Jumanne, 14 Novemba 2017

Mnunuzi Feki wa Nyumba za Lugumi Kupimwa Akili

Mnunuzi Feki wa Nyumba za Lugumi Kupimwa Akili
Bilionea Dkt. Luis Shika ambaye wiki iliyopita alitangaza kununua nyumba za kifahari za mfanyabiashara za Said Lugumi, zilizopo eneo la Bweni JKT jijini Dar es salaam anatarajiwa kupelekwa hospitali kupimwa afya ya akili.

Hayo yamesemwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Jeshi la Polisi (SACP), Benedict Kitalika, ambapo amesema uamuzi wa kumpeleka hospitali Dkt. Shika  kuchunguzwa afya ya akili yake, umetokana na uchunguzi wa awali ulioonesha anaweza kuwa na tatizo hilo huku akidai kuwa uchunguzi huo utalisaidia Jeshi la Polisi kukamilisha uchunguzi.

“Tunatarajia kumpeleka hospitali wakati wowote ili kuangalia kama kuna tatizo katika afya ya akili au la kutokana na historia yake ya maisha inavyojionyesha, hali ambayo inaweza kutupa majibu sahihi.” amesema Kamishna Kitalika.

Kamishna Kitalika amesema uchunguzi wa awali ulihusisha historia ya maisha yake inayoonyesha ni msomi aliyewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi nchini Urusi kabla ya kurudi nchini na kuishi kwenye chumba kimoja cha kukodi, huku sababu za kurudi kwake zikiwa hazijulikani.

“Na sisi tumejiuliza sana kuhusu utimamu wa akili kama upo sawa au kuna tatizo la kisaikolojia, kwa sababu ukiangalia historia yake inaonyesha wazi ni msomi mzuri ambaye ameshika nafasi za uongozi nchini Urusi, lakini maisha anayoishi nchini si ya kuridhisha. Hatujui amepatwa na nini hadi kufikia hatua ya kukodi chumba kimoja cha kuishi katika Mtaa wa Tabata, huku mwonekano wake ukiwa haupo sawa kisaikolojia.” amesema Kamishna Kitalika.

Hata hivyo, tayari jalada la kesi ya Dkt. Shika limepelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) ili aweze kuangalia kama kuna jinai yoyote iliyotendeka kwa mtuhumiwa huyo au la.

Akizungumzia hilo, Kamishna Kitalika amesema licha ya jalada hilo kuwa mikononi mwa AG, imebainika kuwa baadhi ya kanuni wakati wa mnada wa nyumba za Lugumi hazikufuatwa, ikiwepo ya kulipa asilimia 25 pale pale baada ya mteja kujitokeza hali ambayo inaongeza shaka kwa Dkt. Shika.

“Katika mnada ule, baadhi ya kanuni hazijafuatwa ikiwamo ya kumtaka kulipa asilimia 25 pale pale mara baada ya kununua, lakini suala hilo halijafanyika badala yake waliendelea kupiga mnada nyumba nyingine, hivyo kama taasisi za uchunguzi tunapaswa kufuatilia hatua kwa hatua,” amesema Kamishna Kitalika.

Wiki iliyopita, Dkt. Shika alijitokeza kwenye mnada wa nyumba tatu za Lugumi, mbili zipo Mtaa wa Mbweni JKT na moja ipo Upanga na kushinda minada yote.

Mnada huo ulifanywa na Kampuni ya Udalali ya Yono kwa amri ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambapo Dk. Shika aliahidi kununua nyumba hizo kwa thamani ya Sh bilioni 2.3 lakini alishindwa kulipia asilimia 25 ya fedha hizo ambazo ni shilingi milioni 800 kitu ambacho kilipelekea akamatwe na polisi kwa kosa la kuharibu mnada na utapeli.

Chanzo : Mtanzani 

Dk Cheni Awapa Makavu Wanaomsakama Lulu Kuhusu Dhamana

Dk Cheni Awapa Makavu Wanaomsakama Lulu Kuhusu Dhamana
MSANII mkongwe katika tasnia ya maigizo Bongo na mshereheshaji (MC), Mahsein Awadhi ‘Dk. Cheni’ ambaye ni mlezi wa mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametoa maoni yake kwenye mtandao wa kijamii baada ya kuibuka maneno mengi kwenye mitandao hiyo ambapo watu wengine wanasema Lulu amepewa adhabu ndogo na wengine wakipendekeza angefungwa kwa miaka mitano na kuendelea.

Dk Cheni amewalaumu wasiomtakia mema Lulu akisema mambo yote mabaya yanaweza kumtokea yoyote, kwa hiyo kufurahia jambo baya limpatalo mtu si jambo jema.  Pia ametoa asante kwa wote wanaomwombea mema Lulu na waendeleee kufanya hivyo.

Ujumbe aliotuma msanii huyo ni huu hapa chini:

Linapokukuta jambo wapo wataokuonea huruma na wapo watakaokuwa na furaha ila niwakumbushe jambo hakuna ajuwaye kesho yake kubwa kila mapito mwambie Mungu Asante.

Watanzania walio wengi wanakuombea yaliyo mema Tunakuahidi tupo nawe kukushika mkono kwa kila hatua Maombi yao Mungu atayasikia hata kama hukumu imepita Tupo na wewe na Mungu yupo na wewe.
                             
                             

Yanga Yasajili Straika Mpya wa Maana

Yanga Yasaka Saini Ya Straika Wa Kagera
ZIKIWA zimebaki siku moja kabla ya kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili hapa nchini, uongozi wa Yanga unajipanga vilivyo kuhakikisha unakiimarisha kikosi chake ili kiweze kufanya vizuri katika mechi zake zijazo za Ligi Kuu Bara lakini pia katika michuano ya kimataifa.

Uongozi unahitaji kusajili wachezaji wanne katika dirisha hili dogo la usajili kwa ajili ya kuziba upungufu uliojitokeza katika kikosi hicho tangu kuanza kwa Ligi Kuu Bara msimu huu katika nafasi ya ulinzi, kiungo pamoja na ushambuliaji. Na tayari mazungumzo na straika mmoja wa Kagera Sugar yanaendelea.

Hata hivyo, habari za kuaminika kutoka ndani ya Yanga ambazo Championi Jumatatu limezipata zimedai kuwa mpaka sasa uongozi huo umeishaanza mazungumzo
na baadhi ya wachezaji ambao inawahitaji akiwemo Mtogo Vincent Bossou ambaye ilimuacha baada ya kumalizika kwa msimu uliopita lakini pia kiungo wa Mtibwa Sugar, Mohamed Issa ‘Banka’.

Ukiachana na wachezaji hao ambao taarifa zao zimekuwa zikisemwa sana hivi karibuni pia uongozi huo unadaiwa kuwa katika mazungumzo na Straika wa Kagera Sugar, Jafar Kibaya ambaye ni kati ya washambuliaji mahiri hapa nchini.

Mshambuliaji huyo ndiye aliyeivuruga ngome ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu alipoifungia timu yake bao moja wakati Yanga iliposhinda 2-1 na kuwazidi ujanja mabeki wawili matata wa timu hiyo, Kelvin Yondani na Andrew Vicent Dante ambao imekuwa adimu sana wao kufungwa msimu huu.

Akizungumza na Championi Jumatatu, mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye aliomba kutotajwa jina lake, alisema uongozi huo unajipanga kuhakikisha unamsajili Kibaya ili kuiongezea nguvu safu yake ya ushambuliaji ambayo tangu kuanza kwa ligi kuu imekuwa ikiwategemea Ibrahim Ajibu pamoja na Mzambia, Obrey Chirwa.

“Kwa hiyo kutokana na hali hiyo tumeona ni bora tupambane kuhakikisha tunamsajili Kibaya kwa ajili ya kuja kusaidiana na wachezaji hao kwani Donald Ngoma na Amissi Tambwe kwa sasa siyo wachezaji wa kuwategemea sana.

“Muda mwingi wamekuwa nje ya uwanja, jambo ambalo linatufanya tuwe na wakati mgumu pindi wanapoumia, kwa hiyo Kibaya anatufaa na tayari kocha ametuambia tuhakikishe tunamsajili kwani alimuona tulipocheza na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba na alitusumbua sana,” alisema kiongozi huyo.

Katika mchezo huo dhidi ya Yanga, Kibaya ndiye aliyefunga bao pekee la Kagera ambapo Yanga ilishinda 1-2.
Alipoulizwa suala hilo, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa alisema: “Muda wa usajili bado haujafika kwa hiyo kwa sasa siwezi kuzungumzia hilo, tusubiri kwanza mpaka utakapofika muda huo.”

Hata hivyo, Meneja wa Kagera Sugar, Mohamed Hussein alipoulizwa kama wapo tayari kumuachia mchezaji huyo ajiunge na Yanga alisema: “Waje tuzungumze kama watakuwa tayari kutupatia fedha ambayo tutawaambia haina shida kwani Kibaya bado ana mkataba wa miaka miwili na sisi.

“Tumemsajili msimu huu akitokea Mtibwa Sugar kwa hiyo wakikubali kutupatia fedha tutakayowaambia basi tutawapatia.”

Wabunge Wanaotaka Pensheni Watakiwa Kuanzia Bungeni Kabla ya Kufika Serikalini

Wabunge Wanaotaka Pensheni Watakiwa Kuanzia Bungeni Kabla ya Kufika SerikaliniSerikali imewataka wabunge wanaotaka utaratibu wa kulipwa pensheni mara baada ya kumaliza kipindi cha ubunge urejeshwe, walipeleka jambo hilo kwanza kwenye  Tume ya Utumishi ya Bunge kabla ya kulifikisha serikalini.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde amesema leo Jumanne bungeni kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Vunjo (NCCR_Mageuzi), James Mbatia.

Mbatia amesema sheria ya mwaka 1981 ilikuwa inatambua pensheni kwa wabunge wanaomaliza muda wao na kuihoji Serikali inatamka nini kuhusu kulifufua suala hilo.

Akijibu swali hilo, Mavunde amesema kwa sababu swali la mbunge huyo ni kufufua sheria ya pensheni ni vyema lianzie kwao ( Tume ya Utumishi ya Bunge) ndio lifike serikalini.

Katika swali la msingi, Mbatia ametaka kufahamu Serikali haioni busara kuifanyia marekebisho Sheria ya Maslahi na Mafao ya Majaji namba 3 ya mwaka 2007 au vinginevyo ili majaji waweze kupatiwa huduma muhimu za matibabu wakati wanapostaafu.

Akijibu Mavunde amesema masharti ya kazi na stahili za majaji ya mwaka 2013 kwa maana majaji wa Mahakama Kuu yamefafanua kuwa majaji hao wamejumuishwa katika utaratibu wa matibabu kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHF)wawapo kazini.

Amesema gharama hizo hulipwa na Serikali na hata wanapostaafu wanaendelea kupata huduma hizo kupitia mfuko huo.

"Kwa wale waliostaafu kabla ya masharti hayo kuanza kutumika hawanufaiki na mfuko huo," amesema.

Kuhusu kuangalia kulifanya suala hilo la  kiutawala, Mavunde amesema kwa sababu ni suala la kisheria na sera wanalichukua na kulifanyia kazi. 

Idriss Atuma Salamu za Pole kwa Mama Lulu "Mama Ndio Tunahitaji Kukuangalia Zaidi"

Idriss Atuma Salamu za Pole kwa Mama Lulu "Mama Ndio Tunahitaji Kukuangalia Zaidi"MCHEKESHAJI na mshindi wa Big Brother Africa, Idris Sultan, ametoa pole kwa mama wa mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Kalugira, kwa kipindi kigumu alichokianza jana baada ya bintiye kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kutokana na kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba.

Sultan amesema jamii impe faraja na kumtia moyo wakati akiwa katika huzuni ya kuwa mbali na binti yake.  Pia Sultan amemuelezea Lulu kuwa alikuwa ni rafiki yake wa karibu na ni mwanamke shupavu ambaye huzuni yake ikiwa jela itachukua muda mfupi kabla ya kupata marafiki na kujipa moyo wa kuhimili maisha hayo mapya ya miaka miwili.
Hayo ni maneno aliyoyatuma kwenye akaunti yake ya Instagram kama yafuatavyo:
My last piece on this, Mama Lulu tunakuombea kwa Allah upate nguvu ya kukubaliana na hii hali ambayo ni chungu kwetu sote. Tunalazimika kukubali kwasababu Mungu tu ndiye anajua kubaki na jambo kama hili moyoni kwa mda mrefu hivi linaondoaje amani. Binafsi nampenda sana Lulu na anajua, kwa mda wa miaka michache niliyojuana na Liz najua wewe mama ndio tunahitaji kukuangalia zaidi maana Lulu najua atalia wiki ya kwanza na ya pili, ya tatu atapata kazi jikoni, ya nne anajisomea, ya tano kashapata marafiki kote because your daughter is the strongest woman I have ever met maishani mwangu yani ningekua mwanamke ningekua yeye. Baby is good to go na nitajaribu kuwa positive na kusema kua ntammiss sana ila mara mbili tatu sitoacha kumtembelea na tunasubiri siku anatoka na ku-take over her throne. Hakuna aliyependa haya yatokee ila ndio yametokea we only have God and each other now. Be blessed
                              

Mange Kimambi Afunguka baada ya Lulu kupigwa mvua ya Miaka Miwili

From @mangekimambi_ - Breaking newzzzzzzzz..... Lulu amekutwa na hatia ya kuuwa bila kukusudia na amehukumiwa miaka miwili jela.......
.
.
.
Dah huyu jaji anawaza kama mimi posti yangu niliyoposti masaaa mawili yaliyopita nilisema ningekuwa jaji ningemkuta na hatia ila ningempa adhabu ndogo mwaka mmoja au miwili jela.......
.
.
Jaji ametenda haki....
.
.
Sio kama nimefurahi Lulu kafungwa nilichotaka ni kuona hakuna double standards, nilitaka kuona haki inatendeka. Na Lulu ana deserve hiyo miaka 2 jela labda itampa muda wa kufikiria how her actions affected Mama Kanumba na familia yake. Labda akitoka atakuwa more humble......
.
.
.
Lakini still mwanasheria wa serikali achukulie hatua za nidhamu na afukuzwe kazi!! Alijaribu sana kusabotage kesi ili amsaidie mtuhumiwa......
.
.
PS: December Magu anatoa misamaha kwa wafungwa, sidhani kama atawasahau wafungwa wa kumpa kiki ya kufungia mwaka kama Lulu na kina Babu Seya maana ile barua ya kina Baba Seya had Bashitel written all over it."