Jumanne, 26 Januari 2016

Diamond Platnumz: Baada Ya Nape Nnauye Mimi Ndo Waziri wa Habari Na Michezo Mtarajiwa

Diamond Platnumz amesema akiachana na muziki anataka kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kuweka vitu sawa na kutoa fursa zaidi kwa vijana.

Akizungumza katika kipindi cha Papaso cha TBC FM, Diamond alisema kama akiingia kwenye siasa basi nia yake ni kuwa Waziri wa Michezo.

“Kwa sasa hivi siasa bado ila nikiingia kwenye siasa baadaye akimaliza mheshimiwa Nape nachukua mimi kile cheo cha Waziri wa Michezo,” alisema na kuongeza;

“Kile nakiweza kabisa kwa sababu mimi ukinimbia sijui kuhusu mpira, movie mimi naweza kabisa nikiwa Waziri, nikavifanya na vikawa na maendeleo.

"Ni kitu ambacho naweza siyo nasema nataka kuwa mbunge ila mimi nataka ile siku nimeacha kufanya muziki naingia kwenye siasa basi nakuwa Waziri  wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na kuboresha vitu”

Diamond ambaye hakuweka wazi kwamba ataingia kwenye siasa kupitia chama gani, mwaka jana katika kampeni za uchaguzi mkuu uliomuingiza rais Magufuli madarakani, alishiriki kikamilifu kwenye kampeni za CCM na kutengeneza wimbo pamoja na video.

Le Mutuz Mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu Amvaa Benard Membe..Adai Membe Ametukosea Sana Watanzania....

Lemutuz
Kufuatia kauli za aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa katika awamu ya nne Bernald Membe, kuonekana kupinga juhudi za Rais John Pombe Magufuli kwenye masuala mbalimbali ikiwemo suala la Safari za nje kwa viongozi wa Umma.lemutuzzzzsss

Mtoto wa aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Tanzania John Malecela, anaefahamika kwa jina la Le Mutuz Nation amefunguka ya moyoni na kueleza kuwa anachokifanya Membe sio ustarabu kwa serikali ya Magufuli kwani hajatumia ustarabu kama kiongozi na kuamua kuonesha ubinafsi.

Ameandika Kama Ifuatavyo;

LIVE STRAIGHT TALK:- Morning Guys Membe ametukosea sana WaTanzania kwa kauli zake Kali za kukemea juhudi za Mabadiliko ya Rais Magufuli ambaye ndio kwanza anakaribia kutimiza mwezi wa pili katika Madaraka infact Membe ameonyesha Tabia moja isiyokuwa nzuri sana kwetu wote binadam yaani UBINAFSI au SELFISHNESS...I mean Rais Magufuli anachokifanya ni kile alichokiahidi ambacho hata Membe mwenyewe alikiunga sana mkono kwenye kampeni za Urais na sisi wote Magufuli alisema wazi kwamba Taifa limeoza Membe alikuwa na nafasi kubwa kumkatalia then kwamba sio kweli Taifa halijaoza kwa sababu labda moja ya sababu ya Membe kujitokeza now na kauli Kali ni kujaribu kutetea record ya utawala aliokuwa mshiriki wa karibu na Rais aliyepita basi anakosea sana kwa sababu tulimkataa Lowasaa kwa kuwa alikuwa Rafiki na matajiri na waliotuambia kwamba Lowassa hafai ni pamoja na yeye mwenyewe Membe sasa Leo kweli tena Membe anasimama kushambulia kazi za Magufuli kwa niaba ya Wafanyabiashara? ....Please Membe atuombe radhi WaTanzania Millioni 50 tuliomchagua Magufuli cause sisi bado hatujalalamika kivileee kama yeye mtu Mmoja ambaye hapa anakuwa kigeu geu ni yeye Membe aliyesifia uamuzi wa Magufuli kusimamisha Safari za Nje kwa Maofisa wa Serikali akasema "Tulikuwa tunapishana Juu kwa JUU kama nyumbani kuna moto" Leo Mwezi Mmoja na Nusu later Membe tena amebadilika anasema Safari ni lazima? WHY? .....jana nilikuwa mstaarabu kidogo nilidhani Membe alipitiwa tu lakini kumsikia akizungumza tena Jana nasema HAPANA agenda aliyonayo Membe this time around sio yetu Wananchi ninaanza kuwa na wasi wasi labda Rais JK aliwapa watu wengi vyeo kwa USHAURI wa Membe ndio maana sasa anaumia kuona alikuwa anamshauri vibaya Rais like sio siri Mkurugenzi wa NIDA alikuwa ni Rafiki wa karibu sana wa Membe Jana tu imedhirika huenda amefuja karibu Tsh. 156 Billion za kodi zetu kwenye vitambulisho vya Taifa now niambie kipi cha ajabu Mkurugenzi wa Shirika la Umma amepata wapi mapesa ya ajabu mpaka kujenga MRC pale nyuma ya Shoppers Plaza Mikochen? ...I mean kuna mambo mengine wanatufanya kama Watoto WHY? Membe amezungumza kutetea Wafanyabiashara na mediocre leaders it is wrong atuombe radhi Watanzania..Lemutuz.

Kampuni ya UDA Yakanusha Kufilisika..Yadai ni Njama..Ripoti Kamili ipo Hapa

Mabasi ya UDA
Kumekuwepo na taarifa za uwongo kwenye vyombo vya habari, hasa kijarida cha Dira ya Mtanzania, na mitandao ya kijamii kuhusu uongo kuwa kufilisika kwa Shirika la Usafiri Dar Es Salaam (UDA) Limited.

Menejimenti ya Shirika la Usafiri Dar Es Salaam inakanusha uwongo huo kuwa UDA haijafilisika na haina dalili zozote za kufilisika isipokuwa ni Shirika la namba moja nchini na Afrika Mashariki na Kati linalokuwa kwa kasi ya ajabu kimaendeleo na kibiashara.

Zifuatazo ni takwimu zinazodhihirisha ukweli huu:

UDA imeongeza idadi ya mabasi kutoka mabasi 7 makukuu na mabovu Mwaka 2012 na kufikia takribani mabasi 400 mwaka 2015 yakiwemo mabasi 255 ya kawaida na mabasi makubwa – Hercalus, mapya na ya kisasa kabisa duniani (ya BRT) 140.

Ndani ya miaka 3, kampuni ya UDA imekuwa kwa zaidi ya asilimia 5,000

Kampuni hii imeweza kufanya maandalizi yote ya kuwezesha kuendesha mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART Project) kwa ufanisi mkubwa. Mbali na kununua mabasi, kampuni imeweze kununua mtambo bora na wa kisasa kabisa duniani wa kukusanya nauli na kuongezea mabasi (Intelligent Transportation System – ITS) wenye thamani kubwa kutoka Ubelgiji na Ujerumani. Vile vile kampuni imeweza kusaili na kufundisha madereva wa Kitanzania zaidi ya 300 na kuwaajiri kwa ajiri ya kuendesha mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART Project)

Kampuni imejenga karakana bora na imara na kununua vitendea kazi vya kisasa kwa ajiri ya mabasi yake ya kawaida na mwendo haraka.

Kampuni imepeleka watendaji wake kwenye miradi mbalimbali ya BRT duniani ili kupata uzoefu wa kuwawezesha kuendesha mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART Project) kwa ufanisi. Vile vile Kampuni imeweza kuajiri wataalam kutoka nje (expatriates) kwa ajiri kuongezea nguvu wataalam wake wa ndani.

Kwa takwimu chache hizo hapo juu, Kampuni ya UDA ni namba moja Afrika kwenye sekta ya usafirishaji wa abiria barabarani kwa idadi ya watu inaosafirisha, idadi ya mabasi na ubora wa menejimenti.

Mafanikio haya ya Kampuni ya UDA yanatokana na umahiri wa uendeshaji kutoka Simon Group chini Uongozi thabiti wa Mwenyekiti wake Ndugu Robert Simon Kisena na si vinginevyo, kama washindani wetu wavyojaribu kutuchafua kwamba kuna wanasiasa nyuma yake.

Tunawataka washindani wetu waache tabia ya fisi ya kumfuata mtu anayetembea kwa haraka wakidhani atandondosha mkono wapate kitoweo vinginevyo watakufa njaa.

Imetolewa na Uongozi wa SHIRIKA LA USAFIRI DAR ES SALAAM (UDA) LIMITED.

Maswali 9 ‘Msukule’ Kukutwa Nyumba ya Tajiri Chini ya Shimo la Choo

Hofu imeendelea kutanda maeneo ya Kibamba jijini Dar na kuacha maswali tisa kwa wananchi kuhusiana na mwanamke aliyekutwa kwenye shimo la urefu wa futi kumi, nyumbani kwa mfanyabiashara aliyejulikana kwa jina moja la Mtei.

HALI YA MWANAMKE HUYO
Mwanamke huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 27, aliwashangaza wakazi wa eneo hilo kwani ndani ya  shimo alilokutwa alionekana mchafu, aliyenyongea, akiwa hoi kwa njaa na mtupu kiasi cha kudhaniwa ni msukule (mtu aliyechukuliwa ndondocha).

SIKU YA TUKIO
Ilikuwa Jumanne ya Januari 19, mwaka huu katika shimo hilo lililojengwa na Mtei, inasemekana kuwa, shimo hilo  ni kwa ajili ya chemba ya choo lakini haijaanza kutumika kwa vile nyumba hiyo nayo haijaanza kukaliwa rasmi na familia zaidi ya kuwepo kwa mlinzi.

 Akiwa uchi shimoni.
UWAZI ENEO LA TUKIO
Kufuatia kusambaa kwa taarifa za mwanamke kukutwa shimoni kwenye nyumba ya mfanyabiashara huyo, Uwazi kama ilivyo ada yake, lilitinga eneo la tukio kwa lengo la kuchimba mawili, matatu kuhusu hali halisi.

MAJIRANI WASHANGAZWA
Baadhi ya majirani wa eneo hilo walionesha kushangazwa na tukio hilo huku wakiwa na maswali hayo tisa kuhusu mwanamke huyo ambaye walisema si mkazi wa maeneo hayo na wala hawajawahi kumuona.

 Mwanamke huyo baada ya kutolewa shimoni.

MASWALI YA MAJIRANI
Ni nani aliyemuingiza shimoni mwanamke huyo na kwa madhumuni gani? Kwani kwa jinsi shimo lilivyo, lazima aliingizwa au aliingia kwa kutumia ngazi.

Alikuwa akiishi kwa kula chakula gani kwani wakati anatolewa, muda mwingi alikuwa akilalamikia njaa.

Swali la tatu ambalo majirani walikuwa nalo, mwanamke huyo aliishi ndani ya shimo hilo kwa siku ngapi? Kwani nywele na kucha zake ziliashiria si zaidi ya mwezi mmoja. Swali kuu, aliingia/ aliingizwa lini na muda gani kati ya mchana na usiku?

Je, aliingizwa kwenye shimo hilo akiwa na nguo zake halafu aliyemwingiza/ waliyomwingiza walizipeleka wapi?

Swali la tano ambalo majirani hao walikuwa wakilijadili sana ni, je! Mwanamke huyo ni mgonjwa wa akili au ni msukule? Kama si chochote kati ya hayo mawili, kwa nini alikuwa hapigi kelele?
Sita, majirani hao waliulizana kama siku za karibuni wamewahi kusikia kwenye vyombo vya habari kuna mwanamke mwenye umri huo anatafutwa? Wote walisema hawajasikia.

Wengi walisema huenda mwanamke huyo aliingizwa kwenye shimo hilo na ‘maadui’ wa biashara wa Mtei. Lakini kama ni kweli, walikuwa na lengo gani na walimpata wapi mwanamke huyo na akiwa katika hali gani?

Katika mahojiano na majirani wakati bado akiwa ndani ya shimo amekaa, mwanamke huyo aliweza kujibu maswali karibu yote, lakini swali la anaitwa nani na ameolewa au la, yalimshinda kujibu. Ni kwa nini?

Polisi Mbezi wanasema wamekuwa wakimpigia simu Mtei, lakini hapokei. Ni kwa nini?

MFANYAKAZI WA MTEI SASA
Naye mfanyakazi anayeitunza nyumba hiyo, Richard Pascal alipozungumza na Uwazi kuhusu tukio hilo alikuwa na haya:

 “Ninachokumbuka mimi, Jumanne, wiki iliyopita, saa 3:00 asubuhi, bosi wangu Mtei alikuja. Ni kawaida yake kuja na kukagua mji wake.

 “Nikiwa naendelea na shughuli zangu, aliniita hapa nje. Nilipofika  aliniambia nichungulie ndani ya shimo. Nilifanya hivyo, nikashtuka sana kumwona mwanamke akiwa mtupu huku akinikodolea macho.
“Niliogopa kwa sababu sikutarajia kama kuna mtu anaishi shimoni bila mimi kujua wakati ndiyo nalinda hapa siku zote.”

Hali aliyokuwa nayo.

AWAITA MAJIRANI
“Niliamua kuwaita majirani. Baada ya muda mfupi watu wakawa wamejazana hapa kila mmoja akishangaa na bosi wangu akatoa taarifa Kituo Kidogo cha Polisi Kibamba ambapo askari walifika.
“Lakini na wao walipatwa na mshangao huku wakijiuliza ni vipi mwanamke huyo aliingia shimoni bila kuumia wala kuvunjika?”

POLISI WAMUHOJI
“Mwanamke huyo alipohojiwa na polisi alisema ameishi humo miaka mingi na mara nyingi alipokuwa akihojiwa alikuwa akililia chakula. Polisi waliniomba ngazi, wakaitumbukiza shimoni kisha yeye mwenyewe akapanda haraka mpaka nje.”

APELEKWA TUMBI
“Polisi walimchukua na kumpeleka Hospitali ya Tumbi (Kibaha mkoani Pwani) ambako nadhani anapatiwa matibabu.”

MLINZI APATA WASIWASI
“Mpaka sasa hivi mimi napatwa na wasiwasi. Nitamuomba bosi wangu aniongezee mtu mwingine ili tuwe wawili, kwani mimi hapa ni mgeni. Nimekuja hapa, Desemba 9, mwaka jana.”

SIKILIZA MAHOJIANO
Uwazi lilifanikiwa kunasa mahojiani kati ya mwanamke huyo akiwa ndani ya shimo amekaa na polisi huku wananchi wakiwa nje wakitaka kumuokoa.
Polisi: “We, unaitwa nani?”
Mwanamke: (kimya).
Polisi: “Unakaa wapi?”
Mwanamke: “Mbezi Makabe.”
Polisi: “Umeolewa?”
Mwanamke: (kimya).
Polisi: “Umekuja lini hapo?”
Mwanamke: “Hapa kwangu.”
Polisi: Umekuja lini?”
Mwanamke: “Mi njaa inaniuma bwana.”

UWAZI NYUMBANI ANAKOISHI MTEI
Uwazi lilifika nyumbani kwa Mtei, Kibamba ya Luguruni jijini Dar, hatua chache tu kutoka kwenye Kituo cha Mabasi Kibamba lakini hakupatikana, Uwazi liliacha namba ya simu lakini hakupiga na ilipopigwa, imekuwa ikiita bila kupokelewa.

UWAZI KITUO CHA POLISI
Siku hiyohiyo, Uwazi lilifika Kituo cha Polisi Mbezi ambapo askari mmoja ambaye hakupenda kutaja jina lake kwa vile si msemaji wa jeshi hilo, alisema mpaka sasa wanamtafuta Mtei ili kumsikia kwa kina kuhusu tukio hilo kwa vile yeye ndiye aliyepiga simu polisi kutoa taarifa.
“Huyo Mtei, tunamtaka hapa. Yeye ndiye aliyetoa taarifa ya mwanamke kukutwa kwenye shimo nyumbani kwake. Lakini tulipofika hatukumkuta. Na kila tukipiga simu yake, inaita tu bila kupokelewa,” alisema afande huyo.

UWAZI HOSPITALINI TUMBI
Baada ya hapo, Uwazi lilifunga safari hadi Hospitali ya Rufaa ya Tumbi, Kibaha, Pwani ambapo halikufanikiwa kumpata msemaji, lakini muuguzi mmoja wa hospitali hiyo alikiri kupokelewa kwa mwanamke huyo.

UWAZI LAMBANA MTEI
Juzi, Uwazi lilimpigia simu Mtei na mambo yakawa hivi;
Uwazi: “Wewe ni Mtei?”
Mtei: “Eee, unasemaje?”
Uwazi: “Tunaomba ufafanuzi kuhusu yule mwanamke aliyekutwa kwenye shimo nyumbani kwako…”
Mtei: “Ooh! Siyo mimi, yule ni Mchaga mimi ni Muhaya, nipo Kagera.”
Uwazi likamrudia aliyetoa namba…
“Kwani si ulikuwa unaongea naye sasa hivi na akakwambia yeye si Mtei! Nimesikia maongezi yenu, lakini alisogea mbali. Kwa hiyo sijui zaidi.”

KAMANDA WA POLISI KINONDONI
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, ACP Christopher Fuime alipoulizwa kuhusu tukio hilo,  alikiri kulitambua na kwamba, bado wanalifanyia uchunguzi.
Yeyote anayemjua mwanamke huyo (pichani ukurasa wa mbele) apige simu namba 0715454656 au 0784 339616, chumba cha habari.

Source;Global Publishers

Nyumba ya Mchungaji Lakatware Yasababisha January Makamba Kuchukua Hatua Kali Kwa Maafisa Hawa

 
SAKATA la maofisa watatu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), waliosimamishwa kazi kwa tuhuma ya kukiuka miiko yao ya kazi, limechukua sura mpya, baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, kuagiza wafikishwe mbele ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Pamoja na hayo, Waziri huyo amemsimamisha kazi aliyekuwa mwanasheria wa baraza hilo, John Mnyele kwa matumizi mabaya ya ofisi.

Akizungumza  jana, alisema tayari amemwagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, kuwasilisha mashtaka yanayowakabili maofisa hao watatu Takukuru kwa ajili ya uchunguzi na hatua zaidi, ikiwemo kufikishwa mahakamani.

Maofisa waliosimamishwa kazi kutokana na udhaifu huo ni pamoja na Ofisa Mazingira Mwandamizi Dk Eladius Makene, Mwanasheria Daraja la II Wakili Heche Suguta Manchare ; na Ofisa Mazingira Boniface Benedict Kyaruzi. Wanatuhumiwa kukiuka miiko ya kazi yao katika kusimamia kiwanda cha kusindika minofu ya punda kilichopo mkoani Dodoma.

Pamoja na maofisa hao, pia Mwanasheria Mnyele, anayetuhumiwa kuingia mkataba na Mchungaji Getrude Rwakatare wa kuondoa kesi mahakamani kwa niaba ya NEMC bila kuijulisha ofisi, naye anachunguzwa na taasisi hiyo ya rushwa.

Mama Rwakatare kwa sasa ana kesi mahakamani dhidi ya baraza hilo ya kupinga kubomolewa kwa nyumba yake, inayodaiwa kujengwa mahali pasiporuhusiwa.

Kiwanda hicho cha minofu ya Punda cha China, kilianza kazi hiyo rasmi mwaka 2012 huko Dodoma ambapo pamoja na kuchinja, pia huuza nyama hiyo nje ya nchi, hususan China.

Kiwanda hicho kilipatiwa vibali vyote, ikiwemo cha Mamlaka ya Ukanda Maalumu wa Uwekezaji nchini (EPZA) na cha Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi cha kuchinjia.

Pia, kilikuwa na vibali vingine vya Manispaa. Hata hivyo, hakikuwa na kibali cha masuala ya mazingira kutoka NEMC.

Katika ukaguzi uliofanywa siku za nyuma na Baraza hilo, ilibainika kuwa kiwanda hicho hakina kibali hicho cha mazingira, lakini pia kilikuwa kikilalamikiwa na wananchi wanaokizunguka kutokana na kutofuata taratibu za utunzaji wa mazingira.

NEMC ilibaini kuwa kiwanda hicho, hakikuwa na mfumo wa majitaka, lakini pia kilikuwa kikichoma mabaki yanayotumika kuchinjia ndani ya kiwanda hicho na moshi wake kusambaa maeneo yanayokizunguka.

Kutokana na makosa hayo, baraza hilo lilikifungia kiwanda hicho kama adhabu na kukilipisha faini ya Sh milioni 240.

Juzi Waziri January pamoja na kuwasimamisha maofisa hao watatu kwa kukiuka miiko yao ya kazi, pia aliagiza Mkurugenzi Mkuu wa baraza hilo, Mhandisi Bonaventura Baya, apewe barua ya onyo kali na la mwisho kwa tuhuma za udhaifu katika usimamizi wa watumishi wa baraza hilo, hivyo kusababisha malalamiko mengi kuhusu utendaji wa baraza hilo.

CHADEMA Wamwambia Benard Membe Asiwe Mwoga..Kama Anataka Kuikosoa Serikali Vizuri Ahamie Upinzania Kama Kina Lowassa


Waziri wa zamani wa Mamboya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amekaribishwa kujiunga na Chama Cga Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ikiwa ni siku chache tangu atoe maoni yake akiikosoa serikali ya Rais John Magufuli.

Mwanasiasa huyo mkongwe amekaribishwa na Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob ambaye alimshawishi kwa kutumia mifano ya wanasiasa wakongwe waliokuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliohamia Chadema na Ukawa kwa ujumla akiwemo Edward Lowassa, Frederick Sumaye na Kingunge Ngombale Mwiru.

Wiki iliyopita Membe alinukuliwa akimkosoa Dk Magufuli katika maeneo kadhaa, likiwamo la kubana matumizi, kudhibiti safari za nje na uteuzi wa Baraza la Mawaziri.

Jana, meya huyo kutoka Chadema alisema watu wanamshangaa Membe na kumshambulia siyo kwa sababu amesema mambo ya ajabu, ila yeye si mtu sahihi wa kutoa kauli hiyo.


“Watu hawashangai alichosema (Membe) kwa sababu siyo hoja ngeni, zimesemwa sana na wapinzani. Wanachoshangaa ni yeye (Membe) kusema hayo. Hafanani na hoja anazoziongea,” alisema.

Jacob ambaye alikuwa diwani katika manispaa hiyo katika Serikali ya Awamu ya Nne alisema, hoja zilizotolewa na Membe ni nzuri na kama zingetolewa na mpinzani zingeonekana zina mashiko zaidi.

"Asiwe vuguvugu, hicho ndicho kinachompa shida. Kama anataka kuja huku asiwe na wasiwasi chama changu kitampokea na hata hayo anayoyaongea yatakuwa na mantiki na watu watamsikiliza kwa sababu ni upinzani,” alisema na kuongeza;

“Avuke moja kwa moja kama walivyofanya akina Kingunge (Ngombale Mwiru), (Edward) Lowassa, na (Frederick) Sumaye kuhamia upinzani.”

Jacob alisema Sumaye na Lowassa ambao waliwahi kuwa mawaziri wakuu na Kingunge aliyekuwa kada mkongwe wa CCM, walikuwa viongozi wa ngazi za juu, lakini walihamia upande wa pili (upinzani) na sasa wanaisimamia na kuikosa Serikali kwa uhuru.

“Asiwe mwoga kwamba ataishi maisha gani, Sumaye na Lowassa wamekuwa mawaziri wakuu wakaondoka na maisha yanaendelea.”

Hata hivyo, Jacob alisema Membe hakupaswa kukosoa sera ya Rais Magufuli ya matumizi na Rais kudhibiti safari za nje, kwa sababu yeye amenufaika nayo.

“Nadhani hakuwa mtu sahihi kusema hayo, alipaswa kwanza kumtafuta mtu mwingine aseme halafu yeye afuate baadaye, lakini kuanza kusema yeye moja kwa moja wakati alikuwa ananufaika na anachopinga Rais, anaonekana anamwonea wivu na mgongano wa masilahi.

“Sasa anapoanza yeye kujibu inashangaza. Kwa sababu yeye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje, iliyokuwa inafanya matumizi makubwa halafu unakosoa unaonekana kabisa unaonyesha kuna mgongano wa masilahi,” alisema na kuongeza:

Jacob alisema kwa mpinzani kusema hivyo angeonekana anataka kumuwajibisha Rais ili hayo mambo yaangaliwe kwa kina zaidi.

Alitoa mfano wa waziri wa zamani, Dk Makongoro Mahanga na kusema alipoikosa Serikali hakushambuliwa kwa sababu alishahama kutoka CCM na sasa yupo upinzani.

“Alipozungumzia suala la matumizi ya ardhi, Serikali haikujibu ilikaa kimya kwa sababu aliyeongea ni mtu sahihi,” alisema na kuongeza.

" Kwanza alikuwa kwenye Baraza la Mawaziri na pili hivi sasa yupo kwenye upande wa kuishambulia na kuikosoa Serikali na kuiwajibisha.”

Faiza Ally Awapa Makavu Live Wale Wote Wanaosema Amekosea Kuweka Video ya Mtoto Instagram Akimuomba Hela Mbunge Sugu


Baada ya Video ya mtoto wa Joseph Mbilinyi kuwekwa mtandaoni ikionyesha akiomba hela ya kusuka huku akilia , Mama mzazi wa mtoto huyo aliyeweka Video hiyo mtandaoni amewajibu watu walio comment kwa kumwambia amekosea kwani anamzalilisha mtoto na baba yake ambaye ni mbunge wa Mbeya Mjini.....
"NYINYI MNAOSEMA KAMA NIMESHINDWA KUMLEA MTOTO NIMUACHIA BABA YAKE- NAWAONA WAPUMBAVU TU KAMA WAPUMBAVU WENGINE WOTE..... KUTAKA KUISHI NA MWANANGU SIO SABABU YA BABA KUTOKUJUA MTOTO ANA KAA WAPI! ANAKULA NINI- ADA ANAPATA WAPI NA SHULE ANA SOMA IPI... NDIO NINA HAKI YA KUKAA NA MWANANGU LKN SIO KWAMBA KWA SABABU NAISHI NAE NDIO SABABU YA KUTOMKUTUNZA MWANAE.... NA PUMBAVU ZENU WALE WANAO SEMA NA MZALILISHA SASA MNTAKA NIMPEJE UJUMBE IKIWA SINA MAWASILIANO NAE ? KAMA SIO KUTUMIA MITANDAO ..... ? NAO MNAOSEMA NIMESHINDWA MNAJUA NALIPA KODI KIASI GANI? ADA SH NGAPI ? MATUMIZI NA MNAJUA NAPATAJE MANINA ZENU? AU MNAZANI KUWA SINGLE MAMA MCHEZO - PUMBAVU ZENU NYOTE MNAO SHANGAA MIMI KUONYESHA HISIA ZANGU..... KUNA NYAKATI ZINGINE UNASHINDWA KUJIZUIA UKIWA KAMA MZAZI UNAPO KOSA MSAADA WOWOTE KWA MZAZI MWENZIO SPECIAL AKIWA NA UWEZO WA KUTOA.... NA SI KWAMBA NIMESHINDWA ILA NIMEKASIRIKA NA KUSIKITIKA SANA PALE MWANANGU ANAPO HITAJI NA NAKUA SINA KWA WAKATI HUO NA NIKITIZAMA BABA YAKE ANAO UWEZO LKN ANA NIKOMOA KWA AJILIA YA KUMUACHA - HII HAINGILIANI KABISA NA KUTO KUMJALI MWANANO- NA ZAIDI AKIWA AMESIMAMA BUNGENI KUTETEA WANANCHI IKIWA VIZAZI VYAKE VINA HANGAIKA IKIWA KAKA YAKE SASHA AMBAE AMEMTOA MJINI BAADA KUJULIKANA NA KUMPELEKA MTWARA AMEKUA MLEVI HUKO WKT BORA ANGEMUACHA HAPA GARAGE ALIKUA ANA JIPATIA RIZIKI YAKE ...... WANAO WOTE WAWILI HAWAJALI ..... KAMA MZAZI INAUMA ...... NYIO MSIO JUA UCHUNGU WA MTOTO WALA UGUMU WA KUWA SINGO MAZA FUNGENI MIDOMO YENU VISEBENGO WAKUBWA SUBIRI YENU !!!!!!!!!!! NA BAADA YA YOTE KUNIPELEKA MAHAKANI NATOA HELA ZANGU NA KESI INAZUNGUSHWA..... KILA NINAPO FIKA MAHAKAMANI LZM NILIPE NA ADA YA MWANASHERIA m.2 ...... KAMA  SIO KUKOSA UBINAADAMU NI NINI ????? - SIKILIZENI SINA ASILI YA KITUMWA NIKO KATIKA TAIFA HURU NA NITASEMA NA KUFANYA KILE NINACHO AMINI..... NA NINA AMINI KIONGOZI BORA ANA ANZIA NYUMBANI........... LKN MWISHO WA SIKU YOTE MAISHA NITASIMAMA TU NA NITAWEZA LKN WKT MWINGINE BINAADAMU LZM TUSEME YALIYO MOYONI ILI TUENDELEE NA YAJAYO...... NARUDIA TENA KWA YOYOTE ANAE SHANGAA HILI NI MPUMBAVU NA AMETOKA KWENYE FAMILIA ZA KINAFKI ZINAZO FUNIKAGA VITU AMBAVYO HAVI STAHILI KUFUNIKWA!!!!!!!!!!" Faiza Ali

Bosi wa TP Mazembe Asalimu Amri Kwa Samatta..Huu Ndio Uamuzi Alioutoa


HATIMAYE mmiliki wa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Moise Katumbi amekubali mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta kujiunga na KRC Genk ya Ligi Kuu ya Ubelgiji.
Mchezaji huyo alitarajia kurejea jana nchini kwa ajili ya safari ya Ubelgiji kwenda kuanza maisha mapya katika soka la Ulaya.
Samatta tayari amekwishasaini mkataba wa awali na Genk wa miaka minne na sasa anakwenda kukamilisha taratibu zilizobaki.
Samatta na Genk wanataka kukimbizana na muda ili kuwahi kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili.
Meneja wa Samatta, Jamal Kisongo alisema kuwa hatimaye Katumbi ameridhia Samatta aende klabu anayoipenda ili kuendeleza soka lake.
Katumbi alikuwa anataka Samatta aende Nantes ya Ufaransa, ili kucheza soka huko, lakini mchezaji huyo hakupenda kwenda huko na alikuwa tayari kubaki Congo kumalizia mkataba wake unaomalizika Aprili.

Hii Ndio Itakuwa Safari ya Kwanza Kwa Rais Magufuli Kusafiri Kwenda Nje ya Nchi Toka Awe Rais


wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli huenda akasafiri kwa mara ya kwanza nnje ya nchi toka aingie madarakani mwishoni mwa mwaka jana kuelekea nchini Ethiopia  ambapo atakutana na viongozi wa serikali na Nchi za Afrika zaidi ya 50 katika kikao cha 26 cha Mkutano wa Umoja wa Afrika Mjini Addis Ababa, Ethiopia baadaye wiki hii.Masuala ya amani na ulinzi yatakuwa katika ajenda ya juu hasa ikichukuliwa kile kinachoendelea katika nchi ya Burundi na pia mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika katika nchi za Burkina Faso na Somalia.
Viongozi wa serikali na nchi za Afrika wanatazamiwa kushiriki katika kongamano la 26 la Baraza Kuu la Umoja wa Afrika, litakalofanyika kati ya Januari 30 na 31 ambapo pia watamchagua Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Nchi za Afrika(AU).Kwa mara nyingine tena viongozi wa Umoja wa Afrika(AU) wanatazamiwa kushinikiza kufanyika mageuzi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Licha ya pingamizi kutoka nchi 5 wanachama wa kudumu wa baraza hilo huko nyuma, viongozi wa AU wamesema kwa mara nyingine tena watashinikiza mageuzi katika chombo hicho, wakisisitiza kuwa muundo wa sasa wa baraza hilo hauakisi hali halisi ya siasa na uchumi wa dunia katika karne hii ya 21.Kamati ya nchi 10 za Kiafrika juma lililopita ilifanya kikao na kuafikiana kuwa maslahi ya nchi Afrika katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ndio miongoni mwa ajenda kuu za kikao cha Addis Ababa. Nchi hizo ni Algeria, Libya, Senegal, Sierra Leone, Namibia, Zambia, Uganda, Kenya, Equatorial Guinea na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Viongozi hao wanatazamiwa kurejea mwito wao wa kutaka nchi mbili za Kiafrika ziwe wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Kwa sasa nchi 5 wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la UN ni Marekani, China, Russia, Ufaransa na Uingereza.Viongozi wa Kiafrika wanazituhumu nchi wanachama wa baraza hilo kuwa hazina demokrasia na kwamba zimekuwa zikitumia kura zao za veto kwa ajili ya maslahi yao binafsi.Viongozi wa Umoja wa Afrika aidha wanapendekeza kuongezwa idadi ya nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutoka 20 hadi 25.Hii itakuwa ni nafasi kwa Rais Magufuli kufanya safari ya nje ya nchi kwa mara ya kwanza tokea achaguliwe kuwa Rais wa Tanzania.Rais magufuli kwa sasa amekuwa gumzo katika majukwaa ya kimataifa kutokana na aina ya uongozi wake ambao wachambuzi wa kisiasa wanadai ni nadra kuupata kwa viongozi wan chi za Afrika ambapo rushwa, ufisadi, uvivu na ubadhirifu wa mali ya umma ni moja ya maisha ya viongozi wakuu wa nchi.