Alhamisi, 22 Oktoba 2015

Familia ya Mwanamuziki Diamond Yammwaga Rasmi Zari..Sababu Hizi Hapa

THE game is over! Sasa ni wazi kuwa familia ya staa mkubwa wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Plutnamz’ imemtema rasmi mzazi mwenzake Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kwa kile wanachodai …. “Tumechoshwa na uzungu wake”, Risasi Mchanganyiko linaweza kuandika.

Chanzo kilicho karibu na familia hiyo kililiambia gazeti hili kuwa kina taarifa kuwa mama Latiffa ‘Tiffah’ hatarejea tena nchini kutokana na kushindwana na wanafamilia, kwani wanaendekeza uswahili, kitu ambacho yeye hakiwezi.
“Familia ya Diamond ndiyo imemchoka, unajua yule hajazoea mambo ya kiswahili swahili, ametofautiana nao sana na ndiyo maana hata wao wamesema hawamtaki tena, wanahitaji mswahili mwenzao,” kilisema chanzo hicho.

FAMILIA YA DIAMOND HII HAPA
Ili kujua ukweli wa maelezo hayo, mwandishi wetu alimtafuta mama mzazi wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ kupitia simu yake ya mkononi, na alipoulizwa, alihamaki na kuanza kufoka, akidai hataki kuingiliwa mambo yake ya ndani na kwamba kama kuna mtu anataka kujua zaidi amfuate Zari huko kwao (South Afrika).

“Hata kama ni kweli, mimi na huyo sijui Zari wenu tumegombana wewe yanakuhusu nini? sipendi kuingiliwa kwenye mambo ya familia yangu, ninachojua ni kwamba hayupo hapa na maisha yanaendelea,” alisema Mama Diamond na kukaa kimya huku simu ikiwa hewani.
Wakati simu ikiwa hewani, ghafla sauti ya kiume ilisikika na kujitambulisha kwa jina la Anko Salum, aliyemtaka mwandishi kuachana na habari hizo, kwani ni za ndani na zitamalizwa na wenyewe kama familia.

Wakati mwandishi wetu akiendelea kuzungumza na Anko Salum, ghafla tena sauti nyembamba na kali masikioni ilisikika na mwanahabari wetu akaibaini kuwa ni ya Esma, ambaye ni dada wa Diamond.
“Mbona mnatufuatilia sana jamani? Nani anafuatilia mambo yenu? Nafasi ya Zari imefika mwisho, tunamkaribisha mwingine yeyote, kama kuna msichana mrembo unamjua, tuletee nyumba yetu ni kubwa sana, na sisi tunaruhusiwa kuoa hata wanawake wanne, Zari ameishia hapo, tena hatujagombana naye, lakini tumechoshwa na uzungu wake, awamu hii tunahitaji mswahili mwenzetu.
“Zari ameenda kwao, kulea watoto wake na kuangalia ustaarabu mwingine, tunamtakia kila la kheri, lakini hatuna ugomvi naye kabisa,” alisema Esma.Jitihada za kumpata Diamond hazikuzaa matunda kutokana na namba yake ya mkononi kutokuwa hewani kila alipopigiwa, hata hivyo jitihada zaidi zinaendelea kumtafuta.

Source:Global Publishers

Picha 16 Za MAFURIKO Ya Lowassa Huko Tanga- Jana Oktoba 21

Mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na Vyama vya Ukawa, Edward Lowassa, akipunga mkono wakati akiwasili kwenye Viwanja vya Indian Ocean katika mkutano wa kampeni mjini Tanga jana Jumatano 21/10/2015
















CHADEMA Wafichua Mbinu Zilizopangwa Kuvuruga Uchaguzi wa Jumapili hi

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chadema, Reginald Munisi (kulia) akifafanua jambo. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara, Prof. Abdallah Safari
**
ZIKIWA zimebaki siku tatu kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefichua mikakati iliyopangwa kuvuruga uchaguzi huo.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chadema, Reginald Munisi amebainisha mipango ‘ovu’ inayoratibiwa ili kuvuruga uchaguzi mkuu huku mipango hii ikishirikisha baadhi ya makampuni ya simu za mkononi, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na wakurugenzi wa uchaguzi katika majimbo mbalimbali.

Munisi ametaja baadhi ya mipango hiyo kama ifuatavyo, huku akitahadharisha watakaoshiriki mipango hiyo kuwa wataliingiza taifa katika machafuko bila sababu ya msingi.

Mpango wa kukata mawasiliano ya simu na data; upo mpango wa kuzuia mawasiliano ya simu za mkononi kwa kusitisha huduma ya kupiga na kupokea simu, kuzuia ujumbe mfupi wa maneno (sms), kuzuiwa kwa intaneti (data) na hivyo mawasiliano kuwa magumu, hasa wakati wa matokeo kubandikwa vituoni.

Mpango huu unatajwa kuwa na lengo la kukwamisha watu kuwasiliana na kupeana matokeo yatakayokuwa yakibandikwa vituoni ili kujumlisha na kupata matokeo ya jumla ya nafasi za udiwani, ubunge na urais. Utekelezaji wa mpango huu utashirikisha baadhi ya makampuni ya simu ambayo hakutaka kuyataja.

“Tunaziomba kampuni za simu zenye mpango huo, kuacha mara moja kwani zitajiongeza katika orodha ya watuhumiwa watakaoenda ‘The Hague’ mara baada ya uchaguzi kumalizika,” alieleza Munisi bila kuyataja makampuni hayo kwa kuwa bado chama hicho kinakusanya vielelezo.

Mpango wa kukata umeme maeneo yenye nguvu kubwa ya upinzani; maeneo ambayo vyama vya upinzani vina nguvu kubwa umeme utakatwa baada ya giza kuingia ili kuhakikisha mchakato wa kuhesabu na kujumlisha matokeo unaingia dosari na hata vurugu kutokea ili katika taharuki hiyo wizi wa kura uweze kufanyika.

Baadhi ya wakurugenzi wa uchaguzi kutoruhusu mawakala wa akiba wa upinzani kuapishwa; wakati uapishaji wa mawakala ukiendelea katika maeneo mbalimbali nchini, baadhi ya maeneo vyama vya upinzani vinazuiwa kuapisha mawakala wa akiba na wakurugenzi kutaka mawakala waape idadi sawa na idadi ya vituo vya kupigia kura.

Mkakati huu unalenga kuvifanya vyama vya upinzani vikose mawakala wa akiba iwapo itatokea dharura miongoni mwa wale walioapishwa, dharura zinazoweza kujitokeza ni kuumwa, kusafiri nje ya vituo, au kutekwa kabla ya kufika katika vituo vyao.

Iwapo mawakala hao watakosekana kwa dharura, baadhi ya vituo watabaki mawakala wa CCM pekee kwani hakutakuwa na mawakala wa akiba wa kuziba nafasi zao kwa kuwa ni lazima mawakala wawe wamekula viapo vya kisheria ili kupata uhalali wa kufanya kazi hiyo.

Reginald Munisi ameleza kuwa Chadema na Ukawa kiujumla wamejipanga vyema kuzikabili mbinu hizo chafu huku akiwaonya wale watakaoshiriki mipango hiyo kuachana nayo mara moja kwani tayari imefahamika na wanaweza kukumbana na nguvu ya Umma.

Madai ya Kumuua Mwigizaji Kanumba LULU MICHAEL Mahakani Tena...

Stori: Na Brighton Masalu
MAMBO yameiva! Nyota wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ (20) yu mbioni kupanda tena Kizimba cha Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam kwa ishu yake ile ya madai ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa msanii wa filamu nchini, marehemu , Amani lina ripoti mkononi.
Nyota wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kutoka ndani ya mahakama hiyo jijini Dar, kesi hiyo ilisimama kwa muda wa mwaka mmoja na zaidi kutokana na matatizo yaliyo nje ya uwezo wa mahakama, lakini sasa matatizo hayo yameisha hivyo kesi hiyo itaanza kurindima siku yoyote kuanzia sasa.
NI BAADA YA MWAKA MMOJA NA MIEZI NANE
Tangu kusimama kwa kesi hiyo, mwaka 2013, ilitarajiwa kuanza tena kusikilizwa Februari 17, 2014 lakini ikakwama kutokana na matatizo mbalimbali ya kimahakama.
ITAANZA UPYA
Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, mwendesha mashtaka wa serikali atamsomea mashtaka upya Lulu lakini neno la msingi kwenye mashtaka hayo ni; mnamo Aprili 7, 2012 anadaiwa kumuua bila kukusudia, Steven Kanumba.
“Baada ya kuulizwa, Lulu akiwa kama Elizabeth Michael atajibu anachotaka kutoka moyoni kulingana na ukweli anaoujua kisha jaji atampangia tarehe ya kurudi tena,” alisema mtoa habari huyo.
MAHAKAMA ITATUMIA MWONGOZO WA JAJI MKUU
Tofauti na madai ya awali kwamba, kesi hiyo ingeendeshwa kwa siku 730, habari za uhakika zinasema kuwa, kesi itakapoanza safari hii haitasimamishwa mpaka siku ya hukumu. Kwa hiyo itategemea na kasi ya hakimu husika.
“Lakini pia, kauli ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman anayoitoa kila Siku ya Sheria Duniani (Februari 3) kwamba kesi zote za jinai zisipitishe miaka miwili, itazingatiwa,” kilisema chanzo.
Kikaongeza: “Lakini nadhani ikianza safari mwaka huu, naamini mpaka mwaka 2017 itakuwa imemalizika kama sheria ya miaka miwili itazingatiwa.”

Marehemu  Steven Charles Kanumba ‘The Great’ enzi za uhai wake.

CHENI BADO MDHAMINI

Chanzo hicho kilisema kuwa, bado mcheza sinema maarufu Bongo, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ anaendelea kutambulika na mahakama kama mdhamini wa Lulu. Kwa hiyo, anatakiwa kuendelea na jukumu la kumlinda Lulu ili asiruke dhamana (asitoroke, asikiuke masharti ya dhamana).
MASHAHIDI WAJIPANGE
Chanzo kilisema baadhi ya mashahidi muhimu nao watapewa taarifa ya kimaandishi ili tarahe ya kesi wafike mahakamani.
Mashahidi hao ni Dokta Kidume ambaye alikuwa akimtibu Kanumba pia ndiye alikuwa mtu wa pili kufika kwenye chumba cha marehemu mara baada ya kuanguka na kupoteza maisha.
Seth Bosco naye anatakiwa kujiandaa kupokea wito huo kwani yeye siku ya tukio alikuwa nyumba moja na marehemu (vyumba tofauti). Yeye alimshuhudia Kanumba akiwa katika hali mbaya baada ya kutoelewana na Lulu na kukimbia kwenda kumwita Dokta Kidume.
WAKILI WA LULU AZUNGUMZA
Peter Kibatala ni wakili maarufu jijini Dar. Yeye ndiye mwanasheria katika kesi ya Lulu. Amani lilimtafuta ili kujua hatima ya kesi hiyo na madai kwamba iko njiani kuanza upya. Alisema:
“Aaa! Sijajua. Lakini kwa kawaida mahakama itakapoona mambo yameanza, kesi inatakiwa kuanza kusikilizwa itatakiwa kutoa taarifa siku sita kabla.”
AMZUNGUMZIA LULU
Wakili Kibatala alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, mteja wake (Lulu) amekuwa akimpigia simu mara kwa mara akitaka kujua tarehe ya kesi yake kuanza tena.
“Hata Lulu mwenyewe amekuwa akinipigia simu kuulizia ni tarehe ngapi kesi yake itaanza tena. Nitapewa taarifa siku sita kabla,” alisema mwanasheria huyo.
LULU PRESHA INAPANDA
Naye rafiki wa karibu wa Lulu, akizungumza na gazeti hili huku akiomba hifadhi ya jina lake, alisema:
“Ninyi mnaandika Lulu siku hizi anakunywa sana pombe. Mnajua hayuko sawasawa. Ile kesi yake ya kumuua (bila kukusudia) Kanumba inamtesa sana kichwani.
“Ukimya wa kesi unamfanya ashindwe kujua hatima yake. Kila akikumbuka anampigia simu wakili wake. Mbaya zaidi kuna watu wanamwambia kesi inaweza kukaa kimya kwa muda mrefu halafu siku moja ikalipuka na kuwa nzito. Kwa hiyo wakati mwingine mjue hilo.”
WASOMAJI WETU
Baadhi ya wasomaji wa Magazeti Pendwa ya Global Publishers  wamekuwa wakipiga simu chumba cha habari na kuulizia kama kesi ile ilifutwa kinyemela au kihalali.
“Jamani Global, mimi shida yangu ni kuulizia kuhusu ile kesi ya Lulu na Kanumba. Hivi bado ipo au ilishafutwa kinyemela. Maana si mnajua watu maarufu tena huenda kuna kubebana,” aliwahi kuuliza msomaji mmoja.
LULU ASAKWAJumatatu na Jumanne iliyopita, simu ya Lulu ilipopigwa iliita muda mrefu bila kupokelewa. Hata hivyo, baadhi ya watu wake wa karibu walisema Lulu huwa hapokei simu ambayo jina halipo kwenye simu yake.
Source:GPL


Hatimaye Mama Maria Nyerere Ampigia Kampeni Magufuli

CCM tayari wameshatengeneza video ya mama Maria Nyerere akiwaomba akina mama wotewampigie kura Magufuli. Video hii iko inasambaa Whatsup.

Kaongea mengi kuwa ni mchapa kazi na Mwadilifu. Swali langu kwa bibi angu mama Maria, ikiwa CCM itashindwa, heshima yote tunayokupa sisi wananchi itakuwaje? Maana yake wote watakaoongoza rohoni mwao watakuwa wanajua kabisa hukuwapenda ila basi.

Ni bora mama ungebaki neutral. Na ungejikita kutuombea tuchaguane kwa Amani ili uendeleee kuwa Mama wa Taifa.

Ila tutasamehe tukiamini imekulazimu, maana hakuna jinsi

UKAWA Watishia Kutoshiriki Uchaguzi Mkuu wa Jumapili

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinachoungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kimetishia kutoshiriki katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Chadema, Reginald Munisi amesema wanadhamilia kutoshiriki katika uchaguzi huo kutokana Tume yaTaifa ya Uchaguzi (NEC) kutokuwa na msimamo katika kazi zake.

Anasema zikiwa zimebaki siku tatu wananchi kuelekea kwenye uchaguzi mkuu lakini NEC hadi sasa haina msimamo na kuonekana kuyapuuza madai mengi yenye hoja yanayotolewa na Ukawa.

Akiyataja baadhi ya madai ambayo NEC imeyapuuza ni kutotoa ushirikiano wa kufafanua juu ya upigaji kura kwa watu ambao hawakuona majina yao kwenye daftari la kupiga kura na kutotoa sababu ya utofauti wa namba za kupigia kura kutoka kwenye daftari na kwenye kitambulisho.

Munisi ameongeza kuwa, NEC wamepuuza kutoa ufafanuzi juu ya picha ambazo haziitajiki katika upigaji kura, kutoa ufafanuzi juu ya listi mpya ya wapiga kura iliyosemwa na Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva, kwamba kutakuwa na watu wa ziada ambao hawapo kwenye daftari, Je, wanatoka wapi na wapo wangapi? Amehoji.

Kwa mtindo huu ambao NEC inaenda nao wa kukubali watu wasiokuwa kwenye daftari wapige kura na hata wasiokuwepo kwenye orodha wapige kura mbona hawakutushirikisha sisi wadau wa uchaguzi? Inaweza kupelekea uvunjifu wa amani. Hilo ndio bao la mkono ambalo lilisemwa na hatutaki litokee,” anasema Munisi.

Munisi amesema sababu nyingine kubwa ambayo inaweza kupelekea wasishiriki kwenye uchaguzi ni kuhusu madudu yaliyopo ndani ya daftari la wapiga kura, ambapo hadi sasa NEC haijatoa jibu linaloeleweka juu ya makosa ambayo yalionekana kwenye daftari.

Sababu nyingine ya kutaka kutoshiriki amesema, “Hatuna imani na ujumlishaji wa matokeo ya kura kwa njia ya mashine zao za kujumlisha kwani zinamapungufu mengi. Tuliomba tume itumie njia ya kawaida kwa njia ya kalukuleta ili kila mtu alidhike lakini walidai tunawaingilia kazi zake. Sisi hatutakubali,” amesema Munisi.

Kwa mujibu wa Munisi amesema, hadi sasa bado wanaendelea na uchunguzi kwenye madaftari ya wapiga kura ambapo amesema wameshakagua katika mikoa tisa na kubaini matatizo mengi zaidi yakiwemo ya picha hewa, picha za watu wawili na majina ya kiume kwenye picha za kike.

“Hapo hatujafanya katika majimbo yote tulifanya baadhi. Bado tunaendelea na uchunguzi hadi kesho, tukiona makosa yanazidi kiwango cha kufanya uchaguzi usiende vizuri basi tunaiomba NEC ipeleke uchaguzi mbele,” amesema Munisi.

Aidha, ameitaka NEC kutoa orodha maalumu ya vituo vya kupigia kura kwani hadi sasa Ukawa bado hawajajua idadi kamili ya vituo hivyo wanashindwa kuwaapisha mawakala kwa idadi ya vituo kubadilishwa kila siku.

Katibu Mwenezi wa CCM Nape Nnauye Apata Ajali Mbaya ya Gari

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amepata ajali mbaya jana usiku akiwa njiani kuelekea Lindi akitokea jijini Dar es Salaam.
Nape ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtama, Lindi  alipata ajali hiyo baada ya tairi la mbele la gari aliyokuwa akiendesha aina ya Toyota Land Cruiser kupasuka na kupinduka mara kadhaa katika eneo la Nyangao mkoani Lindi.
Katika gari hilo, Nape alikuwa peke yake na ndiye alikuwa akiendesha gari hilo ambapo amepata majeraha madogo  ila anaendelea vizuri.
Akizungumza na mtandao huu, Nape amesema: “Namshukuru Mungu nimetoka salama na nawaomba wananchi wasiwe na hofu japo ajali ilikuwa mbaya maana gari lilipinduka mara kadhaa, nimepata majeraha madogomadogo na michubuko ila ni mzima.
Gari limeharibika vibaya ila ninachoshukuru nilikuwa nimefunga mkanda na ‘air bag’ nazo zimenisaidia.”
Kabla ya ajali hiyo, Nape alikuwa jijini Dar es Salaam ambapo aliungana na mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli aliyekuwa na mikutano kadhaa ya kampeni katika jiji la Dar na baada ya shughuli hiyo alikuwa akirejea Lindi kuendelea na kampeni kwenye jimbo lake la Mtama.

Source:GPL

Muonekano wa Gari ya Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye, Toyota Land Cruiser Baada ya Kupata Ajali Mbaya Jana Usiku

 Muonekano wa gari ya Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye, Toyota Land Cruiser baada ya kupata ajali mbaya jana usiku akiwa njiani kuelekea Lindi akitokea jijini Dar es Salaam.

Magufuli Asimamisha Jiji La Dar.......Asema Tanzania Inahitaji Rais Mkali. CHADEMA Wampokea Kwa Ishara Ya Vidole Viwili Juu

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema nchi inahitaji rais mkali ili mambo yaende huku akishangazwa na mmoja wa vigogo kufungua kesi kupinga mradi wa maji.

Amesema watu wa aina hiyo watakiona na anamuomba Mungu kwa siki tatu zilizobaki apewe urais kwa vile hao ndiyo ataanza kushughulika nao.

Kauli hiyo aliitoa   Dar es Salaam jana kwa nyakati tofauti katika mikutano ya kampeni iliyofanyika   Kigamboni, Mbagala, Temeke, Ubungo na Kinondoni.

Alisema hayuko tayari kuona watu wanaendelea  kupoteza maisha kwa   kipindupindi huku kigogo huyo akikimbilia mahakamani.

Kitendo cha kigogo huyo  kufunga njia ya maji kwa kujenga bomba la majitaka kimesababisha wananchi wa   Dar es Salaam  kupoteza maisha kwa kuugua kipindupindu, alisema.

Ninajua hapa Temeke kuna mtu amekimbilia mahakamani na kukwamisha mradi wa maji lakini mahakama haitoi haki kwa wakati.

“Zimebaki siku nne ninichague kuwa rais, mtu anachelewesha mradi wa maji kwa kwenda mahakamani ngoja nipate urais. Amejenga juu ya njia ya maji watu wanakufa kwa kipindupindu haki ya Mungu ngoja nipate urais.

“…tunahitaji rais mkali mambo yaende kesi ni lazima iamuriwe kama Serikali tumeshindwa tukate rufaa. Tena huyo mtu aliyefungua kesi ana udugu na mmoja wa wagombea wa Ukawa,” alisema Dk. Magufuli.

Mgombea huyo wa urais alisema  atakapochaguliwa Jumapili atakwenda kuanza na hilo.

“Haiwezekani, haiwezekani, haiwezekani mradi wa maji una manufaa wao wanakunywa maji ya Kilimanjaro wananchi wanateseka. Lakini watu wachache kwa tamaa zao na madaraka yao wanakwamisha.

Wanasema mimi ni mkali, hapana nina hofu ya Mungu, tunaomba kesi hii iamuriwe kama tumeshindwa tukate rufaa,” alisema Dk. Magufuli

Mgombea huyo wa urais alisema yeye ni mtu wa uamuzi makini anayekuja kuijenga Tanzania mpya na yenye matumaini kwa watanzania wote.

Alisema anashangazwa na watu wanaohangaika na uamuzi mgumu kwani wanaofanya hivyo ni majambazi, wezi na mafisadi pekee.

Dk. Magufuli, alisema ataongoza taifa kwa umakini kwa kuleta maendeleo ya kweli.

Alisema anashangazwa na watu wanaopita na kujinasibu kwa kuleta uamuzi mgumu wakati ndiyo walioleta matatizo katika nchi na hata kusababisha kero ya umeme kila kukicha.

Watakuja wapinzani wetu na kusema eti wanakuja na uamuzi mgumu, jamani uamuzi mgumu hufanywa na majambazi, wezi na wauaji wa watu wenye albino. Inashangaza sana hawa watu msiwakubalie hata kidogo.

… hivi jana itokee upate mume au mke anayetamba kwa kuwa na uamuzi mgumu si atakunyonga kitandani. Eti atafanya uamuzi mgumu mbona hujinyongi kwa kamba?  Mimi kwangu Magufuli kazi tu,” alisema Dk. Magufuli.

Akizungumzia ujenzi wa daraja la Kigamboni, Dk. Magufuli alisema litakamilika mwezi ujao na wananchi wa eneo hilo watavuka bure ila watu wenye magari ndiyo watakaolipa ada.

Alisema yeye ni mtu anayesimamia sheria hivyo katu hawezi kuzivunja   kwa kutoa ahadi za uongo kwa lengo la kutafuta kura za watanzania.

“Daraja la Kigamboni litakamilika mapema mwezi ujao na litakapokamilika wakazi wa Kigamboni watapita bure ila wenye magari watalipia kama ilivyokuwa kwenye kivuko cha pantoni.

Kigamboni ya sasa imekuwa na maendeleo na kwa sababu mbunge wenu, Dk. Ndugulile (Faustine) ni mfuatiliaji nami nawaomba mumchague ninamuhitaji.

“Alipambana kwa ajili ya yenu na sasa ninasema hapa Rais Jakaya Kikwete amenisaidia sana kwa kuiteua Kigamboni kuwa wilaya nami kazi yangu itakuwa ni kuleta maendeleo ya kweli,” alisema.

Mgombea huyo wa urais alisema kwa mujibu wa sheria, ardhi ni mali hivyo kwa Kigamboni kujengwa mji mpya ni hatua kubwa ya maendeleo.

Dk. Magufuli aliwataka wakazi hao kuhakikisha wanasimamia haki zao ikiwamo kumiliki ardhi yao na hata kushirikiana na wawekezaji.

Ardhi ni mali na hapa Kigamboni sasa mji mpya   wakija wawekezaji kwanza wawape noti na hata mshirikiane pamoja kutokana na ardhi yenu,” alisema.

Chadema wampokea Ubungo  huku  wakimshangilia  Lowassa
Mgombea huyo wa urais wa CCM alipofika katika Kituo cha Mabasi Ubungo, alisimamishwa na wafuasi wa Ukawa  ambao  walimnyoonshea  vidole  viwili  juu  huku  wakimshangilia  Mgombea  wao  kwa  kuimba  Lowassa!!!  Lowassa!!

Baada  ya  hali  hiyo,Magufuli  aliwasalimia wafuasi  hao  wa  Ukawa  kwa  ishara  ya  salamu  zao  na  kuwaambia  kuwa  maendeleo  hayana chama.

Maendeleo hayana chama iwe Chadema, CCM, CUF na hata Ukawa mimi kwangu ni kazi tu,” alisema.....Tazama  Video  Hii https://youtu.be/NI_JKb9KJSc