumbukumbu zangu zinaniambia Diamond na Mwana FA ni miongoni mwa waliowahi kufanya show zao wao wenyewe lakini viiingilio havikufika shilingi laki moja.
Nimekuandikia hiyo sentensi hapo juu nikiweka kumbukumbu vizuri wakati huu ambapo imebaki miezi miwili kufanyika kwa show ya Jose Chameleone wa Uganda ambae amepanga kuifanya show yake mwenyewe nchini kwao December hii huku kiingilio kikiwa ni zaidi ya laki sita za Tanzania ambazo ni shilingi milioni moja za Uganda.
j chameleone 1
 
Kwenye Exclusive interview na youngluvega.com Jose Chameleone amesema >>> ‘nachekelea watu ambao wanasema Milioni? nani atampa hiyo milioni? watu wengi wanauliza mbona milioni moja? msanii mmoja? kuna watu ambao hawajapata bahati ya kumuona Chameleone akiwa anafanya mazuri yake, kuna matajiri flani wanataka kuja kwenye show yangu lakini wanaogopa wakija kuna cameraman wengi wanawasumbua na vitu kama hivyo’
  1. ‘Sio eti nimetaka kujipandisha bei lakini nataka kuwajali pia wale ambao hawawezi kunitembelea kwenye show za kawaida, najua watu wanashangaa na kuuliza mbona milioni?? …….sio sababu wewe au mimi hatuna milioni ndio wote hatuna milioni, kuna watu ambao milioni ni kama elfu moja, elfu kumi au laki moja’
  2. ‘Usiulize wanaotengeneza Benz mbona wanauza bei kubwa zaidi ya Toyota, kama huna hela ya Benz nunua Toyota, sio kwa ubaya lakini nataka nijali watu wote.. hii ni kwa wale wasioweza kuja kwenye show za elfu 10 na elfu 20, na wao wapate wakati wao…. hii hela ni kwa ajili ya kuwasaidia watu wa Karamoja wanaoishi kwenye maisha duni’