Jumamosi, 12 Desemba 2015

Yaya Toure ametwaa tuzo ya mchezaji bora Afrika wa BBC 2015 na kuingia katika rekodi za Okocha na Kanu …



Kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast na klabu ya Manchester City ya Uingereza Yaya Toure alikuwa ni mmoja kati ya wachezaji watano waliokuwa wanawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika inayotolewa na shirika la utangazaji la Uingereza BBC, Yaya Toure amefanikiwa kuibuka na ushindii wa baada ya kupata kura nyingi zaidi ya Pierre-Emerick AubameyangAndre AyewYacine Brahimi na Sadio Mane.
86610826_afoty-2015
List ya wachezaji watano waliokuwa wanawania tuzo ya mchezaji bora wa BBC
Kutwaa tuzo hiyo kwa Yaya Toure kunamfanya kuwa mchezaji wa tatu kuingia katika rekodi ya wachezaji wa zamani wa Nigeria Nwankwo Kanu na Jay-Jay Okocha ambaoo kila mmoja katwaa tuzo hiyo mara mbili, rekodi ambayo inashikiliwa na wachezaji watatu kwa sasa ikiwemo Toure.
e
List ya wachezaji waliowahi kutwaa tuzo hiyo
Toure kwa mara ya kwanza alifanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa BBC mwaka 2013, baada ya ushindi wa tuzo hiyo hii ni moja kati ya sentensi za Yaya Toure “Najivunia kupokea tuzo hii kutoka kwa mashabiki wangu siwezi kuamini”

Baada ya Nape Kula Shavu la Uwaziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo.. TFF yatoa Tamko Hili



Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za pongezi mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye kufutia kuteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo katika serikali ya awamu ya tano.
Katika salamu zake, Malinzi amempongeza Nape na kusema TFF ina imani nae katika nafasi hiyo, na kuahidi kushirikiana katika michezo na haswa katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya mpira wa miguu nchini.
Aidha pia Malinzi amewapongeza Paschal Kihanga, Mwenyekiti wa chama cha soka moa Morogoro kwa kuchaguliwa kuwa Meya wa manispaa hiyo, na James Bwire mmiliki wa shule ya Alliance kwa kuchaguliwa meya wa manispaa ya Nyamgana.
Malinzi amewatakia kila la kheri katika nafasi hizo walizozipata za kuwatumikia watanzania, na kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini anawatakia kila la kheri na kuahidi kushirikiana nao.

Rais Magufuli Amwaga Mabilioni Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu..Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania Wasema Haya



Shilingi billion 473 zimetengwa kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini kwa mwaka huu ikilinganishwa na Shilingi bilioni 341 zilizotolewa  mwaka jana ikiwa ni ongezeko la Tsh. bilioni 132 katika bajeti ya mwaka huu.
Hayo yalisemwa  jana jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania(Tahliso)  bwn. Nzilanyingi  John  alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuaandaa mdahalo kujadili hotuba ya Rais Dkt. John Magufuli aliyoisoma Dodoma wakati wa ufunguzi wa bunge la kumi na moja .
Alisema kuwa kwa kipindi kifupi kumekuwa na  mabadiliko ya haraka yaliyotokea katika sekta ya elimu nchini kwa mwaka huu  kwani kuna ongezeko la zaidi ya wanafunzi 1800 waliopata mkopo ikilinganishwa na mwaka uliopita ambapo ni wanafuzi 34128 pekee ndio waliofanikiwa kupata mkopo.
“Mpaka sasa jumla ya wanafunzi 51,675 wa mwaka wa kwanza wamepata mkopo na lengo ni kufikia 53,032, pia jumla ya wanafunzi 91 wa shahada ya uzamili  na wanafunzi 113 wanaosoma vyuo vya nje tayari wamepata mkopo” alisema John.

Aliongeza kuwa katika kipindi kifupi kijacho bodi ya mikopo imehakikisha kutoa mikopo kwa wanafunzi zaidi ya elfu moja wanaochukua Diploma maalumu ya ualimu Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na hivyo kukamilisha adhma yao ya kutoa mikopo kwa wanafunzi 53,032.
Aidha shirikisho hilo ambalo ni umoja wa viongozi wa serikali za wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini umeandaa mdahalo wenye lengo la kutoa fursa kwa watanzania wengi kujadili hotuba hiyo  na namna rais alivyoanza kutekeleza majukumu yake katika nafasi hiyo.
Mdahalo huo utafanyika jijini Dar es Salaam tarehe 13 mwezi huu katika ukumbi wa Nkurumah na wazungumzaji wakuu katika mdahalo ni Mtaalamu mbobevu wa uchumi kutoka chuo kikuu cha Mzumbe Prof.Honest Ngowi, Dkt. John Lingu kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwanadiplomasia Christopher Liundi.