Alhamisi, 17 Desemba 2015

Rais Magufuli: Kwa Mara ya Kwanza Serikali Inakusanya Takribani Trilioni 1.3 Kwa Mwezi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli amesema kwa mara ya kwanza Serikali itakusanya takribani trilioni 1.3 kwa mwezi.

Pia amewahakikishia watanzania kuwa ahadi yake ya kutoa elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne ni lazima itekelezwe.

Amempongeza Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kazi nzuri ya ukusanyaji wa kodi.

Nyimbo 5 za Diamond zilizopo Store Zitaendelea Kumuweka Kileleni kwa Miaka 10 – Asema Mpiga Picha Wake

Diamond Platnumz ni msanii ambaye (angalau kwa sasa) haoneshi dalili za kushuka kimuziki hivi karibuni. Tunayo mifano mingi ya wasanii wa Bongo ambao waliwahi kufanya vizuri sana na baadaye kupotea kabisa kwenye ramani ya muziki.

Diamond ambaye ameachia ngoma mpya ‘Utanipenda’ wiki iliyopita ambayo imekuwa gumzo kwa watu wa kila rika, ana akiba ya hits na collabo za maana, ambazo kwa mujibu wa mpiga picha wake zinampa uhakika wa kuendelea kukaa kileleni kwa miaka mingine kumi ijayo.

Japo zipo collabo kubwa za kimataifa alizoisha fanya, ameamua kufunga mwaka kwa kuachia wimbo mwingine kabisa ambao hakuna aliyefahamu kama upo wala utafanya vizuri, hii inathibitisha silaha zilizosalia kwenye ‘benki’ yake ya nyimbo huenda yakawa ni mabomu makubwa zaidi.

Collabo zinazosubiriwa kwa hamu ni pamoja na ile ya Diamond na Ne-yo, Diamond na P-Square, Diamond na Usher na zingine.

Wafanyakazi Wanne wa Serekali Wakiuka Amri ya Rais Magufuli ya Kusafiri Nje ya Nchi Bila Ruhusa ya Rais..Wafukuzwa Kazi

Rais Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa watumishi waandamizi wanne wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU ambao walisafiri nje ya nchi licha ya Rais Magufuli kupiga marufuku safari za nje kwa watumishi wa umma.

Watumishi hao ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nikitas ambao walisafiri nje ya nchi licha ya kunyimwa kibali cha safari kutoka kwa Rais ama Katibu Mkuu Kiongozi.

Agizo hilo la Rais Magufuli  lilitolewa jana na Balozi Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari.

Balozi Sefue amewataka watumishi wengine wa umma kutii agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na kuonya kuwa atakayekiuka atachukuliwa hatua kali.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Disemba 17, Siri Kung'oka Hoseah wa Takururu Hii Hapa

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya Disemba 17, Siri Kung'oka Hoseah wa Takururu Hii Hapa

Rais Magufuli Awahakikishia Watanzania Kutimiza Ahadi Yake Ya Elimu Bure.......Aipongeza TRA kukusanya Trilioni 1.3 Ndani Ya Mwezi Mmoja,Atoa ONYO kwa Wakuu Wa Mikoa

Rais Magufuli amempongeza Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Dkt. Philip Mpango kwa kazi nzuri ya ukusanyaji wa mapato inayofanywa na mamlaka hiyo ambayo imeongeza ukusanyaji wa Mapato na kwa mara ya kwanza mwezi huu ukusanyaji wa mapato hayo unatarajiwa kuwa zaidi ya shilingi Trilioni 1 na Bilioni 300

Kutokana na mafanikio hayo amewahakikishia watanzania kuwa fedha kwa ajili ya kutimiza ahadi ya kutoa elimu bure kwa shule za msingi na sekondari ambazo ni kiasi cha shilingi Bilioni 131 zitatengwa mwezi huu na kupelekwa moja kwa moja katika shule husika.

Amesema wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa watapatiwa nakala za taarifa za ugawaji wa fedha hizo na kuonya kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayethubutu kuzitumia vibaya.

Dkt. Magufuli ameongeza kuwa fedha hizo ambazo ni pamoja na fedha za maendeleo, fedha za mitihani na fedha vifaa vya kufundishia zitaanza kutumwa kila mwezi kuanzia mwezi huu wa kumi na mbili.

Zitto Kabwe Amtetea Prof Mohongo Kwa Kuchaguliwa Kuwa Waziri, Adai Mwenye Ushahidi Dhidi ya Muhongo Aende Mahakamani

Waliosema Ufisadi ni Mfumo ndio wanasema leo Prof. Muhongo hafai kuwa Waziri sababu ya Tegeta Escrow. Sijui lini mahakama ilimhukumu Muhongo! Sijui lini Muhongo kawa Mfumo. Tujifunze kuweka akiba.

Prof. Sospeter Muhongo alikuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati wa sakata la ‪TegetaEscrow‬.

Kamati ya Bunge ilipendekeza na Bunge kuazimia kuwa Muhongo avuliwe madaraka yake ya Uwaziri. Prof. Muhongo alijiuzulu.

Akafanyiwa uchunguzi na Kamishna wa Maadili kutamka kuwa hakukutwa na kosa la kimaadili. Unajengaje hoja kuwa hana haki ya kuteuliwa kuwa Waziri?

 Keshaadhibiwa kwa kosa la awali, kwa kujiuzulu. Sheria ipi inasema hana haki ya kuteuliwa tena?

Niliongoza Kamati ya PAC. Nina uhakika Waziri muhongo kwenye sakata lile alishauriwa vibaya na kujikuta anatetea ubadhirifu.

Lile nifunzo kubwa kwake na ninavyomuona sasa hatarudia tena makosa yale. Kuna mambo ya msingi lazima afanye sasa

1) Azuie kuanzia sasa malipo ya 'capacity charges' kwa kampuni ya kitapeli ya IPTL na atumie sheria kutwaa mitambo ya IPTL na kumilikisha TANESCO

2) Amtake Waziri wa Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi kumkamata mara moja anayejiita mmiliki wa IPTL na afunguliwe mashtaka ya utapeli, wizi wa udanganyifu na uhujumu uchumi; huyo mmiliki na washirika wake ambao ni raia wa Tanzania

3) Amtake Gavana wa Benki Kuu na FIU kuichukulia hatua za kisheria Benki ya Stanbic ikiwemo kupiga faini ya kurejesha fedha zote zilizokua kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.

Hizo ndio hoja za msingi na sio uteuzi wa Prof. Muhongo. Mwenye ushahidi dhidi ya Muhongo si aende Mahakamani? Tuache siasa za porojo porojo

By: Zitto Kabwe

Waziri Atoa Mkwara Jeshi la Polisi Atoa Siku Mbili Aletewe Taarifa Kuhusu Udhibiti wa Madawa ya Kulevya na Watu Kubambikiwa Kesi

Waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga amefanya ziara ya ghafla leo Dec 16 2015 katika makambi mbalimbali ya Jeshi la Polisi Dar es salaam na kutoa amri kwa viongozi wa jeshi hilo siku mbili za kuhakikisha amepata taarifa kuhusu  udhibiti wa dawa za kulevya.

“Wapo wajanja wana mbinu nyingi, lakini hawawezi kutuua. Na mimi hili ni jambo nitalivalia njuga, lakini kwanini katika ukamataji wa dawa za kulevya sisi tulioko kwenye operesheni tunakaa pembeni? Nataka jibu siku ya Ijumaa”

Kuhusu watu kubambikiziwa kesi, Waziri limemgusa na kalizungumzia pia “Hili la kubambika watu kesi tunaweza kuliondoa hata leo, kikubwa ni kuwa na nidhamu, inakuwaje unambambika mtu kesi ili akuletee pesa? Hiki ni kitendo cha rushwa na tuliangalie kwa pamoja na tutaliongea kwa undani Ijumaa”