Ijumaa, 20 Novemba 2015

Alikiba Atolea Ufafanuzi Post ya ‘Utata’ Aliyoandika Instagram, na Ampongeza Diamond Kwa Ushindi wa AFRIMA

Alikiba ametolea ufafanuzi post yake ya Instagram iliyozua mjadala kwa mashabiki mbalimbali wa muziki ambao waliipokea kwa hisia tofauti.

Siku ya Jumatatu Nov.16 Muimbaji huyo wa single mpya ‘Nagharamia’ aliandika, “Asanteni sana najua mmepiga kura sana lakini nilikuja kugundua baada ya kufuatilia kuwa kuna mambo yanaendelea ya watu wanadiriki hata kupoteza pesa zao kwaajili yangu ila nawaomba fans msinielewe vibaya I will always be there for you #hapakazitu #kingkiba,post ambayo baadae aliifuta.

Kupitia kipindi cha Ala Za Roho cha Clouds Fm na Diva The Bawse, king Kiba amesema kuwa watu walimuelewa vibaya kwenye post hiyo na ndio sababu kubwa ya kuamua kuifuta,

watu walinielewa vibaya mimi nilikua nawaambia mafans wangu, sababu wao ndo wananipigia Kura mimi sikumaanisha kuhusu tuzo walinielewa vibaya” alisema Kiba.

Hata hivyo licha ya kwamba yeye hakushinda kipengele hata kimoja kati ya vinne alivyotajwa kuwania kwenye tuzo za AFRIMA 2015, lakini hakumpongeza hata msanii mmoja wa Tanzania aliyeshinda ambao ni Diamond na Vanessa Mdee. Kusuhu hilo Alikiba alisema,

Siwezi ku-post kitu kuhusu Kushinda Kwao, unajua hakuna uzalendo. watu wangapi wanafanya Vitu vizuri hawapongezwi? Mimi nafanya vingapi? Sisi sio wazalendo…Unajua watu mimi hawanijui Wanahisi kama mimi nina ringa hivi au nina wivu, ila mimi nawapenda wasanii wote pia mziki mzurialisema Alikiba.

Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Diamond ukoje kwa sasa, ndipo alimpongeza Platnumz kwa ushindi wa tuzo 3.

Mimi sina tatizo na Diamond, nasikia kashida tuzo 3, nampongeza Sana sababu tumepata mtu ambaye anatutambulisha kimataifa ni Kitu poa Sana…Mimi na Diamond we are goodalimaliza Alikiba.

Wazanzibari Wanaoishi Uingereza Waandamana Wakitaka Maalim Seif Sharif Hamad Atangwe mshindi wa Kiti cha Urais

Wazanzibari wanaoishi nchini Uingereza jana walifanya maandamano wakidai haki ya kutangazwa ushindi wa Chama Cha Wananchi (CUF) katika uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika Octoba 25 mwaka huu
Maandamano hayo yaliandaliwa na Jumuiya ya Zanzibar Welfare Association (ZAWA) ambapo wazanzibari hao walitoka maeneo mbali mbali katika miji yao na kukusanyika katika eneon la  Downing Street kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron na uongozi huo kukabidhi barua yao yenye malalamiko kutaka suala la Zanzibar lishughulikiwe.
Maandamano hayo yalifanyika kwa lengo la kuongeza shindikizo kwa mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuchukua hatua za haraka ya kuhakikisha Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) inakamilisha kazi ya kutangaza matokeo ya uchaguzi huo.

Zanzibar  iliingia katika mkwamo wa kisiasa baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salum Jecha Octoba 28 kutangaza kuufuta uchaguzi wote kwa madai kwamba ulikumbwa na matatizo mbali mbali.

Wakati jecha akitoa tangazo la kufuta matokeo bila ya kushauriana na tume yake alikuwa tayari ameshatangaza matokeo ya kura za urais za majimbo 31 kati ya 54 ya Zanzibar pia washindi wa nafasi za uwakilishi na udiwani katika majimbo hayo walishatangazwa na walishakabidhiwa vyeti vyao.

Rashid Ali ambaye ni kiongozi wa ZAWA  alisema jana kuwa wamewasilishwa barua hiyo wakiamini kwamba suala la Zanzibar litashughulikiwa ili wananchi wa Zanzibar waweze kuendelea na maisha yao ya kawaida.

Mwakilishi wa ZAWA, Hassan Khamis alisema wameamua kupeleka barua kwenye ofisi za waziri Mkuu wakiamini suala hilo litashughulikiwa ikiwa ni pamoja na serikali ya Tanzania kuchukua hatua madhubuti na za haraka kaika kushughulikia suala hilo ambalo limewaweka wazanzibari roho juu.





Nina Wasiwasi na Naibu Spika Kama Atalihimili Bunge Hili

Sina wasiwasi ni elimu yake wala uwezo wake wa kujieleza, ila nina wasiwasi na hekima yake na busara zake kama zinaweza kustahimili mikiki mikiki ya bunge kama alivyoonyesha Anne Makinda.

Nafikiri wote tunaujua uwezo wa Prof. Muhongo kielimu lakini alifeli somo la hekima.

Najua bunge lina sheria zake kanuni zake miiko yake na desturi zake, lakini ni mara ngapi tumeona sheria zikikiukwa na wabunge wenyewe.

Kama tukisema yeye atakuwa "Iron Lady" kuwa kila mbunge akikosea anamhukumu kulingana na kanuni atafukuza wangapi, naje kama atafukuza karibu nusu ya wabunge ataonekana ni Naibu Spika mzuri au kiti kimemshinda.

Tuchukue mfano wa refa wa mpira wa mguu anayewatoa wachezaji kwa red kadi kila wanapofanya rafu, hivi timu ikibaki na nusu ya wachezaji huyo refa atakuwa bora?

Najaribu tu kumwangalia huyu Naibu Spika asije siku moja akatoa machozi kwa kuzomewa au kuulizwa maswali ya kuudhi akakiaibisha kiti.

Namuomba sana Spika Job Ndugai ajaribu kumsaidia msaidizi wake.

Tujadili kwa mstakabali wa nchi yetu.

By QuinineJamii Forums

Yanayojiri Bungeni Dodoma Muda Huu..Wabunge wa Ukawa Walianzisha na Kutolewa Nje ya Bunge na Spika

Wabunge  wanaounga  umoja  wa  Katiba  Ya  Wananchi, UKAWA  wametolewa  nje  ya  ukumbi  wa bunge  muda  huu  baada  ya  kugoma  kutambua  ujio  wa  Dr Shein bungeni  na  kuanza  kuzomea  huku  wakisema  Maalim Seif....Maalim Seif

Spika  wa  bunge,Job Ndugai  aliwataka  wabunge  hao waache kuzomea  na  badala  yake  wakae chini  lakini  wakakaida, hali  iliyomfanya  awaamuru  watoke  nje kwa  hiari  yao  kabla  nguvu  ya  dola  haijatumika  kuwatoa.

Model Maarufu Bongo Aibua Shutuma Nzito Kwenye Tasnia ya Mitindo..Adai Tasnia Imejaa Machoko ili Usonge Mbele ni Lazima Uwakaze

Model wa Kiume Anayejulikana kama @calisah Huku Instagram Ameibuka na Tuhuma nzito iliyopo kwenye Tasnia hiyo ya Mitindo na Urembo ...

Ameandika Haya Kwenye Ukurasa Wake wa Instagram:

|Sikutaka kuandika chochote kuhusiana na tuzo za swahilifashionweek. Ila naamini waliopo kwenye category zote ndio waliostahili kuwepo...

Na naamjni waliangalia vigezo vyao na kuhisi pengine wao ndio waliostahili. Mtazamo wangu kwa upcoming models wote wanaotamani kesho na kesho kutwa kuja kua model km mimi au mwingine yeyote. Tambueni hii tasnia imeandamwa na machoko (gays) sasa basi...... hawa watu wanahisi wanauwezo wa kukontro models wake kwa kukidhi haja zao. Na ikiwa utaenda nao sawa bc watakutumia vizuri na watamtumia mtu mwingine yeyote mwenye muonekano mzuri kwakua wao wanajua kua ili usongee mbele ni lazima uwakaze. 

Na usipo wakaza utaanza kuona safari yako inaanza kua ngumu na watatafuta njia yeyote ili wakuzime na ikiwemo kutaka kupandisha watu juu ambao walikua hawapo kwenye hiyo level ili tu wakuoneshe kua wao wanapower. Kuna ma_disigner wengi sana ktk hii tasnia yetu. Msibabaike kwa vitisho na msikubali kuuza utu wenu ili mpate show au kuwepo kwenye award yoyote, mkifanye hivyo mtatumiwa na kuachwa na kisha wao kwenda kutafuta wengine, they always looking for what new. Sijakasirika kutokuwepo kwenye tuzo za swahilifashionweek or nah kwani nilijua muda mrefu kua siwezi kua huko na ndio maana hua sijishulishagi kwenda hata kwenye cast, na sijawahi kwenda kwenye cast yoyote ya swahilifashionweek tangu inaanza.

Cz I naw evrythng. ..... Models kama hamtakua makini mtaendea kutumiwa kwa kuafurahisha watu kila cku, sitaki na wala sitataka kua kua kwenye award yoyote na wala hakuna quma yeyote ninarmuogopa cz hakuna anaenipa hela ya kula kati yenu nyote, taftani hao models wenye njaa.... wawakaze halafu ndio muwape tuzo zenu, "Ushauri wangu kwa models wengine ambao wamekua_dissaponted. Tulieniii..... tengenezeni portfolio zenu nzuri na mtafute kazi nje ya nchi.... tuige mfano kwa @daxx_cruz @flavianamatata na wengine waliotangulia... mkibaki hivyo hamtafkia kokote kwa kutegemea wakina @martinkadindaofficial na kina @mustafahasanali they got nothing to help u... Hakuna yeyote kati yao mwenye uwezo wakukuangusha ikiwa utajiweka vizuri na kufokas soko la mbele. Msikubali kubaika na kuuza utu wako ili mpate jina bila ya hela|  Calisah

LIVE TOKA BUNGENI: Rais Magufuli Ampa Hongera Zitto Kabwe Kwa Kutokuleta Fujo Bungeni na Kubakia Ndani ya Bunge Wakati Ukawa Wametoka

LIVE TOKA BUNGENI:Muda huu Rais Magufuli Anatoa Hotuba yake ndani ya Bunge na Amempa Hongera Zitto Kabwe Kwa Kutokuleta Fujo Bungeni na Kubakia Ndani ya Bunge Wakati Ukawa Wametoka Baada ya Kutolewa na Spika kutokana na Utovu wa nizamu walioonyesha kwa Kupiga Makelele

JE Unakichukuliaje Kitendo cha ZITTO KABWE Kubaki Bungeni Wakati Wabunge wa Upinzani Wote Wametoka Nje ?

JE Unakichukuliaje Kitendo cha ZITTO KABWE Kubaki Bungeni Wakati Wabunge wa Upinzani Wote Wametoka Nje Kushinikiza Maalim Seif Atangazwe Mshindi wa Urais Zanzibar?

TOA MAONI YAKO