Ijumaa, 21 Novemba 2014

Kipa wa Chelsea yuko sokoni.

Chelsea+v+Southampton+Premier+League+aQgqk_Wv1pBx
Klabu za Arsenal , Liverpool na Real Madrid ziko kwenye vita kali ya kuwania kumsajili kipa wa Chelsea Petr Cech .
Chelsea inaalzimika kumuuza kipa huyo kwa kuwa hana nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza baada ya kurudi kwa kipa Mbelgiji Thibaut Courtois .
Hadi sasa Chelsea haijapoteza mchezo wowote msimu huu huku Thibaut akicheza kwenye mechi karibu zote hali inayomfanya Cech kulazimika kutafuta mahali kwingine ambako atakuwa chaguo la kwanza .
Cech ameidakika Chelsea kwa mafanikio makubwa kwa muda wa miaka 11 tangu aliposajiliwa kwa mara ya kwanza akitokea Rennes ya Ufaransa .
Cech analazimika kuondoka baada ya kupokonywa nafasi kwneye kikosi cha kwanza.
Cech analazimika kuondoka baada ya kupokonywa nafasi kwneye kikosi cha kwanza.
Katika kipindi hicho Cech amefanikiwa kutwaa mataji kadhaa yakiwemo matatu ya ligi kuu ya England , UEFA Champions league na UEFA Europa League bila kusahau kombe la Fa na kombe la Carling ambalo siku hizi hufahamika kama Capitol One Cup.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari kocha wa Chelsea Jose Mourinho alikanusha taarifa kuhusu Cech kuwa mbioni kuhama ambapo alisema kuwa hajawahi kupata taarifa yoyote kama hiyo .
Thibaut Courtois ndio kipa namba moja kwenye ikosi cha Chelsea.
Thibaut Courtois ndio kipa namba moja kwenye ikosi cha Chelsea.
Kwa upande mwingine wakala wa Cech Viktor Kolar ameendelea kushikilia msimamo ulioripotiwa na vyombo vya habari kuwa kuna klabu zisizopungua tano ambazo zimeonyesha nia ya kumsajili kipa huyo .
Hadi sasa inafahamika kuwa Arsenal ndio iko kwenye nafasi ya juu kumsajili Cech kwa thamani ya puandi milioni 7 lakini kumekuwa na ishara toka kwa klabu za Ac Milan , As Roma , Real Madrid na Liverpool za kutaka kumsajili Cech .

Ni Diamond Platnumz kwenye XXL leo Novemba 21, isikilize hapa full interview…

e0a8228fb8L 
Kupitia youngluvega.blogspot.com siku ya juzi ulipata taarifa kuhusu msanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz kuachia nyimbo yake mpya ambapo kwa mara ya kwanza ilionyeshwa kupitia kituo cha MTV, na jana ikawa siku rasmi ambayo Diamond aliachia nyimbo hiyo.
Leo Novemba 21, Diamond amesikika kwenye show ya XXL ambapo amezungumzia mambo mengi, baadhi ya yale aliyoyazungumzia ni pamoja na story zilizoenea mitandaoni kwamba mahusiano ya msanii huyo na Wema yameisha pamoja na story ambayo imetokana na kuenea kwa picha mitandaoni za msanii huyo na Zari the Boss Lady kutoka Uganda.
Hii ni sehemu ya mahojiano aliyofanya Diamond kwenye XXL:
Adam Mchomvu :”…Nataka kujua ile vibe ya Fiesta that day, story zilikuja ooh Diamond kazomewa.. kazomewa kazomewa..na vitu kama vile, sijapata chance ya kukusikia wewe una kipi cha kuzungumzia kuhusiana na that situation..?
Diamond :- “… Siku zile kwangu ilikuwa kama mchezo, unajua muziki ushakuwa kama sio fani tena, ushakuwa kama siasa.. So, lazima uichukulie hivyo wewe mwenyewe kama msanii ujue una control vipi kwa sababu sio mara ya kwanza vitu kama hivyo vishatokea Maisha.. Maisha yalitupwa mpaka na mayai viza kabisa.. Ni vitu ambavyo vikitokea naonaga kama ni kawaida…
B 12  :-“…Kwa hiyo ukweli uko wapi kati yako wewe na Wema Sepetu?...”
Diamond  :- “…Kuna vitu vitu fulani nadhani kuvizungumza sio vizuri… Lakini ikifikia kuvizungumzia vinazungumziwa… Uzuri wa mahusiano yetu ni kwamba kila mtu anafahamu… Haijafikia kuweka wazi ndio maana ninapoulizwa inakuwa ni swali gumu kulijibu..
B 12 :- “.. Ni gumu kwa upande wako lakini yeye yuko tayari kuzungumza kwamba it’s over kati yangu mi’ na Diamond…
Diamond  :- “… Sijui…
B 12  :- “...Hii ngoma kama umemzungumzia yeye direct hivi… watu wamekuza akili zao zikaenda mbali zaidi kimawazo lakini, kwamba inawezekana ile singo umemwimbia yeye hivi kwamba bado unamzimia japokuwa bado kama kakutosa hivi…
Diamond  : “.. Waswahili wanasema ‘A’ na ‘B’ yote majibu, halafu ukisikiliza ile nyimbo kama kweli mtu mwenye ufahamu wako, kweli kabisa hauwezi kuwa na maswali mengi …
Kuhusiana na mahusiano yake na Zari the Boss Lady, Diamond amejibu hivi:
Diamond  :- “.. Zari ni rafiki yangu tu, alipokuja hapa mimi ndio nilikuwa mwenyeji wake Tanzania na kama mimi ndiyo mwenyeji sikutaka kuleta roho za kibaguzi, unajua hata alipokuja Davido pia ilibidi awe na mimi karibu ili hata kesho na kesho kutwa  mimi nikiwa Nigeria basi Davido anipokee hivyo hivyo…
Iko hapa full Interview ya Diamond kwenye XXL, unaweza kuisikiliza kwa kubonyeza play.