Jumapili, 14 Septemba 2014

MAYWEATHER AMCHAPA TENA MAIDANA


Floyd Mayweather (kushoto) akimtupia konde mpinzani wake Marcos Maidana.

Maidana akijibu mashambulizi wakati wa pambano hilo.

Mayweather akimshambulia mpinzani wake.

UGANDA YAHARIBU SHAMBULIZI LA KIGAIDI

 
Vikosi vya usalama nchini Uganda 
Maafisa wa polisi nchini Uganda wameimarisha usalama katika maeneo mengi ya uma katika mji mkuu wa Kampala kufuatia kukamatwa kwa washukiwa kadhaa wa makundi ya kigaidi na vilipuzi.
Msemaji wa polisi ameiambia BBC kwamba jaribio la kutekeleza mashambulizi limetibuliwa.
Awali ,ubalozi wa Marekani mjini Kampala ulisema kuwa mamlaka ilitibua shambulizi la kigaidi lilokuwa limepangwa na washukiwa wa kundi la Alshabaab.
Ubalozi wa Marekani umewataka raia wake nchini Uganda kuendelea kukaa majumbani mwao.
Ubalozi huo tayari ulikuwa umeonya kuhusu shambulizi la kulipiza kisasi dhidi ya maeneo ya Marekani na kundi la Alshabaab ili kujibu shambulizi la angani la Marekani lililomuua kiongozi wa kundi hilo mapema mwezi huu.

WANACHAMA 100 WA BOKO HARAM WAUAWA



 
jeshi la Nigeria
Jeshi la Nigeria linasema kuwa limewaua zaidi ya wanamgambo 100 wa kundi la Boko Haram kufuatia shambulizi la wapiganaji hao siku ya ijumaa kazkazini mashariki mwa jimbo la Borno.
Vikosi vya serikali vimeripotiwa kuyakamata magari na risasi wakati vilipokuwa vikiimarisha usalama katika mji wa Konduga,yapata kilomita 35 kutoka mji mkuu wa jimbo hilo, Maiduguri.
Wapiganaji wa Boko Haram wameiteka miji kadhaa na vijiji katika majuma ya hivi karibuni wakikaribia kuelekea Maiduguri.