Jumatano, 17 Septemba 2014

Vyombo vya habari,usalama vyakutana TZ


Uhasama wa kiutendaji kati ya vyombo vya habari na vya ulinzi na usalama nchini Tanzania huenda ukapungua kwa kiasi kubwa baada ya pande hizo kuanza kukaa pamoja na kujadili mambo yanayokwamisha utekelezaji wa majukumu yao.
Baraza la Habari Tanzania limeitisha mkutano wa mashauriano kati ya vyombo vya habari na vyombo vya ulinzi, usalama na sheria ili kutambua kazi, haki na wajibu wa kila upande kwa maslahi ya umma.
Kila upande umekuwa ukitetea kuwa unatekeleza majukumu yake kwa maslahi ya umma. Hata hivyo vyombo vya habari ndivyo ambavyo vimeelekeza lawama zaidi kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuwa vinakandamiza uhuru wa vyombo vya habari kupata na kutoa taarifa zenye maslahi kwa umma.
Kwa upande wake vyombo vya ulinzi na usalama vimekuwa vikivilaumu vyombo vya habari kwa kutoa habari na hata kulazimisha kutoa habari zinazohatarisha usalama wa umma.
Akizungumza katika mkutano huo Makamu wa Rais wa Tanzania Dokta Gharib Bilal amesema katika ulimwengu wa sasa suala la habari limetanuka kiasi kwamba sheria zilizopo kusimamia vyombo vya habari hazina budi kuangaliwa upya ili kukidhi mazingira ya sasa.
“Si rahisi tena kudhibiti mawasiliano ama taarifa kwa kutumia sharia tulizojiwekea kama nchi maana jambo linaweza kudhibitiwa nchi moja na kutangazwa nchi nyingine na likarejea kule kule lilikodhibitiwa.” Amesema.
Hata hivyo Dokta Bilal amesema kuna umuhimu wa kuangalia mbinu za kukabiliana na mawasiliano yenye kuhatarisha usalama wa umma.
Amesema vyombo vya habari na vyombo vya usalama vina mipaka ya utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Dokta Bilal amesema mikwaruzano ya vyombo hivi inatokana na chombo kimoja kutaka kupata habari hata katika mazingira ambayo vyombo vya usalama vinaona ni hatari.
Kwa upande wake katibu mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania Mukajubi Mukajanga amesema,”vyombo vya usalama na sheria na vyombo vya habari vina uhusiano wa mashaka.Kuna wakati ambao wanadhani wanahitajiana wanakuja pamoja na kuna wakati ambapo kuna uhasama mpaka watu wanapigwa….”
Bwana Mukajanga amesema kutokana na umuhimu wa vyombo hivi kushirikiana katika masuala mbalimbali ya kijamii, baraza lake likaamua kuwakutanisha pamoja ili kujenga moyo wa kuaminiana.
Baraza la Habari Tanzania limewakutanisha waandishi wa habari na vyombo vya ulinzi na usalama ili kujadili mambo yanayokwamisha utekelezaji wa majukumu yao.

OMBI LA WAFUNGWA HUKO KENYA

 
Mkuu wa magereza anasema hakuna nafasi za kuweka vyumba vya faragha kwa wafungwa kushiriki tendo la ndoa.

Kamishna-Generali wa Magereza nchini Kenya Isaiah Osugo amekataa ombi la wafungwa kuruhusiwa kufanya tendo la ndoa na wake zao wakiwa gerezani.
Katika mazungumzo ya kipekee na BBC Swahili, Osugo amesema hili ni jambo ambalo linahitaji kuwepo vyumba vya faragha kuwaruhusu na yote haya yanahitaji pesa nyingi.
Mara kwa mara baadhi ya wafungwa nchini Kenya hasa wale ambao wamefungwa maisha na wale wlaiofungwa kwa miaka mingi wametoa ombi kwa serikali waruhusiwe kufanya tendo la ndoa na wake zao.
Wengi wao wanadai kuwa wakitoka jela na hupata wake zao wametoroka na hivyo basi ndoa zao kusambaratika.
Lakini Osuogo amesema hilo kwa sasa sio jambo la muhimu kwao.
"kwa sasa hatuna nyumba ya kumpa mfungwa starehe kama hii. Tuna vyumba ambavyo wafungwa wanalala wawili, wengine watatu na kuna wale wanalala kama hamsini kwa chumba kikubwa kabisa, na tunazidi kujenga ili tuwape nafasi ya kutosha,'' anasema Osugo.
"Hatujafikia hapo bado, kama mtu anataka hiyo strarehe ni vizuri ajizuie kufanya makosa asiletwe jela kwa sababu akiwa ndani ajue hapa ni mahali pa kumrekebisha.''
Na je barani Afrika kuna nchi ambayo inaruhusu jambo hili?
"Nilisikia Afrika Kusini walijaribu lakini sijui kama walifanikiwa. Unajua tena hao wana wafungwa wachache lakini sidhani kama nchi yoyote ya Afrika inawapa wafungwa ruhusa ya kuonana na mabibi wao kwa starehe kama hizo.''
Osugo anasema tofauti na baadhi ya mataifa ya ulaya ambayo yanawapa wafungwa nafasi hii, Afrika bado iko mbali sana kwa mambo kama haya.
"Nchi kama Canada wanaruhusu wafungwa saa 72 kuonana na wapenzi wao kwenye nyumba nzuri ambazo ziko ndani ya jela. Hapa sisi hatuwezi. Na tukianza hivyo si wafungwa wote watataka.''
Osugo anasema kwa hivi sasa wana mambo mengi mhimu ya kutekeleza, na endapo ombi hili la wafungwa litatekelezwa basi litakua la mwisho kabisa kufanyika lakini hajasema ni lini Kenya itaweza kuwaruhusu wafungwa kujamiIana na wake Zao.
Ombi hili ni la wafungwa wa kiume hapa Kenya lakini kwa upande wa wafungwa wanawake ni nadra sana watoe ombi kama hili.

Sentensi 4 kwanini maandamano ya CHADEMA Dodoma kesho yamezuiliwa.

stop 
Polisi Dodoma wametangaza kuyazuia maandamano ya chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA yaliyokua yamepangwa kufanyika Alhamisi ya tarehe 18/09/2014 ambapo wametaka Wananchi wayapuuze.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi wa Polisi Emmanuel Lukula amesema kufuatia viongozi wa CHADEMA kutaka kufanya maandamano kuelekea viwanja vya ofisi za bunge kwa ajili ya kupinga bunge la katiba linaloendelea, maandamano hayo ni batili na yanakiuka Sheria iliyoliwekwa kwa bunge hilo.
Ripoti ya Polisi iliyosambazwa Septembet 17 2014 inasema Kamanda Lukula ametaja sababu za msingi za kuzuia maandamano haya kuwa ni:- 1 . siku ya maandamano ya tarehe 18/09/2014 ni siku ya kazi kwa sababu yalipangwa kufanyika kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa sita mchana hivyo yataathiri ufanisi wa watu waliopo makazini/maofisini.
kamanda 2 
2. Bunge maalumu la Katiba linaloendelea kwa sasa lipo kisheria na hakuna tamko lolote lililotolewa na Mahakama yoyote kulisitisha hivyo moja ya kazi ya jeshi la polisi ni kulinda sheria na wale wanaofuata sheria.
Kuna kesi Mahakamani ya kupinga Bunge hilo kuendelea na hadi sasa shauri hilo linaendelea Mahakamani hivyo kwa CHADEMA kuandamana ni kuingilia Uhuru wa Mahakama.
kamanda 1 
Baadhi ya wilaya barua za kufanya maandamano zimechelewa kufika kwa wakuu wa polisi wilaya kabla ya saa 24 kisheria hivyo Kamanda Lukula amesisitiza kuwa CHADEMA Mkoa na Wilaya za Dodoma wayasitishe maandamano na kama hawajaridhika wakakate rufaa kwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi.

Habari njema! Fastjet tena kwenye headlines!! wameanza kwenda Uganda.


Screen Shot 2014-09-17 at 9.33.46 AM
Screen Shot 2014-09-17 at 9.33.46 AM
Shirika la ndege la Fastjet limepata sifa kubwa nchini Tanzania kutokana na kusafirisha kwake abiria na kuanza kuiunganisha Afrika kwa kasi ambapo baada ya kuanzisha safari za nyumbani kati ya Mwanza – Dar, Kilimanjaro – Dar na Mbeya – Dar sasa hivi wamevuka mipaka.
Fastjet wamevuka mipaka na kufanya safari kati ya Dar – Johannesburg, Dar – Lusaka, Dar – Harare na sasa ni Dar – Entebbe.
Screen Shot 2014-09-17 at 9.33.38 AM
Picha zote hizi zimepigwa wakati ndege ya Fastjet ikiwa inaondoka Dar es salaam kuelekea Entebbe.
Screen Shot 2014-09-17 at 9.33.25 AM
Screen Shot 2014-09-17 at 9.33.12 AM
Screen Shot 2014-09-17 at 9.33.01 AM
Screen Shot 2014-09-17 at 9.32.54 AM
Screen Shot 2014-09-17 at 9.32.37 AM
Screen Shot 2014-09-17 at 9.32.24 AM
Screen Shot 2014-09-17 at 9.33.58 AM
Screen Shot 2014-09-17 at 9.34.08 AM

NI ZAIDI YA VIPODOZI,NI ASILI VISIVYO NA KEMIKALI;ORIFLAME.

Ni aina mbali mbali za vipodozi kwa wanaume na wanawake,vimetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu visivyo na kemikali.Ni vipodozi asili kabisa kulingana na ngozi yako jaribu aina hizi uone maajabu ya vitu asilia.

Bidhaa hizi ni mali ya kampuni ya Oriflame ambazo zimethibitishwa na wataalamu wa kimataifa na wa taifa.Baadhi ya bidhaa zake ni Cleaning Gel,Face Toner,Lotions,Lipstick,Perfumes,Bioclinic,Ecollagen,Optimals,Essentials Scrub,Gel Wash,Essentials soap,Pure skin scrub,Eye shadow,Mascara,Deodorant,Shower Gel,Foot cream,Baby oil na nyinginezo nyingi kutokana na mahitaji yako.
Utapata bidhaa hizi kutoka kwa wakali wao mashuhuli anaepatikana Dar es salaam anaetambulika kwa jina la LIGHTNESS MALUGU anapatikana kwa namba 0767792969 kwa maelezo zaidi na kufanya manunuzi.Bei zao ni nafuu sana ambazo anaweza kununua hadi mtu wa hali ya chini kabisa.
KWA MWONEKANO MZURI,MATUNZO YA NGOZI YAKO,NYWELE NA AFYA YAKO TUMIA BIDHAA KUTOKA ORIFLAME PEKEE.
Kwa mawasiliano zaidi 0767792969.