Jumanne, 9 Septemba 2014

NYAMA YA KIBOKO YAWALETEA MAAFA.

Watu kumi walikanyagwa na gari lililokuwa linakwenda kwa mwendo wa kasi walipokuwa wanajaribu kujipatia angalau kipande cha nyama ya Kiboko mwishoni mwa wiki. Taarifa hii ni kwa mujibu wa mtandao wa Daily Nation. Kiboko huyo alikuwa amegongwa na gari na kufariki Jumamosi jioni katika mkoa wa Limpopo wakati ambapo wanakijiji walikimbia katika sehemu hiyo angalau kujipatia...

EBOLA INAENEA KWA KASI NCHINI LIBERIA.

Ugonjwa wa Ebola unaenea kwa kasi nchini Liberia huku maelfu ya watu wakiambukizwa upya na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka katika muda wa wiki tatu zijazo. Hii ni kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO. Shirika hilo linasema kuwa njia zinazotumika kukabiliana na janga la Ebola hazijafanikisha vita dhidi ya Ebola. Takriban watu 2,100 wamefariki kutokana na ugonjwa...

EURO 2015:ENGLAND YAIFUNGA USWISI

England imeanza kusaka tiketi ya kucheza fainali za kombe la Ulaya kwa kuifunga Uswisi. England imeanza harakati hizo za kucheza fainali hizo zitakazofanyika huko Ufaransa baada ya kuishindilia Uswisi mabao 2-0 usiku wa kuamkia leo. Mshambuliaji mpya wa Arsenal, Danny Welbeck, aliibuka nyota wa kocha Roy Hodgson kwa kazi nzuri ya kutumbukiza kimiani mabao yote mawili,...

WACHUNGUZI WASEMA MH17 ILIDUNGULIWA.

Wachunguzi wa Kijerumani dhidi ya ndege ya abiria ya Malaysia ambayo ilipata ajali huko Ukraine mwezi July na kuripuka angani wanaeleza kua ndege hiyo baada ya kukumbwa na kitu chenye ncha na kugongwa mara kadhaa na vifaa vyenye mionzi mikali ndio chanzo cha ajali. Mwandishi wa youngluvega.blogspot.com amesema kwamba ushahidi huo ni wawazi na kwamba ndege hiyo ilishambuliwa...

Wasanii waliporudi tena kutoa misaada kwa majeruhi wa ajali ya Musoma baada ya Fiesta.

  September 05 zaidi ya watu 35 walipoteza maisha yao kutokana na ajali ya mabus mawili kugongana uso kwa uso eneo la Saba saba ambalo liko nje kidogo na mji wa Musoma,wasanii waliahidi kwenda kutoa misaada kwa watu waliokutwa na matatizo ya ajali hiyo. Asubuhi ya leo September 08 kabla wasanii kuanza safari ya kurudi Dar walitiza ahadi yao kwa ndugu na jamaa...