Jumanne, 8 Desemba 2015

Maneno ya DC Paul Makonda kuhusu kufanikisha kutatua mgomo wa kiwanda cha URAFIKI Dar..


Siku chache zilizopita wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha urafiki walifanya mgomo kwa madai ya kutolipwa mishahara yao kwa muda mrefu kupelekea mkuu wa wilaya ya Kinondoni, DC Paul Makonda kuagiza shughuli zote za kiwanda hicho zisimame mpaka mgogoro wa kimaslahi kati ya wafanyakazi na wamiliki wa kiwanda hicho utakapotatuliwa.

Sasa leo kupitia kwenye ukurasa wa instagram DC Paul Makonda aliandika maneno kuhusu namna alivyotatua mgogoro huo na kufanikisha kile kiasi wanachotakiwa kulipwa wafanyakazi kiwanda cha nguo cha URAFIKI kilichopo eneo la Shekilango Dar es Salaam.
Asante Mungu kwa kuniwezesha kuwatetea wanyonge wenzangu na wafanyakazi wa kiwanda cha urafiki na kufikia kulipwa kiwango 150000 tofauti na hapo zamani walipokuwa wanalipwa 80000 kwa mwezi….Jambo ambalo wameliomba tangu 2007′>>>>Paul Makonda

Huyu ndio kocha anayenyemelea kibarua cha Louis van Gaal Man United, kakiri hapa …


Kuna mengi yanaendelea katika soka, tetesi na uvumi katika soka ni moja kati ya vitu vinavyo ingia katika headlines kila siku, vilabu vingi duniani vimekuwa vikijitahidi kuweka usiri katika mambo yake, headlines za kocha wa Manchester United Louis van Gaal kutaka kuachia ngazi klabu hiyo zinazidi kuchukua nafasi.
Jumamosi ya December 5 kocha huyo alikiri kuwa yupo tayari kuondoka Man United kama wachezaji wa klabu hiyo watapenda aondoke, kwani kumekuwa na uvumi kuwa wachezaji hawana mahusiano mazuri na kocha huyo, stori zilizotoka December 7 ni kuwa uongozi wa klabu ya Man United unapanga kumuongezea mkataba, yote hayo yanaandikwa na vyombo vya habari.
Stori ni kuwa kocha wa zamani wa klabu ya Chelsea na Real Madrid muitaliano Carlo Ancelotti amekiri kuvutiwa na kujiunga na Man United licha ya kuwa hana mpango wa kujiunga na timu yoyote katikati ya msimu, swali ambalo alijibu mara baada ya kuulizwa kama angependa kuwa kocha wa Man United.
MADRID, SPAIN - JUNE 26:  Carlo Ancelotti holds a press conference after he was presented as Real Madrid's new head coach at Estadio Bernabeu on June 26, 2013 in Madrid, Spain.  (Photo by Denis Doyle/Getty Images)
Carlo Ancelotti
“Sio kwamba natafuta klabu iliyo na mipango mikubwa sana kwani naweza kusubiri kwa sasa sababu sina mpango wa kujiunga na timu katikati ya msimu, tusubiri hadi mwisho wa msimu kwani nina mipango ya kurudi kazini msimu ujao. kuhusu kuvutiwa na nafasi ya kuwa kocha wa Man United, bilashaka hakuna kocha asiyevutiwa na nafasi ya kuwa kocha wa Man United” >>>> Carlo Ancelotti
Louis van Gaal ambaye ni kocha wa klabu ya Man United ana mkataba na klabu hiyo hadi mwaka 2017 ila amekuwa akihusishwa kuwa na mpango wa kuachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu na kupanga mipango ya kustaafu ili apate muda wa kupumzika na mkewe, stori ambazo zimekuwa zikiandikwa katika vyombo vya habari mara kadhaa.

Mawaziri wa Jakaya Kikwete Hawajahama Nyumba za Serikali

Wakati Watanzania wakisubiri kufahamu sura zitakazoingia kwenye baraza jipya la mawaziri katika Serikali ya Rais John Magufuli, baadhi ya mawaziri wa awamu iliyopita ya Jakaya Kikwete hawajaziachia nyumba za Serikali walizokuwa wanaishi.

Kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma, mawaziri wanastahili kuishi kwenye nyumba za Serikali kuanzia pale uteuzi wao unapotangazwa ili kuanza kutekeleza majukumu yao wakiwa katika mazingira salama, wao na familia zao. Haki hiyo hukoma mara moja; pale wanapovuliwa wadhifa huo au baraza husika linapovunjwa baada ya kukamilisha muhula wake au sababu nyingine yoyote.

Maandalizi ya Rais Magufuli katika uteuzi yanakwenda sambamba na taasisi zinazohusika kutekeleza wajibu wao wa kuandaa makazi ya wateule wanaotarajiwa, lakini zinakwamishwa na mawaziri ambao hawajahama.

“Tumepata fedha za kutosha kukarabati nyumba zenye uhitaji huo kutoka wizarani. Nyumba 15 zipo katika utekelezaji. Kuna baadhi tunasubiri waliomo wahame ili tuweze kuendelea,” alisema Mhandisi Edwin Nnunduma, kaimu mkurugenzi wa ushauri wa Wakala wa Nyumba za Serikali Tanzania (TBA).

Nnunduma alisema kila kitu kipo tayari na mapokezi ya viongozi hao hautacheleweshwa kwa namna yoyote ile kwa kuwa nyumba zipo za kutosha kuwahifadhi ili walitumikie Taifa kwa viwango vinavyohitajika.

Takwimu zinaonyesha kuwa wakala huyo anasimamia jumla ya nyumba 93 na kati ya hizo 29 zilikuwa zinakaliwa na mawaziri wa Serikali iliyopita ya Rais Jakaya Kikwete ambao, kwa mujibu wa kanuni walistahili kuziachia mara tu baada ya Rais Magufuli kuapishwa, Novemba 5.

Kwa mujibu wa Nnunduma, ukarabati huo unahusisha nyumba 35 ambazo zinajumuisha 29 za mawaziri na sita wanazoishi baadhi ya makatibu wakuu wa wizara.

Taarifa zilizolifikia Mwananchi zinaeleza kuwa wapo baadhi ya mawaziri ambao wamekaidi kuondoka kwenye nyumba hizo, licha ya kanuni na sheria kuwataka kufanya hivyo na agizo la Katibu Mkuu Kiongozi lilikwishatolewa likiwataka kurudisha magari na nyumba za Serikali.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Mnunduma alisema, “Kuna waraka wa Katibu Mkuu Kiongozi uliowataka wahame kwenye nyumba hizo ndani ya siku 30 baada ya kuapishwa kwa Rais mpya. Muda huo uliisha jana (juzi), naamini bado baadhi hawajahama mpaka sasa. Nilikuwa safarini hivyo sina uhakika ni nani na nani hawajafanya hivyo.”

Novemba 5, mara baada ya kuapishwa kwa Rais Magufuli, Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, aliwaagiza mawaziri na manaibu waziri kurudisha magari ya Serikali ikiwa ni siku yao ya ukomo wa uongozi. Katika agizo hilo, alisema baada ya bendera ya Rais anayemaliza muda wake kuteremshwa na kabla ya ile ya Rais mpya kupandishwa, magari hayo yanatakiwa yabadilishwe namba kwa kuondoa herufi ya cheo na kuwekwa zile za Serikali.

Wakati urejeshaji wa magari ulifanywa mara moja, uhamaji kwenye nyumba za Serikali ulipewa muda wa siku hizo 30, ili kutoa fursa kwa familia husika kuandaa mazingira hayo ikiwa ni pamoja na kusafirisha mali husika za viongozi hao na walio nao.

Kukawia huko kwa baadhi ya mawaziri kunaelezwa kuwa huenda kukawa na sababu mbili; ama uhakika wa kurudi kwenye baraza jipya au kutokana na ukosefu wa mahali pa kuhamia baada ya utumishi kukamilika na muda wa kutafuta mahali pengine penye hadhi sawa na yao kuwa changamoto.

“Wapo baadhi ya mawaziri ambao walichaguliwa siku za mwisho ambao kabla ya hapo walikuwa wanaishi majimboni kwao. Mwezi mmoja uliotolewa unaweza usitoshe kwa wao kutafuta nyumba nyingine hapa mjini itakayowafaa kulingana na mahitaji yao,” kilisema chanzo ambacho hakikutaka kutajwa.

Uchunguzi wa gazeti hili katika mitaa Mikocheni, Masaki na Kijitonyama ziliko nyumba za mawaziri ulibaini baadhi zikifanyiwa ukarabati na baadhi ya walinzi waliohojiwa wakibainisha kuwa mawaziri wengi walishaondoka katika makazi hayo.

Hata hivyo, ofisa wa TBA anayeshughulikia makazi ya mawaziri Kanda ya Masaki, Juma Hamis alisema mawaziri waliokuwa wamebakia kwenye eneo lake ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi, Hawa Ghasia.

“Kwa taarifa nilizonazo, hawa mawaziri wanahama leo (jana) kwani tayari wameanza kuhamisha baadhi ya vitu vyao,” alisema Juma.

Hata hivyo, Makamba alipoulizwa alisema hajawahi kuishi kwenye nyumba ya Serikali tangu aanze kuwatumikia wananchi kwa nafasi tofauti alizowahi kuzitumikia.

Alisema, “Siku zote naishi kwenye nyumba yangu. Tangu nilipokuwa ikulu na hata nilipoondoka na kuwa waziri.”     

After Lots of Rumors Finally Quick Racka Confirms Dating Kajala

There have been lots of speculations and rumors about Kajala dating Bongo Flava singer Quick Racka. Media did write about their secret relationship although they both denied it. Even Quick Racka had tattoo of Kajala's name. But speaking with Clouds fm Quick Racka was asked wheather he is still with Kajala or have already parted ways the singer replied they are still together ...

"Sometimes some things have to stay private because when love life get in public all the time rumors spread all the time too so sometimes it is better to be private but we are doing good...words on the streets are lots but we are the ones who know the truth" said Quick Racka

Umeiona video mpya ya Belle 9 ‘Burger Movie Selfie’?ninayo hapa……


Belle 9 baada ya kutambulisha rasmi single yake mpya Burger Movie Selfie katika vituo mbalimbali vya radio Dec 7 2015,  sasa time hii pia ametusogezea na video mpya ya single hiyo.
Kwa mujibu wa msanii huyo ni kwamba video imeshutiwa Morogoro na director GQ wa Morogoro, itazame hapa.

Kutokuwapo Kwa Mawaziri Kumeokoa Mamilioni

Uamuzi wa Rais John Magufuli kukaa zaidi ya mwezi mmoja bila kuteua Baraza la Mawaziri huenda ukawa umeisaidia Serikali kwa kuokoa takribani Sh683.3 milioni za walipa kodi, bila kuhusisha gharama za ununuzi wa ‘mashangingi’.

Kiasi hicho cha fedha kimetokana na hesabu inayokadiriwa kuwa matumizi ya waziri iwapo Rais Dk Magufuli angeendelea na ukubwa wa Baraza la Mawaziri la mwisho la Rais Jakaya Kikwete la mawaziri 55, kati ya hao 24 wakiwa manaibu waziri.

Hata hivyo, Dk Magufuli ameshatangaza kuwa na baraza dogo la mawaziri, ingawa hajaweka bayana litakuwa na jumla ya mawaziri wangapi.

Kwa mujibu wa aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole-Medeye, Waziri hulipwa mshahara wa kati ya Sh3.8milioni mpaka Sh 5milioni kwa mwezi ambazo ni sawa na mshahara wanaolipwa wabunge.

Kwa mantiki hiyo, kwa mawaziri 55, Serikali ilitakiwa ilipe Sh209 milioni kwa ajili ya mishahara ya Novemba, lakini hazikulipwa kwa kuwa bado kiongozi huyo hajawateua.

Kanuni za kudumu za utumishi wa umma toleo la mwaka 2009, zinaitaka Serikali kumpatia nyumba mtumishi anayetakiwa kupatiwa huduma hiyo kwa aidha kumpa nyumba ya Serikali au kumkodishia nyingine yenye hadhi ili aweze kutimiza wajibu wake ipasavyo.

Kanuni hizo zinamtaka Wakala wa Majengo (TBA) kufanikisha zoezi hilo la kutoa huduma za nyumba au kusimamia ukodishaji wa nyumba husika ya mtumishi.

Mawaziri ni miongoni mwa watumishi wanaopatiwa nyumba za Serikali ambazo nyingi zinapatikana katika maeneo ya vigogo ya Masaki, Oysterbay au Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa tovuti ya uuzaji na ukodishaji nyumba na viwanja ya Lamudi, nyumba za bei ya wastani ambayo inaweza kwenda na hadhi ya waziri inakodishwa kwa kiasi kisichopungua Sh5 milioni kwa mwezi.

Hivyo basi, kama nyumba za mawaziri hao ambazo hukarabatiwa na kuhudumiwa na TBA, zingekuwa zimekodishwa kutoka kwa watu binafsi kwa kipindi cha mwezi mzima basi Serikali ingelipa Sh275 milioni.

Ili kutimiza majukumu yao vyema wakiwa bungeni mjini Dodoma, mawaziri pia hupatiwa nyumba za kuishi tofauti na zile za Dar es Salaam ambazo zipo chini ya TBA.

Hata hivyo, Ole-Medeye alisema Serikali huwalipa mawaziri Sh800, 000 kwa mwezi kwa ajili ya huduma za nyumba za Dar es Salaam, mawasiliano na ankara nyingine za kumsaidia kimaisha.

Iwapo kiwango hicho cha Sh800, 000 kwa mwezi kingetumika kumlipa kila waziri kama sehemu ya fedha za makazi, bado Serikali ingehitajika kutoa Sh44 milioni kwa ajili ya gharama za kuhudumia nyumba na mawasiliano.

“Hivi Sh800, 000 utapata wapi nyumba ya kukodi akaishi waziri? Kwa bei ya sasa nyumba za kiwango hicho ni Dola za Marekani 3,000 (Sh6 milioni) au zaidi.

“Sasa fedha hiyo umlipe mtumishi wa ndani, gharama za umeme, mawasiliano na maji ndiyo maana nasema uwaziri ni kazi ya kuhudumia jamii,” alisema Ole-Medeye akieleza kuwa waziri hupatiwa posho ya Sh80, 000 kwa siku akiwa mikoani kwenye ziara.

Gharama za posho za mawaziri hao zingetegemea na siku ambazo wangekaa mikoani kwa kipindi hicho cha siku 31, na hivyo si rahisi kujua kiwango chake.

Gharama za samani

Miongoni mwa mambo ambayo Serikali hugharamia kwa mawaziri wake ni samani za ndani ya nyumba, ambazo pia huongezeka au kupungua kulingana na ukubwa wa baraza.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk Adelhelm Meru alisema ununuzi wa samani za ndani ya nyumba za waziri husimamiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kwa wizara zote na hununuliwa kila baada ya miaka mitano.

Hata hivyo, Dk Meru alitoa angalizo kuwa matumizi ya waziri husika huchangiwa pia na ukubwa wa wizara na kiwango cha bajeti.

“Mawaziri wengine wanaishi kwenye makazi yao na siyo wote wamepewa makazi ya Serikali.

“Lakini wanapewa huduma ya umeme, maji, posho ya majukumu na gari,” alisema Dk Meru.

Mashangingi

Mawaziri pia hupatiwa magari kwa ajili ya usafiri na mara nyingi huwa na ama Toyota Land Cruiser VX V8 au GX V8 ambayo hujulikana kama “mashangingi.”

Ili kufanikisha shughuli zao, kila waziri hupatiwa lita 1,000 kwa mwezi za mafuta. Kwa bei elekezi ya sasa ya Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (Ewura), iliyoanza kutumika Desemba 2, bei ya dizeli jijini Dar es Salaam ni Sh1,823 kwa lita.

Gari moja la waziri mmoja iwapo lingetumia lita zote 1,000 Serikali ilitakiwa kulipa Sh1.823 milioni ambazo kwa baraza zima ingekuwa jumla ya Sh100.3 milioni.

Pia, magari hayo huitaji kufanyiwa matengenezo kwa kila baada ya kilomita zinazoshauriwa na mtengenezaji.

Dk Meru alisema kwa kawaida kila gari hufanyiwa matengenezo baada ya kilomita 5,000 kwa kiasi cha wastani Sh1.8 milioni kila moja.

Kwa maana hiyo, katika Serikali ya “hapa kazi tu” inayohimiza viongozi wa kutoka maofisini kwenda kusikiliza shida za wananchi vijijini, hapana shaka kuwa mawaziri hao wangekuwa ama wameshatimiza kilomita zinazohitaji matengenezo au wanakaribia.

Serikali kufanikisha matengenezo hayo, ingeweza kulipa kampuni husika ya matengenezo Sh99 milioni kwa mwezi.

Gharama hizo ni mbali na fedha za kununua magari hayo ambayo kila moja linakadiriwa kugharimu Sh250 milioni, hivyo mawaziri 55 wangetafuna Sh13.75 bilioni.

Unafuu wa gharama katika eneo la ununuzi wa mashangingi hayo utakuwa dhahiri iwapo Rais Magufuli atatekeleza ahadi yake ya kuteua baraza dogo, mathalan, akiteua mawaziri 20 atakuwa ameokoa mashangi ya mawaziri 35, sawa na Sh8.75 bilioni.

Ukimya wa Rais Magufuli kutoteua Baraza la Mawaziri kwa kipindi cha mwezi kumeibua mtizamo tofauti miongoni mwa wachambuzi wa masuala ya Siasa na utawala, wengi wakisema kuna faida nyingi kuliko hasara.


Rekodi 5 za kuvutia za Lionel Messi ambazo hazijawahi kuvunjwa na mchezaji yoyote …


Lionel Messi ni staa wa soka wa kimataifa wa Argentina ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya FC Barcelona ya Hispania aliyojiunga nayo mwaka 2001 na mwaka 2003 akaanza kuichezea FC Barcelona C. Lionel Messi anatajwa kuwa ni moja kati ya wachezaji soka wenye rekodi za kusisimua zaidi duniani. Hizi ni rekodi 5 za kusisimua za Lionel Messi stori kutoka sokkaa.com

5- Lionel Messi sio tu anatajwa kuwa mchezaji bora wa Dunia, ila wachambuzi wa masuala ya soka wanamuita ni moja kati ya wachezaji bora wa soka waliowahi kutokea katika historia ya soka. Messi ndio mchezaji pekee ambaye amewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia Ballon d’Or mara 4, kwani hakuna mwingine aliyewahi kufanya hivyo.

Leo-Messi3

4- Mwaka 2012 Lionel Messi alifanikiwa kuvunja rekodi ya Muller ambaye alikuwa amefunga jumla ya goli 85 kwa mwaka, rekodi ambayo ilidumu toka mwaka 1972 ila Lionel Messi mwaka 2012 amevunja rekodi hiyo kwa kufunga jumla ya magoli 91 katika mechi za mashidano yote na kuvunja rekodi iliyodumu kwa miaka 40 bila kuvunjwa.

Leo-Messi-d

3- Staa huyo wa Argentina ndio mchezaji pekee mwenye rekodi ya kufunga magoli katika mechi 21 mfululizo za Ligi Kuu, rekodi ambayo aliiweka msimu wa 2012/2013.
BARCELONA, SPAIN - FEBRUARY 23: Lionel Messi of FC Barcelona celebrates after scoring his team's second goal during the La Liga match between FC Barcelona and Sevilla FC at Camp Nou on February 23, 2013 in Barcelona, Spain. (Photo by David Ramos/Getty Images)

2- Ni mchezaji wa kwanza kuzifunga mfululizo timu zote za Ligi Kuu, msimu wa 2012/2013 Lionel Messi alifanikiwa kuzifunga mfululizo timu zote 19 pinzani katika Ligi Kuu Hispania, licha ya kuwa Cristiano Ronaldo amewahi kufanya hivyo msimu wa mwaka 2011/2012 ila Lionel Messi amefunga mfululizo yaani kwa kufuatana.

Messi13

1- Lionel Messi ndio mchezaji pekee aliyewahi kutwaa mara mbili tuzo ya golden ball ya michuano ya klabu Bingwa Dunia ambayo mwaka huu inafanyika Japan, rekodi ambayo aliiweka mwaka 2009 na 2011.
Spain's FC Barcelona midfielder Lionel Messi holds the Golden Ball trophy for the best player during the awarding ceremony after the final match at the Club World Cup soccer tournament in Yokohama, near Tokyo, Sunday, Dec. 18, 2011.(AP Photo/Hiro Komae)