Jumapili, 6 Desemba 2015

Wakati Tanzania Tukiwa Tunashangilia Kusimamishwa Maofisa TRA, Kenya Wanafanya Hivi...

Kwa wanaofatilia siasa za kenya kulikua na skendo iliyokua inamuhusu waziri wa uhuru Anne Waiguru, huyu Anne Waiguru alikua ni waziri mtu mkubwa na maarufu serikalini.

Zimepotea 795 milion kshs ambazo ni kama 16 billion tz shs amewajibishwa na nyumbani kwake kumepekuliwa na maofisa wa kupambana na rushwa na kukuta mamilioni ya pesa kwenye mabunda, soon atafunguliwa mashtaka na kufungwa.

Juzi hapa Tanzania ufisadi wa escrow umetu cost zaidi 300 billions lakini hakuna hata mmoja aliyepekuliwa na wote wamerudi kua wabunge.

Tunatakiwa kuiga wakenya, sio tunatimua maofisa wa tra na muhimbili alafu tunaanza kujiisifu sana bado tuna safari ndefu kwenye hii vita dhidi ya ufisadi.

Sina nia ya kubeza anachofanya Magufuli, nampongeza ila tunapaswa kushinikiza yafanyike zaidi ya hapa na tumuunge mkono.


Kenya wana upinzani imara ndio maana kukitokea ubadhirifu kidogo tu wanaibana serikali hadi inawachukulia hatua wahusika.

Tusiwabeze wapinzani wa serikali tuwasapoti maana wao ndio wanaweza kuibana serikali kwa niaba yetu panapofanyika madudu kama haya

Kanye West Ametumia zaidi ya Milioni 130 Kuuzuia Mkanda wa ‘Ngono’ Kusambaa, Mkanda Huo Umemuhusisha Nani?

Star  wa hip hop nchini Marekani, Kanye West, ameamua kutoa kiasi cha dola milioni 130, kwa ajili ya kuzuia mkanda wa ngono wenye picha zinazofanana na mke wake usiingie sokoni.

Kwa mujibu wa mtandao  wa US,  msanii huyo aliamua kafanya hivyo kwa kuwa ndani ya filamu hiyo kuna mrembo anafanana na mke wakewe Kim Kardashian.

Nimeona bora nifanye hivyo kwa kupunguza maneno ambayo yangejitokeza, ni filamu ambayo ina mambo mengi ndani yake, lakini inaweza kuharibu mwonekano wa familia yetu japokuwa hakuna mhusika ndani yetu,” alisema Kanye.

Harmonize: ‘Directors’ wa Video Kutoka South Africa, Wanatuheshimu Sana Wasanii Kutoka Tanzania.

Chipukizi wa Bongo flava anayeunguruma poa na hit yake ‘Aiyola’, Harmonize amesema waongozaji wa video za muziki kutoka Afrika kusini huwa wanaonesha heshima ya hali ya juu wanapokutana na wasanii kutoka Tanzania.

Akifunguka mbele ya kipaza sauti cha Timesfm.co.tz, Mkali huyo ambaye jina lake halisi ni Rajab amedai sababu kubwa ya kupewa heshima ni kwa kuwa mziki wetu ni wa pili kwa ukubwa Barani Afrika ukiwatoa Nigeria.

“Labda mi niseme kitu kimoja” alisema “Directors wa kule(Afrika kusini) wanajua kabisa ili uweze kuhit Afrika mashariki ni lazima utusue Tanzania, na hilo liko wazi sisi ni wa pili kimuziki Afrika na tunaushindani mkubwa na Nigeria tu.

huduma huwa zinakuwa nzuri kiukweli, wanatu treat poa yani hadi unaona heshima unayopata” alimaliza.

Rungu la TRA Yalishukia BAKWATA...Magari 82 Yaingizwa Kwa Jina lao Bila Kulipiwa Kodi..Watwangwa Barua Nzito

Rungu la TRA Yalishukia BAKWATA...Magari 82 Yaingizwa Kwa Jina lao Bila Kulipiwa Kodi..Watwaga Barua Nzito, Isome HApa chini:

Katibu Mkuu Tamisemi Akagua Miundombinu ya Mfumo wa Mabasi Yaendayo Haraka

WATOA huduma katika kipindi cha mpito cha mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam, kampuni ya UDA-RT wameihakikishia serikali na wananchi kuwa matayarisho yanaendelea vizuri tayari kwa huduma hiyo kuanza Januari 10 mwakani.


Ahadi hii ilitolewa wakati wa ziara iliyofanywa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini, alipokuwa akikagua miundombinu katika mabasi yanayotarajiwa kutoa huduma hiyo.


Siku chache zilizopita, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliwataka wahusika wote wa mradi huo kuhakikisha unaanza mara moja ili kupunguza adha ya usafiri Dar es Salaam.

“Tulitaka kujiridhisha kama mabasi haya yako tayari kutoa huduma hii,” alisema Sagini mbele ya waandishi wa habari na kuwataka wahusika kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa haraka.

Mabasi 140 yanayomilikiwa na kampuni ya UDA-RT yatatumia mfumo wa kisasa wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) wa ukusanyaji nauli, mifumo ya utoaji taarifa na maeneo maalum ya wazee na walemavu. 

Mwenyekiti wa UDA-RT, Robert Kisena aliwataka wananchi kujali mabasi hayo mara huduma itakapoanza.

“Wananchi wajali mabasi haya, madereva nao wana wajibu wa kuhakikisha magari haya yanadumu,” alisisitiza.

Alisema kuhujumu mabasi hayo mapya au miundombinu ya mradi huo ni sawa na wananchi kujihujumu wenyewe, kwani huduma hiyo ni kwa ajili yao. 

Alisema tayari kazi ya kufunga vifaa vinavyotakiwa katika mabasi hayo imeshakamilika kwa baadhi ya mabasi na inaendelea kwa mengine.

Msemaji wa UDA-RT, Said Mabruk alisema magari yote yanayotakiwa kuanza kwa huduma hiyo ya mpito yana madereva na walishapewa mafunzo na kwamba ni matumaini yao kuwa huduma itaanza kwa wakati uliopangwa.

Awamu ya kwanza inahusisha kilometa 20.9 za njia maalumu kutoka Kimara hadi Kivukoni, barabara ya Msimbazi kutoka Faya hadi Kariakoo- Gerezani na sehemu ya barabara ya Kawawa kutoka Magomeni hadi njia panda eneo la Morocco.

Tibaigana Afunguka...Huyu Ndiye Rais Niliyemtaka

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna mstaafu Alfred Tibaigana amesema Rais John Magufuli amepatikana wakati sahihi, kwa kuwa nchi inamhitaji kiongozi ambaye akitoa amri inatekelezwa mara moja.

Kauli ya Tibaigana inakuja takribani miezi 15 tangu aliposema anatamani kuiona Tanzania ikimpata rais dikteta kwa kuwa nchi haiwezi kupiga hatua iwapo mkuu wa nchi hataweza kukemea na kutoa amri watu wakatii.

Akizungumza katika mahojiano maalum na gazeti hili nyumbani kwake katika Kijiji cha Katare, wilayani Muleba Mkoa wa Kagera, hivi karibuni, Tibaigana alisema anaamini changamoto nyingi zinazowakabili Watanzania zitatatuliwa na Rais Magufuli.

Akitolea mfano utaratibu wa Rais Magufuli wa kufanya ziara za ghafla kwenye sekta mbalimbali za umma, Tibaigana alisema: “Watu hawafanyi kazi na viongozi ni waoga wa kutoa uamuzi, ziara ya Rais Magufuli (Hospitali ya) Muhimbili imesababisha hospitali nyingi kuboresha huduma, siyo lazima afike kila mahali akitoa kauli hatua ichukuliwe.”

Kamanda huyo mstaafu alisema hata uamuzi wa Rais Magufuli wa kufuta safari za nje kwa viongozi wa umma mpaka kwa kibali maalumu, umekuja wakati mwafaka kwa kuwa baadhi ya safari hazikuwa na masilahi kwa taifa.

“Safari zinatumia pesa nyingi na nyingine huwa siyo za lazima, kwa uzoefu wangu wa kukaa Serikalini hata baadhi ya wafanyakazi wa ndani hulipwa kama waajiriwa kwa kufanyiwa mipango na mabosi wao,’’ alisema.

Tibaigana ambaye aliwahi kugombea ubunge Jimbo la Muleba Kusini miaka mitano iliyopita kupitia CCM na kushindwa kwenye kura ya maoni, alipendekeza Bunge la 11 kufanyia marekebisho baadhi ya sheria ili ziwe kali kwa watu wanaohujumu uchumi.

Maagizo yatekelezwa

Kauli ya Tibaigana imekuja wakati Rais Magufuli ameanza kazi ya kutafuta na kuziba mianya ya upotevu wa fedha, alianzia Hazina na kupiga marufuku safari zote za nje kwa viongozi na kusema zitakuwa zinaruhusiwa kwa kibali maalumu.

Dk Magufuli pia aliamuru mashine za MRI na CT-Scan katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) zitengenezwe na kuagiza Sh3bilioni zitolewa kugharimia matengenezo kati ya Sh7bilioni zilizokuwa zinahitajika.

Vilevile, aliagiza Sh4bilioni zilizokuwa zitumike katika Maadhimisho ya Sherehe za Uhuru Desemba 9, kutumika kupanua barabara ya Morocco kwenda Mwenge, kazi ambayo utekelezaji wake unaendelea.

Rais huyo wa Awamu ya Tano na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa nyakati tofauti walitembelea maeneo muhimu kwa uchumi wa nchi kama Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bandari na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) na kuibua vitendo vya ufisadi na ukwepaji wa kodi.

Akizungumzia hali hiyo, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana anasema kinachoonekana ni uzembe au udhaifu kwa watumishi wa umma ambao mbali na kuwa wazito katika kutoa uamuzi, lakini ni wazito katika kutambua uzito wa tatizo.

Alisema lipo tatizo kubwa kwa viongozi wengi kukosa uwajibikaji licha ya dhamana kubwa walizopewa na kusema wakati umefika wa kuangalia upya mfumo wa uteuzi wa viongozi wa ngazi mbalimbali nchini.

“Hii ni dalili ya kuwa na viongozi wasiowajibika…maana haiwezekani mashine muhimu inaharibika na mkurugenzi na madaktari wake wanakaa kimya tu kama vile hakuna kilichotokea… hii inaonyesha kuwa tabia ya uwajibikaji haipo serikalini,” alisema Dk Bana.

Alisema kama ambavyo wafanyakazi wa Serikali wanaweza kudai mishahara kwa kugoma, kunapotokea kukosekana kwa vitendea kazi, watumie nguvu ileile kudai ili waweze kufanya kazi.

Alisema haiingii akilini kuona baadhi ya watendaji wa Serikali wakiwamo wakuu wa mikoa, wilaya na hata makatibu wakuu kukaa kimya licha ya Rais kuonyesha njia kipindi kifupi tangu ashike nafasi hiyo.

Profesa George Shumbusho wa Chuo Kikuu cha Mzumbe alisema uchapaji kazi wa viongozi katika eneo lolote unategemea na umakini na ufuatiliaji wa kiongozi mkuu.

“Baba katika familia akiamua mambo yaende yataenda tu… ni kawaida katika mabadiliko, binadamu kujaribu wakiona huna mchezo watafanya kazi wakiona ni nguvu ya soda mtarudi kule kule” alisema Profesa Shumbusho.

Alisema watendaji walio wengi walionekana kulala na kufanya kazi kwa mazoea kutokana na wakuu wao na akasema sasa wameanza kuamka kutokana na kasi ya mtendaji mpya na akasema kasi ya utendaji inaweza ikawa kubwa zaidi endapo rais naye ataendelea kuonyesha njia. 

Jakaya Kikwete Aibukia 'Sauzi' Magufuli Akitumbua Majipu Magogoni Aliyomwachia....

Wakati Rais John Magufuli akitimiza siku 31 akiwa amejifungia Ikulu kutatua kero za nchi bila kusafiri nje ya nchi, Rais mstaafu Jakaya Kikwete (pichani) ameendelea kujumuika katika hafla za kimataifa baada ya kuonekana nchini Afrika Kusini juzi akiwa mwalikwa wa Mkutano wa China na Afrika.

Tangu aingie madarakani Novemba 5, Rais Magufuli amepiga marufuku safari za nje kwa watendaji wa serikali bila ya kibali maalumu cha Ikulu.
Alifikia uamuzi huo baada ya kubainisha katika hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge la 11 mwezi uliopita kuwa safari za kimataifa zinatafuna mabilioni ya fedha za walipa kodi.

Rais Magufuli hajasafiri kwenda nje ya nchi mbali na kwenda Dodoma kwa ajili ya kumwapisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na kuzindua Bunge.
Picha zilizotumwa na Ofisi ya Makamu wa Rais jana, zilimwonyesha JK akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, aliyemwakilisha Rais Magufuli kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika na China, uliomalizika jana jijini Johannesburg.

JK ameonekana katika picha hizo akitembelea mabanda ya maonyesho ya mkutano huo ulioandaliwa na China ili kujadili mikakati ya ushirikiano baina yake na Afrika. 

Ni mara ya pili kwa Kikwete kwenda nje ya nchi tangu Rais Magufuli aingie madarakani. Novemba alionekana katika Jiji la Addis Ababa Ethiopia.

Kwenye utawala wake wa miaka 10, Rais mstaafu huyo alilaumiwa kusafiri mara nyingi nje ya nchi akiwa na msururu wa viongozi na wasaidizi wake hivyo kutumia gharama kubwa, lakini alijitetea kuwa huenda nje kutafuta fedha za maendeleo.

Wakati akihutubia Bunge mjini Dodoma mwezi uliopita Rais Magufuli alisema safari za nje ziliigharamu nchi Sh. bilioni 356 kuanzia mwaka 2013 hadi 2015.

Alisema kati ya kiasi hicho karibu Shilingi bilioni 200 zilitumiwa kwa tiketi za ndege, kadhalika bilioni 68 zilitumiwa kwa mafunzo ya nje wakati bilioni 104 ziliishia kwenye mifuko ya vigogo na maofisa kwa ajili ya posho.

Rais Magufuli alisema mabilioni hayo ya safari yangejenga kilometa 400 za barabara kwa kiwango cha lami akitaja ile inayotoka Urambo Tabora hadi Kigoma mjini.

Katika kutimiza azma ya kupinga safari za nje , Rais Magufuli alikacha kwenda kwenye mkutano wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Madola, uliofanyika visiwa vya Malta wiki mbili zilizopita.

Aliagiza Balozi wa Tanzania jijini London Uingereza na maofisa wengine wanne kuiwakilisha nchi kwenye mkutano huo hatua iliyookoa karibu Shilingi milioni 700 ambazo zingegharamia safari hiyo.

NICKSONLUV


TECNOMILES waachia Ngoma yao inayofanya vizuri ulimwenguni play hapo chini kuona video 
                                  Teknomiles - Wash

[Audio] Kauli ya Januari Makamba kuhusu kumkejeli Rais Magufuli


January Makamba ameamua kutoa ufafanuzi wa picha mbalimbali zilizowekwa katika akaunti yake ya Instagram ambazo zinadaiwa kumkashfu Rais Magufuli baada ya kumnyima Uwaziri Mkuu.
Hizi ndo Picha alizoweka ambazo zinadaiwa kumkejeli Rais Magufuli
Picha hii inaonyesha   sokwe mtu wakiwa wamevalia suti  na  huyo mtu anayeonekana kurukia kamba huku nyuma ana mkia lakin akiwa amevalia kaptula peke yakePicha hii inaonyesha Nguruwe wakiwa wamepewa heshima ya zulia jekundu ambayo ni heshima ya kipekee anayopewa binadam pekee 
 Picha hii inamuonyesha mtu akiwa amewasha moto kwa kutumia kuni ambazo chanzo chake ni ngazi anayotakiwa kutumia kutokea nje ( juu ) 
  
Msikilize January Makamba akiongea hapo chini

Ujerumani Yamsifu Rais Magufuli Kwa Kupambana na Ufisadi Kwa Vitendo.....Yaahidi Kumpa Ushirikiano

Serikali ya Ujerumani imeeleza kufurahishwa na kasi ya kupambana na rushwa na ufisadi ya Rais John Magufuli na kuahidi kumpa ushirikiano katika masuala ya maendeleo.

Ujerumani inakuwa nchi ya kwanza ya kigeni kuvutiwa na kasi ya Rais Magufuli ambaye ameonekana kuelekeza nguvu katika si tu kupambana na maovu hayo tangu aapishwe Novemba 5, bali pia kuchochea maendeleo ya watu wenye kipato cha chini.

Aidha, Ujerumani imesema inasubiri kuona vipaumbele vya maendeleo vitakavyoainishwa na serikali ya Rais Magufuli ili iweze kuisaidia utekelezaji.

Pongezi hizo zilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Afrika, Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani, Georg Schmidt.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara yake ya siku tano hapa nchini, Schmidt alisema katika kipindi cha mwezi mmoja tu, Dk. Magufuli ameweza kushughulikia masuala muhimu ya kijamii ikiwamo kuboresha huduma za afya na kuwashughulikia wakwepa kodi.

Kasi ya Rais Magufuli, alisema, itasaidia kuokoa fedha nyingi ambazo zitakapokusanywa zitachangia miradi mbalimbali ya maendeleo kama alivyofanya tayari kwenye afya na elimu.

Mkurugenzi huyo alisema ziara yake nchini ilikuwa na lengo la kuangalia hali ya maendeleo nchini baada ya uchaguzi, miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali yake pamoja na kukuza ushirikiano baina ya nchi mbili hizo.

Alisema ameshakutana na baadhi ya watendaji wa serikali, wabunge, wanaharakati, watendaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na kuitembelea Mahakama ya Haki za Binadamu iliyopo mjini Arusha.

Alisema pia amekuja kuangalia fursa za kibiashara nchini kwa sababu wawekezaji wengi duniani huvutiwa kwenda kuwekeza kwenye mataifa mbalimbali iwapo nchi hiyo ina usalama wa kutosha.

Akizungumzia suala la Zanzibar, Schmidt aliwataka wananchi kuwa na subira wakati mazungumzo yakiendelea katika jitihada za kutatua mgogoro huo.

“Mazungumzo yanaendelea ya usuluhishi tunasisitiza utulivu, amani na tuna imani mwafaka mzuri utafikiwa,” alisema.
Alisema kwa sasa serikali ya Ujerumani itazielekeza fedha nyingi kwa serikali ya Tanzania ili kushughulikia wakimbizi kutoka Burundi wanaokimbia machafuko.

“Tuna jukumu na wajibu wa kushughulikia mgogoro wa Burundi na fedha zilizokuwa zinakwenda Burundi sasa zitaelekezwa Tanzania kwa kuwa wanapokea wakimbizi wengi zaidi,” alisema Schmidt.