Alhamisi, 18 Septemba 2014

UJIO WAKE STEVE RNB,NI NOUMA


steve 1
Ni baada ya kimya kirefu kutoka kwa msanii Steve rnb sasa amerudi na ngoma kali.Unaweza kuiskiliza online au kudownload kuihifadhi katika kifaa chako.

MAN CITY YAANZA VIBAYA UEFA

 
Man City ilipata kichapo cha goli moja bila jibu
Mechi zilizochezwa usiku wa kuamkia leo za Klabu Bingwa barani ulaya ambapo Manchester City walianza vibaya michuano hiyo baada ya kupata kichapo cha goli moja bila majibu kutoka kwa wenyeji wao Bayern Munich ya Ujerumani.
Goli la Bayern Munich lilifungwa na Jerome Boateng katika dakika 90
Wakati Man City wakiadhibiwa ugenini na Bayern Munich, wenzao Chelsea wakiwa nyumbani Stamfode Bridge walitoka sare ya goli moja kwa moja na Schalke.
AC Roma ya Italia wao waliadhibu CSKA Moscow ya Urusi kwa jumla ya magoli 5 -1 huku Ajax na Paris St. Gamaine ya Ufaransa zikitoka sare ya moja kwa moja.
Bacelona wao waliamua kuushikisha adabu Apoel ya Syprus kwa kuifunga goli moja bila majibu wakati FC Porto ya Ureno wakifungulia mvua ya magoli iliyoambatana radi pale ilipowanyeshea wapinzani wao Bate Borisov ya Belarus kwa jumla ya magoli 6 bila majibu.
Matokeo mengine NK Maribor ya Slovenia ilitoka sare ya 1 - 1 na Sporting Lisbon ya Ureno huku Athletic Bilbao ya Hispania zikitoka uwanjani bila kufungana na Shaktar Donetsk ya Ukraine.

Polisi wadaiwa kutesa raia Nigeria


Polisi nchini Nigeria wamedaiwa kuwatesa wanaume na wanawake pamoja na watoto. Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International.
Shirika hilo limechapisha ripoti yake ambayo inadai kwa watu huzuiliwa kinyume na sheria Kaskazini Mashariki mwa Nigeria ambako jeshi la serikali linapambana na wanamgambo wa Boko Haram.
Serikali ingali kujibu tuhuma hizo.
Shirika hilo linasema kuwa jeshi la Nigeria pamoja na polisi hutumia mbinu tofauti kuwatesa watu ikiwemo kuwapiga, kuwadunga misumari na kuwang'oa meno, ubakaji na dhuluma nyinginezo za kingono.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo wanajeshi huwatesa watu zaidi katika eneo la Mashariki ambako vita dhidi ya Boko Haram ni vikali zaidi.
Shirika hilo linasema kuwa kati ya watu efu tano na elfu 10 wamekamatwa tangu mwaka 2009 na kunyongwa katika kambi za wafungwa.
Ripoti hiyo yenye mada, "Welcome to hell fire", inatoa taswira mbaya sana kuhusu haki za binadamu kote nchini Nigeria, na inasema kuwa vituo vingi vya polisi vina afisaa wa polisi anayesimamia mateso na kutaka watu kulipa hongo ili kukwepa mateso hayo.
Licha ya kuharamisha mateso, shirika la Amnesty linasema kuwa wanasiasa nchini humo bado hawajapitisha sheria inayowachukulia hatua wale wanaohusika na mateso dhidi ya raia wasio na hatia.