Ijumaa, 16 Septemba 2016

STAA WA GENK KATAJWA KATIKA LIST YA KIKOSI BORA CHA WIKI EUROPA, MAN UNITED HAKUNA


Usiku wa Septemba 15 2016 michuano ya Europa League ilichezwa barani Ulaya, klabu ya KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta ilicheza dhidi ya Rapid Wien ya Austria na kufungwa goli 3-2, magoli mawili ya Genk yalifungwa na Leon Bailey.
Baada ya mchezo huo kumalizika Septemba 16 shirikisho la soka barani Ulaya UEFAkupitia account yao rasmi ya twitter walitoa majina ya wachezaji 11 wanaounda timu bora ya wiki na kwa KRC Genk ametajwa mjamaica Leon BaileyBailey anaingia katika kikosi hicho kati ya zaidi ya wachezaji 528 waliocheza mechi za Europa jana.

TOP 5: WATU MAARAFU ZAIDI DUNIANI KATIKA MITANDAO YA KIJAMAA


Mitandao ya kijamii ni miongoni mwa vitu vyenye nguvu na ushawishi mkubwa katika tasnia mbalimbali, leo Septemba 16 2016 naomba nikusogezee TOP 5 ya watu maarufu duniani kwenye mitandao ya kijamii ambapo ili uweze kujikusanyia watu ni lazima uwe na ushawishi na mvuto fulani kwa watu au kutokana na kazi yako nzuri.
Katika TOP 5 hii jina la mwanaume aliyetajwa ni mmoja tu na ndio staa wa soka pekee aliyekuwemo katika list hiyo Cristiano Ronaldo ambaye yupo nafasi ya pili akizidiwa na mrembo Tylor Swift kwa tofauti ya followers milioni 8, wakifuatiwa na Katty Perry,Selena Gomez na muimbaji Rihanna.

Magazeti ya Tanzania September 17, 2016 kuanzia, Udaku, Hardnews na michezo


September 17 2016 naanza kwa kukusogezea post ya stori zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye, Michezo na hardnews ili ujue kinachoendelea mtu wangu.. usiache kukaa karibu yangu kwenye facebook, twitter na instagram @millardayo ili niwe nakutumia kila kinachonifikia.
img_20160917_050927
img_20160917_050939
img_20160917_050951
img_20160917_051006
img_20160917_051018
img_20160917_051029
img_20160917_051041
img_20160917_051052
img_20160917_051103
img_20160917_051115
img_20160917_051128
img_20160917_051139
img_20160917_051150
img_20160917_051139
img_20160917_051213
img_20160917_051225
img_20160917_051237
img_20160917_051250
img_20160917_051302img_20160917_051313
img_20160917_051325
img_20160917_051336
img_20160917_051347
img_20160917_051357
img_20160917_051408
img_20160917_051419
img_20160917_051430
img_20160917_051443
img_20160917_051453
img_20160917_051503
img_20160917_051514
SOURCE:MILLAD AYO

MIMI SISHINDANI NA MTU YEYOTE - BARAKA THE PRINCE


Msanii Baraka The Prince ambaye ameachia kazi yake mpya yenye jina la 'Nisamehe' amefunguka na kusema kuwa katika muziki hakuna mtu ambaye anashindana naye kwa kuwa yeye anasimama mwenyewe na aina ya muziki anaofanya haufanani kabisa wasanii wa WCB

Baraka The Prince alisema haya kupitia kipindi cha Planet Bongo na kudai kuwa muziki anayofanya yeye ni wasanii wachache ambao wanafanya na kusema mara nyingi yeye anafanya jambo kutokana na mipango yake na matakwa ya mashabiki ila hafanyi kazi kwa kuangalia nani kafanya nini na nani.
"Siku zote mimi nasimama kama Baraka The Prince sijawahi kufanya kitu sababu fulani kafanya ila siku zote mimi huwa nafanya kazi kwa kuangalia mashabiki zangu wanataka nini na kuangalia mipango yangu. Kwanza sijawahi kufikiria kushindana na mtu yoyote yule kwenye muziki kwa sababu mimi najua nina muziki wa tofauti kabisa na miziki yao wanaofanya wao, watu wengi watafanya muziki wa mchaka mchaka watafanya nini lakini ukija upande wangu mimi watu tunaofanya muziki huu tunahesabika lakini kwenye miziki yao kuna watu karibia mia na kitu mpaka wengine hawajatoka wanafanya miziki yao" alisema Baraka The Prince

Mbali na hilo Baraka The Prince alisema kuwa yeye alikuwa na mipango ya kufanya kazi na Alikiba miaka mitano nyuma na anasema alijua kuwa wimbo wake wa sita lazima aimbe na Alikiba na imekuwa hivyo.

"Mimi nilikuwa na mipango ya kuja kufanya kazi na Alikiba miaka mitano nyuma na nilipanga kabisa wimbo wangu wa sita lazima niimbe na Alikina na imekuwa, mimi ni mtu ambaye huwa naishi kwa mipango saizi wimbo wangu wa kumi nishajua nitafanya na nani kama Mungu atazidi kutupa uhai, lakini pia ukiangalia muziki ninaofanya mimi na Alikiba ni sawa japo kuwa Alikiba yeye ni mtu wa kubadilika lakini nikisikiliza wimbo wowote wa Alikiba najifunza kitu hivyo yeye ni miongoni mwa wasanii walionivutia kwenye muziki huo wa Bongo Fleva" aliongeza Baraka The Prince

KUTOKA BUNGENI: RAISI MAGUFULI KUHAMIA DODOMA RASMIMWAKA 2020



Leo Septemba 16, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma hotuba ya kuahirisha mkutano wa nne kwa Bunge la 11 uliodumu kwa muda wa wiki mbili, amesoma ratiba ya serikali kuhamia Dodoma.

“Ili kufanikisha azma ya Serikali kuhamia Dodoma, tayari imeandaliwa ratiba itakayowezesha Serikali kuhamia Dodoma kwa awamu, kuanzia mwezi Septemba, 2016 hadi mwaka 2020, bila ya kuathiri bajeti yetu ya mwaka 2016/2017 kama ifuatavyo”–


1. Septemba 2016 – Februari 2017.

Waziri Mkuu na Mawaziri wote, Makatibu Wakuu wote, Manaibu Makatibu Wakuu wote watahamia Dodoma katika Awamu ya Kwanza. Aidha, kila Wizara itatakiwa kuhamisha Watumishi wa Idara moja au mbili, na wakati huo huo kuendelea kuweka utaratibu wa kupeleka Watumishi wa Idara nyingine kuhamia Dodoma;

2. Machi 2017 – Agosti 2017.

Kipindi hiki kitawapa fursa watendaji wa wizara mbalimbali kuweka katika Bajeti zao za mwaka 2017/2018 gharama za kuendelea kuhamisha watumishi wake kuja Dodoma.

3. Septemba 2017 – Februari 2018.

Katika awamu hii, Wizara zitaendelea na uhamishaji wa Watumishi wa Idara zilizo ndani ya Wizara.

4. Machi 2018 – Agosti 2018.

Katika kipindi hiki, Wizara zinatakiwa kuendelea kuhamisha watumishi wake.

5. Septemba 2018 – Februari 2020.

Katika kipindi hiki, Wizara zinatakiwa kuendelea kuhamisha watumishi wake.

6. Machi 2020 – Juni 2020.

Katika kipindi hiki, Ofisi ya Rais ikiongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, watakuwa wanahamia Dodoma.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitumia wasaa huu kuzishauri Wizara zote kuanzisha mifumo ya utunzaji kumbukumbu wa kielektroniki badala ya kuhama na mafaili kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma, tunataka Dodoma iwe ya kielektroniki, alisisitiza Waziri Mkuu.

WABUNGE WOTE WA CUF WAMKATAA PROFESA IBRAHIM LIPUMBA



Wabunge wote wa Chama cha Wananchi (CUF) wametangaza rasmi kutomtambua aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba.

Wamemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi kutomkumbatia mwanasiasa huyo aliyebobea katika uchumi, ikielezwa kwa sasa hana sifa za kuwa mwenyekiti wa chama hicho, labda aanze upya mchakato.

Wameeleza msimamo huo jana mjini Dodoma na Mbunge wa Viti Maalumu, Riziki Mngwali ambaye pia ni Kiongozi wa Wabunge wa CUF katika mkutano baina ya waandishi wa habari za Bunge na wabunge wa CUF isipokuwa Mbunge wa Jimbo la Kaliua, Magdalena Sakaya aliyesimamishwa uanachama, ingawa anaendelea kutimiza majukumu yake bungeni.

Mngwali alisema Profesa Lipumba amekuwa akijaribu kukiyumbisha chama na hivi karibuni kudai amekaririwa akisema anasubiri barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa ya kuthibitishiwa kuendelea na uenyekiti wake.

“Wakati anajiuzulu uenyekiti Agosti 5, mwaka jana aliutangazia umma na kudai anakwenda Rwanda kwa kazi aliyodai ya utafiti ili aje kuisaidia serikali, lakini inashangaza sasa anataka kujirejeshea uenyekiti. Hilo hatukubali kwa kuwa chama kina taratibu zake,” alisema.

Aliongeza kuwa, alikiacha chama katika wakati mgumu kuelekea Uchaguzi Mkuu, lakini kikaimarika zaidi kwa kupata wabunge 43, madiwani 287, kuongoza manispaa mbili na halmashauri za wilaya tatu, hivyo wanashangazwa kuona akitaka kurejea, tena kwa kutumia nguvu.

“Tunataka ifahamike kwa dhati kuwa, sisi wabunge, hatumtambui tena Profesa Lipumba kama Mwenyekiti wa CUF,” alisema Mngwali na kumtaka Msajili kutomuidhinisha Lipumba, kitendo alichodai kitachochea mgogoro ndani ya chama.

Aliongeza kuwa badala ya kutumia mabavu kutaka kurejea madarakani, ni vyema akabaki na heshima yake, kwani amekitendea mambo mengi chama hicho na kwamba wanamheshimu, hivyo afuate taratibu za kichama kutaka kuwania tena uenyekiti.

Mngwali alisema wamekubaliana na uamuzi wa Baraza Kuu la Uongozi wa CUF wa kuwasimamisha uanachama Lipumba na wenzake tangu Agosti 28, 2016 kutokana na kile kinachodaiwa kukiuka Katiba ya chama hicho. 

Miongoni mwa tuhuma zao ni kusababisha vurugu wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Uchaguzi Agosti 21, mwaka huu jijini Dar es Salaam uliokuwa unalenga kumthibitisha Juma Duni Haji kuwa Mwenyekiti mpya.

Hata hivyo, kutokana na vurugu zilizoibuka, mkutano huo ulivunjika. Mbali ya Lipumba na Sakaya, wengine waliositishiwa uanachama ni Abdul Kambaya ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, Ashura Mustapha, Omar Mhina, Thomas Malima, Kapasha M. Kapasha, Mohamed Habib Mnyaa, Haroub Shamis na Mussa Haji Kombo.

Ashura ni mjumbe wa Baraza Kuu na aliwahi kuwa Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma CUF wakati Mnyaa na Kombo, walikuwa wabunge kipindi cha 2010/2015, Mnyaa akiwakilisha Jimbo la Mkanyageni na Kombo Jimbo la Chake Chake, kisiwani Pemba.

Kutokana na kusimamishwa kwa viongozi hao, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alimtangaza Julius Mtatiro aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara kuwa kiongozi wa Kamati ya Uongozi wa muda inayowajumuisha pia wabunge Katani Ahmed Katani na Savelina Mwijage ambao ni wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa.

UKIFANYA HAYA MAMBO MAPENZI YATANOGA KWA ASILIMIA 90


Wanaume wengi hupuuzia hili, huona kama ni jambo lisilo na maana sana kwao na wenzi wao. Hali ni tofauti sana kwa wanawake ambao hupenda kuwasifia wanaume zao. Nitakupa mifano miwili ya namna wanandoa wa jinsia mbili tofauti wanavyotambulishana kwa jamaa zao. Kwa mafano manakutanata kwenye majumuiko ya harusi na sherehe kama hizo. Mme 1 akamtambulisha mkewe kwa jamaa zake, huyu ni mama Rick mke wangu. Mme wa 2 akamtambulisha mkewe, huyu ni my lovery sweetheart wife, nampenda sana kuliko wanawake wote duniani. Kama upo kwenye huu utambulisho umeona tofauti gani? hao wanawake wa pande mbili watajisikiaje? Nahisi umejifunza kitu hapo

MALENGO SHIRIKISHI
Wanaume wengi wana ulemavu mmoja; hawapendi kuwashirikisha wanawake katika mambo yao. Wanapenda kufanya mambo yao kwa siri na wakati mwingine ikilazimika kumwambia mkewe basi kwa mshtukizo baada ya kukamilisha jambo husika. Siku hizi dunia imebadilika, kuna mambo mengi. Kuna suala la hasara katika biashara, utapeli, kifo cha gafla, ajali n.k. Mkeo ndiye rafiki yako mkubwa kuliko wote, ndiye ndugu yako wa karibu zaidi kuliko yeyote. Mmeshirikiana kuzaa watoto na kujenga maisha pamoja. Yeye anapaswa kujua mambo yako, ndiye mtetezi wako nambari wani. Mweleze juu ya malengo yako, wakati mwingine anaweza kukusaidia sehemu ambayo hukutarajia. Hata hivyo, kumshirikisha katika malengo yako, kunampa nguvu na nafasi ya kujiona mama katika familia yenu. Lakini ngoja nitoe angalizo, kuna wanawake ambao huwezi kumshirikisha from A to Z ya malengo yako kutokaa na tabia na mienendo ya maisha, hope kila mtu anafahamu strength and weakness ya wake na waume zetu, so be careful in some extent.

KIPAUMBELE/CONCERN
Kuna wakati wanawake huwa na mambo yao binafsi. Kazini au kifamilia. Inawezekana akatatizika katika eneo fulani ambalo kwa namna moja ama nyingine atahitaji usaidizi wako. Ikitokea mkeo akawa katika hali hiyo, msikilize. Mathalani ana tatizo la kifamilia, amekuambia mmoja wa wazazi wake anaumwa, msaidie. Si lazima kifedha, lakini kuonesha kujali kwako tu, kutampa matumaini na faraja kwamba anaishi na mtu sahihi. Acha kupuuza mambo yake; hata yale madogo, kama ya ‘mtoto wa dada amerudishwa ada shuleni’. Msikilize, mshauri panapofaa kufanya hivyo na ukiweza msaidie hata kifedha. Katika upande wa pili ni hivyo hivyo. Labda una tatizo binafsi, kikazi au kifamilia, mshirikishe. Unaweza kushangaa jambo ambalo uliamini unaweza kulimaliza peke yako, kwa kumshirikisha likawa jepesi zaidi na mambo yakaenda vyema. Kipaumbele kwa namna yoyote ile, kunaongeza mapenzi zaidi kwa mwanamke.
"Together we swim in the same pool"

USAFI
Asilimia kubwa ya wanawake wanapenda sana usafi. Ni aghalabu kukutana na mwanamke asiyejipenda. Ndiyo maana wanaitwa mapambo ya nyumba au ua la nyumba! Ni kwa sababu ya hulka yao ya kupenda sana usafi. Mwanamke anavutiwa sana na mwanaume mtanashati. Usafi wako unamfanya ajiamini kuwa na wewe. Hata nyumbani kwako, lazima uishi katika nyumba safi. Hata anapokuja kukutembelea, anakuta mazingira masafi kuanzia sebeleni hadi chumbani. Anapokukuta katika hali ya usafi, inakuwa rahisi zaidi yeye kuanzia hapo alipokukuta na kuendelea mbele. Rafiki yangu, kama uko mbali na usafi, ujue kuwa itakuwa vigumu kupata mdada wa ukweli – yule wa ndoto zako. Wanaume wengine wanapanga kutoka outing na wapenzi wao, mkifika huko mwanamke anajuta WHY amekubali kukutana na wewe maana utamkuta mwanaume hajapasi Tshirt/shirt, kwapa linapumua, ukiongea mdomo unatoa harufu inakuwa tabu tupu. Mwanume ukijipenda unatakuwa mtanashati tu

KUJIAMINI
Mwanamke anajisikia salama zaidi akiwa na mwanaume ambaye anajiamini – mwenye uwezo wa kutetea hoja zake na kujieleza sawia. Siyo anayebabaika. Suala la msimamo binafsi, kwa mwanamke ni kubwa kuliko hata kumnunulia manukato mapya! Mathalani unakuwa naye katika mtoko, angependa kukuona ukiwa katika hali halisi ya maisha yako, usiyeyumbishwa na mwenye kutoa maamuzi yasiyoyumba. Wakati mwingine, mwanamke anaweza kukupima hata katika jambo ambalo amekosea yeye, ataangalia unavyotoa maamuzi yako, lakini pia atafuatilia kuona kama utakuwa mwepesi wa kuyabadilisha. Anataka kuona msimamo wako muda wote. Mwenye kujiamini na mawazo yasiyo na matege wala makengeza! Usiyebadilika kama kinyonga! "Men believe on your standing hills"

ANAYEJALI na KUFUATILIA
Wanawake wanapenda sana wanaume wanaowajali. Wanaowaona wao ni kila kitu na wanaotoa kipaumbele kwao. Kama huna tabia hiyo, ujue upo katika nafasi kubwa ya kumkwaza mpenzi wako. Mjali mpenzi wako kwa kila hali lakini pia uwe na kiasi. Kumjulia hali kila wakati na kutaka kujua maendeleo yake, kutakupa nafasi kubwa ya kuendelea kudumu katika uhusiano hai. Wanaume wengi ni wavivu, si tu kuwatumia hata SMS za “mambo dia?” wapenzi wao lakini hata kujibu tu, “niko poa, Si hulka ya wanaume kutumatuma SMS – inajulikana, lakini angalau ukiweza kulifanya hili hata kidogo tu hata mara moja kwa wiki, utakuwa unajiongezea pointi kwa mwenzi wako na kumpa courage ya kufurahia mapenzi ya ndoa.

MAANDALIZI YA TENDO LA NDOA
Tendo la ndoa halina maana ya kukomoana. Jenga mazoea ya kufanya maandalizi kamili kabla ya tendo. Sikiliza hisia za mwenzako. Ukiweza kumjulia mke wako katika eneo hili, ni wazi kwamba utazidisha upendo wake kwako, lakini pia atakuwa katika kuta za uaminifu. Unapokuwa kazini mchokoze "aisee nasikia hamu leo" hayo ndo maandalizi ya saikolojia. kupitia sms hiyo utasikia feeling zake, ataji-express. Kufikia jioni/usiku utashangaa unashikwa mkoni kupelekwa kitandani. Akatafute nini nje wakati wewe ndiye mganga wake unayeweza kumtibu barabara? Jiamini katika shughuli, fanya mazoezi ya viungo hata kukimbia ili uongeze pumzi ya kutoa dozi kitandani.
Epuka mapenzi ya kubakana, unafika tu bed unamvuta unamvua na kuanza kupanda kifuani......nooooooo hapo hakuna maandalizi ya kisaikolojia wala ya kimwili, hii itampekea kuchukia tendo because there is no any enjoyment

OUTING SOMETIMES
Kulingana na budget yako, si vibaya mara moja kumtoa mpenzi wako outing walau mara moja ndani ya miezi sita hata mwaka kama budget ni shida. Kwa wale wenye familia unaweza toka mkaspend 1 or 2 days outing na mkeo. Kuna mambo mmeo/mkeo anaogopa kukufanyia kulingana na mazingira ya hapo nyumbani na familia kwa ujumla. Lakini mkitoka nje LAZIMA mta-experience the difference for SURE. Pia ni njia mojawapo ya kuboresha na kupalilia penzi lenu na kuongeza uaminifu kati yenu

KINYWAJI KILICHOPEWA JINA ‘Poteza Ubikira’ CHAZUA GUMZO CHINA


Kinywaji maarufu kwa jina ”blackout in a can’ nchini Marekani kimeingia nchini China na kuzua gumzo kwa watumiaji wa kinywa hicho.

Four Loko , ni kinywaji kilicho na ladha ya matunda na asilimia 12 ya pombe kilitumika sana katika sherehe nchini Marekani kabla ya kuondolewa madukani katika majimbo kadhaa hadi pale viungo vyake viliporekebishwa.

Na sasa kimepata umaarufu mkubwa nchini China , huku raia wakikiita ‘Lose Virginity’ kwa kuwa wanahisi kinywaji hicho kina nguvu zaidi.

Wananchi kadhaa wamepakia kanda za video wakinywa kinywaji hicho cha mililita 695.

Kinywaji hicho kiligonga vichwa vya habari hivi majuzi baada ya wanawake watatu walio katika umri wa miaka 20 kuficha na kuingiza kinywaji hicho katika baa moja ya karaoke,kupoteza fahamu baada ya kunywa na kupoteza vitu vyao vyote kwa wezi.

Four Loko kimeelezewa katika mitandao ya kijamii nchini China kuwa kinywaji kilicho na pombe pamoja na kafeini.

Baadhi ya watu wanadai kwamba mchanganyiko huo unakifanya kinywaji hicho kuwa na nguvu na kina uwezo wa kumfanya mtu kupoteza fahamu baada ya kunywa chupa moja tu

FIESTA YARUDISHA PENZI LA SHILOLE NA NUH MZIWANDA


Wapenda Kunyapia nyapia Udaku wa Mastaa wa Bongo wameachwa njia panda baada ya mastaa Nuh Mziwanda na Shilole kuanza tena kuwa karibu kwa kupostiana kwenye page zao za mitandaoni, Wawili hao ambao siku za njuma walikuwa wapenzi wa kupika na kupakuwa waliachana na kila mmoja kuchukua hamsini zake lakini msimu huu wa Tamasha la Fiesta inasemekana wamekuwa karibu kutoka na kuwa ni wamoja wapo katika watumbuizaji wa Tamasha hilo huku wakisafiri mikoa mbali mbali kitu ambacho kimewaweka karibu zaidi

Nuh Amepost Picha hii katika ukurasa wake wa Instagram:

Baada ya Muda Shilole naye Akajibu Mapigo kwa kuweka picha ambayo inaonyesha alimpiga Nuhu Mziwanda wakiwa katika Chumba cha Hotel.....
Wajuzi wa Kunyapia nyapia Udaku Wanadai Picha hiyo aliyopost shilole na kuiifuta inaujumbe mzito ndani yake , Kuwa inawezekana wawili hao huko walipo kwenye Tamasha wanalala chumba kimoja...

RUBBY ATANGAZA KUJISIMAMIA MWENYEWE BAADA YA KUTEMANA NA CLOUDS FM, ADAI SASA NI YEYE NA MASHABIKI WAKE


Msanii wa Bongo Fleva, mwanadada Ruby ambaye amewahi kutamba na wimbo wake wa “Na Yule’ amefunguka na kusema kwa sasa amebadili uongozi wake na kujisimamia yeye kwani anataka kusimama yeye pamoja na mashabiki zake.

Ruby alisema hayo kwenye kipindi cha eNewz na kudai kuwa yeye aliamua kubadili uongozi kwa sababu anataka kusimama yeye kama yeye kwenye muziki kwa kutegemea mashabiki wake, pia Ruby anadai Tanzania ukimchana mtu ukweli unaonekana wewe ni mkorofi au mgomvi.

“Unajua hata mtoto anapokuwa kwa wazazi inafika wakati anahitaji kuanza maisha yake mwenyewe, hivyo mtoto akiondoka kwa wazazi haina maana kuwa hauna wazazi ‘No’ wala haina maana kuwa umeondoka nyumbani kuna matatizo bali unakuwa umeanza maisha yako mwenyewe, ni sawa na mimi saizi nimebadili uongozi wangu na niko mimi kama mimi kwani nataka kusimama pamoja na mashabiki zangu. Watu wanasema sijui mimi ni mkorofi hao ni wao kwani mtu ukimchana ukweli unaonekana wewe ni mkorofi ni bora ukamwambia mtu ukweli kwani ukweli utakuweka huru” alisema Ruby

SERIKALI YAANZA MAZUNGUMZO YA KUWAOKOA MADEREVA 12 WALIOTEKWA CONGO

Serikali imeingilia kati na kuanza mazungumzo ya kuwaokoa madereva 12 wa malori kutoka Tanzania waliotekwa nchini Kongo (DRC) na kundi la waasi wa Mai Mai.
loritanzania

Waasi hao mbali na kuwateka madereva hao wametoa saa 24 kuanzia juzi saa 10 jioni walipwe fedha kiasi cha Dola za Marekani 4,000 kwa kila dereva ili waweze kuwaachia.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mindi Kasiga, alisema waasi hao wametishia kuwaua mateka hao endapo hawatalipwa kiasi hicho cha fedha hadi kufikia jana saa 10 jioni.

Mindi alisema katika tukio hilo, madereva wawili wa Kitanzania walifanikiwa kutoroka na ndiyo waliosaidia kutoa taarifa kuhusu tukio hilo.

“Serikali imepokea taarifa za kutekwa kwa malori 12 katika eneo la Namoyo Jimbo la Kivu Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, jana (juzi) Septemba 14, 2016. Kati ya malori hayo manane yanamilikiwa na mfanyabiashara wa Kitanzania, Azim Dewji na mengine yanamilikiwa na wafanyabiashara kutoka Kenya.

“Kwa taarifa zilizopatikana watekaji ni kikundi cha waasi cha Mai Mai ambao baada ya kuyateka magari hayo, waliwashusha madereva na kuwapeleka porini na kisha kuteketeza kwa moto malori manne ambayo yote ni ya Dewji.

“Waasi hao wametoa saa 24 kuanzia jana saa 10 jioni walipwe fedha kiasi cha Dola za Kimarekani 4,000 kwa kila dereva ili waweze kuwaachia,” alisema Mindi.

Alisema Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeshachukua hatua za awali za kuwasiliana na Serikali ya DRC ili kuhakikisha kuwa madereva hao wanaachiwa haraka iwezekanavyo wakiwa salama kabisa.

Alisema tukio la aina hiyo ni la pili kutokea ambapo katika mwaka jana masheikh kutoka Tanzania walitekwa nchini DRC lakini kwa ushirikiano wa Serikali hizo mbili juhudi ziliweza kuzaa matunda na masheikh hao kuachiwa huru bila madhara yoyote.

“Serikali ingependa kuushauri umma wa Watanzania hususan wafanyabiashara kuomba taarifa ya hali ya usalama kwa maeneo yenye matatizo ya kiusalama kama Mashariki ya Kongo hususan Kivu ya Kusini kabla ya kusafiri kwenda maeneo hayo,” alisema Mindi.

SAKATA LA REDIO KUFUNGWA MAGIC FM YATAKIWA KUOMBA RADHI SIKU TATU MFULULIZO, REDIO 5 ZAFUNGIWA MIEZI


August 29 2016 Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye alitangaza kuvifungia vituo viwili vya radio kwa muda usiojulikana ambavyo ni Magic Fm ya Dar es salaam na Radio 5 ya Arusha kwa makosa ya kutangaza na kutoa habari za kichochezi.

Waziri Nape alielekeza kamati ya maudhui kuviita vyombo hivyo na kuwasikiliza kwa kina kisha kushauri hatua zaidi ya kuchukua.

Leo September 16 2017 kamati imetoa maamuzi ambapo Magic FM wamepewa onyo kali na kutakiwa kuomba radhi kwa siku tatu mfululizo kuanzia kesho September 17 2016, Redio 5 imepewa adhabu ya kulipa shilingi milioni 5, kufungiwa miezi 3 na kuwekwa chini ya uangalizi wa mwaka mmoja.

ZOMBE AACHIWA HURU, MSHIRIKA WAKE AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA


Mahakama ya Rufaa imemhukumu aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni, Christopher Bageni kunyongwa hadi kufa katika kesi ya vifo vya wafanyabiashara wa madini iliyokuwa ikimkabili yeye pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi Abdallah Zombe na maofisa wenzake wawili.

Katika hukumu hiyo, Zombe na maafisa wengine wawili wameachiwa baada ya kushinda rufani hiyo dhidi yao.

Hukumu hiyo imehitimisha mvutano wa muda mrefu wa kisheria kati ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na maofisa hao kwani baada ya kimya kirefu hukumu hiyo imetolewa.

Watuhumiwa wengine katika kesi hiyo walikuwa ni, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Kituo cha Polisi Urafiki, Mratibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Ahmed Makelle na Rajabu Bakari.

Hukumu hiyo imekuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu, wakiwamo ndugu wa marehemu hao, wanasheria na jamii kwa jumla baada ya miezi minne, majuma mawili na siku mbili, tangu rufaa iliposikilizwa.

DPP alikata rufaa akipinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyowaachia huru Zombe na wenzake wanane katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wawili wa madini kutoka Mahenge, Morogoro na dereva wa teksi, mkazi wa Dar es Salaam.

Katika kesi ya msingi, Zombe na wenzake walidaiwa kuwaua kwa kukusudia wafanyabiashara Sabinus Chigumbi, maarufu Jongo na ndugu yake, Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na Juma Ndugu, aliyekuwa dereva wa teksi wa Manzese.

Walidaiwa kutenda makosa hayo Januari 14, mwaka 2006, katika msitu wa Pande, uliopo wilayani Kinondoni baada ya kuwakamata wafanyabiashara hao Sinza, walipokuja Dar es Salaam kuuza madini.

Agosti 17, 2009, Mahakama Kuu iliwaachia huru washtakiwa hao ikisema baada ya kusikiliza ushahidi na hoja za mawakili wa pande zote iliridhika kuwa hawakuwa na hatia ya mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili.

Badala ya kosa la mauaji ambalo adhabu yake ni kunyongwa hadi kufaa, DPP aliiomba Mahakama imtie hatiani Zombe kwa kosa la kuwalinda wahalifu, ambao adhabu yake ni kifungo kisichozidi miaka saba jela.

Wakili wa Serikali Mkuu (PSA), Timon Vitalis alidai DPP alifikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa hakuna ushahidi wa kumtia hatiani Zombe kwa kosa la mauaji.

ALICHOKIZUNGUMZA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI CONGO KUHUSU MADEREVA WALIOTEKWA


Jana ziliripotiwa habari za kutekwa kwa madereva wa malori kutoka Tanzania na Kenya kutekwa na kundi la waasi nchini Congo. Leo September 16 habari zilizoripotiwa na BBC Swahili zimedai kuwa watu wameokolewa na jeshi la nchi hiyo.

BBC imezungumza na waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo ambapo kuwa madereva wote wameokolewa na vikosi vya jeshi la nchi hiyo na wako salama. BBC imesema utekaji wa madereva hao ulifanywa na watu wenye silaha katika kijiji cha Matete kuelekea Namoya kilichopo Mji wa Kivu Kusini Mkoa wa Manyema.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Congo alipoongea na BBC kwa njia ya Simu, amesema ni magari saba ya kampuni ya Simba inayomilikiwa na mfanyabiashara Azim Dewji kutoka Tanzania ndio yaliyochomwa.

Waziri huyo amesema tukio hilo halijafanywa na waasi kama ilivyoanza kuripotiwa, ila ni majambazi tu ndio waliofanya tukio hilo.

>>>Ni majambazi tu wanatoka porini walipoona magari yanatembea wakayasimamisha katikati ya pori na kuangalia kama kuna pesa wanyang’anye lakini hawakukuta pesa wakaamua kuwachukua madereva na kukimbia nao porini kisha wakayachoma magari 6 na moja halikuteketea.:- Waziri Mambo ya Ndani Congo.

MAJAMBAZI, MALI ZA WIZI NA SILAHA VYAKAMATWA DAR



Kikosi maalum cha kupambana na ujambazi wa kutumia silaha cha Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kimefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 5 wa makosa ya ujambazi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali.

Kamishna wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Saimoni Sirro akionesha baadhi ya vifaa vilivyokamatwa.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam Kamishna Saimoni Sirro wakati akitoa taarifa ya kukamatwa majambazi wa 5 na kukutwa na silaha aina ya shotgun, bastola 3 na risasi 49.

Katika tukio lingine Polisi mnamo tarehe 5.9.2016 majira ya saa 8 usiku maeneo ya Magomeni mtaa wa Makumbusho waliokota begi lililokuwa na bastola mbili, sambamba na hilo wamefanikiwa kukamata magari 4 ya wizi, hati za magari na watuhumiwa wawili wa uhalifu huo wamekamatwa.
Jeshi hilo limetoa wito kwa viongozi wa serikali za mitaa kupitia kamati za ulinzi wa mitaa kuimarisha ulinzi na kuwataka wamiliki wa nyumba za kupanga kuhakikisha wanaweka kipengele cha kuwepo na picha katika mikataba ya kupangisha nyumba zao kutokana na uwepo wa wimbi la uhalifu.

Wakati huo huo Kamanda Sirro amesema Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kipindi cha siku 11 wamefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi 882,570,000 ikiwa ni tozo za makosa ya usalama barabarani na makosa mengineyo.