Jumatatu, 22 Septemba 2014

WATU 115 WAFARIKI KANISANI NIGERIA

 
Muhubiri T.B Joshua amewashangaza wengi kwa kusema aliona ndege ikizunguka jengo hilo kabla ya kuporomoka

Serikali ya Afrika Kusini inasema kuwa watu miamoja na kumi na tano wengi wao wakiwa raia wa Afrika Kusini, walifariki baada ya kanisa kuporomoka nchini Nigeria.
Idadi kamili ya raia wa Afrika Kusini waliofariki ilikuwa 84.
Ndege iliyowabeba manusura wa mkasa huo, kumi na sita kati yao wakiwa wamejeruhiwa vibaya, imewasili mjini Pretoria.
Zaidi ya watu 300 kutoka Afrika Kusini walikuwa wametembelea kanisa hilo la 'All Nations' mjini Lagos, ambalo linaongozwa na mhubiri T.B. Joshua.
Inaarifiwa jengo hilo liliporomoka kutokana na ujenzi mbovu.
Mhubiri TB Joshua, amezua wasiwasi baada ya kuzungumzia kuona ndege iliyokuwa inazunguka juu ya kanisa hilo kabla ya jengo lenyewe kuporomoka.

MANUEL"CHELSEA NI TIMU NDOGO"

Pellegrini ameikejeli Chelsea kwa kucheza kama timu ndogo 
Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini ameikejeli Chelsea kwa kucheza kama timu ndogo timu hizo zilipoambulia sare ya Moja kwa moja uwanjani Etihad.
Andre Schurrle ndiye aliyeiweka Chelsea mbele kabla ya mchezaji wa akiba Frank Lampard kuisawazishia man City ambayo ilikuwa na wachezaji . Pellegrini, 61,alisema "nafikiri tulicheza dhidi ya timu ndogo iliyokuwa inalinda ngome yake wala haitaki kucheza mbele.
Sio jambo la kufurahisha kamwe .
Wachezaji wangu 10 walilinda ngome yao na kupata bao la kusawazisha hadi tamati ya mechi.''
Pellegrini alifananisha mchezo wa Chelsea na ule wa Stoke ambayo iliilaza City 1-0 mwezi uliopita nyumbani kwao.
''Nafkiri tulicheza dhidi ya timu sawa na ile ya Stoke .Ilikuwa vigumu sana kwetu kufunga bao kwa sababu walikuwa wanalinga ngome yao badala ya kucheza mchezo wa hadhi inayostahili''
Sina haja ya kuwatathmini hata kidogo hilo nawachia timu zingine ''
City ilitoka nyuma na kusawazisha hata baada ya mlinzi wa kutegemewa Pablo Zabaleta kuoneshwa kadi ya pili ya njano baada ya kumchezea visivyo mshambulizi mpya wa Chelsea Diego Costa.
Kwa upande wake kocha wa Chelsea Jose Mourinho alikataa kata kata kujibu madai hayo ya Pellegrini akisema ''mbona yeye husema kuwa hazungumzi kuhusi mimi na timu yangu ilihali anaendelea kupiga domo ?
Usiniulize chochote kumhusu Manuel"

MASHABIKI WAMTUKANA BALOTELLI

Ujumbe wa Balotelli ulioibua hisia za ubaguzi wa rangi kwenye mtandao wa twitter 
Polisi nchini Uingereza wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio ambalo mshambulizi wa Liverpool kutoka Italia Mario Balotelli alitukanwa kutokana na rangi ya ngozi yake kupitia kwa mtandao wa kijamii wa Twitter.
Polisi katika mji wa Merseyside wameanzisha uchunguzi kufuatia matusi hayo yaliyotokea baada ya mshambulizi huyo wa Liverpool kutuma ujumbe akiicheka kichapo cha Manchester United mikononi mwa timu ndogo ya Leicester siku ya jumapili.
Baloteli aliandika ''Man Utd...LOL'' na ujumbe wake ukasambazwa zaidi ya mara 150,000 na mashabiki wake.
Hata hivyo miongoni mwa mwa wale waliouona ujumbe huo walimfokea kwa kuicheka United na wakamtusi kwa misingi ya rangi yake.
Japo ni raiya wa Italia Balotelli mwenye umri wa miaka 24 ana asili ya kiafrika.Polisi wanafanya Uchunguzi kujua ni nani waliomtukana Balotelli. 

Polisi tayari wamefunga kurasa kadha zilizotuma jumbe hizo huku wakianza uchunguzi waliozimiliki ni kina nani na wanaishi wapi iliwakamatwe na kujibu mashataka ya ubaguzi wa rangi.
Kundi linalopigania kumaliza ubaguzi wa rangi katika michezo Kick It Out lilisema kuwa baada ya kuarifiwa kuwepo kwa matusi yenye kumdhalilisha Balotelli, kundi hilo lilianzisha uchunguzi kwa ushirikiano na polisi wa mitandao ya kijamii.
Sio mara ya kwanza kwa Mshambulizi huyo kudhulumiwa kwa misingi ya rangi yake .
Balotelli ambaye alikuwa uwanjani Liverpool ilipolazwa 3-1 na West Ham jumamosi amewahi kudhulumiwa kwa misingi ya rangi yake timu ya Italia ilipokuwa ikijifua kwa kombe la dunia mwezi mei mwaka huu .
Awali pia aliwahi kutukanwa akiwa Inter Milan na pia akihudumu AC milan.

EPL: Matokeo ya Man City vs Chelsea haya hapa


Home » General News » EPL: Matokeo ya Man City vs Chelsea haya hapa

EPL: Matokeo ya Man City vs Chelsea haya hapa

IMG_7407.JPG
Baada ya Man United kupokea kipigo kutoka kwa Leicester City, miamba mingine ya ligi kuu ya Uingereza Chelsea ilijitupa uwanjani kucheza na Manchester City.
Mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Etihad umeisha kwa matokeo ya sare 1-1.
Dakika chache baada ya Pablo Zabaleta kutolewa kwa kadi nyekundu Chelsea walipata goli la kwanza kupitia mchezaji aliyetokea benchi Andry Schurrle.
Akitokea benchi mchezaji wa zamani wa Chelsea Frank Lampard aliunganisha krosi ya James Milner na kuisawazishia Man City.
Mpaka mpira unamalizika Man City 1-1 Chelsea.

PICHA HIZI ZINAONESHA SHANGWE YA SERENGETI FIESTA 2014 MKOANI MOROGORO NI SHEEEEEDAH


.
.
Show ya Serengeti Fiesta 2014 iliyofanyika Jumapili,Sept 21 kwenye uwanja wa Jamhuri Stadium imefana baada ya wakazi wa (88.5) Morogoro kupokea kwa shangwe burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali
Tazama picha za wasanii wakiwa jukwaani
.
.
.
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Kesi ya Emmanuel Mbasha imesogezwa tena mpaka October.

 
Kesi ya mwimbaji wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha imepigwa kalenda kwa mara nyingine tena kwa sababu Hakimu anayeendesha kesi hiyo kupata shughuli nyingine nje ya ofisi.
Mbasha alipanda kizimbani katika mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi yake hiyo ambapo mwendesha mashtaka Kiyoja Catherine aliahirisha kesi hiyo kutokana na Hakimu Williberforce Luwhego kupata dharura.Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena 17 October mwaka huu ambapo Mahakama itaanza kusikiliza ushahidi ambapo upande wa mashtaka utakuwa na mashahidi wanne kwenye kesi hii inayomkabili mume wa Flora Mbasha anaekabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo ya ubakaji.
Mara ya mwisho kabla ya hii kuahirishwa Flora Mbasha alikwenda Mahakamani kwa mara ya kwanza akiwa na watu wake na hakukutana wala kuongea na mume wake ambapo muda mfupi kesi hiyo ikaahirishwa.