Jumatatu, 29 Septemba 2014

Omar Gonzalez White House

Mlango huo unavyoonekana 
Taarifa kutoka mjini Washngton zinaeleza kua mwanamume mmoja aliyekua ameshikilia kisu mikononi mwake aliruka uzio wa makao ya Rais wa Marekani Brack Obama na kukimbia kuelekea kwenye makazi hayo mwezi huu .
Maafisa wa Ikulu hiyo wamemtambua mtu huyo kua ni Omar Gonzalez,askari wa zamani aliyepigana Iraq, alikua pamoja na kisu,alikuwa akikimbilia katika mlango mkuu wa makazi ya Rais Obama kabla hajakatwa na maofisa wa Ikulu hiyo maarufu kama White House .
Taarifa zinaeleza kuwa kiboksi chenye kengele ya tahadhari kilikuwa kimezimwa .Mkuu wa shughuliza siri za ikulu hiyo Julia Pearson anatarajiwa kuhojiwa kufuatia tukio hilo na jopo la wanasheria.
Wakati hayo yakitukia Rais Obama na familia yake hawakuwa katika Ikulu hiyo.

NI KIVUMBI LIGI YA MABINGWA ULAYA

 
Katika michuano ya Klabu Bingwa barani Ulaya leo kuna kivumbi kingine ambapo CSKA Moscow itakuwa na kibarua kigumu pale watakapowakaribisha Bayern Munich.
Wakati huo huo Man City waliopigwa bao moja na Bayern Munich watakutana na AC Roma iliyowapiga CSKA Moscow mabao matano katika mechi iliyopita.
Paris St G ya Ufaransa wao wanakutana uso kwa uso na Barcelona
Ukumbumbuke katika mechi ya wikendi iliyopita Paris St G walitoka sare na Ajax bao moja kwa moja.
Ajax inakutana leo na Apoel Nic ambayo ilipigwa na Barcelona bao moja katika mechi ya awali.
Sporting Lisbon ya Ureno leo wanapepetena na Chelsea ya England. Meneja Jose Mourinyo amesema kutokana na umuhimu wa mechi hii atajitoa muhanga kwa kumchezesha mshambuliaji machachari Diego Costa.
Schalke waliotoka moja moja na Chelsea wanacheza na NK Maribor ambayo wiki iliyopita ilitoana jasho na Sporting Lisbon kiasi cha kutoka na bao moja kwa moja.
BATE Bor itakipiga na Ath Bilbao
Shakt Donsk inashuka dimbani dhidi ya FC Porto iliyowachapa mabao sita BATE Bor
Mechi kamili za leo hizi hapa
  • CSKA v Bayern Munich
  • City v Roma
  • Paris St G v Barcelona
  • Sporting v Chelsea
  • Apoel Nic v Ajax
  • Schalke v NK Maribor
  • BATE Bor v Ath Bilbao
  • Shakt Donsk v FC Porto

Taarifa kuhusu kifo cha msanii wa bongofleva Side Boy Mnyamwezi.

rip
Ingawa Nafasi yake katika muziki wa Bongo Fleva ilikuwa ikipanda taratibu kulingana na aina ya muziki aliokuwa akiumba,single iliyomtambulisha zaidi kwenye muziki wa Bongo Fleva inaitwa Kua uone ambayo alimshirikisha Ally Kiba.
sideeee
Mchana wa jana imetoka taarifa kuwa amefariki dunia ambapo kwa zaidi ya mwezi mmoja alikua amelazwa kwenye hospitali ya Nyangao iliyopo Mkoani Lindi ambako ndiko nyumbani kwao.
ss
Mipango ya mazishi imepangwa ambapo atazikwa kesho huko huko Lindi,Rest In Peace Side Boy,moja ya post zake kwenye mtandao wa Facebook aliandika ‘habari za usiku huu wapendwa!dua zenu zinahitajika coz hali yangu c poa kabisa’
Hii ni moja ya post za mwisho za Side boy kwenye page yake ya facebook
Hii ni moja ya post za mwisho za Side boy kwenye page yake ya facebook
Hii ni post nyingine kati ya post zake za mwishomwisho, mtoto Nasra ni yule aliekua amefichwa kwenye box kwa miaka minne
Hii ni post nyingine kati ya post zake za mwishomwisho, mtoto Nasra ni yule aliekua amefichwa kwenye box kwa miaka minne
Side Boy Alitoa single kadhaa ikiwemo Hujafa hujaumbika,Jifungue salama,Usimdharau Usiyemjua na Kua Uone,Hii ni moja ya single zake ambayo ili hit miaka 6 iliyopita inaitwa Kua uone.