Jumatano, 12 Novemba 2014

Mwanamke ajitoa mhanga chuoni Nigeria

 
Wapiganaji wa Boko Haram wamekuwa kero kwa serikali na wananchi wa Nigeria 
Mwanamke mmoja amejilipua katika chuo cha mafunzo Kaskazini mwa Nigeria.
Walioshuhudia shambulizi hilo wanasema kuwa bomu lililipuka huku mwanamke huyo akijiandaa kuingia katika ukumbi uliokuwa umejaa wanafunzi mjini Kontagora.
Idadi ya majeruhi bado haijulikani , lakini mwalimu mmoja alimbia BBC kuwa aliona miili minne ikiwa katika hali mbaya.
Wapiganaji wa kiisilamu Boko Haram wanaendesha harakati za kivita dhidi ya serikali ya Nigeria, harakati ambazo zimekuwa zikiendelea kwa miaka mitano iliyopita.
Kundi la Boko Haram, limeyatangaza kuwa dola za kiisilamu baadhi ya majimbo wanayoyadhibiti, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. .
Kadhalika kundi hilo limekuwa likifanya mashambulizi na mauaji Kaskazini Mashariki mwa Nigeria tangu kuanzisha harakati zake mwaka 2009.
Watu wanasema walisikia mlio mikubwa kabla ya watu kuanza kukimbilia usalama wao.
Wanajeshi walikimbia kwa harakan katika kituo hicho baada ya shambulizi na hata kuziba eneo zima.
Tatu kati ya miili minne iliyoonekana ilikuwa ya wanawake.
Baadhi ya walioshuhudia shambulizi hilo walisema kuwa mwanamke aliyekuwa amejifunga mabomu hayo pia aliuawa.
Takriban watu 7 walijeruhiwa vibaya ingawa walikimbizwa hospitalini kwa matibabu.

Soma kuhusu binti aliyeamua kuongeza titi la tatu katika mwili wake

tt
Kweli duniani kuna vituko na ndivyo ilivyotokea kwa binti mmoja mwenye umri wa miaka21 baada yakufanyiwa upasuaji wa kuongeza titi la tatu katika mwili wake.
Binti huyo aliyejulikana kama Jasmine Tridevil alitumia pauni 12,000 za kimarekani sawa na zaidi ya milioni20 za kitanzania kwa ajili ya kufanya upasuaji ili  mradi aongeze kiungo hicho.
Katika makala iliyoandikwa na Gazeti la JAMBOLEO msichana huyo kutoka Marekani alisema kuwa alianza kuhifadhi fedha kwa ajili ya upasuaji huo kwa miaka miwili iliyopita ilimradi atimize azma yake.
Madaktari waliomfanyia upasuaji huo walikata sehemu ya nyama ya tumbo lake kwa ajili ya kupachika kiungo alichokua akikitaka katika sehemu ya kifua chake.
Awali aliita zaidi ya madaktari 50 ili kufanya zoezi hilo lakini walikataa kumfanyia upasuaji huo na ndipo baadhi ya madaktari wakajitokeza na kukubali.
Hata hivyo kwa mujibu wa mmoja wa madaktari hao alisema titi la tatu halitakua na uwezo wa kufanya kazi kama yalivyo mengine mawili ila kikubwa anapenda kuwa katika hali hiyo.
Akizungumzia hatua ya wazazi wake baada ya kitendo chake alisema kuwa hawakupendezwa nacho hadi kufikia hatua ya kukataa kuongea naye kabisa.

Alichojibu Guardiola baada ya kuulizwa kama ataifundisha tena Barcelona

516501_heroaMiaka takribani mitatu baada kuacha kuifundisha klabu ya FC Barcelona, kocha Pep Guardiola amezungumzia kama ikitokea nafasi ya kurudi Nou Camp – atakubali kuifundisha timu hiyo.
Akizungumza na gazeti la Mundo Deportivo Guardiola ambaye alijiunga na Bayern Munich mwaka 2013 baada ya mapumziko ya mwaka mmoja baada ya kuondoka Barca – amesisitiza haoni namna anaweza kurudi kuifundisha klabu hiyo, kwa sababu alishamaliza kazi yake.
Boss huyo wa Bayern Munich alitumia miaka minne Nou Camp – akitengeneza timu ambayo inatajwa kuwa bora kuliko zote katika historia ya soka wakishinda makombe mawili ya ulaya na La Liga mara 3 kuanzia mwaka 2008 mpaka 2012.
Baada ya miezi 12 ya mapumziko, Guardiola aliteuliwa kuwa kocha wa Bayern Munich mwaka jana, japokuwa mara kwa mara imekuwa ikiripotiwa kwamba anaweza kurejea kuifundisha Barca kwa muhula wa pili.
Lakini wakati kocha huyo mwenye miaka 43 akiwa anakiri kwamba atarudi Catalonia kwenda kuishi na mkewe, anasema sio kwenda kuifundisha Barca tena.
“Kwa haraka haraka tu naweza kukwambia kwamba sitoifundisha tena Barca. Naamini kuna maduara kwenye maisha – langu mie na Barca lilishaisha,” aliiambia Mundo Deportivo.
“Mke wangu anafanya kazi jijini Barcelona na wazo ni kurejea tena hapa na kuishi na familia yangu, lakini sijui lini hiyo itakuwa.”

Breaking Rapper Geez Mabovu amefariki dunia usiku huu

Geez Mabovu 
Kabla mwaka 2014 haujaisha idadi ya watu maarufu wa Tanzania waliotangulia mbele za haki imezidi kuongezeka na hii ni baada ya taarifa kutoka Iringa zilizoanza kusambaa kuanzia saa tatu usiku November 11 2014.
Taarifa zilizothibitishwa ni kwamba rapper Geez Mabovu ambae ni maarufu kwenye muziki wa hiphop Tanzania, amefariki dunia kwenye hospitali aliyokua amelazwa nyumbani kwao Iringa alikokwenda wiki mbili zilizopita kutokea Dar es salaam.
Geez Mabovu 2
Geez 3
Hii ni picha ya July 2013 ambayo ni mara ya mwisho Geez Mabovu ameonekana kwenye millardayo.com akiwa na Baba yake Dully Sykes maeneo ya Kinondoni Dar es salaam nje ya Bar ya msanii Dudubaya aliyokua ameifungua wakati huo.
Dennis ambae alikua mtu wa karibu wa Geez Mabovu amethibitisha pia kuhusu kifo cha Geez Mabovu na kusema rapper huyu aliondoka Dar kwenda Iringa akiwa kwenye hali ambayo sio nzuri kiafya.
Kwa mujibu wa Denis, Geez atazikwa kesho jioni November 13 2014. #RIP