Ijumaa, 9 Juni 2017

Kajala Aibuka na Haya Kuhusu Wema Sepetu..Adai Hata Mwanae ni Shahidi..!!!



TASNIA ya filamu nchini imepambwa na wasanii wa kike wenye urembo unaovutia macho na hakika kwenye orodha ya waingizaji wenye kipaji, uwezo na mvuto huwezi kumuacha, Kajala Masanja.

Huyu ndiyo bosi wa kampuni ya Kajala Entertment,  ambayo imetengeneza filamu nyingi ikiwemo ile ya Sikitu ambayo chini ya mpicha Farid Uwezo iliweza kufanikiwa  kuliteka soko hilo la filamu.


Juma3tata wiki hii lipo na mrembo huyu, mpenzi wa chakula aina ya ndizi na samaki sato ambapo amefunguka mambo kadha wa kadha yanayohusu maisha yake ya ustaa na yale ya kawaida.

MKASA WA JELA WAMFUNZA

“Nina mfano halisi kabisa katika maisha na nitahakikisha namfunza mwanangu Paula asije akakutana na mkasa ulionikuta mimi na kufanya niingie jela kwa kuwa nilimsapoti mtu hata kwa yale yasiyostahili kisa nilikuwa nampenda,” alisema Kajala.

HATAKI KUFANYA TENA KOSA

Kajala amezidi kulifahamisha Juma3tata kuwa hapendi kulikumbuka tukio lile lililomfanya akae jela kwa muda wa mwaka mmoja na kumwacha mtoto wake kwenye wakati mgumu na hataki tena kufanya uzembe uliosababisha kosa lile.

 “Naweza sema ni uzembe ambao nilijitakia mwenyewe,  kumwamini mtu wakati kabisa najua ananiingiza shimoni ni kitu ambacho hakitafutika maishani mwangu, sitafanya kosa tena” anasema Kajala.

AWAONYA WAREMBO WENGINE

“Nataka wasichana wenzangu wajifunze kupitia mimi yaani hata kama unampenda mtu, usikubali akushawishi uvunje sheria za nje, jitahidi ujinasue kwani mwisho wake ni mbaya sana,” anasema.

HATASAHAU HURUMA YA WEMA SEPETU

Mara baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 7 au faini ya shilingi milioni zaidi ya kumi, Kajala na ndugu zake  waliingiwa na hofu kwani fedha hiyo ilikuwa ni kubwa kwao na hapo ndipo Wema Sepetu alipoibuka shujaa.

“Kama asingekuwa Wema Sepetu kunilipia zile  pesa sijui sasa hivi ningekuwa wapi, kwani hata ndugu zangu walichanganyikiwa kusikia kiasi kikubwa kile cha fedha ila moyo wa huruma wa Madame ulisababisha nitoke, siachi kumwombea katika sala zangu mwanangu pia analijua hilo,” anasema Kajala.

AZIPONDA TIMU MTANDAONI

Aidha aliweka wazi kusikitishwa timu katika mitandao ya kijamii zinazoibua maneno ya kuchochea ugomvi kati yake na Wema kitu kinachomuumiza kwani kwake ni mtu wa thamani mno.

KUFA KWA SOKO LA FILAMU

Katika hatua nyingine  mrembo huyo  alizungumzia anguko la filamu huku akikanusha taarifa hizo kwa kuwa wasanii wa bongo bado wanapiga kazi huku wengine wakishirikishwa na wasanii wa mataifa mengine.

“Kama soko la filamu limekufa basi wasanii wasingepata kazi za nje, sasa hivi wasanii tunaitwa kufanya filamu nchi za nje kwa malipo mazuri, tamthilia zetu pia zinaruka kwenye ving’amuzi mbalimbali, nchi nyingi zinazojifunza Kiswahili zinategemea filamu zetu kwa hiyo tunazidi kuvuka mipaka na kufanya vizuri,” anasema Kajala.

AWACHANA WASAMBAZAJI

Kajala amewataka wasambazaji kuwalipa wasanii kwa wakati mara wanapowekeana saini mikataba ya kusambaza filamu zao na siyo kuwalipa wasanii kwa awamu kitu kinachowafilisi wasanii.

 “Wasambazaji wa Kihindi waache  kutuzungusha kwenye malipo, kingine waache kubagua wasanii, waache kuangalia staa gani yupo ndani ya filamu ndiyo wanunue, waangalie ubora wa kazi na siyo sura,” anasema.

ANAAMINI KWA WASANII WACHANGA

Staa huyu wa filamu amesema anaamini katika vipaji vya wasanii wachanga, anaamini kuna kazi nzuri zinatengenezwa na wasanii wachanga lakinni wasambazaji huzikataa kwa sababu hawana ustaa.

Vita Ya Malipo Kiduchu Haijawahi Kumuacha Modo Salama!


Amber Lulu
AMANDA Swartbooi moja kati ya wauza nyago katika video Afrika akitokea Afrika Kusini. Amanda ametokea kujizolea umaarufu kwa kipindi kifupi cha mwaka jana ambapo ametokea katika video kadhaa Afrika ikiwemo Coolest Kid ya Davido akimshirikisha Nasty C wa Afrika Kusini, Four4 ya JR pamoja na Show Me ya Rich Mavoko akiwa na Harmonize.

Licha ya kufanya poa huko, ameshawahi kukiri kuwa kuuza nyago katika video hizo kunamlipa kwani kumempa mafanikio ya kujisomesha katika Chuo Kikuu cha Afrika Kusini (UNISA) akiwa mwaka wa pili katika masomo ya biashara. Ukija Bongo wapo wauza nyago katika Video za Kibongo ambao ni ‘visu’ lakini wanaangushwa na malipo kiduchu kutoka kwa wasanii husika kiasi cha kufikia kuangalia kazi nyingine za kufanya huku baadhi wakijiingiza katika muziki.
Agness Masogange


Katika makala haya nimekuchambulia baadhi tu ya wauza nyago (modo)ambao vita hii ya malipo kiduchu haijawahi kuwaacha salama kwani wengine wameamua kuachana na kuuza sura na wengine kujiingiza katika kuimba.

Alikuja kwa kasi, akavuma katika Video ya Kwetu ya Rayvanny na baada ya hapo akatokomea. Kutokana na kuitendea haki video hiyo, wengi walimtabiri kama miongoni mwa wauza nyago watakaokuja kuliteka soko. Hajashiriki tena katika kuuza sura kwenye video nyingine hadi sasa huku ikisemekana kukwepa malipo kiduchu kwa kila anayemfuata kufanyanaye kazi.


Alianza kuuza sura katika Video ya Naogopa ya Mirror kisha katika Remix ya Burger Movie Selfie ya Belle9 na baada ya hapo aliamua kuachana na suala la kuuza nyago na kujiingiza rasmi kwenye Muziki wa Bongo Fleva. Lulu anasema malipo kiduchu na mastaa wengine wakitaka kumtumia bure katika video zao ndivyo vilivyomkimbiza kwenye kuuza sura na kuamua kuimba ambapo kwa sasa anabamba na Ngoma ya Usimuache.

lulu Diva
Ni modo ambaye pia muuza nyago katika video za Kibongo. Kutokana na malipo kiduchu katika video hizo kumemfanya kupotea kimyakimya katika orodha wauza sura Bongo. Ameshawahi kukiri kulipwa kiasi kikubwa katika video moja tu (Salome ya Diamond) tangu aingie katika kuuza nyago huku akiwa na kumbukumbu ya kulipwa kiduchu katika Video ya Magubegube ya Barnaba.
Gigy Money



Naye ni miongoni mwa wauza nyago walioanza kupotea kwenye ramani ya muziki Bongo kisa hazilipi. Alianza kutokea katika Video ya Masogange ya Belle9 na baada ya hapo akaonekana kwenye Video ya Magubegube ya Barnaba iliyotoka 2012. Mara ya mwisho kuonekana katika ulimwengu wa wauza nyago ilikuwa katika Video ya Msambinungwa ya Tunda Man akishirikiana na Ali Kiba iliyotoka mwanzoni mwa mwaka 2014.

Wema Sepetu Amzimikia Rayvanny Amtabiria Makubwa Tuzo za BET


Wema Sepetu na Raymond

RayVanny ni msanii pekee kutoka Tanzania na Afrika Mashariki ambaye anatuwakilisha kwenye tuzo za BET zitakazofanyika Marekani baadaye mwezi huu akiwania Viewers Choice Awards ama (Pendekezo la Mashabiki ama watazamaji) huku BET wakitangaza namna ya kuwapigia kura wasanii ili washinde tuzo hizo.

Pamoja na baadhi ya mastaa kama Elizabeth Michael kumpigia na kumuombea  kura RayVanny kwenye kurasa zao za Social media, Wema Sepetu naye ametumia ukurasa wake wa Instagram kumpigia kura RayVanny akiandika:

Umechaguliwa tu kuwania lakini kwangu wewe ni mshindi tayari …Unastahili kabisa! V-Vanny Boy. Na haiishii hapa Tuendelee kupiga kura. 
Wasanii wanaowania tuzo ya Viewers Choice Awards pamoja na RayVnanny ni pamoja na  Dave (UK ) Jorja Smith (UK) Amanda Black (South Africa) Changmo (South Korea) Daniel Caesar (Canada) Remi (Australia) Skip Marley (Jamaica).

Mkurugenzi wa Zamani FBI Amlipua Trump..!!!

                       

Aliyekuwa Mkuu wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), James Comey ameishtumu Ikulu ya Marekani kwa kumharibia jina na kusema uongo kuhusu shirika hilo.

Comey ambaye aliyefutwa kazi ghafla na Rais Donald Trump alisema hayo jana Alhamisi, baada ya kuanza kutoa ushahidi mbele ya maseneta nchini Marekani kuhusu tuhuma kwamba Urusi iliingilia Uchaguzi Mkuu wa Marekani mwaka uliopita.

Mkuu huyo wa zamani wa FBI amewaambia maseneta waliomhoji kuwa alikuwa na mazungmzo ya siri na Rais Trump. Aidha, ameshtumu matamshi ya Ikulu ya Marekani kuwa FBI ilikosa imani naye.

Trump alimfuta kazi Comey Mei 9, mwaka huu baada ya FBI kutangaza kuchunguza madai ya Urusi kuingilia Uchaguzi wa Marekani, madai ambayo Urusi imekanusha.

Comey amesema, Trump alimwambia asitishe mchakato wa FBI kumchunguza Michael Flynn, aliyekuwa mshauri wake wa masuala ya usalama wa Taifa kwa madai kuwa alikuwa na mawasiliano ya karibu na maofisa wa Urusi kipindi cha uchaguzi.

Duh..Kijana wa Kiume Akamatwa Akimfanyia Mtihani wa Chuo Mpenzi Wake wa Kike..!!!



Imetokea huko Zimbabwe,wote wamekamatwa wapo polisi kijana wa kiume alidai aliamua kumsaidia mpenzi wake maana amerudia mara nne anafeli tu.




Kamanda wa Pwani Afafanua Mauaji ya Watu Watatu..!!!


Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amesema kwa taarifa alizonazo, watu wawili wamepigwa risasi katika kijiji cha Nyamisati, Kibiti, kisha waliofanya uhalifu huo kuwachukua majeruhi na kuondoka nao.

Awali taarifa zilizotolewa na mashuhuda wakazi wa kijiji hicho zilisema watu watatu wameuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia leo.

Lakini akizungumza na Mwananchi leo asubuhi, Kamanda Lyanga amesema watu wawili wamejeruhiwa kwa risasi na wahalifu kutokomea nao kusikojulikana.

“Tunaendelea na uchunguzi.” Amesema Kamanda Lyanga