Jumanne, 11 Novemba 2014

Rais Goodluck kugombea tena urais

 
Rais Goodluck amekuwa akikosolewa kwa mamna anavyoshughulikia swala la Boko Haram

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amethibitisha rasmi kuwa atagombea tena kiti hicho mwaka ujao.
Katika sherehe ya kufana katika mji mkuu Abuja, Bwana Jonathan alimwagiwa sifa na wafuasi wa chama chake, kabla ya kujitangaza kama mgombea.
Amekuwa rais wa taifa hilo maaruifu barani Afrika tangu mwaka 2010.
Waandishi wa habari wanasema uchaguzi wake utakuwa mkali hususan kama upinzani utaungana dhidi ya mtu mmoja.
Mbali na siasa , eneo la Kaskazini Mashariki ya Nigeria, linaendelea kukumbwa na vurugu huku Boko Haram wakiwa tu ndio wameteka mji mwingine wa Mahia na kujiongezea idadi ya miji wanayodhibiti.
Rais Jonathan alitoa wito wa kimya cha dakika moja kwa vijana 46 waliouawa Jumatatu katika shambulizi la kujitoa mhanga dhidi ya shule ya upili ya kuchochea zaidi hali.
Rais Jonathan amekuwa akikosolewa kwa kushindwa kushughulikia suala la wanamgambo wa Boko haram ipasavyo.
Lakini wanasiasa wa vyama vyote wanaonekana kuwa na ajenda ya kupata mamlaka zaidi kuliko kumaliza harakatai za wapiganaji wa Boko Haram ambao wamekuwa kero kwa taifa hilo.

Taarifa kuhusu ajali ya moto ulioteketeza shule ya msingi.

fire-and-explosion-accidents
Hii sio picha halisi ya ajali ya moto huo.
Moto mkubwa umeteketeza majengo ya Shule ya msingi Filbert Bayi na kisha kusambaa na kuteketeza mabweni yote ya Wanafunzi pamoja na madarasa.
Mwenyekiti wa shule hiyo Filbert Bayi amesema moto huo ulianza saa nane usiku katika bweni la wanafunzi wa kike na kisha kusambaa shule nzima kutokana na gari za zimamoto kuchelewa kufika mapema.
20141111_130601
Hakuna mwanafunzi yoyote aliyejeruhiwa wala kudhurika kutokana na moto huo.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani kamishna mwandamizi wa Polisi Litrichi Matei amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa taarifa kamili juu ya chanzo cha moto huo zitatolewa baada ya uchunguzi kukamilika.
Bonyeza play kusikiliza taarifa iliyoripotiwa na televisheni ya TBC 1 kuhusu ajali hiyo.

HATMA YA AFCON 2015 ?

Confederation_of_African_Football_logo.svg
Shirikisho la soka barani afrika CAF limewaondoa mashindanoni waliokuwa wenyeji wa michuano ya AFCON Morocco baada ya taifa hilo kushikilia msimamo wake wa kutokuwa tayari kuandaa michuano ya AFCON mwaka 2015 kutokana na hofu ya kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola.
Morocco ambao walikuwa wamefuzu moja kwa moja kama wenyeji hawatatweza kushiriki michuano hiyo na badala yake nafasi waliyokuwa nayo itakwenda kwa timu nyingine ambayo itachukua jukumu la kuandaa michuano hii .
Nchi ambazo CAF inafanya nazo mazungumzo kuhusiana na kuwa mwenyeji wa AFCON 2015.
Nchi ambazo CAF inafanya nazo mazungumzo kuhusiana na kuwa mwenyeji wa AFCON 2015.
Awali CAF ilitoa mpaka jumamosi iliyopita kwa Morocco kuthibitisha uamuzi wake ambapo taifa hilo lilishikilia uamuzi wake wa kutokuwa tayari kuandaa mashindano haya huku kukiwa na hofu ya kusambaa kwa ugonjwa wa ebola .
Hatua inayofuata kwa CAF ni kufanya mazungumzo ya haraka na mataifa kadhaa yaliyoonyesha dhamira ya kuwa wenyeji wa michuano hii ili kuhakikisha inafanyika kama ilivyopangwa hapo awali katika ratiba ya kila mwaka ya CAF .
Mwenyeji mpya wa mashindano haya yatakayoanza januari 17 hadi Februari 8 atatajwa jumatano Tarehe 12 baada ya kamati kuu ya shirkisho hilo kujiridhisha na uwezo wa moja wapo kati ya mataifa yaliyojitokeza .

Tanzania vs Uganda katika Kickboxing.

shijaa
Mtanzania anayefanya vizuri kwenye mchezo wa kickboxing Emmanuel Shija hivi karibuni ataipeperusha bendera ya Tanzania nchini Uganda wakati atakapopanda ulingoni kupambana na  Mganda Moses Golola katika pambano la kuwania ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati katika mchezo wa Kickboxing.
Mganda Moses Golola ambaye atapanda ulingoni kupambana na Mtanzania Emmanuel Shija.
Mganda Moses Golola ambaye atapanda ulingoni kupambana na Mtanzania Emmanuel Shija.
Pambano hilo linatarajiwa kufanyika nchini Uganda mwishoni mwa wiki hii huko Jinja kwenye ukumbi wa Hoteli ya Crested Crane ambapo bondia toka Uganda Moses Golola amekuwa akijitamba kumpiga Mtanzania huyo ambaye kwa upande wake amekuwa mkimya akichagua kutojisifia sana na badala yake kufanya mazoezi ya nguvu ili aonyeshe uwezo wake siku ya pambano .
Shija ana rekodi nzuri inayoonyesha kuwa katika mapambano 28 amefanikiwa kushinda mara 25 huku akipoteza mara tatu na hajatoka sare hata mara moja .
Emmanuel Shija akiwa na moja ya mataji aliyowahi kutwaa nje ya nchi kwenye mchezo wa Kick-Boxing.
Emmanuel Shija akiwa na moja ya mataji aliyowahi kutwaa nje ya nchi kwenye mchezo wa Kick-Boxing.
Moses Golola amekuwa na kawaida ya kujisifu kwa mbwembwe nyingi kabla ya mapambano yake hali ambayo mwenyewe anadai inamsaidia kuwatia hofu wapinzani wake na kumpa faida ya kupata ushindi hata kabla ya kupanda ulingoni kwa kuwafanya wapinzani wake wapoteze hali ya kujiamini .
Mganda huyo amepanda ulingoni mara 24 ambapo amefanikiwa kushinda katika mapambano 19 huku akipoteza mara 4 pekee na katika michezo hiyo amefanikiwa kushinda mara 11 kwa mtindo wa Knock-Out.
Emmanuel Shija akiwa nchini Uganda ambako ameambatana na Rapa ambaye ni bondia David Mrope Maarufu kama Zola D.
Emmanuel Shija akiwa nchini Uganda ambako ameambatana na Rapa ambaye ni bondia David Mrope Maarufu kama Zola D.
Mara ya mwisho katika pambano lake Moses Golola alichakazwa na Mmarekani Richard Abraham katika pambano lililofanyika nchini Uganda .
EMA SHIJA
Emmanuel Shija ambaye  hafahamiki sana miongoni mwa Watanzania , amekuwa akifanya vizuri katika mapmbano yake ambayo karibu yote yamekuwa yakifanyika nje ya nchi kwenye mataifa kama Falme za kiarabu na Hispania ambako amejijengea jina kubwa .

Shija akiwa kwenye mazoezi nchini Uganda ambako atapanda ulingoni kupambana na Moses Golola .
Shija akiwa kwenye mazoezi nchini Uganda ambako atapanda ulingoni kupambana na Moses Golola .