Jumatano, 26 Oktoba 2016

Magazeti ya Tanzania October 26, 2016 kuanzia, Udaku, Hardnews na michezo

October 26 2016 naanza kwa kukusogezea post ya stori zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye, Michezo na hardnews ili ujue kinachoendelea .. usiache kukaa karibu yangu kwenye facebook @nicksonluvega , twitter @nicksonmoses na instagram @nicksonluv ili niwe nakutumia kila kinachonifikia.
20161026_041718
20161026_041734
20161026_041746
20161026_041757
20161026_041807
20161026_041815
20161026_041824
20161026_041831
20161026_041846
20161026_041854
20161026_041905
20161026_041914
20161026_041925
20161026_041933
20161026_041945
20161026_041953
20161026_042003
20161026_042011
20161026_042021
20161026_042031
20161026_042041
20161026_042049
20161026_042059
20161026_042106
20161026_042117
20161026_042125
20161026_042134
20161026_042140
20161026_042151
20161026_042159
20161026_042233
20161026_042241

Rais Magufuli Aongoza Kura Kuwania Tuzo ya ‘Forbes Africa Person of The Year’

Rais John Magufuli anaongoza  kura za kuwania tuzo ya ‘Forbes Africa Person of The Year’, ambayo hutolewa kwa watu walioonyesha mchango kwa jamii.

Huku zikiwa zimebaki siku 21 kwa mshindi wa tuzo hiyo kutangazwa, Rais Magufuli anachuana na Rais wa Mauritius,  Ameenah Gulib;  Mwendesha Mashtaka wa Afrika Kusini, Thuli Madonsela; Mwanzilishi wa Capitec Bank, Michiel Le Roux na Taifa la Rwanda.

Mpaka jana jioni, Dk Magufuli alikuwa anaongoza kwa asilimia 75 likifuata Taifa la Rwanda na nafasi ya tatu alikuwa Madonsela wa Afrika Kusini.

Rais Magufuli anayetimiza mwaka mmoja madarakani wiki ijayo, utendaji wake umeonekana kuwagusa wananchi wa kipato cha chini, hasa kwa falsafa yake ya Hapa Kazi, uwajibishaji na mikakati yake ya kubana matumizi ili kuokoa fedha kwa kuzuia sherehe zisizo na tija.

UKOCHA: Pluijm Amwaga Mboga Yanga

Usemi wa Waswahili kuwa, ukimwaga ugali, nami namwaga mboga umetimia kwa klabu ya soka ya Yanga  ambayo licha  ya uongozi wake jana kukanusha kuajiriwa kwa kocha Mzambia George Lwandamina na kuachana na Mdachi Hans van der Pluijm, mzungu  huyo ametangaza kujiuzulu kazi hiyo.

Mapema jana,  katibu mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit alisema uongozi wao hauna taarifa  za ujio wa Lwandamina wala haujafanya mawasiliano yoyote na mkufunzi huyo. “Kwanza, hizo taarifa nasikia kwako, hatujazungumza naye na wala hatujui kama amekuja, anaweza kuwa amekuja kwa shughuli zake. Kocha Yanga ni Hans Pluijm,” alisema Baraka.

Lwandamina alikanusha akisema kwamba ujio wake nchini hauna maana kwamba amekuja kusaini mkataba Yanga, ingawa alikiri kwamba timu hiyo inamhitaji na kama ikichangamka yuko tayari kufanya kazi nchini.

Sababu za uamuzi wa Pluijm

Akizungumza uamuzi wake wa kujiuzulu, Pluijm alisema uwapo wa kocha huyo nchini umemchukiza na kuamua kumuandikia mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji barua ya kujiuzulu nafasi yake.

Pluijm alisema hajafurahishwa na mambo yalivyokuwa yakifanyika na kwamba licha ya uongozi wa klabu yake wakati wote kukanusha hawana mpango na Lwandamina, lakini anao uhakika wako katika mazungumzo na kocha huyo wa Zesco United.


Alisema kuna nafasi Yanga walitaka kumpa, lakini ameshindwa kukubaliana nayo kutokana na mambo yalivyofanyika.

Pluijm alitajwa kubadilishiwa wadhifa na kuwa mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo na nafasi yake kuchukuliwa na Lwandamina. “Unajua hakuna siri katika dunia ya sasa, sijafurahi mambo yalivyokuwa yanafanyika hawakutanguliza heshima kwangu, nimewaandikia barua ya kujiuzulu ili waniache niondoke vyema,” alisema Pluijm na kuongeza: “Sikupanga kuondoka Yanga kwa ubaya, lakini hili sikulifurahia, nawashukuru wanachama na mashabiki pamoja na uongozi na wachezaji wangu kwa kunipa nafasi ya kufanya kazi hapa na kesho (leo) nitakwenda kuwaaga wachezaji wangu,” alisema Pluijm.

Jana asubuhi, Pluijm alisema hana nafasi ya kuzungumzia ujio wa Lwandamina na kusisitiza kuwa kwa sasa anahitaji kutuliza akili kwani anasubiri taarifa rasmi.

Huku akicheka Pluijm alisema: “Nimesikia mengi, yameandikwa na kusemwa juu yangu kuondoka Yanga, lakini najiamini, mimi ni kocha mwenye kiwango, nimefanya kazi kubwa Yanga na ninazidi kuendelea kufanya, ingawa sishangazwi na yanayosemwa kwani vitu kama hivyo ni kawaida kutokea duniani.

“Nimeifanyia Yanga vitu vingi tangu iliponiajiri hadi sasa, kama kuna mabadiliko nitaambiwa na waajiri wangu, nami nitaeleza misimamo wangu.”

Wengine wanasemaje

Kocha msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja alisema kuondolewa kwa Pluijm hashangazwi nako kwani ndivyo mpira ulivyo kokote duniani. “Hata Mourihno (Jose) alitimuliwa Chelsea, hivyo ni kawaida ya makocha, lakini mimi sioni udhaifu wa Pluijm naangalia mafanikio aliyowapa Yanga hadi imecheza mashindano ya kimataifa na kufika mbali tu,” alisema Mayanja.

Mwanasoka wa zamani wa Yanga na Pan African ambaye pia ni kocha, Mohammed Adolph ‘Rishard’ alisema timu kucheza mfululizo kwa kiwango kile kile ni ngumu hivyo haoni sababu ya Yanga kumuondoa Pluijm.

“Sioni kama Yanga iko katika kiwango kibovu nafikiri ni uchovu kwani hata ukiangalia Azam  ndiyo tatizo linalowasumbua, timu haiwezi kucheza misimu miwili mfululizo kwa kiwango kile kile, sasa wanapobadilisha kocha wategemee mambo mawili, timu kuendelea kuwa kama ilivyo au kuzidi kuporomoka zaidi,” alisema Rishard.

Diamond Platnumz Awatupia Madongo Walio Kuwa Wanasema Hajanunua Nyumba South Afrika...Adai Uswahili wake Unamlipa

Diamond Jana amefika kwa mara ya kwanza kwenye nyumba ambayo alinunua South Afrika na Kuandika Yafuatayo....

"Asa kunya nakunya mie makalio yanawauma wengine, eti inahuu....? Wambie wasininunie mie, wakazane....halaf hii clip naomba wanangu mnisaidie kuwatag wote waliokuwa busy kupost na kuzungumza Kuwa nyumba hii si yangu....waambie hizi ndio kwanza rasharasha clip hata kupost sijaanza bado....soon naamia ndani😂😂...halaf nlisahau, wakikwambia mie mswahili wambie Mswahili haswaaa👌... halaf uswahili wangu najua kuutumia na umefanya leo niwe na kibanda south asa wao Uzungu wao Umewapa mini"

Jamaa Yake Amemwekea Tego, Msichana Yupo Tayari Kunipa Papucha ila Anaogopa Tutanasiana au Ntapata Tatizo

Nimempata dada mmoja mitaa fulani, ni mzuri sana na she is sexy. Kiukweli tumependana nami nilivyomuona tu siku ya kwanza pale ofisini nilimpenda nikaomba tuwe na ukaribu. Tukaanza ukaribu basi juzi juzi hapa nikamwambia mi natamani mambo flani. Yule dada alinikubalia lakini akasema shida kubwa ni kuwa jamaa yake mshirikina alimwekea dawa hivyo tukikutana naweza pata matatizo, anasema watu wa Morogoro/waruguru ndo zao hizo.

Sasa hajui atafanyaje maana anasema aliwahi achana na jamaa akawa na mtu mwingine yule jamaa aliyetembea naye alipata matatizo makubwa sana hadi ikabidi yule dada arudi akamwambie Mluguru amwachie jamaa awe salama. Toka kipindi hicho dada amekuwa hana amani anashindwa sasa afanyeje. Aliniambia maneno haya kwa uchungu sana nami nikimwona kiukweli anataka sana nimkandamize yaani hata tukiongea hivi namwona tu jinsi macho yanavyochoka nami mzuka unapanda natamani nimnaniii hivyo hivyo lakini ananikataza anasema coz she loves me hapendi nipate shida.

Sasa hapa wadau nifanye nini? Mambo kama haya sisi wengine hatushiriki ushirikina matatizo yetu ni K tu lakini kwa waganga hatujawah kwenda. Sasa hapo nafanyaje?

Tusaidiane tafadhali maana hali inakuwa ngumu sana kwetu sote.

Rais Magufuli ametajwa kuwania tuzo ya ‘Forbes Africa Person of The Year’, ingia hapa kumpigia kura

Rais Dkt John Pombe Magufuli ametajwa kuwania tuzo ya ‘Forbes Africa Person of The Year.’

Anachuana na watu wengine wanne wakiwemo: Rais wa Mauritania, Ameenah Gulib, Mwanzilishi wa Capitec Bank, Michiel Le Roux na Thuli Madonsela wa Afrika Kusini pamoja na watu wa Rwanda.

Zimebaki siku 22 za kupiga kura. Unaweza kumpigia kura Rais Magufuli kwa kubonyeza hapa. Hadi sasa Rais Magufuli anaongoza kwa asilimia nyingi (73%).

Mwaka huu tuzo hizo zitatolewa jijini Nairobi, Kenya November 17.

Wafuatao ni washindi wa tuzo hiyo miaka ya nyuma

Mohammed Dewji (Tanzania)– 2015
Aliko Dangote (Nigeria)– 2014
Akinwumi Adesina (Nigeria) – 2013
James Mwangi (Kenya) – 2012
Sanusi Lamido Sanusi (Nigeria)- 2011

Edward Lowassa Anena Mwaka Mmoja wa Rais Magufuli

 Aliyekuwa mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa amechambua mwaka mmoja wa uongozi wa Rais John Magufuli tangu aingie madarakani akisema kuna mafanikio machache katika baadhi ya maeneo, lakini maisha ya wananchi yamezidi kuwa magumu.

Lowassa ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015 aliungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), alisema hayo jana katika andishi lake kwa vyombo vya habari.

Mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa waziri mkuu katika Serikali ya Awamu ya Nne kabla ya kujiuzulu mwaka 2008, amesema katika andishi hilo kwamba, “kile ambacho tulikisema wakati ule kwa nini tunataka mabadiliko, hivi sasa kila mtu anakiona.

“Kwamba pamoja na mafanikio machache katika baadhi ya maeneo, lakini maisha yamezidi kuwa magumu, ajira imeendelea kuwa bomu linalosubiri kulipuka, elimu bure iliyoahidiwa siyo inayotekelezwa, utumishi wa umma umekuwa kaa la moto.”