Jumanne, 14 Novemba 2017

Mnunuzi Feki wa Nyumba za Lugumi Kupimwa Akili

Mnunuzi Feki wa Nyumba za Lugumi Kupimwa Akili
Bilionea Dkt. Luis Shika ambaye wiki iliyopita alitangaza kununua nyumba za kifahari za mfanyabiashara za Said Lugumi, zilizopo eneo la Bweni JKT jijini Dar es salaam anatarajiwa kupelekwa hospitali kupimwa afya ya akili.

Hayo yamesemwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Jeshi la Polisi (SACP), Benedict Kitalika, ambapo amesema uamuzi wa kumpeleka hospitali Dkt. Shika  kuchunguzwa afya ya akili yake, umetokana na uchunguzi wa awali ulioonesha anaweza kuwa na tatizo hilo huku akidai kuwa uchunguzi huo utalisaidia Jeshi la Polisi kukamilisha uchunguzi.

“Tunatarajia kumpeleka hospitali wakati wowote ili kuangalia kama kuna tatizo katika afya ya akili au la kutokana na historia yake ya maisha inavyojionyesha, hali ambayo inaweza kutupa majibu sahihi.” amesema Kamishna Kitalika.

Kamishna Kitalika amesema uchunguzi wa awali ulihusisha historia ya maisha yake inayoonyesha ni msomi aliyewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi nchini Urusi kabla ya kurudi nchini na kuishi kwenye chumba kimoja cha kukodi, huku sababu za kurudi kwake zikiwa hazijulikani.

“Na sisi tumejiuliza sana kuhusu utimamu wa akili kama upo sawa au kuna tatizo la kisaikolojia, kwa sababu ukiangalia historia yake inaonyesha wazi ni msomi mzuri ambaye ameshika nafasi za uongozi nchini Urusi, lakini maisha anayoishi nchini si ya kuridhisha. Hatujui amepatwa na nini hadi kufikia hatua ya kukodi chumba kimoja cha kuishi katika Mtaa wa Tabata, huku mwonekano wake ukiwa haupo sawa kisaikolojia.” amesema Kamishna Kitalika.

Hata hivyo, tayari jalada la kesi ya Dkt. Shika limepelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) ili aweze kuangalia kama kuna jinai yoyote iliyotendeka kwa mtuhumiwa huyo au la.

Akizungumzia hilo, Kamishna Kitalika amesema licha ya jalada hilo kuwa mikononi mwa AG, imebainika kuwa baadhi ya kanuni wakati wa mnada wa nyumba za Lugumi hazikufuatwa, ikiwepo ya kulipa asilimia 25 pale pale baada ya mteja kujitokeza hali ambayo inaongeza shaka kwa Dkt. Shika.

“Katika mnada ule, baadhi ya kanuni hazijafuatwa ikiwamo ya kumtaka kulipa asilimia 25 pale pale mara baada ya kununua, lakini suala hilo halijafanyika badala yake waliendelea kupiga mnada nyumba nyingine, hivyo kama taasisi za uchunguzi tunapaswa kufuatilia hatua kwa hatua,” amesema Kamishna Kitalika.

Wiki iliyopita, Dkt. Shika alijitokeza kwenye mnada wa nyumba tatu za Lugumi, mbili zipo Mtaa wa Mbweni JKT na moja ipo Upanga na kushinda minada yote.

Mnada huo ulifanywa na Kampuni ya Udalali ya Yono kwa amri ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambapo Dk. Shika aliahidi kununua nyumba hizo kwa thamani ya Sh bilioni 2.3 lakini alishindwa kulipia asilimia 25 ya fedha hizo ambazo ni shilingi milioni 800 kitu ambacho kilipelekea akamatwe na polisi kwa kosa la kuharibu mnada na utapeli.

Chanzo : Mtanzani 

Dk Cheni Awapa Makavu Wanaomsakama Lulu Kuhusu Dhamana

Dk Cheni Awapa Makavu Wanaomsakama Lulu Kuhusu Dhamana
MSANII mkongwe katika tasnia ya maigizo Bongo na mshereheshaji (MC), Mahsein Awadhi ‘Dk. Cheni’ ambaye ni mlezi wa mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametoa maoni yake kwenye mtandao wa kijamii baada ya kuibuka maneno mengi kwenye mitandao hiyo ambapo watu wengine wanasema Lulu amepewa adhabu ndogo na wengine wakipendekeza angefungwa kwa miaka mitano na kuendelea.

Dk Cheni amewalaumu wasiomtakia mema Lulu akisema mambo yote mabaya yanaweza kumtokea yoyote, kwa hiyo kufurahia jambo baya limpatalo mtu si jambo jema.  Pia ametoa asante kwa wote wanaomwombea mema Lulu na waendeleee kufanya hivyo.

Ujumbe aliotuma msanii huyo ni huu hapa chini:

Linapokukuta jambo wapo wataokuonea huruma na wapo watakaokuwa na furaha ila niwakumbushe jambo hakuna ajuwaye kesho yake kubwa kila mapito mwambie Mungu Asante.

Watanzania walio wengi wanakuombea yaliyo mema Tunakuahidi tupo nawe kukushika mkono kwa kila hatua Maombi yao Mungu atayasikia hata kama hukumu imepita Tupo na wewe na Mungu yupo na wewe.
                             
                             

Yanga Yasajili Straika Mpya wa Maana

Yanga Yasaka Saini Ya Straika Wa Kagera
ZIKIWA zimebaki siku moja kabla ya kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili hapa nchini, uongozi wa Yanga unajipanga vilivyo kuhakikisha unakiimarisha kikosi chake ili kiweze kufanya vizuri katika mechi zake zijazo za Ligi Kuu Bara lakini pia katika michuano ya kimataifa.

Uongozi unahitaji kusajili wachezaji wanne katika dirisha hili dogo la usajili kwa ajili ya kuziba upungufu uliojitokeza katika kikosi hicho tangu kuanza kwa Ligi Kuu Bara msimu huu katika nafasi ya ulinzi, kiungo pamoja na ushambuliaji. Na tayari mazungumzo na straika mmoja wa Kagera Sugar yanaendelea.

Hata hivyo, habari za kuaminika kutoka ndani ya Yanga ambazo Championi Jumatatu limezipata zimedai kuwa mpaka sasa uongozi huo umeishaanza mazungumzo
na baadhi ya wachezaji ambao inawahitaji akiwemo Mtogo Vincent Bossou ambaye ilimuacha baada ya kumalizika kwa msimu uliopita lakini pia kiungo wa Mtibwa Sugar, Mohamed Issa ‘Banka’.

Ukiachana na wachezaji hao ambao taarifa zao zimekuwa zikisemwa sana hivi karibuni pia uongozi huo unadaiwa kuwa katika mazungumzo na Straika wa Kagera Sugar, Jafar Kibaya ambaye ni kati ya washambuliaji mahiri hapa nchini.

Mshambuliaji huyo ndiye aliyeivuruga ngome ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu alipoifungia timu yake bao moja wakati Yanga iliposhinda 2-1 na kuwazidi ujanja mabeki wawili matata wa timu hiyo, Kelvin Yondani na Andrew Vicent Dante ambao imekuwa adimu sana wao kufungwa msimu huu.

Akizungumza na Championi Jumatatu, mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye aliomba kutotajwa jina lake, alisema uongozi huo unajipanga kuhakikisha unamsajili Kibaya ili kuiongezea nguvu safu yake ya ushambuliaji ambayo tangu kuanza kwa ligi kuu imekuwa ikiwategemea Ibrahim Ajibu pamoja na Mzambia, Obrey Chirwa.

“Kwa hiyo kutokana na hali hiyo tumeona ni bora tupambane kuhakikisha tunamsajili Kibaya kwa ajili ya kuja kusaidiana na wachezaji hao kwani Donald Ngoma na Amissi Tambwe kwa sasa siyo wachezaji wa kuwategemea sana.

“Muda mwingi wamekuwa nje ya uwanja, jambo ambalo linatufanya tuwe na wakati mgumu pindi wanapoumia, kwa hiyo Kibaya anatufaa na tayari kocha ametuambia tuhakikishe tunamsajili kwani alimuona tulipocheza na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba na alitusumbua sana,” alisema kiongozi huyo.

Katika mchezo huo dhidi ya Yanga, Kibaya ndiye aliyefunga bao pekee la Kagera ambapo Yanga ilishinda 1-2.
Alipoulizwa suala hilo, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa alisema: “Muda wa usajili bado haujafika kwa hiyo kwa sasa siwezi kuzungumzia hilo, tusubiri kwanza mpaka utakapofika muda huo.”

Hata hivyo, Meneja wa Kagera Sugar, Mohamed Hussein alipoulizwa kama wapo tayari kumuachia mchezaji huyo ajiunge na Yanga alisema: “Waje tuzungumze kama watakuwa tayari kutupatia fedha ambayo tutawaambia haina shida kwani Kibaya bado ana mkataba wa miaka miwili na sisi.

“Tumemsajili msimu huu akitokea Mtibwa Sugar kwa hiyo wakikubali kutupatia fedha tutakayowaambia basi tutawapatia.”

Wabunge Wanaotaka Pensheni Watakiwa Kuanzia Bungeni Kabla ya Kufika Serikalini

Wabunge Wanaotaka Pensheni Watakiwa Kuanzia Bungeni Kabla ya Kufika SerikaliniSerikali imewataka wabunge wanaotaka utaratibu wa kulipwa pensheni mara baada ya kumaliza kipindi cha ubunge urejeshwe, walipeleka jambo hilo kwanza kwenye  Tume ya Utumishi ya Bunge kabla ya kulifikisha serikalini.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde amesema leo Jumanne bungeni kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Vunjo (NCCR_Mageuzi), James Mbatia.

Mbatia amesema sheria ya mwaka 1981 ilikuwa inatambua pensheni kwa wabunge wanaomaliza muda wao na kuihoji Serikali inatamka nini kuhusu kulifufua suala hilo.

Akijibu swali hilo, Mavunde amesema kwa sababu swali la mbunge huyo ni kufufua sheria ya pensheni ni vyema lianzie kwao ( Tume ya Utumishi ya Bunge) ndio lifike serikalini.

Katika swali la msingi, Mbatia ametaka kufahamu Serikali haioni busara kuifanyia marekebisho Sheria ya Maslahi na Mafao ya Majaji namba 3 ya mwaka 2007 au vinginevyo ili majaji waweze kupatiwa huduma muhimu za matibabu wakati wanapostaafu.

Akijibu Mavunde amesema masharti ya kazi na stahili za majaji ya mwaka 2013 kwa maana majaji wa Mahakama Kuu yamefafanua kuwa majaji hao wamejumuishwa katika utaratibu wa matibabu kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHF)wawapo kazini.

Amesema gharama hizo hulipwa na Serikali na hata wanapostaafu wanaendelea kupata huduma hizo kupitia mfuko huo.

"Kwa wale waliostaafu kabla ya masharti hayo kuanza kutumika hawanufaiki na mfuko huo," amesema.

Kuhusu kuangalia kulifanya suala hilo la  kiutawala, Mavunde amesema kwa sababu ni suala la kisheria na sera wanalichukua na kulifanyia kazi. 

Idriss Atuma Salamu za Pole kwa Mama Lulu "Mama Ndio Tunahitaji Kukuangalia Zaidi"

Idriss Atuma Salamu za Pole kwa Mama Lulu "Mama Ndio Tunahitaji Kukuangalia Zaidi"MCHEKESHAJI na mshindi wa Big Brother Africa, Idris Sultan, ametoa pole kwa mama wa mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Kalugira, kwa kipindi kigumu alichokianza jana baada ya bintiye kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kutokana na kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba.

Sultan amesema jamii impe faraja na kumtia moyo wakati akiwa katika huzuni ya kuwa mbali na binti yake.  Pia Sultan amemuelezea Lulu kuwa alikuwa ni rafiki yake wa karibu na ni mwanamke shupavu ambaye huzuni yake ikiwa jela itachukua muda mfupi kabla ya kupata marafiki na kujipa moyo wa kuhimili maisha hayo mapya ya miaka miwili.
Hayo ni maneno aliyoyatuma kwenye akaunti yake ya Instagram kama yafuatavyo:
My last piece on this, Mama Lulu tunakuombea kwa Allah upate nguvu ya kukubaliana na hii hali ambayo ni chungu kwetu sote. Tunalazimika kukubali kwasababu Mungu tu ndiye anajua kubaki na jambo kama hili moyoni kwa mda mrefu hivi linaondoaje amani. Binafsi nampenda sana Lulu na anajua, kwa mda wa miaka michache niliyojuana na Liz najua wewe mama ndio tunahitaji kukuangalia zaidi maana Lulu najua atalia wiki ya kwanza na ya pili, ya tatu atapata kazi jikoni, ya nne anajisomea, ya tano kashapata marafiki kote because your daughter is the strongest woman I have ever met maishani mwangu yani ningekua mwanamke ningekua yeye. Baby is good to go na nitajaribu kuwa positive na kusema kua ntammiss sana ila mara mbili tatu sitoacha kumtembelea na tunasubiri siku anatoka na ku-take over her throne. Hakuna aliyependa haya yatokee ila ndio yametokea we only have God and each other now. Be blessed
                              

Mange Kimambi Afunguka baada ya Lulu kupigwa mvua ya Miaka Miwili

From @mangekimambi_ - Breaking newzzzzzzzz..... Lulu amekutwa na hatia ya kuuwa bila kukusudia na amehukumiwa miaka miwili jela.......
.
.
.
Dah huyu jaji anawaza kama mimi posti yangu niliyoposti masaaa mawili yaliyopita nilisema ningekuwa jaji ningemkuta na hatia ila ningempa adhabu ndogo mwaka mmoja au miwili jela.......
.
.
Jaji ametenda haki....
.
.
Sio kama nimefurahi Lulu kafungwa nilichotaka ni kuona hakuna double standards, nilitaka kuona haki inatendeka. Na Lulu ana deserve hiyo miaka 2 jela labda itampa muda wa kufikiria how her actions affected Mama Kanumba na familia yake. Labda akitoka atakuwa more humble......
.
.
.
Lakini still mwanasheria wa serikali achukulie hatua za nidhamu na afukuzwe kazi!! Alijaribu sana kusabotage kesi ili amsaidie mtuhumiwa......
.
.
PS: December Magu anatoa misamaha kwa wafungwa, sidhani kama atawasahau wafungwa wa kumpa kiki ya kufungia mwaka kama Lulu na kina Babu Seya maana ile barua ya kina Baba Seya had Bashitel written all over it."

Jumatano, 5 Julai 2017

Madhara ya Kutofanya Tendo la Ndoa Muda Mrefu



Habari zenu, nimeona niwaletee hili nina imani mtajifunza hasa kwa wale wasiofahamu,Ukikaa Muda Mrefu bila Kufanya tendo la Ndoa madhara yake ni kama haya:

Hasira za mara kwa mara katika mambo madogo,kupendelea sana kuangalia picha za uchi,Kusahausahau,Kupendelea story za mapenzi,Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi (Mke),Kupenda kurukiarukia mambo ya watu wengine (tabia ya kufuatilia mambo yasiyokuhusu),Kuumwa na kichwa,Kukakamaa mgongo (wanaume),Kuingiliwa kirahisi na jini mahaba,Kupoteza umakini ktk kazi (efficiency),Siku ukikutana kimwili na mwenye virusi bila kinga utaambukizwa kirahisi mno,Waweza ku-develop tabia mpya ambayo hukuwahi kuwa nayo ili iwe mbadala

Jumanne, 4 Julai 2017

NILIIBIWA sana Facebook – Mch Anthony Lusekelo Afunguka


Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu kama ‘Mzee wa Upako’ amefunguka kuwa yeye ni moja ya Wachungaji ambao wapo nyuma sana kwenye mitandao ya kijamii na kukiri kuwahi kuibiwa kwenye mtandao wa Facebook na watu wanaotumia jina lake.

 

Mzee wa Upako amesema kutokana na kuwa na elimu ndogo ya mitandao ya kijamii amewahi kuibiwa na watu mitandaoni waliokuwa wanawatapeli waumini wake kwa kutumia jina lake na kuwaomba watu hela.

“Nina akaunti ya Instagram na nimewafuata watu wanne tuu Magufuli, Jakaya, BBC na vyombo vingine vya habari….(kuhusu Facebook) kule niliibiwa sana kuna watu walikuwa wanatumia jina langu wanajiita Mzee wa Upako na kuwachangisha watu pesa,” amesema Mch. Antony Lusekelo kwenye mahojiano yake na kipindi cha Chomoza cha Clouds TV.

Hata hivyo Mzee wa Upako amesema kwa sasa kwenye simu yake hakuna hata Group moja la WhatsApp huku akidai kuwa wingi wa simu za kawaida zinazoingia ndiyo unamfanya asijiunge na makundi hayo kwani yanamaliza chaji

Ijumaa, 16 Juni 2017

Mapenzi yamekua Rahisi Sana Ndo Maana Ndoa Hamna Siku Hizi

Eeh ndo hivyo, akina dada wengi wanajirahihisha sana wala hawaoni aibu kuzungusha kwa vijana wa mtaani na maofisini.Zamani nasikia msichana unaweza ukafukuzia miaka mi 2 na kuendelea nowdays ukitoka nae tu appointment chupa ya pili ikikolea kichwani akili yote inakimbilia chini kazi kwako tu kuangusha kwa ubua

Kingine material things, watu wengi wako kimaslahi ndo maana anaweza easily aka confuse mapenzi na pesa hii ni kutokana na economic liberalisation sijui? Utaona mdada ana mpenzi wake atakuambia i love my guy blah blah nyingi lakini sasa kama huyo Guy hawezi kumnunulia Iphone 7 wala hawezi ku offord outing za zanzibar weekend, we muambie tu twende Zanzibar this week lazima lovely Guy atoswe na lazima ujilie tu huko.

Mapenzi yakishakua tu biashara basi tambua kuwa soko lake litatawaliwa na demand and supply kwa kuwa kuna wadada wengi mjini supply ni kubwa lakini wanalazimika kushusha bei, utu tena katika mapenzi taratibu unapotea hapa ni chapa tu ilale. Kwanini wanaume waweke ndani wakati kinapatikana tu kirahisi? Na hata hiki kilichokua ndani kutokana na ushindani wa soko kinaweza kikachukuliwa?

Alinisaliti, Nilichomfanyia Hatokaa Anisahau Daima


Jumamosi iliyopita nikiwa katika matembezi ya hapa na pale katika fukwe moja hapa jijini,nimekaa na co worker napata juice ya baridi huku yeye akiisindikiza siku na castle light.wanaingia wanawake wawili mmoja mnene sana kimaumbile.wanaketi meza jirani kidogo na tulipo sisi,Ghafla nakosa amani,mapigo ya moyo yanaongezeka.. Nakua nawatazama sana hawa wanawake,ila wao naona hawa ja pay attention kwetu hivyo hawajatuona..baada ya muda huyu co worker ananiuliza kama kuna tatizo,najishtukia kidogo najikaza namwambia hamna tatizo lolote.ila kiukweli macho na akili yote imehamia kwa huyu mwanamke mnene,kila nikimtizama nahisi kumfahamu licha ya kutoonana nae kwa muda mrefu sana, ni jioni tulivu,anakuja muhudumu wanatoa oda,baada ya muda mhudumu anarudi na Smirnoff (vodka) club soda,glass mbili na vipande vya limao. Wanafungua wanaanza kunywa taratibu, muda unaenda nakosa uvumilivu namfuata huyu mwanamke, nafika walipokaa namshika begani,


"Habari yako???"
Ghafla anashtuka sana,Ananiangalia kwa muda kisha anainuka na kunikumbatia humu akitaja jina langu. Ananiachia na kunitizama tena kwa Mara nyingine,kisha anaanza kuniuliza
"Za masiku? Upo kweli? Mbona unazidi kua kijana?unafanya sana mazoezi eh?nimekutafuta sana mbona, blah blah blah + maswali mengi yasiyo na mwisho.
Mara ya mwisho namuona alikua binti mwenye umbo lililojengeka ipasavyo,nashindwa kuvumilia namuuliza " ndugu huu unene ni wa uzazi nini???anacheka anajibu hapana ni maisha tu.anaangalia mezani kwetu na kuhoji kulikoni mbona unakunywa juice unatumia dawa nini??natabasamu namwambia nipo kwenye dozi kweli(japokua si kweli)Tunaongea mawili matatu narudi mezani kwangu huku tukiwa tumeahidiana tutaongea zaidi maana bado tupo sana.


Huyu mwanamke ni nani????

August 2008, nafamiana na huyu msichana mrembo,baada ya urafiki wa muda tunaanza mahusiano ya kimapenzi. Mimi nafanya kazi katika shirika la kiserikali yeye akiwa mwaka wa pili chuo, baada ya muda mapenzi yananawiri sana ikafika hatua nikawa nimemtambulisha kwa baadhi ya ndugu jamaa na marafiki,katika kipindi cha mwaka na nusu hivi mpaka ilipofikia hatua anahitimu chuo kwa kweli kwangu alikua 'perfect woman'. Akaniteka haswa nikasahau habari za wanawake wengine kabisa, anahitimu chuo natumia influence yangu namtafutia kazi kwenye kampuni flani hapa hapa jijini, anaanza kazi na tunaanza kuishi wote.(japo kwao aliwaambia kua anaishi kwa rafiki wake wa kike)...muda unaenda huku mapenzi yakishamiri, asubuhi nampeleka kazini na mimi naenda ofisini,akitoka anakuja kunisubiri(ye anawahi kutoka) tunarudi wote nyumbani.


Baada ya mwaka tunaanza process za ndoa,hakutaka kuzaa kabla hatujaoana. Utaratibu wa kutambulishana unafanyika,ndoa inapangwa baada ya miezi nane kutokana na majukumu ya kikazi,kila mmoja ana furaha moyoni mwake. Nampa full power kwenye baadhi ya miradi yangu asimamie yeye..simfatilii huko kwenye hio miradi wala kuhoji financial status zaidi ya kumwambia awe makini maana nataraji kuanza ujenzi mwingine inaweza kufika mahali nikahitaji msaada wake..namuonea huruma anavyotoka kazini mapema na kuja kunisubiri mimi kila siku ya kazi, namfundisha kuendesha gari,anapata kauzoefu hatimaye siku yake ya kuzaliwa namfanyia surprise namnunulia gari.. Mipango ya harusi inaendelea pande zote mbili


Usaliti unaanza
Nikiwa sijui hili wa lile akaanzisha tabia mpya ya kuchelewa kurudi nyumbani, nikawa natoka kazini nampigia hapokei(hili halikunipa shida sana maana alikua si mzoefu sana barabarani hivyo akiwa anaendesha hapokei simu) nafika nyumbani simkuti,akirudi kila siku sababu mpya, muda si muda akaanza tabia anaondoka na gari asubuhi akirudi jioni anakuja kachelewa na gari haji nalo,analiacha kazini,sababu anazotoa yani nilikua hata sijielewi,Mara naona uvivu kuendesha,jioni sioni vizuri blah blah blah, alikua na mdogo wake kaanza 1st year udsm pale akamfanya kama cover story yake, kila akichelewa anadai alikua nae anampa company.simu zangu akawa mgumu sana kupokea,akabadilika ghafla. Kuna siku kachelewa kurudi,nimekaa sebleni nakunywa whisky na kujisomea kitabu Fulani,alivyofika akaniambia Ana akshi sana twende chumbani, baada ya mambo mambo ile nataka kuingia ikulu nikahisi kabisa hii ikulu imedukuliwa na wajanja,the thing is am old enough na huyu mwanamke namjua sana so nika notice something haipo sawa hapa.nikakaza moyo konde nikaingia mchezoni japokua akili haikuwa sawa kabisa. Bado kama miezi minne ndoa inakuja,maisha yamebadilika, ye anawahi kutoka kazini ila kufika nyumbani kila siku ananikuta mimi, nyumbani hapiki kuna mahali akawa anapitia chakula karibu kila siku(napajua)

Nikaanza upelelezi, sina tabia ya kugusa simu yake na sikuona sababu ya kuanza kufanya hivyo,kuna siku nampigia,after kama missed call 5 anapokea,ni SAA 3 usiku hajarudi nyumbani,namuuliza alipo ananiambia bado bado kuna foleni,basi namwambia ptia chakula anasema haya,nawasha gari naenda hii sehemu anapochukulia chakula napaki kwa mbali kidogo najibana mahali nakunywa bia yangu taratibu,muda si muda anaingia my wife to be na kijana mmoja,wanafungiwa chakula wanaenda parking,jamaa anamtolea mkoba kwenye gari kisha wana French kiss jamaa anaondoka wife anachukua bajaji anaondoka pia. Hapa ndo nikaelewa kwanini gari analiacha kazini,after work kuna MTU anakuja kumchukua.

Naamini humu tu watu wazima na kila mmoja wetu anafahamu hisia za usaliti zilivyo hivyo sihitaji kuelezea.. Narudi nyumbani SAA 9 usiku nikiwa nimelewa sana,nafika nalala sebleni huku wife to be akijifanya analalamika sana,najitahidi kumpuuza, kesho yake nashindwa kwenda kazini.simuulizi chochote,, baada ya siku mbili anarudi kachelewa,baada ya kumkiss nagundua amekunywa, ndugu nlikua sijawahi kumpiga mwanamke maishani mwangu ila hio siku nilimpa kichapo vijana wa sasa hivi wana msemo wao kua 'sio cha nchi hii' yani pombe ikakatika akanieleza anavyogawa uroda a-z!!! Nikasaidiana na mlinzi tukampeleka hospitali maana alipasuka ikabidi wamshone bila ganzi maana alikua amekunywa pia. kesho yake baada ya kujadiliana tukawasiliana na pande zote mbili harusi isogezwe miezi minne mbele kutokana na sababu mbalimbali.


Time for revenge
Nlijitahidi sana kumsamehe lakini sikuweza,akawa mnyenyekevu kupita kiasi lakini moyo wangu ukakataa kabisa,sikumwambia MTU yoyote na mipango ya harusi inaendelea, nikawa chapombe,si kazini si nyumbani pombe akawa ndo rafiki yangu.. Sina hisia na huyu mwanamke tena,kilichobaki na kumfanyia kisasi kisha nimuache(sina moyo wa kusamehe,I tried but it didn't work).kila aina ya kisasi naona kama hakitoshi,I went crazy kuna muda nlitamani ata kumuua yanii... Nakaa naye namwambia achukue likizo ya bila malipo twende vacation ya kimya kimya kabla ya harusi tuone ni jinsi gani tunaweza rejesha penzi..naongea na bosi wangu(long time friend) namwambia a-z bila kumficha, kuna nafasi zilitoka kwenda kuongeza ujuzi nje pale kazini sikufatlia maana ziliingiliana na ratiba ya harusi,tuka force na bosi pale akanichomeka. Nikatumia ka ushawishi kidogo kwenye hii kampuni ya bidada wakampa ka likizo japokua kishingo upande sana


Vacation inaanzia unguja na huyu mwanamke,mi napanga kisasi tu,ye anajua tunaenda tafuta muafaka,nshakua pombe MTU hapo... Kwa kifupi Mwezi mzima tulitembea mikoa kadhaa hapa nchini,katika kipindi hiko chote sikuwahi kupata hisia nae tena,nlimpa tabasamu la kinafiki muda wote. Tulipokua znz mwanzo wa vacation nikamshawishi sana nianze 'kuruka ukuta'(samahani kama ntamkwaza MTU hapa) anakua mgumu ila baada ya ushawishi na influence ya pombe anakubali. Yani nlikua simjali hata kidogo,akawa Analia kila siku kua namuumiza lakini nikawa nampoza kinafiki,mwezi mzima nikamfanyia uchafu bila huruma.

Tunarudi jijini,naenda kwa mama namwambia kua Hamna mke pale wala ndoa,naanza maandalizi kimya kimya ya kwenda nje,narudisha usamamizi wa miradi yangu yote,siku si siku bidada yupo kazini nabadilisha lock za milango,natoa kila chake nampa mlinzi na kinote ampe kikiwa na maneno machache tu. Nakaa kwa boss kwangu siku mbili naenda nje

Nakutana na binti wa kitanzania(RIP) nje,nae kachoshwa na mahusiano,tunasaidiana 'kupambana na baridi la ulaya' katangulia mbele ya haki Ila kaniachia zawadi ya mapacha(boy and a girl). Ni mwaka wa pili tangu tumzike na ilikua ndio siku yangu ya mwisho kunywa pombe!!!!!

Maisha yanasonga,sitaki kusikia habari za kuoa maana najua sina moyo wa kusamehe na maisha ya sasa ndo mwendokasi kwelikweli. Sasa hivi watoto wangu ndo dunia yangu, +work and gym.
Eway huyu mwanamke jumamosi alinipa namba ila nikazifuta,maisha safari ndefu wakuu. Poleni kwa Uzi mrefu

The best revenge is forgiveness, don't follow my path

Simba Walimdaka Niyonzima Airport...Yanga Yaambulia Patupu


WAKATI Yanga wakimsubiria kiungo wao mchezeshaji, Haruna Niyonzima atue nchini kwa ajili ya kumuongezea mkataba watani wao wa Simba wenyewe hawakauki Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere ili wamsainishe. Hiyo, ikiwa ni siku chache tangu tetesi zienee kuwa kiungo huyo anayemudu kucheza namba nane tayari amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba. Kiungo huyo, hivi sasa ni mchezaji huru anayeruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu nyingine kutokana na mkataba wake kumalizika mwezi ujao kwa mujibu wa kanuni za Fifa.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, kutoka kwa ndugu wa karibu wa Niyonzima viongozi wa Simba walikuwa tayari wapande ndege kumfuata kiungo huyo Rwanda, lakini ilishindikana kutokana na kukatishwa tamaa na meneja wake.

Mtoa taarifa huyo, mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji ‘Mo’ ndiye alikuwa anawasiliana na Niyonzima kwa ajili ya kwenda kumsainisha nchini Rwanda kwa dau la shilingi milioni 70. “Nikwambie ukweli tu, ni ngumu Niyonzima kwenda kusaini mkataba wa kuichezea Simba, kwani mpango wao wa kwanza walioupanga umeshindikana kwani walipanga wamfuate Rwanda alipokuwa kwenye majukumu yake ya timu ya taifa.

“Mipango hiyo ilishindikana ni baada ya meneja wake kuuzuia
uongozi wa Simba usiende huko na badala yake wamsubirie hadi ataporejea nchini na baada ya kuona wamekwama, viongozi hao wa Simba wakaanza kwenda kumwinda uwanja wa ndege kwa kukagua muda wa ndege wa Rwanda Air na mratibu wa hilo ni Mo.

“Lakini wakati wakipanga hayo, Bin Kleb (Abdallah), yeye aliwasiliana na Niyonzima na kumwambia mara baada ya kutua nchini asionane na yeyote zaidi yake yeye,” alisema mtoa taarifa huyo. Championi Ijumaa,lilimtafuta Niyonzima na kuzungumza naye moja kwa moja kutoka Rwanda kuhusiana na taarifa za yeye kusaini Simba alisema kuwa: “Hayo maneno tu wanaongea, nikuhakikishie mimi sijasaini Simba na kama unakumbuka mimi nilikwambia nimeichezea kwa amani Yanga miaka sita hivi sasa.”

Kalapina Awataka Wale Waliomteka Roma Mkatoliki Wakamteke na Yeye ili Awaonyeshe Kazi

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mmoja wa Watu wanaoaminika kuwa ni Mbabe kama siyo Mtemi na Ngumi Jiwe wa kutukuka Kalapina jana wakati akihojiwa na Kipindi cha XXL kinachorushwa na Clouds fm aliamua kutema nyongo / kuvunja ukimya juu ya Kitendo cha Msanii mwenzake na mshikaji wake Roma Mkatoliki Kutekwa.

Kalapina ambaye anasifika mno kwa Usela / Uhuni na ukorofi ambao kiuhalisia kweli anauweza alianza kwanza kwa kumpa pole Roma Mkatoliki kwa yote yaliyomkuta ila hakusita pia kumlaumu kidogo Roma kwa kumwambia kuwa asingekubali kirahisi rahisi kubebwa na kuingizwa katika Gari na Kutekwa.

Ifuatayo ni nukuu Kuntu kabisa kutoka kwa Kalapina ambayo nadhani ni ujumbe tosha kwa Wazee wa Ununio mkabala na Mahaba Beach ( Watekaji )

“ Nakuambia Mimi nina hamu sana hao Watekaji siku wakosee tu waje waniteke Mimi kisha wajue kuwa kuna Watu tumebarikiwa kwa Ukorofi na Ukorofi tunaujua. Mimi wakija kama 10 na kutaka kuniteka basi nakuhakikishia lazima wakati wanafanikiwa kuniingiza katika Gari lao na kuniteka basi tayari name huku nyuma nitakuwa nimeshawaua Watatu au Wanne huku waliobaki nikiwaachia maumivu ya Kutukuka kabisa. Mdogo wangu Roma ulilegea sana na siku nyingine usifanye hivyo ukiona Mtu anataka kukuteka au ana nia mbaya nawe usimcheleweshe na badala yake mpe Kipondo / Kipigo pale pale “ mwisho wa kumnukuu Kalapina.

Haya Watekaji ( Wazee wa Ununio mkabala na Mahaba beach ) Kalapina huyo anawakaribisheni mkamteke na Yeye ili mkapate Kipondo / Kipigo ambacho inawezekana hata huko Chuoni Kwenu Wakufunzi wenu ama hawakuwafundisha au walisahau kuwafundisha.

Alichokisema Kafulila Baada ya Serikali Mkoani Kilimanjaro Kuharibu Shamba la Mbowe..!!!

ALIYEKUWA Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila amelaani hatua ya Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa kutumia mamlaka yake kuvamia na kuharibu shamba la Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
Juzi, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya walivamia shamba la Mbowe nyumbani kwake Machame na kuharibu miundombinu, mali, mboga na mimea kadhaa.
Akizungumza Dar es Salaam juzi, Kafulila alisema amesoma na kusikia kuwa Mkuu huyo alitumia mamlaka yake kufanya kitendo hicho, jambo ambalo aliliita ni laana ya hali ya juu.
“Nimesoma na kusikia kuwa Mkuu wa Wilaya ametumia mamlaka yake kuvamia na kuharibu shamba la Mwenyekiti wa Chadema ambalo ni uwekezaji wa kilimo cha mboga kwa soko la ndani na nje ya nchi,” alisema.
Alisema kitendo hicho ni cha kushangaza, kwa kuwa shamba hilo lina thamani ya mamilioni ya fedha, lakini mtu anatokea na kuharibu miundombinu kwa kuwa ni kiongozi tena bila sababu za msingi jambo ambalo halileti picha nzuri kwa jamii.
“Huu ni uamuzi unaoweza kufanywa na Serikali za kishenzi kama Somalia au Sudani na Burundi. Nasita kuamini kama huko ndiko Rais John Magufuli anataka kutupeleka,” alisema na kuongeza:
“Naamini atachukua hatua kali dhidi ya DC huyu, kwani ni doa lenye viashiria vya chuki za kisiasa kwa kiwango cha unyama, chuki ambayo hakika sidhani kama inaweza kuwa maelekezo ya kiongozi anayemtaja Mungu na kuomba maombi siku zote.”

UVCCM Wampa za Uso Lowassa Kuhusu Sakata la Makinikia..!!!


Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) umemtaka Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Rchmond Edward Lowassa kuacha uongo kwani hana historia ya kupigania maslahi ya umma.
Aidha, imesema madai ya lowassa kwamba aliwahidi wananchi angeunda Tume ya kupitia mikataba ya madini kama angeshinda urais ni uongo na kutaka kujitafutia umaarufu wa kisiasa. 
Pia umoja huo umemtaka Lowassa kuonyesha ushahidi video ya matamshi yake wakati akiwa katika mkutano wa hadhara akihutubia mkoani Geita ikionyeaha kama kweli alitoa matamshi hayo. 
Hayo yalielezwa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka alipozumgumza waandishi wa habari jana ofisini kwake Upanga jijini Dar Es Salam. 
alisema Lowassa hama nguvu za uzalendo wa kupigania au kuzungumzia mapambano dhidi ya ubadhirifu wa mali za umma kwasababu hata kujiuzulu kwake kulitokana na shinikizo la bunge huku akihusishwa na sakata la ufisadi. 
Shaka alibainisha kuwa hakuna ushahidi wala kumbukumbu inayoonyesha kuwa Lowasa siku moja aliwahi kutetea maslahi ya umma wakati akiwa serikalini kama Waziri au alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete. 
"UVCCM tumemestushwa na matamshi ya Lowasa yanayodai wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu akiwa Mkoani Geita kuwa aliwahi kutamka kama angeshinda urais angeunda Tume ya kupitia mikataba ya madini , hakuna ushahidi huo na hawezi kuthibitisha ni uongo mtupu "Alisema Shaka. 
Shaka alisema kama kweli angekuwa na ujasiri huo wakati alipokuwa waziri mkuu angeweza kutamka maneno hayo au kumshauri Rais iundwe Tume lakini alishindwa kwa sababu hana ujasiri na uzalendo kama anavyotaka kuwaaminisha wananchi baada ya kuona Rais John Magufuli akiungwa mkono kitaifa na kimataifa. 
Kaimu huyo Katibu mkuu alikumbushia kuwa alichosikika akisema Lowasa ni kwamba akiwa Rais atawakaribisha wawekezaji zaidi pamoja na marafiki zake wenye nguvu za fedha na mitaji mikubwa ili kuiendeleza migodi na uchimbaji wa madini ambayo itamtajirisha kila wananchi bila kuelezea mbinu za utekelezaji huo.
"Waziri pekee jasiri, mzalendo na aliyekuwa mchapakazi kwa bidii katika serikali ni Dk Magufuli kwani hata Lowassa alipomnadi Dk Magufuli wakati akiwania ubunge mwaka 2005 alimtaja mbele ya wananchi kwamba ni jembe na turufu muhimu "Alisema Shaka. 
Aidha alieleza sifa peke ya Lowassa akiwa serikali ni tabia yake ya kumshauri jambo Rais na kama litafanyika, hugeuka na kuwaambia watu kwamba yeye ndiye akiyemshauri Rais na kama si yeye kisingefanyika. 
Shaka alisema upo ushahidi kwamba aliwahi kumshauri suala fulani Rais mstafu Mzee Ali Hassan Mwinyi kisha akawaambia wapambe wake kwamba yeye ndiye aliyeshauri kitendo kilichomfanya Mwalium Julius K. Nyerere amwite kilichjambo lililomfanya mwalimu Julius Nyerere amwite Lowassa nyumbani kwake msasani na kumkanya. 
"Lowasa aliitwa mbele ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa UVCCM Sukwa Said Sukwa nyumbani kwa mwalimu Msasani akasemwa vikali sana na mwalimu kwa kitendo hicho pia akaonywa aache kutumia magazeti kusaka uongozi na umaarufu"Alieleza Shaka
Pia Shaka alimtaka Lowassa kuacha tabia ya kutaka kuvika joho lisilo na hadhi yake na akumbuke tuhuma ambazo amewahi kurushiwa na viongozi wa chadema wakipita huku wakimnadi nchi nzima haziwezi kufutika kwa mtindo anaotaka wa kujifagilia kwa uzushi. 
Hata hivyo kaimu katibu mkuu huyo alisema si kweli kama ujasiri, uzalendo na utashi wa kutaka kufanya mabadiliko ya kiuchumi, kupambana na ufisadi na kupitia mikataba michafu haiwezekani kufanyika bila katiba mpya kama anavyodai Lowasa. 
"Ujasiri, uzalendo na uthubutu wa kutenda mambo yoyote magumu hakuhitaji mabadiliko ya katiba , aidha kwa kuwepo wa katiba mbaya au nzuri kwasababu vitu hivyo havishabihiani , katiba iliopo ni nzuri na Dk Magufuli ataleta maajabu ya kihistoria chini ya katiba ya sasa "Alisisitiza Shaka 
Alimtaka Lowasa kufuta ndoto na matumaini kwamba itatokea siku moja akawa Rais wa nchi hii na kuacha kueneza uzushi kuwa alikatwa jina lake kwa kumhofia angepitia mikataba ya madini. 
"Jina la Lowassa liliondolewa kwasababu kadhaa ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka, viongozi wa CHADEMA kumnanga nchi nzima pamoja na ukiukaji wake wa taratibu, miiko na maadili huku akitumia nguvu za fedha kutaka ateuliwe jambo ambalo CCM imelikataa "Alisema Shaka .
Baadhi ya vyombo vya habari jana vilimnukuu Lowassa akimpongeza Rais Dk Magufuli kwa kuunda Tume ya kupitia mikataba ya madini huku akijigamba naye aliwaahidi wananchi wakati kampeni akiwa mkoani Geita kwamba akishinda urais angeunda Tume jambo ambalo pia lilifanya jina lake kukatwa ndani ya CCM.

Maajabu Marekani Imesaini Mkataba wa Kuizia Qatar Ndege za Kivita Aina ya F-15 kwa $12billions..!!


Wengi Mnakumbuka Sekeseke la Juzi ambapo Marekani waliishutumu Qatar kusaidia kifedha Mitandao ya Ugaidi.
Balozi mbalimbali zilifungwa na Sasa Marekani na Qatar wamesaini deal ya Kuuziana ndege za Kivita aina ya F-15 zenye Thamani karibia Tsh. 25Trillions

Madiwani wa Moshi Wasusa Semina Kisa Malipo ya Posho Kuwa Madogo..Wataka Walipwe Laki Moja Kwa Kikao..!!

HALI ya taharuki imeibuka katika Halmashauri ya Moshi baada ya madiwani kugomea mafunzo ya utaratibu ulioboreshwa wa uendeshaji  ruzuku ya maendeleo kwenye mamlaka za Serikali za mitaa (LGDG), wakishinikiza kulipwa posho ya Sh 100,000 kila mmoja. 
Mafunzo hayo yaliyokuwa yanasimamiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), yalihusisha madiwani wote na wakuu wa idara jana katika ofisi za Halmashauri. 
Taharuki iliibuka baada ya madiwani hao kuingia ukumbini na kabla ya mafunzo kuanza, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Michael Kilawila aliwatangazia kuwa kutokana na mafunzo kutokuwa ya kisheria, Halmashauri itapaswa kutoa posho zao kupitia makusanyo ya ndani. 
Kilawila alisema kutokana na hali hiyo na mapato kuwa madogo, kila diwani atalipwa Sh elfu 60,000 kama posho ya siku moja ambapo siku mbili za mafunzo hayo kila mmoja angepokea Sh 120,000.
Baada ya tamko hilo hali iligeuka baada ya madiwani hao kuonesha kutoridhishwa na kiwango hicho cha posho na kugonga meza wakishinikiza kulipwa Sh 100,000 kwa siku kama wanavyolipwa kwa vikao vingine vinavyotambulika. 
Waliposhindwa kuelewana, madiwani hao walisusia mafunzo hayo na kuondoka hali iliyowalazimu wakufunzi kutoka Tamisemi kufundisha wakuu wa idara peke yao. 
Akizungumzia sintofahamu hiyo, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Butamo Ndalahwa alisema lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha madiwani kwa kushirikiana na wananchi, wanaibua miradi.
Ndalahwa alisema mafunzo hayo yanafanyika katika halmashauri zote nchini na kuwa madiwani hao waligoma wakitaka posho kubwa bila kujali kuwa mafunzo hayo yangenufaisha wananchia ambao ndio waliowachagua. 
Mkurugenzi huyo akionesha masikitiko, alisema jambo hilo la kugomea mafunzo litasababisha maendeleo ya Halmashauri kurudi nyuma kwa kukosa elimu ya uibuaji miradi ambayo inakubalika. 
“Nimesikitishwa kwa kiasi kikubwa, madiwani wameonesha kutangulia mbele maslahi yao badala ya kutumikia wananchi waliowachagua, tumewaelimisha kuhusu posho, kwa nini tunawapa Sh 60,000 lakini hawakutaka kuelewa na badala yake waligonga meza ovyo na kutoka nje,” alisema Ndalahwa. 
Kilawila alipotafutwa kwa njia ya simu kuzungumzia suala hilo na hatima yake, alisema hawezi kuzungumzia jambo lolote mpaka kikao cha madiwani kitakapokaa ili kutoa maazimio. 
“Ninachoweza kusema sasa ni kwamba siwezi kuzungumza lolote,  mtafute Mkurugenzi, mimi nasubiri ni kikao cha madiwani ili kutoa maazimio ya kilichotokea leo,” alisema Kilawila.

Friji Lateketeza Jengo la Ghorofa 27 kwa Muda wa Dakika 15..!!!


MOTO uliozuka kwenye jengo la ghorofa 27 lililoko London Magharibi kwa dakika 15 baada ya friji kulipuka, itakuwa ni moja ya ajali mbaya kupata kutokea katika historia ya nchi hii huku kukiwa na hofu ya kutokuwa na manusura katika ghorofa tatu za juu.
Watu sita wamethibitishwa kupoteza maisha katika moto huo ulioligubika jengo la Grenfell Tower lililoko White City, ulioanza baada ya saa saba usiku wa kuamkia jana, lakini kikosi cha upelelezi cha Scotland Yard kilisema jana kuwa idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka.
Kiongozi wa eneo hilo ambaye anashiriki kutambua waliko waathirika, na ambaye hakutaka kutajwa jina, anaamini kwamba hakuna mtu anayeishi katika ghorofa tatu za juu aliyesalimika na jengo hilo linaweza kuporomoka ndani ya saa 24 zijazo.
Alisema: “Tuna orodha ya watu waliopotea – ni wengi. Inawezekana wako wengi zaidi ya 50, pengine hata mamia.” 
Walioweza kukimbia walisema ndani ilikuwa sawa na “jehanamu duniani” wakati wakikanyaga miili na kudai kukosekana kwa ving’ora vya moto huku njia pekee ya kutokea nje ikijifunga.
Kutokana na taharuki hiyo, wakazi wa jengo hilo walionekana wakijirusha na kurusha watoto wao kupitia madirishani, kuchelea kufa kwa kuunguzwa na moto-wengine walitengeneza kamba kwa kutumia mashuka au kuzitumia kama parachuti na kujirusha.
Baraza la mtaa, mmiliki wa jengo hilo na mjenzi walikuwa wakilifanyia matengenezo mwaka jana, walikabiliwa na maswali mazito juu ya jinsi moto huo ulivyopamba haraka na kwa kasi katika jengo hilo lililopachikwa jina la ‘mtego wa kifo’ na walionusurika.
  
Huku kukiwa bado na hofu ya vifo zaidi, ilibainika kuwa waliokufa ni sita huku wengine 74 wakilazwa kwenye hospitali sita za hapa wakiwamo 20 walio katika hali mbaya.
Wazimamoto 200 na mashine 40 za kuzimia moto zilitakiwa ili kukabiliana nao.
Wakazi hao walishalalamika huko nyuma, kuhusu usalama wa moto katika jengo hilo kwa mmiliki wake, Shirika la Usimamizi wa Wapangaji la Kensington and Chelsea (KCTMO), lakini malalamiko yao yakagonga ukuta.

WCB Wabadilike Uimbaji

Nashangaa kuona wasanii wote wanaimba key moja mwisho wa siku haitambuliki huyu ni nani sababu wanaigana kama wataendelea hivi watachokwa hakuna anayetaka kubadika.

Baada yakuja huyo Lava Lava nikazani anakuja na key tofauti kumbe yale yale leo katoa nyimbo mpya inaitwa teja anaimba kama Diamond au harmonize.

Game ya mziki kwa sasa imepoa sana wasanii wajaribu kuja na style mpya kila siku kuimba kwa mazoea ni kero tu kwa wasikilizaji.

Pia wajaribu kutoa na Producers tofauti , midundo ya Laizer tumeshaichoka

Ijumaa, 9 Juni 2017

Kajala Aibuka na Haya Kuhusu Wema Sepetu..Adai Hata Mwanae ni Shahidi..!!!



TASNIA ya filamu nchini imepambwa na wasanii wa kike wenye urembo unaovutia macho na hakika kwenye orodha ya waingizaji wenye kipaji, uwezo na mvuto huwezi kumuacha, Kajala Masanja.

Huyu ndiyo bosi wa kampuni ya Kajala Entertment,  ambayo imetengeneza filamu nyingi ikiwemo ile ya Sikitu ambayo chini ya mpicha Farid Uwezo iliweza kufanikiwa  kuliteka soko hilo la filamu.


Juma3tata wiki hii lipo na mrembo huyu, mpenzi wa chakula aina ya ndizi na samaki sato ambapo amefunguka mambo kadha wa kadha yanayohusu maisha yake ya ustaa na yale ya kawaida.

MKASA WA JELA WAMFUNZA

“Nina mfano halisi kabisa katika maisha na nitahakikisha namfunza mwanangu Paula asije akakutana na mkasa ulionikuta mimi na kufanya niingie jela kwa kuwa nilimsapoti mtu hata kwa yale yasiyostahili kisa nilikuwa nampenda,” alisema Kajala.

HATAKI KUFANYA TENA KOSA

Kajala amezidi kulifahamisha Juma3tata kuwa hapendi kulikumbuka tukio lile lililomfanya akae jela kwa muda wa mwaka mmoja na kumwacha mtoto wake kwenye wakati mgumu na hataki tena kufanya uzembe uliosababisha kosa lile.

 “Naweza sema ni uzembe ambao nilijitakia mwenyewe,  kumwamini mtu wakati kabisa najua ananiingiza shimoni ni kitu ambacho hakitafutika maishani mwangu, sitafanya kosa tena” anasema Kajala.

AWAONYA WAREMBO WENGINE

“Nataka wasichana wenzangu wajifunze kupitia mimi yaani hata kama unampenda mtu, usikubali akushawishi uvunje sheria za nje, jitahidi ujinasue kwani mwisho wake ni mbaya sana,” anasema.

HATASAHAU HURUMA YA WEMA SEPETU

Mara baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 7 au faini ya shilingi milioni zaidi ya kumi, Kajala na ndugu zake  waliingiwa na hofu kwani fedha hiyo ilikuwa ni kubwa kwao na hapo ndipo Wema Sepetu alipoibuka shujaa.

“Kama asingekuwa Wema Sepetu kunilipia zile  pesa sijui sasa hivi ningekuwa wapi, kwani hata ndugu zangu walichanganyikiwa kusikia kiasi kikubwa kile cha fedha ila moyo wa huruma wa Madame ulisababisha nitoke, siachi kumwombea katika sala zangu mwanangu pia analijua hilo,” anasema Kajala.

AZIPONDA TIMU MTANDAONI

Aidha aliweka wazi kusikitishwa timu katika mitandao ya kijamii zinazoibua maneno ya kuchochea ugomvi kati yake na Wema kitu kinachomuumiza kwani kwake ni mtu wa thamani mno.

KUFA KWA SOKO LA FILAMU

Katika hatua nyingine  mrembo huyo  alizungumzia anguko la filamu huku akikanusha taarifa hizo kwa kuwa wasanii wa bongo bado wanapiga kazi huku wengine wakishirikishwa na wasanii wa mataifa mengine.

“Kama soko la filamu limekufa basi wasanii wasingepata kazi za nje, sasa hivi wasanii tunaitwa kufanya filamu nchi za nje kwa malipo mazuri, tamthilia zetu pia zinaruka kwenye ving’amuzi mbalimbali, nchi nyingi zinazojifunza Kiswahili zinategemea filamu zetu kwa hiyo tunazidi kuvuka mipaka na kufanya vizuri,” anasema Kajala.

AWACHANA WASAMBAZAJI

Kajala amewataka wasambazaji kuwalipa wasanii kwa wakati mara wanapowekeana saini mikataba ya kusambaza filamu zao na siyo kuwalipa wasanii kwa awamu kitu kinachowafilisi wasanii.

 “Wasambazaji wa Kihindi waache  kutuzungusha kwenye malipo, kingine waache kubagua wasanii, waache kuangalia staa gani yupo ndani ya filamu ndiyo wanunue, waangalie ubora wa kazi na siyo sura,” anasema.

ANAAMINI KWA WASANII WACHANGA

Staa huyu wa filamu amesema anaamini katika vipaji vya wasanii wachanga, anaamini kuna kazi nzuri zinatengenezwa na wasanii wachanga lakinni wasambazaji huzikataa kwa sababu hawana ustaa.

Vita Ya Malipo Kiduchu Haijawahi Kumuacha Modo Salama!


Amber Lulu
AMANDA Swartbooi moja kati ya wauza nyago katika video Afrika akitokea Afrika Kusini. Amanda ametokea kujizolea umaarufu kwa kipindi kifupi cha mwaka jana ambapo ametokea katika video kadhaa Afrika ikiwemo Coolest Kid ya Davido akimshirikisha Nasty C wa Afrika Kusini, Four4 ya JR pamoja na Show Me ya Rich Mavoko akiwa na Harmonize.

Licha ya kufanya poa huko, ameshawahi kukiri kuwa kuuza nyago katika video hizo kunamlipa kwani kumempa mafanikio ya kujisomesha katika Chuo Kikuu cha Afrika Kusini (UNISA) akiwa mwaka wa pili katika masomo ya biashara. Ukija Bongo wapo wauza nyago katika Video za Kibongo ambao ni ‘visu’ lakini wanaangushwa na malipo kiduchu kutoka kwa wasanii husika kiasi cha kufikia kuangalia kazi nyingine za kufanya huku baadhi wakijiingiza katika muziki.
Agness Masogange


Katika makala haya nimekuchambulia baadhi tu ya wauza nyago (modo)ambao vita hii ya malipo kiduchu haijawahi kuwaacha salama kwani wengine wameamua kuachana na kuuza sura na wengine kujiingiza katika kuimba.

Alikuja kwa kasi, akavuma katika Video ya Kwetu ya Rayvanny na baada ya hapo akatokomea. Kutokana na kuitendea haki video hiyo, wengi walimtabiri kama miongoni mwa wauza nyago watakaokuja kuliteka soko. Hajashiriki tena katika kuuza sura kwenye video nyingine hadi sasa huku ikisemekana kukwepa malipo kiduchu kwa kila anayemfuata kufanyanaye kazi.


Alianza kuuza sura katika Video ya Naogopa ya Mirror kisha katika Remix ya Burger Movie Selfie ya Belle9 na baada ya hapo aliamua kuachana na suala la kuuza nyago na kujiingiza rasmi kwenye Muziki wa Bongo Fleva. Lulu anasema malipo kiduchu na mastaa wengine wakitaka kumtumia bure katika video zao ndivyo vilivyomkimbiza kwenye kuuza sura na kuamua kuimba ambapo kwa sasa anabamba na Ngoma ya Usimuache.

lulu Diva
Ni modo ambaye pia muuza nyago katika video za Kibongo. Kutokana na malipo kiduchu katika video hizo kumemfanya kupotea kimyakimya katika orodha wauza sura Bongo. Ameshawahi kukiri kulipwa kiasi kikubwa katika video moja tu (Salome ya Diamond) tangu aingie katika kuuza nyago huku akiwa na kumbukumbu ya kulipwa kiduchu katika Video ya Magubegube ya Barnaba.
Gigy Money



Naye ni miongoni mwa wauza nyago walioanza kupotea kwenye ramani ya muziki Bongo kisa hazilipi. Alianza kutokea katika Video ya Masogange ya Belle9 na baada ya hapo akaonekana kwenye Video ya Magubegube ya Barnaba iliyotoka 2012. Mara ya mwisho kuonekana katika ulimwengu wa wauza nyago ilikuwa katika Video ya Msambinungwa ya Tunda Man akishirikiana na Ali Kiba iliyotoka mwanzoni mwa mwaka 2014.