Jumanne, 14 Februari 2017

Mwanake ni Sura au Msambwanda?

Kuna hili suala ambalo nimeona sio vibaya tukiulizana kujua utashi wa kila atakayechangia tuone kipi watu wanapenda zaidi inapobidi kuchagua kimoja.

Ni ndoto ya kila mmoja kupata mwanamke aliyetimia kuanzia sura mpaka umbo na kwa sie waafrika toka kale tupo katika umbo tunamaanisha kalio lililoshiba vizuri yani msambwanda kwa lugha ya mtaani.

Lakini kwa bahati mbaya sio mara nyingi mtu hubahatika kupata seti iliyokamili, ndipo hapo napopenda kujua je kati ya binti mwenye sura nzuri lakini nyuma flat screen na binti asiye na sura nzuri ila nyuma amesheheni vizuri au ana umbo zuri upendalo utachagua yupi? Mimi binafsi msambwanda ndio ugonjwa wangu sura sio issue sana.

Karibuni wadau

Upepo Mchafu Wazidi Kumuandama Manji, Asakwa na Uhamiaji Kwa Kosa Hili

Baada ya Sakata la Madawa ya Kulevya kumuandama mpaka kufikia kulazwa Hospitalini, Uhamiaji nao wamekuja na Mpya baada ya kukamata Passport Kadhaa ofisini kwake za watu kutoka nje ambao wanafanya kazi kwenye kampuni yake bila vibali vya uhamiaji....

Diamond Platnumz Athibitisha Kuwa Mbioni Kumrudisha Q-Chief Kwenye Ramani...!!!

Diamond Platnumz amethibitisha kuwa amejipanga kumrudisha Q-Chief kwenye ramani ya muziki baada ya uongozi wake wa QS Mhonda kushindwa kufanya hivyo licha ya kudai kutumia zaidi ya shilingi milioni 200 bila kupata faida.
Kwa muda kulikuwepo na tetesi kuwa Diamond ana mpango wa kumsainisha msanii huyo mkongwe kwenye label ya WCB. Na sasa, ingawa hajasema kuwa amepanga kumsanisha kwenye label hiyo, Diamond amekiri kuwa kwenye mipango ya kufanya kazi na legend huyo.
“Unajua lengo langu kama mimi au sisi vijana wa sasa hivi tunajaribu kuona tunavyoweza kufanya kazi kwa ushirikiano, so tuko na maongezi na bro tunaangalia tunawezaje kufanya kazi kwasababu ni mtu ambaye kwanza mimi namfeel halafu ambaye namuamini,” Diamond ameiambia Dizzim Online.
“Ni mtu ambaye najua kabisa yaani akibonyeza button hii basi huu mji mzima umechafuka. Kwahiyo siwezi kuyaongea mengi sema Watanzania watuombee dua tunachokiplan kifanyike vizuri,” ameongeza staa huyo.
Naye Q-Chief alisema, “mimi nahisi project inayofuata Simba anahusika kwasababu ni mtu ambaye ameniita kwa ushauri nikiwa na QS, amemuambia vitu vingi vya msingi, yeye shahidi hapa, lakini kama ni mtu anayeelewa mdogo wake ameniita amesema nini mpaka mimi nimeelewa na hajafanya maybe [QS] is not ready to do business but Diamond is a business man and I am ready to join a business man so long as kuna misingi. Lakini naamini ngoma inayofuata Diamond amenipa baraka zake.”
Hivi karibuni muimbaji huyo ambaye jina lake kamili ni Abubakar Katwila amekuwa kwenye vita vya maneno na kampuni inayomsimamia ya QS Mhonda anayoishutumu kwa kushindwa kumfikisha popote licha ya uwekezaji mkubwa ilioufanya kwake.
Ndugu zake pia walihoji kuhusu mkataba wa maisha aliosainishwa mtoto wao kwenye kampuni hiyo na kwamba tangu awe chini ya kampuni hiyo hawajaona mabadiliko ya maana kwenye maisha yake.

Mshauri wa Rais Donald Trump Ajiuzulu

Mshauri mkuu wa ikulu ya White House kuhusu usalama wa taifa Michael Flynn amejiuzulu kuhusiana na uhusiano wake na maafisa wa Urusi, vyombo vya habari Marekani vinaripoti.

Bw Flynn anadaiwa kujadili vikwazo vya Marekani dhidi ya Urusi akiwa na balozi wa Urusi kabla ya Rais Donald Trump kuingia madarakani.

Anadaiwa kuwapotosha maafisa wa utawala huo mpya kuhusu mazungumzo yake na balozi huyo.

Awali, vyombo vya habari Marekani viliripoti kwamba Wizara ya Haki ilitahadharisha ikulu ya White House mapema kuhusu mawasiliano ya Flynn na maafisa wa Urusi mwishoni mwa mwezi uliopita.

Walisema Bw Flynn huenda akashurutishwa kuwa kibaraka wa urusi.

Maafisa wakuu wa chama cha Democratic walikuwa wametoa wito kwa Bw Flynn kuachishwa kazi.

Mashirika ya habari ya Associated Press na Washington Post yanasema wizara ya haki Marekani ilitahadharisha kuhusu kile ilichosema ni mambo aliyoyasema Bw Flynn kuhusu mazungumzo yake na balozi wa Urusi.

Ni kinyume cha sheria kwa raia wa kawaida kujihusisha na shughuli za kidiplomasia Marekani.

Mazungumzo kati ya Flynn na balozi wa Urusi yanadaiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka jana, kabla ya Bw Flynn kuteuliwa kuhudumu katika uatawala wa Bw Trump.

Bw Flynn, ni luteni jenerali mstaafu.

Awali alikana kuzungumza kuhusu vikwazo dhidi ya Urusi na balozi huyo, na Makamu wa Rais Mike Pence pia alijitokeza hadharani kumtetea.

Bw Flynn baadaye aliambia maafisa wa White House kwamba kuna uwezekano yeye na balozi huyo walizungumzia vikwazo hivyo.

Gazeti la Washington Post lilisema Kaimu Mwanasheria Mkuu Sally Yates aliambia White House kwamba mshauri wao mkuu wa usalama wa taifa "alijiweka katika hali ya hatari" kwa kuzungumza na Warusi kabla yake kuruhusiwa kisheria kufanya hivyo na kwamba Wizara ya Haki ilifahamu kwamba alimpotosha Bw Pence.

Mwezi uliopita, Bi Yates alifutwa kazi na Bw Trump kwa kukataa kutetea marufuku yake dhidi ya raia wa mataifa saba yenye Waislamu wengi kuruhusiwa kuingia Marekani.

Uvumilivu Unanishinda, Nashindwa Kutunza Bikira Yangu


Mimi ni msichana 21 aged, nishawahi pitia relationship 3( long distance). I never had sex with any of them tho. (im virgin), lakini siku zinavyozidi kwenda naona uvumilivu unanishinda...Marafiki zangu wanadai hiyo kitu ni tamu sana
Sometimes, natamani niende na mwnaume yoyote tuu.  Ushauri wenu tafadhali. "Ndege mjanja asinase kwenye tundu bovu.

Ulinzi waimarishwa Taasisi ya Moyo Muhimbili Ambako Yusuf Manji amelazwa

Hali ya ulinzi imeimarishwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alikolazwa mfanyabiashara Yusuf Manji baada ya kuugua ghafla akiwa polisi alikokuwa akihojiwa.

Manji aliyekuwa akihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini hapa alipelekwa hospitalini hapo juzi jioni akiwa ndani ya gari la wagonjwa aina ya Toyota Land Cruiser lenye nembo ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) huku gari lake aina ya Range Rover likifuata kwa nyuma.

Askari wenye sare na wengine wakiwa na mavazi ya kiraia nje ya wodi aliyolazwa mwenyekiti huyo wa klabu maarufu nchini ya Yanga walionekana wakiimarisha ulinzi.

Ilipofika saa 4:13 asubuhi mfanyabiashara huyo alitoka kwenye chumba hicho na kuongozwa kuelekea upande mwingine wa jengo hilo.

Akiwa amevalia nguo za wagonjwa zenye rangi ya kijani, Manji alitembea taratibu kuelekea upande aliokuwa akielekezwa.

Alipoulizwa kuhusu uwapo wa Manji hospitalini hapo, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi alisema hawezi kuzungumzia taarifa za mgonjwa.

Februari 8, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alitoa orodha ya watu 65, akiwamo Manji ambao aliwataka wafike Polisi kwa ajili ya mahojiano kuhusu masuala ya dawa za kulevya.