Jumatano, 23 Julai 2014

Hospitali ya Muhimbili imesemaje kuhusu mabaki ya binaadamu Tegeta?

Jeshi la Polisi linawahoji watu nane wakiwemo Madaktari wa chuo cha kitabibu cha IMTU kwa madai ya kutupa mabaki ya masalia ya binadamu katika msitu mdogo uliopo eneo la Mpiji kata ya Mbweni wilayani Kinondoni Dar es salaam.
Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova alisema kulipatikana mifuko 85 iliyobeba mabaki ya masalia hayo ya binadamu.
‘Imeonekana mara ya mwisho viungo hivyo vilikua katika chuo cha Udaktari cha IMTU kinachofundisha kwa vitendo pia, sasa tunachunguza na wamekubali kuhojiwa, maswali yanayofata ni kwanini viungo hivyo vilikua pale kwa wingi kiasi hicho? kwa nini vilikwenda kutupwa? ‘ – Kova
Screen Shot 2014-07-24 at 3.44.25 AMKwenye hii ishu pia hospitali ya taifa Muhimbili inachunguzwa ambapo mkuu wa kitengo cha uhusiano kwenye hospitali hii ya taifa Aminiel Aligaesha amesema >> ‘Sisi ni miongoni mwa wanaochunguzwa kwa sababu ni hospitali mojawapo katika jiji la Dar, mabaki yale hayakutoka hospitali ya taifa Muhimbili’
‘Kuharibika kwa tanuru letu la kuchoma taka za kitabibu kama hizo hakuna uhusiano na mabaki ya binadamu yaliyookotwa Tegeta, ni kweli tanuru liliharibika February 2014 na mwezi April tukapata spea lakini tatizo jingine likatokea na kipuri kingine kikaagizwa na mpaka sasa mafundi wanaendelea kuitengeneza’ –Na mimi Nickson Luvega.

Kilichoendelea kesi ya Mbasha Mahakamani July 23 2014, kakubali sentensi mbili tu.

KESI ya ubakaji inayomkabili mume wa Flora Mbasha ambae ni mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili Tanzania Emmanuel Mbasha (32), ilitajwa tena July 23 2014 katika mahakama ya wilaya ya Ilala ambapo Mbasha amesomewa tena mashataka yake huku akikubali sentensi mbili tu kati ya nne zilizosomwa.
Akisoma hoja hizo mbele ya hakimu Wilbert Luago, mwendesha mashtaka wa serikali Nasoro Katunga alisema May 23 2014 mtuhumiwa alimbaka binti aitwaye  Yerusalemu Boazi (17) ambae ni mdogo wa Flora na kumlazimisha asimwambie mtu yoyote ambapo wakati akitenda kosa hilo mkewe Flora hakuwepo nyumbani.
Katunga aliendelea kufafanua kuwa May 25 2014 Mbasha alirudia tena kitendo cha ubakaji baada ya kumuomba binti huyo amsindikize kumtafuta mke wake ambae hakuwepo nyumbani ambapo walipofika Tabata peke yao, Mbasha alimbaka tena binti.
Hizo sentensi zote mbili za juu Mbasha amezikana Mahakamani kwa kusema sio kweli.
Hata hivyo iliendelea kuelezwa kwamba tukio hilo la ubakaji liliripotiwa katika kituo cha polisi Tabata ambako Boazi alipewa PF3 kwa ajili ya kupata matibabu ambapo uchunguzi uliofanywa ulionyesha ni kweli binti huyo aliingiliwa kimwili.
Mbasha 25
Mbasha akiwa na baba yake mzazi Mahakamani.
Katika kesi hiyo ambayo Mbasha anatetewa na wakili Mathew Kakamba, Mbasha alikubali sentensi mbili na kuzikataa mbili zilizobaki kwamba alimbaka binti huyo.
Alichokubali ni kusema ni kweli alimuomba binti huyo amsindikize kumtafuta mke wake ambaye hakuwepo nyumbani na pia alikubali ni kweli Mei 23 2014 mke wake Flora Mbasha hakuwepo nyumbani.
Baada ya kusomewa mashataka hayo na mwendesha mashataka wa serikali, Jaji Luago aliahirisha kesi hiyo hadi August 22 2014 baada ya wakili anayemtetea Mbasha kudai atakuwa na safari kwa siku za karibuni nje ya Mkoa.

Real Madrid yamsajili mkali wa mabao James Rodriguez

rodr
Real Madrid wamekamilisha usajili wa mshindi wa kiatu cha dhahabu katika michuano ya World cup ndani ya Brazil 2014. James Rodriguez
mshambuliaji  kutoka Colombia ana umri wa miaka 23 na amesaini mkataba wa miaka sita na Real Madrid akitokea club ya  Monaco.


Ripoti zinasema gharama ya uamisho ni pauni milioni 63 na kumfanya mchezaji wa nne wa uhamisho wa gharama akiwa nyuma ya Gareth Bale, Cristiano Ronaldo na Luis Suarez.


Kama umesahau ni kwamba Rodriguez alifunga magoli sita katika mechi tano za world cup hadi kuifikisha timu yake ilipofika katika robo fainali. Picha hapo chini ni  James Rodriguez akiwa katika vipimo vya afya Real Madrid.

kk

Baada ya Davido kuambiwa anajionyesha na mali zake kwenye instagram..amejibu kama ifuatavyo..

dadivoMsanii staa wa Nigeria Davido ni mtu ambae huwa anaonyesha kwenye mitandao vitu vingi anavyonunua mfano saa za Rolex za dhahabu, magari ya kifahari, nyumba na vitu vingine ambapo baada ya kuulizwa kuhusu ishu hii ya kupenda kuonyesha mali zake amejibu “sitoweza kusema kama ni kujionyesha kwa mali zangu, yale ni magari yangu, zile pesa zangu na pia ile ni page yangu’
Sio lazima unifollow kwenye instagram wala kunifata kwenye mtandao wowote wa kijamii, ingekuwa tofauti sana kama nataka kujitangazia mali zangu basi ningetumia mabango ya barabarani lakini sifanyi hivyo.
wwwwwwwwwwwwwwwUnadhani ni sahihi kwa mastaa kuonyesha mali zao na pesa kama hivi kwenye mitandao ya kijamii? niachie comment na like yako hapa chini mtu wangu ili twende pamoja.

Picha za actors 10 waliotajwa na Forbes kwa kulipwa pesa nyingi 2014

dola
Forbes.com kwa wakati huu wametoa list ya mastaa 10 wa kiume ambao wamelipwa pesa nyingi zaidi kwenye kazi zao za filamu. Muigizaji mweusi ni Will Smith peke yake kwenye top 10 wengine wote ni wazungu.
1 Robert Downey Jr – $75 million
2
2 Dwayne Johnson – $52 million
1
3 Bradley Cooper  – $46 million
3
4 Leonardo DiCaprio – $39 million
4
5 Chris Hemsworth – $37 million
6
6 Liam Neeson – $36 million
l
7 Ben Affleck – $35 million
5
8 Christian Bale – $35 million
chris
9 Will Smith – $32 million
dd
10 Mark Wahlberg – $32 million
dfff

Listi ya mastaa wa Real Madrid watakao tembelea bongo

http://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2014/07/d8f4b35c644f0423a21a23076ac82592-660x320.jpgVODACOMA Tanzania ni miongoni mwa makampuni yaliyojitokeza kudhamini ziara ya magwiji waliocheza kwa mafanikio makubwa katika klabu ya Real Madrid.
Kikosi cha magwiji hao maarufu kama `Real Madrid Legends` kitafanya ziara ya siku nne nchini kuanzia Agosti 22 mwaka huu na kitacheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya kikosi maalumu cha nyota wa Tanzania.
Akizungumza leo na waandishi wa habari katika hoteli ya New Afrika, jijini Dar es salaam, meneja wa ziara hiyo, Dennis Ssebo amesema  mbali na Vodacom, wadhamini wengine ni Fastjet, Tropical, Pembe Flower, Lake Gas, EFM Radio na Ladger Plaza Bahari Beach.
Ziara hiyo ni mwaliko wa kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), chini ya mkurugenzi wake mkuu, Farough Baghozah na meneja wa ziara hiyo ni Dennis Ssebo.
Wachezaji wa Real Madrid waliocheza La Liga miaka ya nyuma, ligi ya mabingwa kombe la dunia kama vile Mfaransa Zinedine Zidane, Mreno Luis Madeila Figo na Mbrazil Ronaldo de Lima watakuwepo katika ziara hiyo.
Ssebo kabla ya mkutano wa leo, aliuambia mtandao huu kuwa maandalizi ya ziara hiyo yanakwenda vizuri na itakuwa fursa pekee kwa Watanzania kuiona Real Madrid kwa mara ya kwanza barani Afrika.
 “Ninaloweza Kusema ni kwamba,  Watanzania wakae tayari kupokea wachezaji 27 wa zamani wa timu ya Real Madrid na mashabiki 23  kutoka Hispania wanaokuja kuwashangilia magwiji wao. Kwahiyo jumla tunapokea watu 50 kutoka Hispania kwa ajili ya ziara hii”. Alisema Ssebo.
“Ni ziara ambayo tulifikiria itakuwa fupi, lakini wenzetu kumbe wameipenda nchi na wanaifahamu, kwahiyo ni ziara ambayo itachukua takribani siku nne”. Aliongeza.

TBL YATOA MSAADA WA SH. MIL. 45 ZA KISIMA KIJIJI CHA KAMBI YA SIMBA KARATU


Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu akipeana mkono na Mwenyekiti wa Kijiji cha Kambi ya Simba, Damian John wakati wa makabidhiano ya mfano wa hundi ya Sh. Milioni 45 zilizotolewa kwa ajili ya kuchimba kisima cha maji kijijini hapo mwishoni mwa wiki. Wengine ni Meneja Mauzo TBL Mkoa wa Arusha Richard Temba (mwenye miwani) na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Karatu Moses Mabula.
 Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kambi ya Simba, Kata ya Mbulumbulu wilayani Karatu, Arusha, wakati wa hafla ya kuwakabidhi mfano wa hundi ya sh. mil. 45 za kugharamia uchimbaji wa kisima cha maji kijijini hapo, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Mauzo TBL Mkoa wa Arusha Richard Temba na aliyekaa ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Karatu, Moses Mabula. (N.L)

 Wananchi wa kijiji hicho wakishuhudia makabidhiano ya hundi hiyo
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Karatu, mkoani Arusha, Moses Mabula na Meneja Mauzo TBL Mkoa wa Arusha Richard Temba wakiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Maji ya Kijiji cha Kambi ya Simba pamoja na watalaamu watakaochimba kisima hicho cha maji, baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya Sh. Milioni 45 na TBL.

AJALI YA NDEGE YAUA 51 TAIWAN

Taswira kutoka eneo la ajali. Vikosi vya uokoaji vikiwa eneo la tukio. TAKRIBANI watu 51 wamepoteza maisha huku saba wakijeruhiwa baada ya ndege waliyokuwemo kuanguka iliposhindwa kutua kwa dharura huko Taiwan, nchini China. Ndege hiyo ya Shirika la TransAsia iliyokuwa imebeba watu 58 imeanguka eneo la Kaohsiung.

MADEREVA WA VYOMBO VYA MOTO MUWE MAKINI

Gari aina ya Toyota Hilux limetumbukia kwenye mtaro uliopo Sinza-Makaburini jijini Dar es Salaam baada ya dereva aliyekuwa akiliendesha gari hiyo kushindwa kulimudu.Inashauriwa kwa madereva wote wawe makini wawapo barabarani ili kuepusha hasara zisizo za lazima. Pichani wasamaria wema wakishirikiana kulinasua gari hilo.

LOWASSA AKAGUA SHULE ILIYOUNGUA HUKO MONDULI


Kiasi cha wanafunzi 100 wa shule ya sekondari ya Erikisongo wilayani Monduli wamenusurika kifo baada ya vyumba vitano vya mabweni yao kuteketea na moto leo (Jumatano) asubuhi.
Moto huo ambao inaelezwa chanzo chake ni hitilafu ya umeme ilitokea wakati wanafunzi wote wako darasani.
Hakuna mtu yoyote aliyedhurika lakini mali kadhaa za wanafunzi zimeteketea. Kikosi Cha zimamoto kutoka Arusha kilifika wakati tayari mabweni hayo yameshateketea.
Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh Edward Lowassa  ametembelea shule hiyo na kuahidi kuwasafirisha wanafunzi majumbani kwao wakati  utaratibu unafanywa kurejesha katika hali ya kawaida.
Gharama za kuwasafirisha wanafunzi hao ni shilingi laki Saba. Aidha Mh Lowassa amesema kiwanda Cha magodoro Cha Tanform Cha Arusha kimetoa msaada wa magodoro 100 kufuatia kadhia hiyo.
Kikosi Cha zimamoto kikijaribu kupambana na moto ulioteketeza mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo mjini Monduli. Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akikagua mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo mjini Monduli yaliyoteketea kwa moto, akiongozana na mkuu wa shule hiyo mwalimu Agnes Nyange. Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akikagua mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo Monduli mjini yaliyoteketezwa kwa moto. Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akipata maelezo kutoka kwa afisa elimu wa Monduli mwalimu Shaaban Mgunya wakati alipotembelea mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo wilayani Monduli yaliyoteketea kwa moto.

Ajali ya Ndege:Miili imewasili Uholanzi

Miili ya abiria wa ndege ya Malaysia MH17 imewasili Eindhoven
Ndege mbili za kijeshi zinazobeba miili 40 kati ya 282 ya abiria wale waliofariki kutokana na mkasa wa ndege ya Malaysia iliyodunguliwa huko mashariki mwa Ukraine , imewasili Uholanzi.
Theluthi mbili ya waliofariki kwenye mkasa huo yaani 193 ni raia wa Uholanzi na nchi hiyo iko katika siku ya maombolezi ya kitaifa na bendereza ziko nusu mlingoti.
Mfalme na malkia wa Uholanzi , waziri mkuu na viongozi wengine wako Eind-hoven pamoja na jamaa za waliouawa kupokea miili ya marehemu.
Bado haijaeleweka ni miili mingapi kati ya ile wa watu 282 waliouawa , imefikishwa hapo jana.
Miili ya abiria wa ndege ya Malaysia MH17 imewasili Eindhoven
Vifaa vya kurekodia mienendo ya ndege hiyo vimekabidhiwa wapepelezi wa Uingereza na maelezo kuvihusu yatakabidhiwa majajusi wa uholanzi .
Maafisa wa kijasusi wa Marekani wamesema waasi wanaoiunga mkono Urusi waliitungua ndege hiyo kimakosa, lakini hakuna viashiria vyovyote kuhusu tukio hilo,vinavyohusiana moja kwa moja na Urusi.
Waasi wameshutumiwa kuwakwamisha wapelelezi kwa kuwapa ushahidi wenye mashaka na kutoa taarifa zisizo sahihi kuhusu idadi ya miili iliyopatikana.
Katika hatua nyingine maafisa wa nchini Malaysia wamekabidhi kisanduku cheusi chenye kurekodi mawasiliano ndani ya ndege kwa mamlaka za uholanzi.
Chanzo:BBC

TOFAUTI ZA DINI ZISIWAGAWE WATANZANIA ,MWINYI

Futari - 1
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akiongea na watoto wanaotoka katika vituo mbalimbali  vya kulelea watoto yatima vya  jijini Dar es salaam , wakazi wa jiji la Dar es salaam na viongozi mbalimbali wakati wa Futari aliyooiandaa jana usiku katika viwanja vya Karimjee.

Futari - 3
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi akiwasili katika viwanja vya Karimjee kuhudhuria Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (wa pili kutoka kushoto) kwa watoto yatima kutoka vituo mbalimbali vya kulelea watoto hao vya jiji la Dar es salaam. Wengine wanaoonekana kutoka kulia ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Suleiman Kova na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhadi Mussa Salum.

Futari - 7
Baadhi ya akina mama na watoto waliohudhuria Futari hiyo wakipata Chakula.

WAZIRI MKUU AFUNGUA MKUTANO WA TATHMINI YA UTEKELEZAJI BRN

1
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Benno Ndulu akichangia hoja wakati wa mkutano wa kupitia taarifa ya mwaka mmoja ya utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa sasa (BRN) uliofanyika leo Jumatano Julai 23, 2014 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Bashir Mrindoko

2.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akichangia hoja wakati mkutano wa kupitia taarifa ya mwaka mmoja ya utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa sasa uliofanyika leo Jumatano Julai 23, 2014 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Asha- Rose Migiro na (katikati) Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Rais- Usimamizi wa Utekelezaji wa Miradi (PDB), Bw. Omari Issa.

3.

MONACO YAINGIA VITANI NA REAL MADRID KUISAKA SAINI YA TORRES

article-2702058-1FE098CC00000578-953_634x433
Monaco na Atletico Madrid wanaitaka saini ya Fernando Torres.
KLABU ya Monaco imeingia katika vita na Atletico Madrid kuiwinda saini ya mshambuliaji wa Chelsea, Fernando Torres.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania mwenye miaka 30 anahitaji kutafuta timu ya kupata nafasi ya kucheza, lakini Chelsea watasikiliza ofa nzuri zaidi.