Jumamosi, 18 Februari 2017

Hivi Ndivyo Uzuri wa House Girl Ulivyomponza Mke wa MTU Mpaka Akaambukizwa Ukimwi


Inasikitisha sana. Fuatilia mkasa huu mwanzo mwisho....

Mke alimhisi mmewe kuwa anatembea na housegirl wao kutokana na ukweli kuwa, housegirl alikuwa mzuri mno kimuonekano, kiumbo na kwa sura. Alifikiri kumfukuza ila mme aligoma kutokana na uchapakazi wa binti yule. Hivyo, hakuona sababu ya msingi ya kumfukuza. Hakika housegirl alikua akizidi kumnyima usingizi mke wa boss. Kadri siku zilivyozidi kwenda, housegirl alizidi kumeremeta. Kila nguo aliyovaa ilimpendeza. Kila mkao aliokaa alionekana ni wa kimitego na hofu iliendelea kutanda kwa mke wa boss.

Mke alizidi kuhisi na mbaya zaidi kila siku usiku wakati mmewe akiaga kuwa anaenda kuangalia mpira sebuleni baada ya muda mfupi mke alikuwa anasikia miguno chumba mwa housegirl hivyo akajua itakua tu ni mmewe huwa ananyata na kumuingilia housegirl wao ndio maana mme shughuli chumbani siku za karibuni ilionekana kumshinda kwa kuchoka haraka mno.

Jumamosi moja aliamua kumtuma housegirl kijijini kwa safari ya siku mbili bila kumjulisha mmewe wala mtu yeyote pale nyumbani. Usiku ule wa Jumamosi mme alimwambia mkewe utaratibu wake wa kawaida kuwa anaenda kuangalia mpira kwenye tv ya sebuleni. Kama kawaida, mke alikubali na mme akaenda sebuleni. Mke taratibu aliingia chumbani kwa housegirl akajilaza kitandani uchi kama alivyozaliwa. Kama kawaida alisikia mlango ukifunguliwa taratibu akaingia mtu akapanda kitandani na bila kuuliza akavua nguo akaanza kula tunda. Baada ya goli la 5, mke alisema, *_"INATOSHA. LEO NIMEKUKAMATA. KUMBE HIVI NDIVYO HUWA UNAFANYA NA HOUSEGIRL WAKATI UKIWA NA MIMI GOLI MBILI TU UNASEMA UMECHOKA? MCHEZO WAKO HUU NDIYO UNAKUMALIZA NGUVU NA UKIJA CHUMBANI KWANGU UNASEMA UMECHOKA WAKATI HAPA TAYARI MABAO MATANO NA UNATAKA UENDELEE?_*"

Kwa MSHTUKO, ghafla mme alijibu, "SAMAHANI mke wa boss sikujua kama ni wewe. Mimi ni houseboy wenu mkata majani; nisamehe tafadhali!"

Mke alishtuka akapiga kelele kwa kupaniki maana alimjua houseboy wao alivyo mwathirika hata kumuajiri pale kwao ilikuwa ni kwa kumsaidia maana yeye na mme wake wanamjua ni kijana yatima aliyekuwa amezaliwa na UKIMWI kwani wazazi wake walipofariki alitengwa na ndugu ndipo wakamsaidia wakamuajiri kuwa houseboy wao ili akate majani, kuzibua vyoo n.k.

Kelele alizopiga mama zilimkurupusha mmewe sebuleni na kuwasha taa za nyumba nzima kisha akaelekea chumba cha housegirl kujua nini kimemsibu mkewe. Alipoingia hakuamini macho yake kwa kumwona MKEWE AKIWA UCHI WA MNYAMA KITANDANI NA HOUSEBOY WAO AKIMBEMBELEZA UCHI KAMA WALIVYOZALIWA.

*_WIVU MBAYA JAMANI!!!_*

Ama kweli umdhaniaye ndie siye, na usilolijua ni usiku wa giza. Maskini mama mwenye nyumba kajiponza kisa wivu. Alijua mmewe anatembea na housegirl kumbe baba wa watu hana shida na mtu yuko busy na mambo yake. Sasa yamemkuta makubwa mama huyu aibu hii atamuelewa nani mbaya zaidi houseboy ni mwathirika. Je, kama ameambukizwa UKIMWI itakuwaje? Hakika, familia na nyumba nzima imekumbwa na giza nene. NAAMINI WENYE TABIA ZA KUHISI NA KUAMINI TETESI BILA KUTHIBITISHA MTAKUA MMEJIFUNZA KITU.

JE! UNGEMSHAURI MME ACHUKUE MAAMUZI GANI?

Mwanamke Aelezea Jinsi Askari Walivyombaka Msumbiji



Wakati Serikali ikiahidi kufanya uchunguzi wa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu katika kutimua Watanzania nchini Msumbiji, mwanamke mmoja amesema alibakwa na askari watatu kabla ya kuwekwa mahabausu ambako alikaa siku tatu bila kula.

Mwanamke huyo, aliyejitambulisha kwa jina la Halima (si jina lake halisi) ni mmoja kati ya zaidi ya Watanzania 180 ambao wamekuwa wakitimuliwa nchini Msumbiji tangu mwanzoni mwa wiki na wengi wakidai wana hati halali za kuishi nchi hiyo jirani na wengine kulalamikia vitendo vya ukiukwaji haki wakati wa utekelezaji wa operesheni hiyo.

Tayari Serikali imesema kuwa itafanya uchunguzi wa madai hayo, ambayo yanaweza kuharibu uhusiano wa muda mrefu wa Tanzania na Msumbiji.

Halima anasema walianza kufukuzwa usiku wa Jumamosi ya Februari 11, muda ambao askari hao waliutumia kumfanyia kitendo hicho.

Halima anasema kuwa alisikia watu wakivunja geti la nyumba waliyokuwa wakiishi na kudhania ni majambazi, kumbe walikuwa ni askari ambao waliwalazimisha kutoa nyaraka zao zote za kuishi Msumbiji pamoja na pesa.

“Niliwasikia wakivunja geti nikamwambia mume wangu watakuwa ni majambazi kumbe askari, mume wangu akajificha chini ya uvungu, lakini wakamtoa na baadaye kututoa ndani na kuanza kutupiga.”

Anasema baada ya kipigo walilazimishwa kuzoa mali zao kutoka ndani na zikawekwa kwenye gari la polisi na kisha kuwafunga mikono na baadaye kuwapeleka mahabusu.

“Cha kushangaza tulibebeshwa vitu wenyewe kuweka kwenye gari pasipo kuelezwa sababu baada ya hapo askari akanivuta nyuma ya nyumba na kuniingilia kimwili. Nikajua ni mmoja, lakini waliendelea hadi wakafikia watatu,” alisema.

“Ninaona aibu walinibaka kwa njia ya kawaida tofauti na taarifa za wengine wanaosema tulibakwa kinyume na maumbile, si kweli. Nawaomba waelewe hatukubakwa kinyume na maumbile kama wanavyosema ilikuwa kawaida.”

Hata hivyo anaeleza baada ya hapo waliwekwa mahabusu kwa siku tatu pasipo kula, hali iliyowalazimu kunywa maji yaliyokuwa yamewekwa chooni.

“Tulikaa mahabusu siku tatu, hamna kula wala kunywa, chooni tulienda kwa mtutu tukalazimika kunywa maji ya chooni kwa sababu hakukuwa na jinsi na njaa ilizidi. Kwa hiyo inabidi useme unakwenda chooni ili ukanywe maji,” alisema Halima.

Kutokana na hali hiyo, Halima anashangazwa na kauli ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Susan Kolimba kwamba waliorudishwa hawakuwa na nyaraka huku kaimu balozi wa Tanzania nchini Msumbiji akiwatangazia wengine kuondoka ndani ya siku tano.

“Kweli mtu utathubutu vipi kuishi nchi ya watu bila kibali? Hata kaimu balozi na yeye anatukana, kwamba hatujaingia na documents (nyaraka)? Ilibidi atutetee lakini katukana. Mungu atatulipia,” alisema.

Mwanamke mwingine aliyewekwa mahabusu kabla ya kurudishwa nchini, Mary Makundi anasema askari wa kiume walimwambia awape fedha na alipowajibu kuwa hana, walimpekua na kuzikuta.

Anasema walizichukua fedha hizo pamoja na simu kabla ya kumpiga na kutaka kumbaka.

“Walivunja mlango wakanikuta. Wakaniambia niwape nyaraka zangu. Nikawapa nikijua wanazikagua tu na kuniacha, lakini cha kushangaza walizichana mbele yangu na kunitaka niwape pesa na simu. Nikawaambia sina wakanipiga na kunikagua hadi sehemu za siri na kuchukua pesa na simu,” alisema Mary.

“Baada ya hapo walinipiga kwanza kabla ya kunifunga mkono. Askari mmoja akataka kunibaka, nikamwambia kuwa hata kama hawatutaki nchini kwao, hawawezi kuniingilia bila kinga.

“Nilipoona hali imekuwa mbaya, nilisema wacha nigombane nife kwa silaha, lakini si kubakwa.”

Mtanzania mwingine Mohamedi Said ni mmoja wa wafanyabiashara walioambiwa waondoke pasipo kuchukua chochote na anadai kuacha mali zake zote pamoja na nyumba aliyojenga.

“Polisi walikuja ghafla wakatuambia wageni wote tunatakiwa tuondoke. Hapa nina vibali vyote mpaka leseni ya biashara, lakini imebidi niondoke kwa sababu ya usalama wangu,” alisema Said.

“Hakuna anayejua sababu mpaka sasa. Nimekuja nyumbani kufuatilia haki yangu kwa sababu mpaka kibali cha kujengea ninacho.

“Mpaka sasa amekuja kaimu balozi kutoka ubalozi wa Tanzania na amesema kwa ripoti aliyopewa ametupa siku tano tuondoke. Hatujui kwanini siku tano. Utahamishaje vitu kwa siku tano au kumtafuta mnunuzi wa nyumba kwa siku tano kwa sababu imenibidi niache duka kubwa na gari,” alisema Said.

Akizungumzia tukio hilo, mwenyekiti wa Kijiji cha Kilambo kilichopo mpakani na Msumbiji, Mohamed Mkama alisema wananchi wa kijiji chake wamekuwa wakishirikiana na wanakijiji wa vijiji jirani vya Msumbiji, lakini tukio hilo limewashangaza.

Amesema mara nyingi wamekuwa wakitembeleana na hata wengine kutoka upande wa Msumbiji kuja kutibiwa Tanzania kutokana na ujirani mwema uliopo.

“Kijiji changu kina vitongoji vitano ambavyo tumekuwa tukishirikiana na kijiji cha upande wa pili kwa muda mrefu na wengine wana vitambulisho vya uraia mwema, lakini tunashangaa kwanini wanarudishwa pasipo kuelezwa sababu,” alisema Mkama.

Ofisa uhamiaji Mkoa wa Mtwara, Rose Mhagama alisema idadi ya Watanzania waliorudi na kusajiliwa katika mpaka wa Kilambo ni watu 221 hadi kufikia jana mchana.

Makubwa Haya..Ray C Afunguka Kumpenda Rayvanny,Adai Anatamani...!!!

Msanii mkongwe wa Bongo Fleva mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni, Ray C amedai kuwa anamkubali zaidi Rayvanny kutoka lebo ya WCB.
Ray C amesema kuwa amesikia msanii huyo amewaandikia wasanii wengi nyimbo hivyo na yeye anatamani siku moja aje kufanya naye kazi.
“Nampenda sana yule mtoto Rayvanny. Anaandika sana mashairi, nasikia anaandikia wasanii wengi nyimbo hata mimi natamani kufanya naye kazi,” Ray C amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.
Mbali na hilo msanii huyo ameongeza kuwa anamheshimu sana Diamond Platnumz kutokana na kule alipofika kwakuwa muziki wake umefika sehemu ambayo wao hapo mwanzo hawakuwahi kufika.

Baada ya Sekeseke la Madawa ya Kulevya Kutulia,TID Aamua Kumtaja Tena Diamond..!!!

Kwa sasa msanii TID Mnyama anahakikisha anarudisha makali yake ya zamani kwenye muziki. Muimbaji huyo amewaahidi mashabiki wake kufanya kazi na Diamond hivi karibuni.
Akiongea kwenye kipindi cha XXL, kupitia Clouds FM Ijumaa hii, Mnyama amesema kuna nyimbo anayofikiria kumshirikisha Diamond ambaye taarifa hizo tayari ameshazipata.
“Nina ngoma nafikiri itafaa zaidi nikimshirikisha Diamond. Diamond ameshapata habari nafikiri tutaifanya ngoma hiyo soon as possible,” amesema TID.
Kwa sasa msanii huyo ameachia wimbo wake mpya aliomshirikisha rapper Fid Q unaojulikana kama ‘Maisha ya Jela’ pamoja na mwingine uitwao Woman.

Binadamu Kuanza Kuwekewa Moyo wa Plastiki,Soma Hapa Kujua Utakavyofanya Kazi...!!!


NCHINI Marekani kila baada ya dakika 10 mtu mmoja huwekwa kwenye foleni ya watu wanaosubiri kuwekewa moyo mpya ili kuweza kuendelea kuishi. Hali hii hotokea baada ya moyo wa mgonjwa kuonekana hauwezi kufanyiwa matibabu na hivyo njia pekee ya kuokoa maisha yake ni kupata moyo mpya ambao huwekewa kwa njia ya upasuaji (transplant).
Shirika la Umoja wa Kuchangia Viungo, linasema kuwa takribani watu 22 hufariki dunia kila siku nchini Marekani wakiwa katika foleni ya kusubiri mtu wa kujitolea moyo kwa ajili ya kuokoa maisha yao. Hata hivyo, wagonjwa wa aina hii sasa wanaweza kufurahia baada ya ugunduzi wa moyo wa bandia ambao inawezekana wakautumia kwa maisha yao yote (Total Artificial Heart)TAH).
Mtu anayechangia moyo (donor) anaweza kuwa ni mtu ambaye tayari ubongo wake umekufa lakini mwili bado una uhai na hivyo moyo wake kuwa mzima. Mgonjwa wa aina hii hawezi kupona. Mgonjwa yeyote ambaye ana hali mbaya lakini ugonjwa wake hauhusiani na moyo na ambaye hawezi kupona pia anaweza kujitolea moyo. Mtu aliyefariki pia anaweza kutolewa moyo na kusaidia wenye uhitaji lakini mara nyingi hii huwa ni kwa ridhaa yake kabla hajafariki.
Ukiwa umegunduliwa kwa mara ya kwanza takribani miaka 60 iliyopita, moyo wa bandia wa wakati huo uliwawezesha wagonjwa waliokuwa wakisubiri kupata mtu atakayejitolea kupatikana na uliweza kumsaidia mgonjwa kwa muda tu. Ugunduzi huu mpya, unaweza kutoa suluhisho la kudumu kwa kuwa moyo huo unalenga kumwezesha mgonjwa kuishi maisha yake yote.
Historia inaonyesha kuwa, kipindi kirefu ambacho mgonjwa ameweza kuishi kwa msaada wa teknalojia ya moyo wa bandia uliojulikana kitaalamu SynCardia temporary TAH ni miaka minne.
Katika kile ambacho kinaelezwa kama hatua nzuri ya ugunduzi, Kampuni inayohusika na matatizo ya moyo ya nchini Marekani inayojulikana kama SynCardia Systems Inc inaendesha utafiti na kufanya uchambuzi wa kina kuona kama TAH inaweza kuwa suluhisho la kudumu kwa wagonjwa wanaohitaji kubadilishiwa moyo na kushindwa kuupata kwa wakati kutokana na kuongezeka kwa mahitaji.
“Mwishoni mwa miaka ya 1960 wakati wagonjwa walipoanza kuwekewa mioyo mipya kutoka kwa binadamu wengine, upatikanaji wa kiungo hicho muhimu kwa maisha ya binadamu ulikuwa mkubwa. Upatikanaji wake ulikuwa mkubwa kuliko mahitaji lakini kwa sasa mahitaji yameongezeka zaidi na upatikanaji umepungua,” anasema Danald Isaacs ambaye ni Makamu wa Rais wa SynCardia, akiliambia Shirika la Habari la Fox.com.
Idara ya Afya na Huduma za Binadamu ya Marekani inakadiria kuwa watu 4,000 husubiria kupata moyo mpya ili waweze kuendelea kuishi kila siku wakati mioyo 2,300 ikiwa inatolewa.
Ugonjwa wa moyo ni chanzo namba moja cha vifo nchini Marekani ukigharimu maisha ya watu 611,000 mwaka 2015, hii ni kwa mujibu wa Kitua cha Kupambana na Kuzuia Magonjwa cha nchi hiyo (CDC)
Wakati wa kumwekea mgonjwa moyo wa bandia au TAH, daktari huondoa kwa njia ya upasuaji ventrikali ya kulia pamoja na valvu nne kama ambavyo hufanyika wakati mgonjwa akiwekewa moyo ambao hutolewa na binadamu mwingine ambapo huwekwa wa bandia badala yake.
“Asilimia 96 ya mfumo wa kuweka moyo bandia ni ule wa SynCardia Temporary TAH ambao hutoa suluhisho la muda tu,” anasema Isaacs. Takwimu za SynCardia zinaonyesha kuwa wagonjwa 1,123 wamewekewa mfumo huo ambao ni modeli 70cc.
John Beckingham, mwenye umri wa miaka 58 ambaye ni mhandisi mstaafu anayeishi katika eneo la Rochester jijini New York alifanyiwa upasuaji uliofanikisha kuwekewa moyo mpya katika hospitali ya Cleverland, Oktoba mwaka 2015 baada ya kukaa miezi sita kwenye foleni ya kusubiria. Wakati akisubiria alikuwa akitumia mashine maalumu ambayo ilikuwa ikitumia betri  na ambayo ufanisi wake haukuwa sawa na teknalojia hii mpya.

Kudadadeki..Hivi Ndivyo Mbowe Alivyofanikiwa Kuwatoroka Polisi Mchana Kweupe Wakati Wakimtafuta..!!!

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam, limemtaka Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kujisalimisha Polisi mara moja kwa ajili ya Mahojiano yanayohusu vita vya dawa za kulevya baada ya juhudi za kumsaka katika makazi yake kushindikana huku simu yake ya mkononi ikiwa imezimwa 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Simon Sirro amesema Bw. Mbowe aliahidi kwenda mwenyewe juzi tarehe 15, lakini hakwenda lakini jeshi la hilo lilimtafuta usiku na mchana katika makazi yake na kumpigia simu lakini simu yake ilizimwa 
Aidha jeshi hilo limesema watuhumiwa watatu Agnes Masogange, Rashid Idd au Chid Mapenzi na Wallis Latif Nasher ambaye ni muuza magari katika eneo la mikocheni watapandishwa kizimbani Jumatatu kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya lakini pia walibainika wanaotumia dawa hizo baada ya kupelekwa kwa Mkemia Mkuu 
Katika kupambana na Askari feki, jeshi limemtia mbaroni aliyekuwa askari Magereza wa cheo cha Koplo Peter Elias Msigwa aliyekuwa mtumishi katika gereza la keko, ambaye alifukuzwa kazi Desemba mwaka jana, lakini alikamatwa jana akiwa na mavazi ya kiaskari tena akiwa amejipandisha cheo kutoka koplo hadi Sajenti wa Polisi 
Jeshi hilo pia limesema limewatia mbaroni watu 65 kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya pamoja na watuhumiwa 73 wa wizi na ujambazi wa kutumia silaha, mitambo mitano ya Gongo, lita 270 pamoja na Puli 250 za bangi.

Mbeya : Mama Afukua Kaburi la Mwanae,Kisa Kamili Hiki Hapa...!!!

Katika hali isiyo ya kawaida mama mmoja mwenyeji wa mkoa huu wa mbeya mji mdogo wa mbalizi, usiku wa kuamkia leo alienda kaburini alikokua kafukiwa mwanae aliyefariki dunia Siku ya jumatatu na kuzikwa jumanne ya wiki Hii na kufukua kaburi hilo na kuitoa maiti 
Kwa mujibu wa mama huyo maarufu Kama mama vumi anadai aliambiwa na mchungaji kuwa mwanae hajafa Bali Kuna sehemu anafanya kazi hivo aende akaitoe ile maiti kaburini ili iombewe irudi kuwa binadam wa kawaida,
Jana usiku yule mama ndio akaenda kuifanya kazi aliyotumwa na mchungaji wake ambapo leo asubuhi ndio raia wakagundua ishu na kwenda kukinukisha kwa yule mama, polisi walifika eneo la tukio na kumuokoa yule mama toka kwenye mikono ya wananchi wenye hasira Kali na kuondoka nae pamoja na maiti ya mtoto

Makonda Hakukosea Kumtaja Wema Sepetu - Martin Kadinda


Meneja wa zamani wa Wema Sepetu, Martin Kadinda amedai Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda hakukosea kumtaja Wema Sepetu kwenye list yake ya watuhumiwa wa biashara haramu ya madawa ya kulevya kutokana na aina ya marafiki ambao amekuwa nao.


Martin amedai yeye alitumia nguvu nyingi kumshauri muigizaji huyo kuachana na marafiki wasioeleweka.

“Nadhani nilishakaa na Wema nikamwambia jina lako ni kubwa sana, unatakiwa kuwa na nguvu usiwe maarufu tu. Kwahiyo hichi ambacho kimetokea siwezi kuliongelea kwamba ni jambo baya au zuri lakini nadhani hii ni alarm ya kuamka,”


Aliongeza, “Sidhani kama mkuu wa mkoa alikurupuka tu akamtaja Wema, wametajwa watu wengi, labda ni kutokana na marafiki aliyokuwa nao au magroup au labda kuna mtu alienda kule akamwambia mkuu wa mkoa Wema anashiriki jambo hili, kwahiyo sidhani kama mkuu alikurupuka akamtaja Wema hapana. Lazima kuna chanzo ndiyo maana nasema ngoja tuangalie kwa sababu bado kesi iko mahakamani tutajua tu,”


Martin amedai Wema anatakiwa kubadilika na kujitenga na watu ambao wanaweza kumwingiza katika matatizo kama aliyotokea.

Ripoti ya Ugunduzi Mpya wa Bara la 8 Duniani



Wanasayansi wafahamisha kuwa bara la 8 lawezekana kuwa lipo chini ya bahari ya Pasifiki.


Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa katika jarida la Marekani la 'Geological Society of America' ni kwamba bara hilo limepewa jina la Zealandia .


Bara hilo lililokubalika na wanasayansi linasemekana kupatikana katika upande wa Kusini Magharibi mwa bahari ya Pasifiki.


Liko na ukubwa wa kilomita milioni 5 za mraba sawa na thuluthi ya ardhi ya bara la Australia .


Wanasayansi wamesema kuwa bara hilo limefinikwa na maji ya bahari .